Vitu sita ambavyo si viumbe vya Mungu

Vitu sita ambavyo si viumbe vya Mungu

Huwezi kukuthibitishiwa mfumo ambacho umekuzidi intelijensia.Kibinaadamu tu kuna watu ambao mambo wanayoyafanya binadamu wengine hawawezi kufikiria.Nimeshawahi kukupigia mfano wa vitu ambavyo ni Computerised,watu wa dunia ya tatu kipindi cha miaka ya 60 vitu hivyo vilikuwa ni kama miujiza,kwa wakati huo bwana Kiranga ukiombwa uthibitisho wa utenda kazi wa vitu hivi usingeweza kuelezea.

1).Kwahio uwezo wa Mungu kiintelijensia upo juu sana.Binadamu hana uwezo wa kumthibitishia binadamu mwenzie kwa fact za kisayansi au as tangible objects,Kwasababu Mungu mwenyewe ameamua kujificha na kwa uwezo wake hakuna wa kuweza kumfichua.
2).Ni kwamba kule kutoonekana kwake lengo na madhumuni wenyekumuamini wawe wachache.Mwenyezi mungu ameumba Pepo na Moto.Sasa hili suala la kumpinga uwepo Mungu kwa mtu kama wewe Kiranga yaani upo sawa kwasababu tofauti na hivyo Moto usingeumbwa.
Unajuaje kwamba uwezo wa mungu ni mkubwa wakati wewe binadamu huna uwezo wa kumfahamu na mungu kajificha?

Kwa nini mungu muweza yote na mwenye upendo wote anajificha?

Kujificha ni tabia ya mabaya. Wezi, waovu etc. Si tabia ya mwenye uwezo na upendo.

Kwa nini mungu huyu ajifiche? Anaogopa nini?
 
Unajuaje kwamba uwezo wa mungu ni mkubwa wakati wewe binadamu huna uwezo wa kumfahamu na mungu kajificha?

Kwa nini mungu muweza yote na mwenye upendo wote anajificha?

Kujificha ni tabia ya mabaya. Wezi, waovu etc. Si tabia ya mwenye uwezo na upendo.

Kwa nini mungu huyu ajifiche? Anaogopa nini?

Nimekupa sababu kwamba lengo ni kuwaweka waja wake ktk imani ya kweli lakini wewe unaleta sababu zako.wewe unahitaji uthibitisho ambao unapingana na misingi ya imani.

Ukubwa wa imani ni kuamini kitu ambacho haujakithitisha in physical or chemical way.
Hizo sabb ulizoziweka "SUBHANALLAH" yeye ametakasika.kiburi cha watu waovu ni kwasababu ya neema zake.ARRAHMAN mwenye kuneemesha nemeema ndogondogo za hapa duniani.@Kiranga usije ukawa moja kati waja walioghururika au ghiribika na neema hizo.
 
We jamaa ni mpotoshaji tu na huvijui hivyo vitabu vya dini. Unakurupuka. Twende kwenye Quran sura ya 67 Al Mulk-The Sovereignty:
67:1 inasema "Blessed is He in whose hand is dominion, and He is over all things competent"

67:2 [He] who created death and life to test you [as to] which of you is best in deed - and He is the Exalted in Might, the Forgiving -

Imani Yangu (Quran) yaniambia kifo kiliumbwa na Mungu. We hoja yako haina mantiq.
 
Huwezi kukuthibitishiwa mfumo ambacho umekuzidi intelijensia.Kibinaadamu tu kuna watu ambao mambo wanayoyafanya binadamu wengine hawawezi kufikiria.Nimeshawahi kukupigia mfano wa vitu ambavyo ni Computerised,watu wa dunia ya tatu kipindi cha miaka ya 60 vitu hivyo vilikuwa ni kama miujiza,kwa wakati huo bwana Kiranga ukiombwa uthibitisho wa utenda kazi wa vitu hivi usingeweza kuelezea.

