Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 183,582
- 1,105,380
Ajabu ni kwamba haisaidiagi cho chote. Wanapinduana. Anayekuja anaiba weee yeye na marafiki zake lakini hali ya mwananchi wa kawaida inabakia pale pale; na hata kufubaa zaidi. Matatizo ya nchi za Kiafrika (na mtu mweusi po pote duniani) ni makubwa zaidi; na hizi heka heka za kisiasa ni dalili hafifu tu za tatizo lenyewe - ubinafsi wa kinyama, ulafi uliopindukia kimo, kutojiamini, kujichukia, kutojua nafasi yake katika ulimwengu huu na mengine mengi.Bado sisi, bado sisi,bado sisi. Wenzetu West Africa hawapendagi ubwege





