Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

IMG_20220906_195751_944.jpg
 

Mke na mume​

Siku ya kwanza
MUME: Halooo vipi mke wangu salama weye?.
MKE: Salama tu
MUME: Uko wapi?
MKE: Jamani si niko nyumbani?!
MUME: Mhh kama kweli uko nyumbani washa blender nisikie…..mke akawasha blender
MKE: Umesikia?
MUME: Okay haya mi natoka kazini naja

Siku ya pili
MUME: Vipi mko salama huko?
MKE: Tupo kama ulivyotuacha
MUME: kwani uko wapi?
MKE: Niko nyumbani napika
MUME: Washa blender kama kweli uko nyumbani
Mke akawasha blender
MKE: Umesikia?
MUME: Poa ntarudi baada ya masaa mawili

Siku sita baadae mume akaamua kurudi saa 11 jioni bila kumtaarifu mkewe.. Alipofika home kamkuta mdada wa kazi yuko peke yake.
MUME: We mama yako yuko wapi?
MDADA: Sijui, aliondoka na blender toka asubuhi😁
 

Jamaa na demu wake..​

Jamaa: Mambo honey, upo ok?
Mrembo: Sipo ok my dear
Jamaa: Una tatizo gani baby?
Mrembo: Nimetoka hospitali kupima, nna mimba.
Jamaa: Weeeeeh... Usiniletee balaa, hiyo mimba imeingiaje wakati huwa tunatumia kinga muda wote?!
Mrembo Kwani nani kakwambia mimba ni yako? Hebu tuliza huo mshono!
 

Muongo kaumbuka​

Mdada alienda super-market kununua
kuku, bahati mbaya kwenye frij
kulikuwa na kuku mmoja tu, muuzaji
akamtoa akamuweka kwenye
mzani, akaonekana ana kilo moja na robo.

Mdada akamuuliza
muuzaji,’Huna mkubwa zaidi?’ Muuzaji
akamchukua yule kuku na
kujifanya kamrudisha kwenye friji, halafu
akamtoa tena kwenye friji na
kumrudisha kwenye mzani, safari hii
akagandamiza mzani kwa gumba,
kuku akaonekana ana kilo mbili. Mdada
akasema ‘Duh afadhali huyu
mkubwa kidogo, naomba unifungie
nawachukua wote wawili


Mamaaaaa muuzaji sijui atatoa wap kuku wa pili..
Hapo ndipo utagundua kwa nini MUWA siyo TUNDA🤔
 
Back
Top Bottom