1).Kwahio uwezo wa Mungu kiintelijensia upo juu sana.Binadamu hana uwezo wa kumthibitishia binadamu mwenzie kwa fact za kisayansi au as tangible objects,Kwasababu Mungu mwenyewe ameamua kujificha na kwa uwezo wake hakuna wa kuweza kumfichua.
2).Ni kwamba kule kutoonekana kwake lengo na madhumuni wenyekumuamini wawe wachache.Mwenyezi mungu ameumba Pepo na Moto.Sasa hili suala la kumpinga uwepo Mungu kwa mtu kama wewe Kiranga yaani upo sawa kwasababu tofauti na hivyo Moto usingeumbwa.
Tunda la kati ndio Siri ya Mungu ilipovumbuliwa Maana as per Hadith Binadamu alikuwa yupo yupo tu hata hakujijua kama kavaa nguo au lah alikuwa the same na wanyama wenzie kama Nyani till today hajui kama yupo uchi, Joka likatoa Siri kwa Binadamu.... Hizo Siri za Mungu kitambo zilikuwa wazi... na udadisi ulikuwa mkubwa ndio mkawekewa sheria msidadisi sana ni dhambi lol watu wanapaa anga zote za juu na vyombo walivyotengeneza wenyewe na wamegundua uongo mwingi wa Vitabu unavyoviamini kuwa Jua linazunguka Dunia- ni uongo Dunia ni tambalale uongo... Jua linazama kwenye Matope... Uongo... Jua lilisimamishwa vita ipiganwe Waisrael Washinde.. uongo... Maji yaligawanyika waisrael wakapita katikati yake... Uongo kulikuwa na maji kupwa maji kujaa blah blah kibao... Yesu alipaa wakati alisimama juu ya mlima na asubuhi kama ulishawahi ishi sehemu za miinuko mawingu hushuka chini na asubuhi huenda juu so alipokuwa mlimani akiwaaga Wanafunzi wake mawingi ndio yalikuwa yanapanda juu yeye akawa anapandisha mlima hadi upande wa pili akashuka akielea nchi mbali mbali hadi akafika India mji wa Kashmir akaitwa jina lingine na akafika huko na miaka ya uzee 80 na kitu Kabuli lake hadi leo lipo unyayo wake pia
 
Mungu ni lazima awapime kwa mitihani viumbe vyake.Kwani inakuwaje mwalimu nilazima mwalimu kumpima mwanafunzi wake kumpa mwanafunzi mtihani hali yaku yeye mwalimu anajua majibu yake?
 
Nina bro wangu huongea vitu kama hivi! Yeye ni mwana kabala! Saivi kapotea duniani humu humu, hatujui alipo! Sijui kama hayumo kati ya wachangiaji hapa !
Mkuu hv hawa watu kabala wanapatikana wapi hapa tz? Maana kuna baadhi ya vtu nataka nijfunze kutoka kwao
 
Mlaleo
Nasikitishwa maelezo yako ya mwanzo eti kwamba watu wanapaa anga zote.Wakati NASA majuzi wanadai wamegundua sayari inayofanana na dunia hii ila wakadai mwendo wa kwenda huko ni miaka 600 kwa mwendo wa mwenge yaani kimondo.Pengine haujafahamu upana wa anga na ndio maana umerahisisha kwamba wanapaa anga zote.
Kuhusu dunia ni tambarale hio maelezoyake yapo kwenye Isostence adjustiment theory,ambapo uthibitisho wa wanasayansi wa leo wamekubaliana kwamba, vina vya bahari na maziwa ikitokea maji yake yamekauka, kisha ikajazwa milima iliopo hakuna bonde litakalosalia bali dunia itasawazika."Aliemuongoa Mwenyezimungu hakuna wakumpotosha,na aliemtoa katika njia yake hakuna wakumrejesha" Nakushauri urudi ktk njia kuu njia sahihi ambayo Mungu wametuwekea kwa faida yetu.
 
Ili umuelewe huyu jamaa inabidi uwe ukua kidogo sana au unaufahamu mkubwa sana wa mambo ya rohoni, alichoongea kinafanania na ukweli kama unajua ku reason maandiko, ni kweli kifo hakikuongelewa kuumbwa na kulingana na Bible kifo sio tukio Bali roho, pia Giza sio hali ni kitu ndio maana inasemekana kuna nguvu za Giza na wapo ambao wapi upande wa Giza na sio wa Mungu na wanafanya mambo mengi kwa msaada wa nguvu za Giza, pia maradhi sio hali vitu au roho sijuhi nisemeje, pia vita sio hali wala tukio ni kitu Fulani chenye nguvu na vyote hivyo vinashindana na Mungu, ndio maana Mungu akikuacha akiondoa tuu ulinzi wake kwa mtu hayo jamaa lazima tuu wakukamate na wanakushambulia wote, ila kukubaliana na haya unahitaji mtu kwenye ueleewa mpana sana juu ya mambo ya rohoni
dah nimkuelewa sana..haya mambo nimagumu mno ndo maana Munngu akayaficha akatupa elimu ndogo sana kuhusiana na mambo yasiyoonekana, alijua madhara yake mojawapo ni kumuhasi.....ila loly ungetuelezea tu maana unaoneka great thinkers..

uzuri wa haya mambo wawepo wapingaji watoa hoja km wewe. tupe tu ufafanuzi
 
Kwanza nani kakwambia kisichopo kinathibitishika kwamba hakipo?

Pili, nani kakwambia namuamini Einstein?

Tatu, kwa nini nimuamini Edward Milne?

Nne, mungu wako ni sawa na mchezo wa bahati nasibu?

Tano, what is that something beyond scientific investigation and how do you know so?

Sita, kukosa ushahidi wa chanzo cha species na universe ni uthibitisho kwamba vimeanzishwa na mungu?

Saba, ninazosema theories za physics ziko wapi? Logical consistency ni theory ya physics?

