Vitu sita ambavyo si viumbe vya Mungu

Vitu sita ambavyo si viumbe vya Mungu

Kabla ya kusema hivyo, unaweza kuthibitisha mungu na shetani wapo?
ukisema hawachunguziki ina maana pia Hawa thibitiki!! Kama hawathibitiki basi pia uwepo wao hauthibitiki! If that is so basi wanaweza kuwepo Au kutokuwepo! Ila tu watu wameamua ku base upannde wa! Yupo! Sababu ya vitisho. Vya upannde wa pili.
 
ukisema hawachunguziki ina maana pia Hawa thibitiki!! Kama hawathibitiki basi pia uwepo wao hauthibitiki! If that is so basi wanaweza kuwepo Au kutokuwepo! Ila tu watu wameamua ku base upannde wa! Yupo! Sababu ya vitisho. Vya upannde wa pili.
Hata baada ya kuonyeshwa kwamba kuwepo kwa huyu mungu kunaleta irreconcilable contradictions.

Watu wanaamini mungu yupo kwa sababu kubwa hizi.

1. Ni shortcut ya morality. Mtu anayeamini mungu yupo anafikiri kwamba ndiyo njia ya kuwa moral Zaidi na kutoamini mungu kuwapo huwezi kuwa moral. Kufikiri hivi hutokana na uvivu wa kufikiri.

2.Uvivu wa kufikiri tu unaomfanya mtu aamini katika dini aliyoikuta kutoka kwa wazazi. After all, kuanza ku question mambo haya kunaweza kukutenganisha na familia.

3. Speaking of kutengwa na familia, kuna cognitive dissonance inayokuwapo kwa watu ambao washa invest miaka mingi katika kuamini mungu yupo. Hawa wanakuwa kama mtu aliyepotea njia, anaona ushahidi wote kwamba kapotea njia, lakini hataki kurudi nyuma kwa sababu kashatumia muda mwingi sana kwenye mchepuko alikopotea njia, anakuwa anaishi kwa tumaini tu kwamba somehow njia yake ni sahihi despite all the evidence to the contrary. Ndiyo maana utasikia watu waliosoma na kujua mungu hayupo hawaishi ku rationalize Imani ya mungu, kwa kusema kwa mfano, hata kama mungu hayupo, Imani ya mungu inasaidia kuleta harmony duniani na watu wote wakikataa kuamini uwepo wa mungu kutakuwa na fujo.

4. Ujinga na umasikini tu. Mtu hajapata kipande cha muhogo kutia tumboni unafikiri anaweza kuwa na muda wa kuchambua "the problem of evil"? Anataka kuambiwa piga magoti uombe mungu atakujaalia. Ndiyo maana Northern Europe watu walikoelimika Zaidi na kuweza kutatua matatizo ya msingi makanisa yako empty na huku kwetu Africa ambako bado tuna ujinga na umasikini watu wanajazana.
 
uzushi wa jamaa ni huu kwa ufupi
mungu(sijui ni yupi) hakuumba vitu vifuatavyo
1mungu(hakujiumba)
2kifo
3maradhi
4njaa/vita
5giza

jamaa anaelim yake sijui katoa wapi anajua yy.. nmemwambia hapo juu akjipange, maana amekariri, hajui kuwa kabla ya dunia hii haijaumbwa Mungu alikwisha umba galaxies 99, na ya kwetu ni ya mia..
 
Hujaelewa swali.

Swali ni kwamba, kabla ya mtu kuumbwa, kwa mujibu wa mapokeo yenu, mungu aliumba ulimwengu.

Alivyokuwa anaumba ulimwengu huu, alikuwa na uwezo wa kuuumba ulimwengu uwe vyovyote anavyotaka.

Akachagua kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana.

Wakati alikuwa anaweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Kwa nini?

Ukianza kusema habari za binadamu kaumbwa kwa mfano wa mungu unaonyesha hujaelewa swali.

Swali linauliza kabla mtu hajaumbwa.

Mungu alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Kwa nini hakuumba ulimwengu huo?

Unaposema mabaya ni uamuzi wa mwanadamu, mabaya hayo yamewezekanaje bila mungu kuyaruhusu?

Na kwa nini karuhusu yawepo?

Alishindwa kuumba ulimwengu ambao maamuzi ya binadamu yatakuwa kati ya mazuri na mazuri zaidi tu?

