Kwa taarifa yako tu, wapagani si watu wasioamini mungu yupo. Wazungu waliwaita mababu zetu wapagani kwa kuwa hawakuwa wanaabudu mungu sawa na waliokuwa wanamuabudu wao.
Jifunze mambo kabla ya kuandika.
Kukataa kuamini kwamba mungu yupo hakuwezi kuwa kuamini kama vile kunyoa kipara hakuwezi kuwa ni mtindo wa kusuka. Utasemaje naamini kwa sababu nimekataa kuamini mungu yupo? Sitaki kuamini, nataka kujua.
Mambo yaliyo wazi kabisa ni yapi?
Huyo mungu atakayenionyesha live nikimuuliza kwa nini kaacha watu kibao wamekufa bila kumjua kwa yeye kujificha na kutojionyesha live atajitetea vipi?
Ni wazi upo kwenye wakati mgumu sana, kiimani na unataka kujua Mungu wa kweli kwanini katelekeza wanadamu, swali ambalo kimsingi ukijiuliza kwa misingi ya Imani kuu kama ukristo, uislam, na hata uebrania unaweza kupata majibu yatakayokuwa na utata ndani yake, na ndiyo maana umeamua kujikita kwenye sayansi ya kidunia ili kutafuta njia itakayokupa tulizo rohoni, ingawa ukweli unapenda kujua huyo Mungu ni kitu gani na yupo au lah,
Kiufupi naweza kukuhadithia story ya Musa na kitabu chake cha (MWANZO) kiufupi kitabu kile kimeandikwa kwa fasihi sana, na hilo limekuwa ni tatizo kwa watu mpaka leo kwani wamekuwa hawaelewi vizuri kitabu kile.... Kifupi ninachoomba ujue ndugu yangu ni kuwa Mungu ninayetaka umjue, yeye aliumba Binadamu Wanne hapo mwanzo, katika MWANZO watu hao wametajwa kwenye 1.26 na kuthibitishwa kwenye 5.1,2 Watu hao waliumbwa mbinguni, sio hapa Duniani, na hao ndio waliokuwa na uwezo mkubwa zaidi kwa nguvu na Kutawala, Mungu huyo aliwapa watu hawa kazi ya kwenda kutawala Kila kitu Duniani, ila bahati mbaya zogo lilianzia hukohuko mbinguni ambapo Mwanamke mmoja kati ya wale watu wanne yaani Kwa kimisri, Atum, Amun, Ra, na Lilith huyu lilith alimsaliti mwenzie Atum na akaanza kutembea na moja ya malaika mbinguni, ambapo kitu kilichokuja kuzaliwa hapo walikuwa ni majini, hivyo Mungu uzao huo akawa hautambui akamfukuza Lilith mbunguni na huyo mmewe wa kimalaika na hao watoto wao yaani (Majini) Duniani na kuwatupa huko baharini..
Mungu akabaki na wale wanadamu watatu kule mbunguni akamtuma mmoja wapo yaani Atum aje aumalizie ulimwengu kwa maana ilikuwapo dunia, giza na Maji na tayari hao kina lilith na majini walikuwa wameshatupwa Duniani, so wao walikuwapo huko majini,
Atum alipokuja Duniani alifanya kazi aliyotumwa na Mungu wake, ambapo aliumba kila kitu unachokiona sasa kwa kufuata neno/agizo la Mungu, Atum ni mmoja ya miungu anayeabudiwa saana na mababu weusi wa Misri.... Kisha huyohuyo atum ndiye akamuumba mwanadamu mwingine kwa Udongo kwenye mwanzo 2:7 ingawa mle anatajwa kama ni Mungu,
Baada ya ulimwengu na wanadamu kukamilika Dunia ilikuwa ya kuvutia na kupendeza miongoni mwa malaika Mbinguni, baadae ndipo Mungu mbinguni akamshusha huyo aitwaye Amun, kwa mababu weusi wa kale wa misri, au Amen kwa waroma na ndiye wamchaye mpaka sasa wakimuita AMEN au Zeus kwa wagiriki, Huyo Amen na mwenzie RA walishuka duniani hapo ndipo kazi ya MUNGU mkuu wa mbinguni ikawa imekwisha..... maana alikywa ameshaumba Dunia na watawala hivyo dunia ilikuwa inajitegemea, na hao Amun Atum na Ra walipewa nguvu mpaka za kuwaamuru malaika..
Ukiachilia mbali nguvu Tofauti walizokuwa wamepewa kama vile Amun nguvu za radi, maji na nk, Sasa huku kwenye Mwanzo hakuna hata sehemu Moja iliyomtaja Mungu wa Mbinguni, yaani YHWH.. imekuwa ikizungumzia sanasana Amun, ambapo utajiuliza kwanini Mungu kwenye Mwanzo alikuwa hatabiri na kigeugeu! Mara anasema nakula kiapo sitawaangamiza mbele unakuta anaangamiza tena,! So kitu ambacho napenda ujue ni kuwa Mungu aliyezungumziwa kwenye kitabu cha kutoka tu, Mungu anayezungumziwa mle ni Amun, ambaye kiuhalisia si Mungu ni mwanadamu aliyepewa mamlaka ya kutawala, Hivyo Mungu YHWH yupo zake mbinguni, na kazi yake alishamaliza Duniani kwa kutuumba na kutupa viongozi, ila balaa linaanzia hapo ambapo utakuja kugundua kuwa katik uzao wa huyo Amun, kila mwanafamilia anajiita Mungu, Mungu wanakuwa wengi mpaka mtu anaona asiamini tu kama kuna Mungu, Ila kiuhalisia Mungu YHWH yupo na siku ambapo yeye atakuja kuigusa hii dunia hapo ndipo utakuwa mwisho wa kila kitu, huyo ndiyo mmoja apaswaye kuabidiwa kwa haki ila, kwa sasa Dunia bado ipo kwa aliowapa Dunia, maana ni alishaikabidhi kwenye mikono ya kina Amun, Atum, Lilith na Ra...
Magharika kama yale ya moto kutoka juu kama kwenye Sodoma na Ghomola ile ilikuwa ni kazi ya amun maana yeye alipewa nguvu za Moto, radi na Mvua, na sifa zake hizo zinajulikana kabla hata ya Musa hajaanza kuandika Vitabu kutoka kwa mababu Weusi wa kale wa misri..