Nane, nisome vizuri theories mbalimbali zipi? Unaweza kuzitaja kwa majina?

Tisa, unaniponda kwa kukataa uwepo wa mungu kwa kutumia theories tu halafu unanitaka nisome theories tu zaidi?

Kumi, nani kakuambia nimesoma Albert Einstein peke yake?
upo sahihi kwa nadharia yako Mungu hayupo... ila umefanya utafiti wa kutosha au ni imani...but all the same kila mtu na imani yake...
 
Atually we need great thinkers like
VITU SITA AMBAVYO SI VIUMBE VYA MUNGU.

View attachment 331270

Tarehe Mar 2016 niliandika makala juu mahusiano kati Kiza, Mungu, Kifo, Vita, Njaa, na Maradhi. Makala ile ilizua mjadala mkubwa facebook na whatsapp nilipoiweka, na moja jambo kubwa lilotuvuruga ni uwezo na mamlaka ya Mungu katika uumbaji, na hasahasa ile nadharia ya kuwa MUNGU ni muumbaji wa viumbe vyote ilitumiwa sana na watu katika kuikosoa makala yangu.

Awali ya yote nakubali bila kigegezi chochote kuwa Mungu ni muumbaji wa viumbe vyote na ya kwamba ni Mola wa viumbe hivyo. Nakubali kuwa ulimwengu haukuzuka tu wenyewe katika tukio la lisilo ratibiwa. Bali yupo injinia wa Ulimwengu huu ambaye si mwingine bali ni MUNGU.

Misaahafu ya dini za Ibrahim, yaan uislamu, uyaudi na ukristo yote kwa pamoja bila kukhitililafiana inasema ulimwengu na vilivyomo ndani yake havikuzuka kwa bahati mbaya bali vimeumbwa na Mungu.

Kuna viumbe hai kama wanyama na mimea, lakini pia kuna viumbe ambavyo havina uhai kama mawe na mchanga. Vyote hivi Muumbaji wake ni Mungu.

"Mwenyezi Mungu ameumba mbingu na ardhi kwa Haki. Kwa hakika katika hayo ipo Ishara kwa Waumini. " Quran 29:44

"...Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Na Yeye ni Mmoja Mwenye kushinda!..." Quran 13:16

"Mbingu ni mali yako, nchi nayo ni mali yako, Ulimwengu na vyote viujazavyo Ndiwe uliyeupiga msingi wake. Kaskazini na kusini ndiwe uliyeziumba....." Zaburi 89:11-12

Hiyo quran 13:16 inatutanabaisha kuwa Mungu ameumba kila kitu, lakini tujiulize, kitu kilichoumbwa na Mungu kinaitwaje? Kwa vyovyote vile kinaitwa kiumbe. Kama ndivyo tunaweza kuwa sahihi zaidi kama tukisema kuwa Mungu ameumba viumbe vyote badala ya kusema kuwa Mungu ameumba kila kitu.

Twasema kuwa viumbe vyote vimeumbwa na Mungu, je vile ambavyo si viumbe tuna vizungumziaje? Naomba mjue Mungu ameumba viumbe vyote, lakini haimaanishi kuwa ameumba kila kitu. Kuna baadhi ya vitu ambavyo Mungu hakuviumba aidha hakutaka kuviumba au ameshindwa kuviumba.

VITU VIKUU SITA AMBAVYO MUNGU HAKUVIUMBA.

1. MUNGU
Ukisoma misahafu yote mikuu miwili quran na biblia hakuna ushahidi hata mmoja unaonesha kuwa Mungu kaumba Mungu(namaanisha Mungu kujiumba).

Kubwa zaidi katika misahafu hiyo ambayo imeandikwa kwa matakwa yake MUNGU, inaonesha ukuu wa Mungu, uwezo wake, mamlaka yake, utukufu wake, usafi wake na kila aina ya sifa nzuri na tukufu, lakini hatuoni chanzo chake kikiandikwa humo na hatuoni mwisho wake ukiandikwa humo, zaidi ya vitabu hivyo kusema ufalme wa MUNGU na Nguvu zake hazina mwanzo wala mwisho.

"Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi" Ufunuo 1:8

"Na Mola wako Mlezi anayajua yaliyo ficha vifua vyao, na wanayo yatangaza. Naye ni Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye. Sifa zote njema ni zake Yeye, mwanzo na mwisho...." Quran 28:69-70

Kwa aya hizi, na mafundisho mengine ya kinabii kama haya, yanathibitisha bila shaka kuwa ni kweli kuna mambo au vitu ambavyo Mungu hakuviumba na kwasababu hiyo vitu hivyo haviwezi kuitwa viumbe na ingawa viko. Kitu cha kwanza MUNGU, kipo na hakija umbwa.

Wanaosema kuwa MUNGU ameumba kila kitu waje hapa watuambie "MUNGU" kaumbwa na nani? Wakishindwa kututajia basi waishie kusema Mungu kaumba viumbe vyote lakini si vitu vyote.