Kama alishindwa, je ni kweli anaweza yote?

Ama aliweza kuumba ulimwengu usio na mabaya, ila hakutaka tu?

Kama aliweza ila hakutaka tu, kwa nini katubania kwa makusudi? Ni kweli ana upendo wote?

Huyu mungu yupo kweli au ni hadithi tu?
Mkuu labda wewe hujaelewa swali ulilouliza mwenyewe. Nilichojibu ndicho hicho hasa ulichouliza. Nimesema Mungu hakuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana La hasha! Aliumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani hili ndiyo jibu. Mabaya unayodhani ulikuwa ni mpango wa Mungu ni mpango wa wanadamu wenyewe ambao wanauamzi kuacha mabaya au kuendelea nao. Tatizo unachofikiri wewe ulitaka Mungu akuwekee namna ya kufikiria mema tu..hapo nadhani ndo tunapishana me na wewe. Mungu alimtofautisha binadamu na kila kitu. Binadamu alipewa Akili ya kujua mema na mabaya ili aamue mambo yake mwenyewe. Alipewa nguvu,maarifa na utashi..!! Ndo maana nilikuambia hakuna shetani wala Mungu anayewazuia binadamu kuishi kwa wema 100%. Vitu vyote vibaya vinavyokufanya mpaka uone tatizo uumbaji wa Mungu vyote ni matokeo ya wanadamu wenyewe.

Hivi kwa mfano unajua huyu ni mke wa fulani halafu unamtongoza hapo ubaya ni wa Mungu,shetani au wewe mwenyewe!!? Ulitaka Mungu aje akuongoze kukuambia usifanye hivyo wakati unao uwezo wa kujizuia mwengewe!!? Mungu yupo na uthibitisho unao mwenyewe hapo. Pengine angekufanya kipofu usingeweza kutambua uumbaji wake...!!
 
Mkuu labda wewe hujaelewa swali ulilouliza mwenyewe. Nilichojibu ndicho hicho hasa ulichouliza. Nimesema Mungu hakuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana La hasha!

OK, so mungu hakuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana. Mpaka hapo tayari una tatizo kubwa sana la kutatua.

Maana kama mungu hakuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana, na ulimwengu huu mabaya yanawezekana, ina maana mungu hakuumba ulimwengu huu?

Aliumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani hili ndiyo jibu.

Sasa imekuwaje mabaya yanawezekana? Ina maana kuna kitu kina uwezo kumpita mungu kilichofanya ulimwengu uwezekane kuwa na mabaya wakati mungu hakuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana?

Mabaya unayodhani ulikuwa ni mpango wa Mungu ni mpango wa wanadamu wenyewe ambao wanauamzi kuacha mabaya au kuendelea nao.

Mwanadamu amewezaje kufanya mabaya katika ulimwengu ambao mungu hakuumba uwezekano wa mabaya kufanyika?

Lazima uelewe kwamba, ili binadamu afanye baya, inabidi uwezekano wa baya kufanyika uwepo.

Binadamu hawezi kufanya baya katika ulimwengu ambao uwezekano wa baya kufanyika haupo.

Kama vile ambavyo binadamu hawezi kurudi nyuma katika muda katika ulimwengu ambao uwezo wa binadamu kurudi nyuma katika muda haupo.

Sasa binadamu kawezaje kufanya mabaya katika ulimwengu ambao mungu hakuumba uwezekano wa mabaya kufanyika?

Tatizo unachofikiri wewe ulitaka Mungu akuwekee namna ya kufikiria mema tu..hapo nadhani ndo tunapishana me na wewe.

Kama mungu hakuumba binadamu kufikiri mema tu, kamuumba binadamu kuweza kufikiri na kufanya mabaya, utasemaje mungu hakuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana? Unajichanganya.

Mungu alimtofautisha binadamu na kila kitu. Binadamu alipewa Akili ya kujua mema na mabaya ili aamue mambo yake mwenyewe.

Unapoongelea "akili ya kujua mema na mabaya" tayari ushaongelea ulimwengu ambao mabaya yapo. Mimi ninachouliza ni tofauti. Nauliza kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana in the first place? Katika ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, hakuna suala la kujua mema na mabaya kwa sababu mabaya hayapo. Kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana?

