Kwa sisi ambao tumesoma elimu ya dini ya uislam kuna upande fulani unasema kuzika ni kitendo cha kutoshelezana( maana yake mtaani kwako kafa mtu wakatokea wawili au watatu wakamsitiri kwa kumzika inatosha)ila kama kijijini kwako akafa mtu mkamuacha kama kafa mbwa


kijiji kizima mnapata dhambi na hata huyo mbwa mwenyewe kwanza japo ni mnyama ile harufu yake tu itawasumbua nyie majirani mtatafuta sehemu muusitiri mzigo sasa sikwambii mzoga wa binadamu iweje mji mzima washindwe hata watu kadhaa wasindwe kumhifadhi binadamu mwenzao.Hayo masuala mengine ya pesa yamekuja tu miaka ya karibuni,kuna mtu maalum au kikundi maalum ndiyo kazi yao hiyo na wanalipwa.ila kiubindamu kila familia inatakiwa ijue namna ya kuzika ili wahifadhiane aibu ndugu.Asikuambie kuna watu wengine wakifa wanatisha japo ashakuwa mzoga ila ikiwa kwenye familia kukiwa na wajuzi wa jambo hilo wanamsitiri ndugu yao kwa kuzika,kuliko kwenda kutafuta mtu wa nje aje amzike ni wajibu kujifunza sema tu huu usasa ndiyo umetuharibu.