2. KIZA
Ukisoma hiyo quran 28:69-70 na ukisoma vizuri ufunuo 1:8 utagundua mambo yote na habari zote kabla ya uwepo wa MUNGU hayajulikani na huenda anayajua Mungu mwenyewe, lakini kwetu sisi tunaona mambo hayo kwetu ni KIZA.

Kwa hivyo tunaweza kusema kabla ya Mungu hajaumba chochote alikuwako yeye na Kiza, Kiza ni mwanamke na Mungu ni mwanaume. Kwakuwa kwa kipindi hicho walikuwa wenyewe, na wanajuana wenyewe, jambo jepesi twaweza kusema hivi vitu ni ndugu. Ipo siku inshallah nitakuja kufafanua kwanini nasema Kiza mwanamke na Mungu mwanaume.

"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. 3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. 4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza."
Mwanzo 1:1-4

Katika andika hilo la juu tunajifunza yafuatayo.

A. Mbingu na nchi zimeumbwa na Mungu. Maji, ardhi na vitu vya kufananayo ni sehemu ya mbingu ya nchi.

B. Mungu aliumba NURU lakini hakuumba KIZA, tunaambiwa tu Kiza kilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji lakini hatuambiwi Mungu aliumba Kiza.
Hiyo mwanzo 1:3 "Mungu akasema, iwe Nuru; ikawa Nuru"

Alijuaje kuwa Nuru imekuwa kama kabla ya Nuru hiyo kulikuwa hakuna Kiza? Je, mbona hatuoni maandiko yakionesha Mungu akisema iwe Kiza kisha kikawa Kiza?

C. Ukisoma mwanzo 1:2 tunaona Mungu akiumba mbingu na nchi kisha Kiza alikaa juu ya uso wa vilindi vya maji, kwasababu hiyo, nikisema kuwa Kiza alikuwako kabla ya mbingu na nchi nitakosea? Kama alikuwako kabla ya mbigu na nchi, ama kabla ya ulimwengu, nikisema kuwa Kiza na Mungu waliishi wenyewe kabla ya ulimwengu pia nitakosea?

D. Baada ya Mungu kuumba Nuru, hapo ndipo alipofanikiwa, kumfungia KIZA, na athari za Kiza akaziita USIKU na athari za NURU akaziita MCHANA. Kwahivyo Mungu hakumuumba KIZA, ila Mungu kaumba Nuru, Mchana, na Usiku.

Kwahivyo kama tuko pamoja, utakubaliana na mimi kuwa KIZA ni moja ya kitu ambacho Mungu hakukiumba. KIZA si kiumbe, KIZA kimezuka tu kama alivyozuka Mungu mwenyewe. Tafauti kubwa kati ya MUNGU na KIZA ni kuwa Mungu kaumba na ni Mola wa viumbe vyote, lakini Kiza hakuumba kitu chochote kwa hivyo si MUUMBAJI.

Astronomy inatuambia kuwa ulimwemgu umeundwa na vitu vikuu vitatu, normal matter, dark matter na dark energy. Normal matter ndio hujumuisha zile atoms zilizo tumika kuumba Nyota,sayari, na vitu vingine.

Normal matter ni asilimia 5 tu ya ulimwengu wote, 25% ni dark energy na 70% dark matter. Hiyo dark energy na dark matter athari zake zinaonekana katika zenyewe hazionekane. Hii huenda ndio KIZA ambacho kimetajwa katika mwanzo 1:1

Astronomy pia yatuambia ulimwengu unatanuka kwa kasi, na ya kwamba unazidi kuongezeka kutokana ile motion iliyosababishwa na BING BANG, kutanuka kwake ina maanisha unazidi kumeza au ama kuingia katika sehemu mbele zaidi kutokea kule ulipo anzia(kipind cha dark age) Swali kule unapoelekea kuna nini kama si Kiza??

Astronomy pia yatuambia hakuna empty space, kama inavyo onekana, katika space waweza kuona ama kudhani hakuna maada yoyote, lakini kimsingi asilimia kubwa ya space ina dark energy na dark matter. Vitu hivi vinaashiria uwepo KIZA mbali na ulimwengu tunao ujua.

3. KIFO
Kwanza naomba tukumbuke wakati Mungu anafikiria kuumba ulimwengu tayari kulikuwako na KIZA. Ili Mungu awe kuumba ulimwengu ilikuwa lazima kwanza amuondoshe au amuue KIZA. Ili Kiza kiweze kufa shuruti pawe na "KIFO" Hata hivyo, kutokana na nguvu za Kiza, basi kikawa hakijakufa bali kilifungiwa.(Rejea mwanzo 1:3 Mungu akatenga giza na nuru)

Pili naomba mjue kuwa kiumbe hai cha kwanza kuumbwa na Mungu ni "NENO" kisha wakafuatia malaika wakubwa wanne(four Arc Angels) ambao ni Mikaeli, Raphaeli, Rucifer na Gabrieli. Hoja inakuja, Mungu alitumia kipimo gani kujua kwamba amefanikiwa kuumba kiumbe hai? Kwa vyovyote vile ili ajue kuwa amefanikiwa kuumba kiumbe hai ni lazima alinganishe uhai uliopo ndani ya kiumbe hai na mauti(KIFO). Kwa hivyo kilianza KIFO kabla ya UHAI, na bahati nzuri maandiko yanakubali kuwa Mungu kaumba uhai, lakini hayaoneshi kuwa Mungu kaumba KIFO.