Alishindwa kuumba ulimwengu ambao una mazuri tu hauna mabaya na akampa mwanadamu uhuru wa kuchagua mazuri yapi afanye?

Alipewa nguvu,maarifa na utashi..!!

Mungu alishindwa kumpa mwanadamu nguvu maarifa na utashi katika ulimwengu ambao una mazuri tu na hauna mabaya?

Na kama kweli mungu anapenda mwanadamu awe na maarifa, kwa nini hakumpa mwanadamu maarifa awe kama yeye mungu?

Ndo maana nilikuambia hakuna shetani wala Mungu anayewazuia binadamu kuishi kwa wema 100%.

Mungu kwa kuumba binadamu katika ulimwengu ambao mabaya yanawezekana tu na kutompa mwanadamu uwezo wa kuwa mungu tayari kashamzuia mwanadamu kuishi kwa wema 100 per cent.

Vitu vyote vibaya vinavyokufanya mpaka uone tatizo uumbaji wa Mungu vyote ni matokeo ya wanadamu wenyewe.

Utasemaje kwamba vitu vibaya ni matokeo ya mwanadamu wakati mungu kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kufanyika kabla mwanadamu hajaumbwa? Uwezekano wa ubaya kufanyika umekuwapo tangu mwanadamu hajaumbwa, mwanadamu hajaumbwa na uwezo kama wa mungu wa kuepuka mabaya, mwanadamu akifanya mabaya kwa sababu ulimwengu unaruhusu mabaya kufanyika kabla yeye hajaumbwa na kwa sababu yeye kaumbwa na mapungufu yanayomfanya aweze kufanya mabaya, utasemaje mabaya ni matokeo ya wanadamu wenyewe?

Ni kama umpe mtoto mchanga pikipiki halafu umtake aiendeshe resi barabarani wakati unajua kwamba hana uwezo huo, akianguka na kuumia utasema ni matokeo yake yeye mwenyewe au mipango yako?

Hivi kwa mfano unajua huyu ni mke wa fulani halafu unamtongoza hapo ubaya ni wa Mungu,shetani au wewe mwenyewe!!?

Kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao ianwezekana kwa mtu kuwa na tamaa ya kumtongoza mke wa fulani wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauna tamaa ya mtu kumtongoza mke wa Fulani?

Hujajibu hili swali.

Ulitaka Mungu aje akuongoze kukuambia usifanye hivyo wakati unao uwezo wa kujizuia mwengewe!!?

Wapi unalipata hili?

Kwa nini mungu kaumba uwezekano wa mtu kuwa na tamaa ya kumtongoza mke wa Fulani wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauna tamaa ya mtu kumtongoza mke wa Fulani?

Unaweza kujibu hili swali?

Mungu yupo na uthibitisho unao mwenyewe hapo.

Uthibitisho gani? Unaweza kuutaja? Usilazimishe mambo tu.

Pengine angekufanya kipofu usingeweza kutambua uumbaji wake...!!

Hujathibitisha mungu yupo. Una otea otea tu kwa "pengine".

Unaweza kuthibitisha mungu yupo?
 
Samahani mkuu. Mm ni miongoni kati ya watu wasioamini uwepo wa mungu. Nilianza kutoa imani yangu baada ya kujiuliza uwepo wa shetani. Naomba kushare na wewe hilo swali huenda tukapata jibu sahihi. Swali lenyewe ni hili hapa "je, uwepo wa shetani ni mpango wa mungu au ni kufeli kwa mungu? " naomba tujiulize kwa pamoja. Kama ukipata jibu usisite kunielekeza
Mkuuu huna dini nn mkuu..??
 
The effective lie is the one nearly to truth, (hii niliisoma kwa Masonic scipts)
 
Kiranga acha kupotosha umma elimu yako ndogo sana ya philosophy inakusumbuaa...
Inawezekana elimu yangu ya philosophy ndogo.

Lakini inaonekana yako ndogo zaidi, kwa sababu ni Professor jina, hufundishi wapi elimu yangu ya philosophy ni ndogo na vipi niiongeze.
 
Ule mti wa mema na mabaya unadhani MUNGU aliutoa wapi kama maradhi na kifo havikutoka kwake?? Lewiathan ni nyoka anaeishi baharini na yuko Kwenye namna ya roho,,By the way big up kwa kuainisha mambo mazuri.
 
VITU SITA AMBAVYO SI VIUMBE VYA MUNGU.

View attachment 331270

Tarehe Mar 2016 niliandika makala juu mahusiano kati Kiza, Mungu, Kifo, Vita, Njaa, na Maradhi. Makala ile ilizua mjadala mkubwa facebook na whatsapp nilipoiweka, na moja jambo kubwa lilotuvuruga ni uwezo na mamlaka ya Mungu katika uumbaji, na hasahasa ile nadharia ya kuwa MUNGU ni muumbaji wa viumbe vyote ilitumiwa sana na watu katika kuikosoa makala yangu.

Awali ya yote nakubali bila kigegezi chochote kuwa Mungu ni muumbaji wa viumbe vyote na ya kwamba ni Mola wa viumbe hivyo. Nakubali kuwa ulimwengu haukuzuka tu wenyewe katika tukio la lisilo ratibiwa. Bali yupo injinia wa Ulimwengu huu ambaye si mwingine bali ni MUNGU.

Misaahafu ya dini za Ibrahim, yaan uislamu, uyaudi na ukristo yote kwa pamoja bila kukhitililafiana inasema ulimwengu na vilivyomo ndani yake havikuzuka kwa bahati mbaya bali vimeumbwa na Mungu.

Kuna viumbe hai kama wanyama na mimea, lakini pia kuna viumbe ambavyo havina uhai kama mawe na mchanga. Vyote hivi Muumbaji wake ni Mungu.

"Mwenyezi Mungu ameumba mbingu na ardhi kwa Haki. Kwa hakika katika hayo ipo Ishara kwa Waumini. " Quran 29:44

"...Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Na Yeye ni Mmoja Mwenye kushinda!..." Quran 13:16

"Mbingu ni mali yako, nchi nayo ni mali yako, Ulimwengu na vyote viujazavyo Ndiwe uliyeupiga msingi wake. Kaskazini na kusini ndiwe uliyeziumba....." Zaburi 89:11-12

Hiyo quran 13:16 inatutanabaisha kuwa Mungu ameumba kila kitu, lakini tujiulize, kitu kilichoumbwa na Mungu kinaitwaje? Kwa vyovyote vile kinaitwa kiumbe. Kama ndivyo tunaweza kuwa sahihi zaidi kama tukisema kuwa Mungu ameumba viumbe vyote badala ya kusema kuwa Mungu ameumba kila kitu.

Twasema kuwa viumbe vyote vimeumbwa na Mungu, je vile ambavyo si viumbe tuna vizungumziaje? Naomba mjue Mungu ameumba viumbe vyote, lakini haimaanishi kuwa ameumba kila kitu. Kuna baadhi ya vitu ambavyo Mungu hakuviumba aidha hakutaka kuviumba au ameshindwa kuviumba.

VITU VIKUU SITA AMBAVYO MUNGU HAKUVIUMBA.

1. MUNGU
Ukisoma misahafu yote mikuu miwili quran na biblia hakuna ushahidi hata mmoja unaonesha kuwa Mungu kaumba Mungu(namaanisha Mungu kujiumba).

Kubwa zaidi katika misahafu hiyo ambayo imeandikwa kwa matakwa yake MUNGU, inaonesha ukuu wa Mungu, uwezo wake, mamlaka yake, utukufu wake, usafi wake na kila aina ya sifa nzuri na tukufu, lakini hatuoni chanzo chake kikiandikwa humo na hatuoni mwisho wake ukiandikwa humo, zaidi ya vitabu hivyo kusema ufalme wa MUNGU na Nguvu zake hazina mwanzo wala mwisho.

"Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi" Ufunuo 1:8

"Na Mola wako Mlezi anayajua yaliyo ficha vifua vyao, na wanayo yatangaza. Naye ni Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye. Sifa zote njema ni zake Yeye, mwanzo na mwisho...." Quran 28:69-70

Kwa aya hizi, na mafundisho mengine ya kinabii kama haya, yanathibitisha bila shaka kuwa ni kweli kuna mambo au vitu ambavyo Mungu hakuviumba na kwasababu hiyo vitu hivyo haviwezi kuitwa viumbe na ingawa viko. Kitu cha kwanza MUNGU, kipo na hakija umbwa.

Wanaosema kuwa MUNGU ameumba kila kitu waje hapa watuambie "MUNGU" kaumbwa na nani? Wakishindwa kututajia basi waishie kusema Mungu kaumba viumbe vyote lakini si vitu vyote.

2. KIZA
Ukisoma hiyo quran 28:69-70 na ukisoma vizuri ufunuo 1:8 utagundua mambo yote na habari zote kabla ya uwepo wa MUNGU hayajulikani na huenda anayajua Mungu mwenyewe, lakini kwetu sisi tunaona mambo hayo kwetu ni KIZA.

Kwa hivyo tunaweza kusema kabla ya Mungu hajaumba chochote alikuwako yeye na Kiza, Kiza ni mwanamke na Mungu ni mwanaume. Kwakuwa kwa kipindi hicho walikuwa wenyewe, na wanajuana wenyewe, jambo jepesi twaweza kusema hivi vitu ni ndugu. Ipo siku inshallah nitakuja kufafanua kwanini nasema Kiza mwanamke na Mungu mwanaume.

"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. 3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. 4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza."
Mwanzo 1:1-4

Katika andika hilo la juu tunajifunza yafuatayo.

A. Mbingu na nchi zimeumbwa na Mungu. Maji, ardhi na vitu vya kufananayo ni sehemu ya mbingu ya nchi.

B. Mungu aliumba NURU lakini hakuumba KIZA, tunaambiwa tu Kiza kilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji lakini hatuambiwi Mungu aliumba Kiza.
Hiyo mwanzo 1:3 "Mungu akasema, iwe Nuru; ikawa Nuru"

Alijuaje kuwa Nuru imekuwa kama kabla ya Nuru hiyo kulikuwa hakuna Kiza? Je, mbona hatuoni maandiko yakionesha Mungu akisema iwe Kiza kisha kikawa Kiza?

C. Ukisoma mwanzo 1:2 tunaona Mungu akiumba mbingu na nchi kisha Kiza alikaa juu ya uso wa vilindi vya maji, kwasababu hiyo, nikisema kuwa Kiza alikuwako kabla ya mbingu na nchi nitakosea? Kama alikuwako kabla ya mbigu na nchi, ama kabla ya ulimwengu, nikisema kuwa Kiza na Mungu waliishi wenyewe kabla ya ulimwengu pia nitakosea?

D. Baada ya Mungu kuumba Nuru, hapo ndipo alipofanikiwa, kumfungia KIZA, na athari za Kiza akaziita USIKU na athari za NURU akaziita MCHANA. Kwahivyo Mungu hakumuumba KIZA, ila Mungu kaumba Nuru, Mchana, na Usiku.

Kwahivyo kama tuko pamoja, utakubaliana na mimi kuwa KIZA ni moja ya kitu ambacho Mungu hakukiumba. KIZA si kiumbe, KIZA kimezuka tu kama alivyozuka Mungu mwenyewe. Tafauti kubwa kati ya MUNGU na KIZA ni kuwa Mungu kaumba na ni Mola wa viumbe vyote, lakini Kiza hakuumba kitu chochote kwa hivyo si MUUMBAJI.

Astronomy inatuambia kuwa ulimwemgu umeundwa na vitu vikuu vitatu, normal matter, dark matter na dark energy. Normal matter ndio hujumuisha zile atoms zilizo tumika kuumba Nyota,sayari, na vitu vingine.

Normal matter ni asilimia 5 tu ya ulimwengu wote, 25% ni dark energy na 70% dark matter. Hiyo dark energy na dark matter athari zake zinaonekana katika zenyewe hazionekane. Hii huenda ndio KIZA ambacho kimetajwa katika mwanzo 1:1

Astronomy pia yatuambia ulimwengu unatanuka kwa kasi, na ya kwamba unazidi kuongezeka kutokana ile motion iliyosababishwa na BING BANG, kutanuka kwake ina maanisha unazidi kumeza au ama kuingia katika sehemu mbele zaidi kutokea kule ulipo anzia(kipind cha dark age) Swali kule unapoelekea kuna nini kama si Kiza??

Astronomy pia yatuambia hakuna empty space, kama inavyo onekana, katika space waweza kuona ama kudhani hakuna maada yoyote, lakini kimsingi asilimia kubwa ya space ina dark energy na dark matter. Vitu hivi vinaashiria uwepo KIZA mbali na ulimwengu tunao ujua.

3. KIFO
Kwanza naomba tukumbuke wakati Mungu anafikiria kuumba ulimwengu tayari kulikuwako na KIZA. Ili Mungu awe kuumba ulimwengu ilikuwa lazima kwanza amuondoshe au amuue KIZA. Ili Kiza kiweze kufa shuruti pawe na "KIFO" Hata hivyo, kutokana na nguvu za Kiza, basi kikawa hakijakufa bali kilifungiwa.(Rejea mwanzo 1:3 Mungu akatenga giza na nuru)

Pili naomba mjue kuwa kiumbe hai cha kwanza kuumbwa na Mungu ni "NENO" kisha wakafuatia malaika wakubwa wanne(four Arc Angels) ambao ni Mikaeli, Raphaeli, Rucifer na Gabrieli. Hoja inakuja, Mungu alitumia kipimo gani kujua kwamba amefanikiwa kuumba kiumbe hai? Kwa vyovyote vile ili ajue kuwa amefanikiwa kuumba kiumbe hai ni lazima alinganishe uhai uliopo ndani ya kiumbe hai na mauti(KIFO). Kwa hivyo kilianza KIFO kabla ya UHAI, na bahati nzuri maandiko yanakubali kuwa Mungu kaumba uhai, lakini hayaoneshi kuwa Mungu kaumba KIFO.

Wachungaji wetu katika makanisa wanakataa katakata kuwa Mungu kaumba KIFO, wao wanasema KIFO kilisababishwa na shetani, bi maana shetani ndio kaumba KIFO. Huku ni kutokujua, lakini hakuna aliyeumba KIFO, KIFO sio kiumbe na alizuka tu kama alivyo zuka Mungu.

Kama nilivyosema ule muda Mungu anafikiria kuumba uhai, tayari kifo kilikuwako, na kwasababu hiyo, pia haijulikani kati ya Mungu na Kifo na mkubwa(kiumri).

Mungu aliumba uhai, na kwa kupitia huo uhai akaumba mwanadamu, lengo lake lilikuwa mwanadamu aishi milele, lakini kifo kikawa kikwazo katika lengo hili.

Sivyo tu, kwakuwa siku zote KIZA anataka atoke kifungoni, hivyo kila siku anapambana na Mungu kwa lengo la kutaka kumuua, na wakati huohuo Mungu naye anataka kumuua KIZA, mshindi wa pambano hili lazima amtumie "KIFO" na hapa ndipo tunapoona nafasi ya KIFO katika mahusiano ya NURU na KIZA.

Lakini Mungu anasema atakuja kumshinda KIZA na KIFO, na pindi atakapo shinda hakuna roho au mwili utakao kufa.

"na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. " Ufunuo 1:18

4. VITA na NJAA
KIZA baada ya kugundua Mungu ameumba malaika wakubwa wanne, KIZA alichukia na hapo yakazuka mapambano kati ya MUNGU na KIZA. Kwa mapambano hayo ndipo ilipozuka "VITA" mungu alichofanikiwa ni kumfungia KIZA, na funguo zake akakabidhiwa Rucifer. Mark of Darkness ndio Funguo na sehemu alofungiwa KIZA, chapa hii baadae iliitwa mark of cain.

Mnyama wa kwanza kuumbwa na Mungu kabla hata ya wanadamu ni Levithans, hawa ndio ile mijusi mikubwa na Magodizilla. hawa walikuwa na "NJAA" sana kiasi walane wenyewe kwa wenyewe, Hapa Mungu kwa kutumia jeshi lake la malaika waliwaondoa dunia na kuwafungua Purgatory. Hapa pia VITA alihitajika kufanikisha hili.

Tembo na vufaru wanapungua kwa kuuliwa na binadamu, hivi Magodizilla na Levithans waliuliwa na nani? Ikiwa wao walikuwako miaka mingi kabla ya wanadamu? Jibu jepesi ni upanga wa Malaika Mikael na jeshi lakd.

Wakati hayo yakitokea, Darkness akaigeuza ile mark kuwa laana, na laana ile ikasababisha hali ya uasi kwa mtunza funguo. Wakati Mungu anamuumba mwanadamu, na malaika kuambiwa wamsujudie, Rucifer akiwa kesha athiriwa na laana ya funguo akagoma kumsujidia adamu.

Kwa mara nyingine "VITA" ilihitajika katika kumdhibiti Rucifer na kundi lake.

6 MARADHI
mungu hakuumba maradhi, na wala si lengo mungu mwanadamu aumwe na kuteseka kwa maradhi. Ila pale mwanadamu alipoumbwa na afya bora kabisa, na maradhi yakazuka hapo hapo. Baada ya Mungu kuja kumshinda KIFO, pia atakuja kuyashinda MARADHI, na hayo yakitokea katika maisha Paradiso hakutakuwa na KIFO wala MARADHI.

MWISHO.
makala hii haina tafauti na ya juzi, ila leo baadhi ya nukta nimemua kuziongelea kwa undani zaidi ili iweze kujibu maswali na hoja zilizo jitokeza katika makala ya msingi. Hata hivyo najua siwezi kumaliza kila kitu hapa, ila mengine tutajifunza katika mjadala!

Njano5
0622845394


Ukianza kufikiria kuhusu masuala haya unaweza ukajikuta ukitembea mitaani bila nguo kama yule aliyepiga kelele za ereuka, eureka, eureka sijui alikuwa nani -Archimedes ?/ au mwingine? nadhani ni yeye - Archimedes principle.
 
uzushi wa jamaa ni huu kwa ufupi
mungu(sijui ni yupi) hakuumba vitu vifuatavyo
1mungu(hakujiumba)
2kifo
3maradhi
4njaa/vita
5giza

jamaa anaelim yake sijui katoa wapi anajua yy.. nmemwambia hapo juu akjipange, maana amekariri, hajui kuwa kabla ya dunia hii haijaumbwa Mungu alikwisha umba galaxies 99, na ya kwetu ni ya mia..
tupe andiko la hizo galaxies!
 
Mungu na Shetani wana Undugu au Ni Maadui wa Asili? wote wana uwezo si ndio? Maana Hadith inasema Theluthi mbili ya Malaika hawakuasi na Theluthi moja ya Malaika iliasi ikawa Vita Mungu akashinda kutokana na wingi wa Jeshi lake la Malaika theluthi Mbili so ni Sawa na Russia na America Ni Ndugu wote Wazungu na wote wana Nguvu Sababu ya Uwezo wao wamebakia kutishiana tu bila Action..... Shetani hata akufanye nini wewe Mungu Atatizama tu Maana Akianzisha Vita ni Balaa zitapigwa Kinoma na Kwa Sasa Shetani wako ana wafuasi wengi zaidi ndio maana Dunia haiishi Hakuna wa Kuanzishisha Vita ila Mikwara itaendelea na Majigambo... Jamani Raha si Raha.....!

Usinipeleke unavyotaka,unaposema "hadithi inasema" hadithi ipi? umenukuu mambo ambayo hayaeleweki.Na ukisema uwezo wa Mungu upo sawa na wa Shetani basi kwanini tuseme Mungu anauwezo wote???? Weka vizuri hadithi zako kwanza.
 
Thibitisha.

Huwezi kukuthibitishiwa mfumo ambacho umekuzidi intelijensia.Kibinaadamu tu kuna watu ambao mambo wanayoyafanya binadamu wengine hawawezi kufikiria.Nimeshawahi kukupigia mfano wa vitu ambavyo ni Computerised,watu wa dunia ya tatu kipindi cha miaka ya 60 vitu hivyo vilikuwa ni kama miujiza,kwa wakati huo bwana Kiranga ukiombwa uthibitisho wa utenda kazi wa vitu hivi usingeweza kuelezea.

1).Kwahio uwezo wa Mungu kiintelijensia upo juu sana.Binadamu hana uwezo wa kumthibitishia binadamu mwenzie kwa fact za kisayansi au as tangible objects,Kwasababu Mungu mwenyewe ameamua kujificha na kwa uwezo wake hakuna wa kuweza kumfichua.
2).Ni kwamba kule kutoonekana kwake lengo na madhumuni wenyekumuamini wawe wachache.Mwenyezi mungu ameumba Pepo na Moto.Sasa hili suala la kumpinga uwepo Mungu kwa mtu kama wewe Kiranga yaani upo sawa kwasababu tofauti na hivyo Moto usingeumbwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom