.
Salute Kiongozi.Sheria ni sheria na unapaswa kuheshimu hata wakichoma nchi yote ibaki majivu ila sheria itabaki pale pale, yeye ana mahela ya kutosha ya kuajiri jopo la mawakili wampambanie, hivyo haipaswi makajamba wote waingie barabarani na kupora, huu upumbavu hata hapa Kenya huwa tunakua nawo mara moja moja eti tukihisi kiongozi fulani kadhulumiwa tunaanza uporaji, huyo unayempora mtaji wake na kumrudisha zero kisa ujinga wako wa kuabudu mungu mtu.
Poa
navuta picha ni jinsi gani vile nampenda mamaangu
atanisamehe tu huyo mgambo kwa nitakachomfanyia.View attachment 1854823
Kuna watu gari la diamond vifua vinafura moto View attachment 1854873View attachment 1854874View attachment 1854875
Kama Katiba na sheria zao nyingiene zimekaa kwenye mfumo wa kibaguzi basi wazifumue.Siyo kweli japo hoja yako ina mashiko kuhusu uamilifu wa sheria kama msumeno unaopaswa kukereza kote kote bila kujali hadhi ya anayekerezwa. Katika uhalisia wake hata hivyo mambo hayako hivyo. Na ishu ya Afrika Kusini kidogo ni tata kulingana na historia yao ngumu waliyopitia hasa hawa weusi. Ati; Angekuwa ni De Klerk au P.W. Botha ndiyo kafanya kosa alilofanya Zuma (ana sababu nzuri tu); ni kweli angefungwa?
Ni vizuri kuangalia historia ya watu kwa uangalifu ili kuyaweka na kuyatafsiri matendo yao katika muktadha sahihi. Nina marafiki wako huko na wanaeleza mkanganyiko uliopo katika vurugu zinazoendelea na wanasema kuwa ni hisia za ubaguzi pamoja na migongano ya kitabaka; na umasikini sugu kwa hawa weusi. Ukimsikiliza Mh. Malema naye pia anagusia mkanganyiko huu na kumlaumu jaji aliyegoma kujitoa kwenye shauri hili; na Zuma kwa kuwa kichwa ngumu huku akijua hali na fikra za watu zilivyo.
Hata kwenu huko sidhani kama ni kuabudu mtu (Odinga?). Ukichimbua kidogo utakuta kuna sababu zingine za kijamii na hata kiuchumi na kihistoria. Ukabila!