Wachungaji wetu katika makanisa wanakataa katakata kuwa Mungu kaumba KIFO, wao wanasema KIFO kilisababishwa na shetani, bi maana shetani ndio kaumba KIFO. Huku ni kutokujua, lakini hakuna aliyeumba KIFO, KIFO sio kiumbe na alizuka tu kama alivyo zuka Mungu.

Kama nilivyosema ule muda Mungu anafikiria kuumba uhai, tayari kifo kilikuwako, na kwasababu hiyo, pia haijulikani kati ya Mungu na Kifo na mkubwa(kiumri).

Mungu aliumba uhai, na kwa kupitia huo uhai akaumba mwanadamu, lengo lake lilikuwa mwanadamu aishi milele, lakini kifo kikawa kikwazo katika lengo hili.

Sivyo tu, kwakuwa siku zote KIZA anataka atoke kifungoni, hivyo kila siku anapambana na Mungu kwa lengo la kutaka kumuua, na wakati huohuo Mungu naye anataka kumuua KIZA, mshindi wa pambano hili lazima amtumie "KIFO" na hapa ndipo tunapoona nafasi ya KIFO katika mahusiano ya NURU na KIZA.

Lakini Mungu anasema atakuja kumshinda KIZA na KIFO, na pindi atakapo shinda hakuna roho au mwili utakao kufa.

"na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. " Ufunuo 1:18

4. VITA na NJAA
KIZA baada ya kugundua Mungu ameumba malaika wakubwa wanne, KIZA alichukia na hapo yakazuka mapambano kati ya MUNGU na KIZA. Kwa mapambano hayo ndipo ilipozuka "VITA" mungu alichofanikiwa ni kumfungia KIZA, na funguo zake akakabidhiwa Rucifer. Mark of Darkness ndio Funguo na sehemu alofungiwa KIZA, chapa hii baadae iliitwa mark of cain.

Mnyama wa kwanza kuumbwa na Mungu kabla hata ya wanadamu ni Levithans, hawa ndio ile mijusi mikubwa na Magodizilla. hawa walikuwa na "NJAA" sana kiasi walane wenyewe kwa wenyewe, Hapa Mungu kwa kutumia jeshi lake la malaika waliwaondoa dunia na kuwafungua Purgatory. Hapa pia VITA alihitajika kufanikisha hili.

Tembo na vufaru wanapungua kwa kuuliwa na binadamu, hivi Magodizilla na Levithans waliuliwa na nani? Ikiwa wao walikuwako miaka mingi kabla ya wanadamu? Jibu jepesi ni upanga wa Malaika Mikael na jeshi lakd.

Wakati hayo yakitokea, Darkness akaigeuza ile mark kuwa laana, na laana ile ikasababisha hali ya uasi kwa mtunza funguo. Wakati Mungu anamuumba mwanadamu, na malaika kuambiwa wamsujudie, Rucifer akiwa kesha athiriwa na laana ya funguo akagoma kumsujidia adamu.

Kwa mara nyingine "VITA" ilihitajika katika kumdhibiti Rucifer na kundi lake.

6 MARADHI
mungu hakuumba maradhi, na wala si lengo mungu mwanadamu aumwe na kuteseka kwa maradhi. Ila pale mwanadamu alipoumbwa na afya bora kabisa, na maradhi yakazuka hapo hapo. Baada ya Mungu kuja kumshinda KIFO, pia atakuja kuyashinda MARADHI, na hayo yakitokea katika maisha Paradiso hakutakuwa na KIFO wala MARADHI.

MWISHO.
makala hii haina tafauti na ya juzi, ila leo baadhi ya nukta nimemua kuziongelea kwa undani zaidi ili iweze kujibu maswali na hoja zilizo jitokeza katika makala ya msingi. Hata hivyo najua siwezi kumaliza kila kitu hapa, ila mengine tutajifunza katika mjadala!

Njano5
0622845394
u
 
Mungu na Shetani wana Undugu au Ni Maadui wa Asili? wote wana uwezo si ndio? Maana Hadith inasema Theluthi mbili ya Malaika hawakuasi na Theluthi moja ya Malaika iliasi ikawa Vita Mungu akashinda kutokana na wingi wa Jeshi lake la Malaika theluthi Mbili so ni Sawa na Russia na America Ni Ndugu wote Wazungu na wote wana Nguvu Sababu ya Uwezo wao wamebakia kutishiana tu bila Action..... Shetani hata akufanye nini wewe Mungu Atatizama tu Maana Akianzisha Vita ni Balaa zitapigwa Kinoma na Kwa Sasa Shetani wako ana wafuasi wengi zaidi ndio maana Dunia haiishi Hakuna wa Kuanzishisha Vita ila Mikwara itaendelea na Majigambo... Jamani Raha si Raha.....!
Mungu na shetani, mwenye nguvu ni Mungu. Mungu alimuamuru shetani asimuue Ayubu akatii.. inamaana alijua nguvu za MUNGU
 
OK, so mungu hakuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana. Mpaka hapo tayari una tatizo kubwa sana la kutatua.

Maana kama mungu hakuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana, na ulimwengu huu mabaya yanawezekana, ina maana mungu hakuumba ulimwengu huu?



Sasa imekuwaje mabaya yanawezekana? Ina maana kuna kitu kina uwezo kumpita mungu kilichofanya ulimwengu uwezekane kuwa na mabaya wakati mungu hakuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana?



Mwanadamu amewezaje kufanya mabaya katika ulimwengu ambao mungu hakuumba uwezekano wa mabaya kufanyika?

Lazima uelewe kwamba, ili binadamu afanye baya, inabidi uwezekano wa baya kufanyika uwepo.

Binadamu hawezi kufanya baya katika ulimwengu ambao uwezekano wa baya kufanyika haupo.

Kama vile ambavyo binadamu hawezi kurudi nyuma katika muda katika ulimwengu ambao uwezo wa binadamu kurudi nyuma katika muda haupo.

Sasa binadamu kawezaje kufanya mabaya katika ulimwengu ambao mungu hakuumba uwezekano wa mabaya kufanyika?



Kama mungu hakuumba binadamu kufikiri mema tu, kamuumba binadamu kuweza kufikiri na kufanya mabaya, utasemaje mungu hakuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana? Unajichanganya.



Unapoongelea "akili ya kujua mema na mabaya" tayari ushaongelea ulimwengu ambao mabaya yapo. Mimi ninachouliza ni tofauti. Nauliza kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana in the first place? Katika ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, hakuna suala la kujua mema na mabaya kwa sababu mabaya hayapo. Kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana?

Alishindwa kuumba ulimwengu ambao una mazuri tu hauna mabaya na akampa mwanadamu uhuru wa kuchagua mazuri yapi afanye?



Mungu alishindwa kumpa mwanadamu nguvu maarifa na utashi katika ulimwengu ambao una mazuri tu na hauna mabaya?

Na kama kweli mungu anapenda mwanadamu awe na maarifa, kwa nini hakumpa mwanadamu maarifa awe kama yeye mungu?



Mungu kwa kuumba binadamu katika ulimwengu ambao mabaya yanawezekana tu na kutompa mwanadamu uwezo wa kuwa mungu tayari kashamzuia mwanadamu kuishi kwa wema 100 per cent.



Utasemaje kwamba vitu vibaya ni matokeo ya mwanadamu wakati mungu kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kufanyika kabla mwanadamu hajaumbwa? Uwezekano wa ubaya kufanyika umekuwapo tangu mwanadamu hajaumbwa, mwanadamu hajaumbwa na uwezo kama wa mungu wa kuepuka mabaya, mwanadamu akifanya mabaya kwa sababu ulimwengu unaruhusu mabaya kufanyika kabla yeye hajaumbwa na kwa sababu yeye kaumbwa na mapungufu yanayomfanya aweze kufanya mabaya, utasemaje mabaya ni matokeo ya wanadamu wenyewe?

Ni kama umpe mtoto mchanga pikipiki halafu umtake aiendeshe resi barabarani wakati unajua kwamba hana uwezo huo, akianguka na kuumia utasema ni matokeo yake yeye mwenyewe au mipango yako?



Kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao ianwezekana kwa mtu kuwa na tamaa ya kumtongoza mke wa fulani wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauna tamaa ya mtu kumtongoza mke wa Fulani?

Hujajibu hili swali.



Wapi unalipata hili?

Kwa nini mungu kaumba uwezekano wa mtu kuwa na tamaa ya kumtongoza mke wa Fulani wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauna tamaa ya mtu kumtongoza mke wa Fulani?

Unaweza kujibu hili swali?



Uthibitisho gani? Unaweza kuutaja? Usilazimishe mambo tu.



Hujathibitisha mungu yupo. Una otea otea tu kwa "pengine".

Unaweza kuthibitisha mungu yupo?
HAHAHA umejitahidi kuelezea ila ulichoshindwa ni kurudia maswali yaliyopatiwa majibu maybe majibu huyaelewi...

hiv baba kaweka kisu na samaki akamuamuru mwane afute kimoja wapo, mtoto akafuata kisu unafikiri babake ndo alimuamuru afuate kisu? au mtoto akifuata smaki unafikiri baba ndo alimuamuru mwane afate samaki? Huo ni utashi wa mtoto.

basi hata binadamu kufata mema au mabaya ni utashi wa mwanadamu sio wa Mungu au shetani.

mabaya yalikuwepo toka zamani tangu dunia haijaumbwa so Mungu hakutuumba ili tutende mabay
 
Huwezi kukuthibitishiwa mfumo ambacho umekuzidi intelijensia.Kibinaadamu tu kuna watu ambao mambo wanayoyafanya binadamu wengine hawawezi kufikiria.Nimeshawahi kukupigia mfano wa vitu ambavyo ni Computerised,watu wa dunia ya tatu kipindi cha miaka ya 60 vitu hivyo vilikuwa ni kama miujiza,kwa wakati huo bwana Kiranga ukiombwa uthibitisho wa utenda kazi wa vitu hivi usingeweza kuelezea.

1).Kwahio uwezo wa Mungu kiintelijensia upo juu sana.Binadamu hana uwezo wa kumthibitishia binadamu mwenzie kwa fact za kisayansi au as tangible objects,Kwasababu Mungu mwenyewe ameamua kujificha na kwa uwezo wake hakuna wa kuweza kumfichua.
2).Ni kwamba kule kutoonekana kwake lengo na madhumuni wenyekumuamini wawe wachache.Mwenyezi mungu ameumba Pepo na Moto.Sasa hili suala la kumpinga uwepo Mungu kwa mtu kama wewe Kiranga yaani upo sawa kwasababu tofauti na hivyo Moto usingeumbwa.
Afu kitu kingine jeshi la Mungu halilali. so wale watakaomuamini Mungu hasiyeonekana ndo watakuwa mojawapo ya jeshi lake kwa maana hawa watu waliweza kumpiga adui bila kuwa na silaha
 
upo sahihi kwa nadharia yako Mungu hayupo... ila umefanya utafiti wa kutosha au ni imani...but all the same kila mtu na imani yake...
Mungu huyu hahitaji utafiti mkubwa kuona kwamba ametungwa.

Tena amwtungwa na watu ambao hawakuwa na logical consistency.

Imekuwaje mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambaobmabaya yanawezekana?

Unaona contradiction hapo?
 
HAHAHA umejitahidi kuelezea ila ulichoshindwa ni kurudia maswali yaliyopatiwa majibu maybe majibu huyaelewi...

hiv baba kaweka kisu na samaki akamuamuru mwane afute kimoja wapo, mtoto akafuata kisu unafikiri babake ndo alimuamuru afuate kisu? au mtoto akifuata smaki unafikiri baba ndo alimuamuru mwane afate samaki? Huo ni utashi wa mtoto.

basi hata binadamu kufata mema au mabaya ni utashi wa mwanadamu sio wa Mungu au shetani.

mabaya yalikuwepo toka zamani tangu dunia haijaumbwa so Mungu hakutuumba ili tutende mabay
Kosa la kwanza, unalinganisha visivyolingana.

Baba ana kikomo cha uwezo, upendo na ujuzi. Utamfananishaje na mungu ambaye hana kikomo cha uwezo, upendo wala upendo?

Uamuzi wowote atakaoufanya baba utatokana na initial conditions alizonazo.

Utamfananishaje na mungu ambaye habanwi na initual conditions zozote bali yeye ndiye anaamua initial conditions?

Kanuni muhimu kabisa ya kulinganisha vitu ni kwamba ulinganishe vinavyolinganishika.

Umelinganisha baba ambaye ana kikomo cha uwezo, upendo na ujuzi na mungu ambaye hana kikomo cha uwezo, upendo wala ujuzi.

Unaelewa kwamba umekosea kufikiri kama mtu anayelinganisha namba moja na infinity?

Nimekuuliza kwa nini mungu jaumbabukimwengu ambao mabaya yanawezekana kuwapo wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ukimwengu ambao mabaya hayawezekani kuwepo.

Unajibu mabaya yalikuwepo tangu zamani kabla mwanadamu hajaumbwa na mungu hakutuumbabiki tufanye mabaya.

Hivi hata swali kulielewa umelielewa?.
 
Nimekupa sababu kwamba lengo ni kuwaweka waja wake ktk imani ya kweli lakini wewe unaleta sababu zako.wewe unahitaji uthibitisho ambao unapingana na misingi ya imani.

Ukubwa wa imani ni kuamini kitu ambacho haujakithitisha in physical or chemical way.
Hizo sabb ulizoziweka "SUBHANALLAH" yeye ametakasika.kiburi cha watu waovu ni kwasababu ya neema zake.ARRAHMAN mwenye kuneemesha nemeema ndogondogo za hapa duniani.@Kiranga usije ukawa moja kati waja walioghururika au ghiribika na neema hizo.
Kwa nini mungu muweza yote, mjuzi wa yote na nwenye maoenzi yote ahitaji mabaya yawepo ili tu wawe kwenye imani ya kweli?

Alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya na mungu yuko wazi kwa kila kiumbe kiasi viumbe wake wote wana ujuzi wa kweli, si imani tu?

Kulikuwa na lazima gani kwa mungu kuumba ulimwengu ambao watoto wanazaliwa na matatizo ya ubongo kutokana na Zika virus, au wanazaliwa na Ebola, au wanakufa katika tsunami, au wanauawa katika genocide?

Huyu mungu yupo kweli au katungwa na watu tu?
 
Mungu ni lazima awapime kwa mitihani viumbe vyake.Kwani inakuwaje mwalimu nilazima mwalimu kumpima mwanafunzi wake kumpa mwanafunzi mtihani hali yaku yeye mwalimu anajua majibu yake?
Mungu mjuzi wa yote analazimikaje kuwapima kwa mitihani viumbe wake?

Una maana mungu huyu uwezo wake wa kufahamu viumbe wake ni sawa wa walimu wa kibinadamu, bila kuwapa mitihani hawezi kuwajua viumbe wake?

Si wanasema anajua kila kitu? Sasa kama anajua kila kitu mitihani inamsaidia nini?

Kama anahitaji mitihani, ni kweli anajua kila kitu?
 
Ngoja nikujibu mara moja mzee Dotto,

1 Dotto Mungu asingemuumba Mungu kwa sababu ni yeye mwenyewe Hivyo asingejiumba, Huyo Mungu 《YHWH》 ndiye aliyekuwapo kabla ya chochote kuwapo hata hilo Giza unalosema kuwa ni Mwanamke wa (YHWH)
2. Kifo ingekuwa ni changamoto kwa Mungu basi asingemtuma Nabii Yeshua (Yesu) akafa na kufufuka! Ile ilikuwa ni kama funga mdomo ya watu na roho ambao walikuwa na hoja kama yako...
3.. Maradhi yangekuwa ni changamoto kwa Mungu basi watu tungekuwa hatuponi magonjwa, amesema kuwa tunaangamia sababu ya ukosefu wa maarifa ila hakuna Gonjwa lisilo na dawa hapa duniani..
4. Njaa ingekuwa ni changamoto kwa Mungu watu wasingeshiba!
5. Vita ingekuwa ni changamoto kwa Mungu basi tusingeona amani Hapa Duniani katu..
6.Giza ingekuwa ni changamoto kwa mungu basi tusingeona mwanga katu, na hilo ili kuthibitika zaidi hata binadamu wameweza kufanya miale ya mwanga inayong'aza giza lote na kuwa sawa na mchana...!

NB.. Pia naomba utambue kuwa aliyekuja kuuumba ulimwengu hakuwa Mungu ila ni malaika wake, ambaye kwenye bible wamemuita jina la neno, yaani alipewa maagizo ya mdomo aje ayatekeleze ulimwenguni, ila kwa wakati huo Mungu YHWH alikuwa ameshaumba mambo chungu mzima..

Chimbuko la dini la wazee weusi wa Misri wanaamini ulimwengu uliumbwa na Atum naye alikuwa ni Mtu ambaye alikwisha fanywa.
 
We jamaa ni mpotoshaji tu na huvijui hivyo vitabu vya dini. Unakurupuka. Twende kwenye Quran sura ya 67 Al Mulk-The Sovereignty:
67:1 inasema "Blessed is He in whose hand is dominion, and He is over all things competent"

67:2 [He] who created death and life to test you [as to] which of you is best in deed - and He is the Exalted in Might, the Forgiving -

Imani Yangu (Quran) yaniambia kifo kiliumbwa na Mungu. We hoja yako haina mantiq.
Quran inasema kuna watu hawaamini mungu atawafanya mioyobyao isimjue hata wakijaribu vipi kumjua.

Kisha atawahukumu kwa kutomjua.

Ni sawa na baba kakukataza kwenda shule iki usijue kusoma, hak afu usipojua kusima anakuadhibu kwa sababu hujui kusoma.

Huyu mungu anasadikika kweli jwamba ni mungu wa kweku au maandishi ya mtu aliyepagawa jangwani tu?
 
dah nimkuelewa sana..haya mambo nimagumu mno ndo maana Munngu akayaficha akatupa elimu ndogo sana kuhusiana na mambo yasiyoonekana, alijua madhara yake mojawapo ni kumuhasi.....ila loly ungetuelezea tu maana unaoneka great thinkers..

uzuri wa haya mambo wawepo wapingaji watoa hoja km wewe. tupe tu ufafanuzi
Kuficha ni sifa ya uovu, wizi, ubaya, kutojiamini, kuogopa si sifa ya mungu mjuzi wa yote, muweza yote na mwenye upendo wote.

Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwebye uoendo wote angekuwepo asingejificha. Angekuwa yukibwazi kiasi kwamba tusingehitaji imani, tungejua yupo kwa hakika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom