Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

-6015065908541764932_121.jpg
 
Siyo kweli japo hoja yako ina mashiko kuhusu uamilifu wa sheria kama msumeno unaopaswa kukereza kote kote bila kujali hadhi ya anayekerezwa. Katika uhalisia wake hata hivyo mambo hayako hivyo. Na ishu ya Afrika Kusini kidogo ni tata kulingana na historia yao ngumu waliyopitia hasa hawa weusi. Ati; Angekuwa ni De Klerk au P.W. Botha ndiyo kafanya kosa alilofanya Zuma (ana sababu nzuri tu); ni kweli angefungwa?

Ni vizuri kuangalia historia ya watu kwa uangalifu ili kuyaweka na kuyatafsiri matendo yao katika muktadha sahihi. Nina marafiki wako huko na wanaeleza mkanganyiko uliopo katika vurugu zinazoendelea na wanasema kuwa ni hisia za ubaguzi pamoja na migongano ya kitabaka; na umasikini sugu kwa hawa weusi. Ukimsikiliza Mh. Malema naye pia anagusia mkanganyiko huu na kumlaumu jaji aliyegoma kujitoa kwenye shauri hili; na Zuma kwa kuwa kichwa ngumu huku akijua hali na fikra za watu zilivyo.

Hata kwenu huko sidhani kama ni kuabudu mtu (Odinga?). Ukichimbua kidogo utakuta kuna sababu zingine za kijamii na hata kiuchumi na kihistoria. Ukabila!

Yote hayo nayafahamu, historia na mengine mengi tu, ila suala nzima hapa ni kuhusu kuheshimu utawala wa sheria, kama sote tumekubaliana hiyo sheria na katiba ndio itatupa muongozo, haipaswi tuwe na baadhi yetu ambao tukihisi mambo hayaendi tutakavyo basi tuichome nchi. Unamvamia muuza mkaa na kupora magunia yake yote kisa umekerwa kwamba mungu mtu wako amedhulumiwa.

Historia hizo mbovu zipo, huyo hapo Zuma alikua rais wa nchi mwenye mamlaka yote, alipaswa kuongoza kwa mbele kwenye kurekebisha, ila yeye aliendekeza ufisadi na ukabila, sasa ndio haya matunda yake. Hata huyu rais wangu Uhuru, napenda sana utenda kazi wake na uchumi wetu unakua kwa kasi, nchi inaendelea vizuri sana kiuchumi, ila amegoma kurekebisha ukabila, teuzi zake zimekaa hovyoo, kesho akiingia uraiani ujaribu kumkamata aisei huo upumbavu wa Afrika Kusini utakua cha mtoto maana kwetu hapa huwa tunakinukisha kinanuka.
Sasa hivi huyo Zuma anachekelea maana chaos zote hizo anazitumia kujilinda.
 
Back
Top Bottom