Vitu sita ambavyo si viumbe vya Mungu

Vitu sita ambavyo si viumbe vya Mungu

Sitaweza kujibu maswali yako yote, natafuta muda nikuwekee theory mbali mbali zinazotolewa na wataalamu mbali mbali juu ya universe na species namna zinavyotofautiana. Kuhusu kisichokuwepo kutothibitishika, ni swali zuri sana. Maana yake ni hii...wewe umefika mahali ukakuta Gari limepaki na halijazimwa lakini dereva aliyelileta pale hayupo. Huwezi kuthibitisha kwamba gari lile limeletwa pale na dereva? Vinginevyo uthibitishe mechanism ya gari lile kama linaweza kujiendesha lenyewe hadi hapo lilipopaki. Ni rahisi hivyo tu.
Lakini kutuambia kuwa habari za Mungu ni hadithi tu zilizobuniwa na kuandikwa ni sawa na kutuambia kuwa tusiamini historia. Kwamba lazima tuamini tunakiona au kushika au kunusa au kuonja. Km ni hivyo hatupaswi kuamini kuwa hata hao kina Einstein waliwahi kuishi kwa sababu hatuwezi kuwaona. Hakuna haja ya kusema Vasco da Gama aliwahi kuishi.
Sikusema kuwa Mungu ni sawa na bahati nasibu bali nimesema kuwa universe inavyofanya kazi kwa kutegemeana ni vigumu kuwa vimetokea kwa bahati nasibu tu. Ndipo nikalinganisha na aina hiyo ya bahati nasibu.
Nitarudi baadaye Mkuu Kiranga. Nitakuwekea maajabu ya DNA tu uone wanasayansi wanavyokataa kuwa hakuna uwezekano wa kujitengeneza yenyewe.

Unaweza kuthibitisha pembetatu duara haipo?

Must complexity come from even greater complexity?

Unafahamu kwamba hata ukiweza ku prove kwamba DNA haiwezi kujitengeneza yenyewe, bado hujathibitisha kwamba imetoka kwa mungu? That your enterprise is a fool's errand borne out of logical non sequitur that in the end will prove nothing?
 
VITU SITA AMBAVYO SI VIUMBE VYA MUNGU.

View attachment 331270

Tarehe Mar 2016 niliandika makala juu mahusiano kati Kiza, Mungu, Kifo, Vita, Njaa, na Maradhi. Makala ile ilizua mjadala mkubwa facebook na whatsapp nilipoiweka, na moja jambo kubwa lilotuvuruga ni uwezo na mamlaka ya Mungu katika uumbaji, na hasahasa ile nadharia ya kuwa MUNGU ni muumbaji wa viumbe vyote ilitumiwa sana na watu katika kuikosoa makala yangu.

Awali ya yote nakubali bila kigegezi chochote kuwa Mungu ni muumbaji wa viumbe vyote na ya kwamba ni Mola wa viumbe hivyo. Nakubali kuwa ulimwengu haukuzuka tu wenyewe katika tukio la lisilo ratibiwa. Bali yupo injinia wa Ulimwengu huu ambaye si mwingine bali ni MUNGU.

Misaahafu ya dini za Ibrahim, yaan uislamu, uyaudi na ukristo yote kwa pamoja bila kukhitililafiana inasema ulimwengu na vilivyomo ndani yake havikuzuka kwa bahati mbaya bali vimeumbwa na Mungu.

Kuna viumbe hai kama wanyama na mimea, lakini pia kuna viumbe ambavyo havina uhai kama mawe na mchanga. Vyote hivi Muumbaji wake ni Mungu.

"Mwenyezi Mungu ameumba mbingu na ardhi kwa Haki. Kwa hakika katika hayo ipo Ishara kwa Waumini. " Quran 29:44

"...Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Na Yeye ni Mmoja Mwenye kushinda!..." Quran 13:16

"Mbingu ni mali yako, nchi nayo ni mali yako, Ulimwengu na vyote viujazavyo Ndiwe uliyeupiga msingi wake. Kaskazini na kusini ndiwe uliyeziumba....." Zaburi 89:11-12

Hiyo quran 13:16 inatutanabaisha kuwa Mungu ameumba kila kitu, lakini tujiulize, kitu kilichoumbwa na Mungu kinaitwaje? Kwa vyovyote vile kinaitwa kiumbe. Kama ndivyo tunaweza kuwa sahihi zaidi kama tukisema kuwa Mungu ameumba viumbe vyote badala ya kusema kuwa Mungu ameumba kila kitu.

Twasema kuwa viumbe vyote vimeumbwa na Mungu, je vile ambavyo si viumbe tuna vizungumziaje? Naomba mjue Mungu ameumba viumbe vyote, lakini haimaanishi kuwa ameumba kila kitu. Kuna baadhi ya vitu ambavyo Mungu hakuviumba aidha hakutaka kuviumba au ameshindwa kuviumba.

VITU VIKUU SITA AMBAVYO MUNGU HAKUVIUMBA.

1. MUNGU
Ukisoma misahafu yote mikuu miwili quran na biblia hakuna ushahidi hata mmoja unaonesha kuwa Mungu kaumba Mungu(namaanisha Mungu kujiumba).

Kubwa zaidi katika misahafu hiyo ambayo imeandikwa kwa matakwa yake MUNGU, inaonesha ukuu wa Mungu, uwezo wake, mamlaka yake, utukufu wake, usafi wake na kila aina ya sifa nzuri na tukufu, lakini hatuoni chanzo chake kikiandikwa humo na hatuoni mwisho wake ukiandikwa humo, zaidi ya vitabu hivyo kusema ufalme wa MUNGU na Nguvu zake hazina mwanzo wala mwisho.

"Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi" Ufunuo 1:8

"Na Mola wako Mlezi anayajua yaliyo ficha vifua vyao, na wanayo yatangaza. Naye ni Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye. Sifa zote njema ni zake Yeye, mwanzo na mwisho...." Quran 28:69-70

Kwa aya hizi, na mafundisho mengine ya kinabii kama haya, yanathibitisha bila shaka kuwa ni kweli kuna mambo au vitu ambavyo Mungu hakuviumba na kwasababu hiyo vitu hivyo haviwezi kuitwa viumbe na ingawa viko. Kitu cha kwanza MUNGU, kipo na hakija umbwa.

Wanaosema kuwa MUNGU ameumba kila kitu waje hapa watuambie "MUNGU" kaumbwa na nani? Wakishindwa kututajia basi waishie kusema Mungu kaumba viumbe vyote lakini si vitu vyote.

2. KIZA
Ukisoma hiyo quran 28:69-70 na ukisoma vizuri ufunuo 1:8 utagundua mambo yote na habari zote kabla ya uwepo wa MUNGU hayajulikani na huenda anayajua Mungu mwenyewe, lakini kwetu sisi tunaona mambo hayo kwetu ni KIZA.

Kwa hivyo tunaweza kusema kabla ya Mungu hajaumba chochote alikuwako yeye na Kiza, Kiza ni mwanamke na Mungu ni mwanaume. Kwakuwa kwa kipindi hicho walikuwa wenyewe, na wanajuana wenyewe, jambo jepesi twaweza kusema hivi vitu ni ndugu. Ipo siku inshallah nitakuja kufafanua kwanini nasema Kiza mwanamke na Mungu mwanaume.

"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. 3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. 4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza."
Mwanzo 1:1-4

Katika andika hilo la juu tunajifunza yafuatayo.

A. Mbingu na nchi zimeumbwa na Mungu. Maji, ardhi na vitu vya kufananayo ni sehemu ya mbingu ya nchi.

B. Mungu aliumba NURU lakini hakuumba KIZA, tunaambiwa tu Kiza kilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji lakini hatuambiwi Mungu aliumba Kiza.
Hiyo mwanzo 1:3 "Mungu akasema, iwe Nuru; ikawa Nuru"

Alijuaje kuwa Nuru imekuwa kama kabla ya Nuru hiyo kulikuwa hakuna Kiza? Je, mbona hatuoni maandiko yakionesha Mungu akisema iwe Kiza kisha kikawa Kiza?

C. Ukisoma mwanzo 1:2 tunaona Mungu akiumba mbingu na nchi kisha Kiza alikaa juu ya uso wa vilindi vya maji, kwasababu hiyo, nikisema kuwa Kiza alikuwako kabla ya mbingu na nchi nitakosea? Kama alikuwako kabla ya mbigu na nchi, ama kabla ya ulimwengu, nikisema kuwa Kiza na Mungu waliishi wenyewe kabla ya ulimwengu pia nitakosea?

D. Baada ya Mungu kuumba Nuru, hapo ndipo alipofanikiwa, kumfungia KIZA, na athari za Kiza akaziita USIKU na athari za NURU akaziita MCHANA. Kwahivyo Mungu hakumuumba KIZA, ila Mungu kaumba Nuru, Mchana, na Usiku.

Kwahivyo kama tuko pamoja, utakubaliana na mimi kuwa KIZA ni moja ya kitu ambacho Mungu hakukiumba. KIZA si kiumbe, KIZA kimezuka tu kama alivyozuka Mungu mwenyewe. Tafauti kubwa kati ya MUNGU na KIZA ni kuwa Mungu kaumba na ni Mola wa viumbe vyote, lakini Kiza hakuumba kitu chochote kwa hivyo si MUUMBAJI.

Astronomy inatuambia kuwa ulimwemgu umeundwa na vitu vikuu vitatu, normal matter, dark matter na dark energy. Normal matter ndio hujumuisha zile atoms zilizo tumika kuumba Nyota,sayari, na vitu vingine.

Normal matter ni asilimia 5 tu ya ulimwengu wote, 25% ni dark energy na 70% dark matter. Hiyo dark energy na dark matter athari zake zinaonekana katika zenyewe hazionekane. Hii huenda ndio KIZA ambacho kimetajwa katika mwanzo 1:1

Astronomy pia yatuambia ulimwengu unatanuka kwa kasi, na ya kwamba unazidi kuongezeka kutokana ile motion iliyosababishwa na BING BANG, kutanuka kwake ina maanisha unazidi kumeza au ama kuingia katika sehemu mbele zaidi kutokea kule ulipo anzia(kipind cha dark age) Swali kule unapoelekea kuna nini kama si Kiza??

Astronomy pia yatuambia hakuna empty space, kama inavyo onekana, katika space waweza kuona ama kudhani hakuna maada yoyote, lakini kimsingi asilimia kubwa ya space ina dark energy na dark matter. Vitu hivi vinaashiria uwepo KIZA mbali na ulimwengu tunao ujua.

3. KIFO
Kwanza naomba tukumbuke wakati Mungu anafikiria kuumba ulimwengu tayari kulikuwako na KIZA. Ili Mungu awe kuumba ulimwengu ilikuwa lazima kwanza amuondoshe au amuue KIZA. Ili Kiza kiweze kufa shuruti pawe na "KIFO" Hata hivyo, kutokana na nguvu za Kiza, basi kikawa hakijakufa bali kilifungiwa.(Rejea mwanzo 1:3 Mungu akatenga giza na nuru)

Pili naomba mjue kuwa kiumbe hai cha kwanza kuumbwa na Mungu ni "NENO" kisha wakafuatia malaika wakubwa wanne(four Arc Angels) ambao ni Mikaeli, Raphaeli, Rucifer na Gabrieli. Hoja inakuja, Mungu alitumia kipimo gani kujua kwamba amefanikiwa kuumba kiumbe hai? Kwa vyovyote vile ili ajue kuwa amefanikiwa kuumba kiumbe hai ni lazima alinganishe uhai uliopo ndani ya kiumbe hai na mauti(KIFO). Kwa hivyo kilianza KIFO kabla ya UHAI, na bahati nzuri maandiko yanakubali kuwa Mungu kaumba uhai, lakini hayaoneshi kuwa Mungu kaumba KIFO.

Wachungaji wetu katika makanisa wanakataa katakata kuwa Mungu kaumba KIFO, wao wanasema KIFO kilisababishwa na shetani, bi maana shetani ndio kaumba KIFO. Huku ni kutokujua, lakini hakuna aliyeumba KIFO, KIFO sio kiumbe na alizuka tu kama alivyo zuka Mungu.

Kama nilivyosema ule muda Mungu anafikiria kuumba uhai, tayari kifo kilikuwako, na kwasababu hiyo, pia haijulikani kati ya Mungu na Kifo na mkubwa(kiumri).

Mungu aliumba uhai, na kwa kupitia huo uhai akaumba mwanadamu, lengo lake lilikuwa mwanadamu aishi milele, lakini kifo kikawa kikwazo katika lengo hili.

Sivyo tu, kwakuwa siku zote KIZA anataka atoke kifungoni, hivyo kila siku anapambana na Mungu kwa lengo la kutaka kumuua, na wakati huohuo Mungu naye anataka kumuua KIZA, mshindi wa pambano hili lazima amtumie "KIFO" na hapa ndipo tunapoona nafasi ya KIFO katika mahusiano ya NURU na KIZA.

Lakini Mungu anasema atakuja kumshinda KIZA na KIFO, na pindi atakapo shinda hakuna roho au mwili utakao kufa.

"na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. " Ufunuo 1:18

4. VITA na NJAA
KIZA baada ya kugundua Mungu ameumba malaika wakubwa wanne, KIZA alichukia na hapo yakazuka mapambano kati ya MUNGU na KIZA. Kwa mapambano hayo ndipo ilipozuka "VITA" mungu alichofanikiwa ni kumfungia KIZA, na funguo zake akakabidhiwa Rucifer. Mark of Darkness ndio Funguo na sehemu alofungiwa KIZA, chapa hii baadae iliitwa mark of cain.

Mnyama wa kwanza kuumbwa na Mungu kabla hata ya wanadamu ni Levithans, hawa ndio ile mijusi mikubwa na Magodizilla. hawa walikuwa na "NJAA" sana kiasi walane wenyewe kwa wenyewe, Hapa Mungu kwa kutumia jeshi lake la malaika waliwaondoa dunia na kuwafungua Purgatory. Hapa pia VITA alihitajika kufanikisha hili.

Tembo na vufaru wanapungua kwa kuuliwa na binadamu, hivi Magodizilla na Levithans waliuliwa na nani? Ikiwa wao walikuwako miaka mingi kabla ya wanadamu? Jibu jepesi ni upanga wa Malaika Mikael na jeshi lakd.

Wakati hayo yakitokea, Darkness akaigeuza ile mark kuwa laana, na laana ile ikasababisha hali ya uasi kwa mtunza funguo. Wakati Mungu anamuumba mwanadamu, na malaika kuambiwa wamsujudie, Rucifer akiwa kesha athiriwa na laana ya funguo akagoma kumsujidia adamu.

Kwa mara nyingine "VITA" ilihitajika katika kumdhibiti Rucifer na kundi lake.

6 MARADHI
mungu hakuumba maradhi, na wala si lengo mungu mwanadamu aumwe na kuteseka kwa maradhi. Ila pale mwanadamu alipoumbwa na afya bora kabisa, na maradhi yakazuka hapo hapo. Baada ya Mungu kuja kumshinda KIFO, pia atakuja kuyashinda MARADHI, na hayo yakitokea katika maisha Paradiso hakutakuwa na KIFO wala MARADHI.

MWISHO.
makala hii haina tafauti na ya juzi, ila leo baadhi ya nukta nimemua kuziongelea kwa undani zaidi ili iweze kujibu maswali na hoja zilizo jitokeza katika makala ya msingi. Hata hivyo najua siwezi kumaliza kila kitu hapa, ila mengine tutajifunza katika mjadala!

Njano5
0622845394
Samahani mkuu. Mm ni miongoni kati ya watu wasioamini uwepo wa mungu. Nilianza kutoa imani yangu baada ya kujiuliza uwepo wa shetani. Naomba kushare na wewe hilo swali huenda tukapata jibu sahihi. Swali lenyewe ni hili hapa "je, uwepo wa shetani ni mpango wa mungu au ni kufeli kwa mungu? " naomba tujiulize kwa pamoja. Kama ukipata jibu usisite kunielekeza
 
Daaah Njano na hoja zako ngumu kama kawaida. Mmmmh nimekuvulia kofia
 
MBINGU, ANGA, JUA, NA UUMBAJI.

Naelewa kuna galaxy zisizo pungua bilion 100, na si 99 kama unavyosema wewe, na kuna matirioni ya nyota. Najua wataka kusema kuwa Mwanzo Sura ya kwanza inazungumzia uumbaji wa dunia na si uumbaji wa ulimwengu, kwa hivyo wasema Kiza kiliumbwa siku nyingi kabla ya matukio yalihotajwa na Mwanzo sura ya kwanza.

Kabla sijakujibu hoja yako, naomba tujiulize, kwa mujibu wa mwanzo 1:1 na kwa kuzingatia maandiko mengine ya biblia, Mbingu ni nini? na mbinguni wapi? Kisha tujiulize nch ni nini?

Mbingu ni neno la kiroho zaidi lenye maana ya anga.(space). Wana sayansi wanatumia neno "anga" wakati Mungu anatumia neno "mbingu". Kwa hivyo tukijua maana ya anga kwa vyovyote vile pia tutajua maana ya mbingu.

Anga ni eneo kubwa sana(three dimensional region) ambalo huanzia pale atmosphere inapoishia. Naomba ufahamu kuwa atmosphere ni moja kati ya matabaka ya dunia. Hii ina maanisha pale dunia inapoishia ndipo anga huanza. Kwasababu hiyo, ndio maana wanasayansi wanasema Dunia iko angani.

Anga ndio ulimwengu wenyewe, sababu vitu ambavyo vipo angani galaxy, nyota, sayari, vimondo, setelaiti, na nk ndio hufanya ulimwengu. Anga, ambayo kimsingi ndio ulimwengu umeundwa na vitu vifuatavyo.

1. Normal Matter
Ambayo ni asilimia tano ya ulimwengu wote. Galaxy, nyota, sayari, vimondo, na hata viumbe hai vimetokana na NORMAL MATTER.

2. Dark Energy
Ambayo yenyewe ni asilimia 25

3 Dark Matter
Ambayo yenyewe ni asilimia 70 ya ulimwengu wote.

Kwa hivyo nyota zote ziko angani, na nimesema hapo juu kuwa anga ndio mbingu. Kama wanasayansi wanasema nyota ziko angani, tujiulize Mungu anasema nyota ziko wapi?

"Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze"
Isaya 13:10

"Umeongeza wafanya biashara wako kuwa wengi kuliko nyota za mbinguni;...."
Nahumu 3:16

"katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni,..."
Mwanzo 22:17

"Ametukuka aliye zijaalia nyota mbinguni, na akajaalia humo taa na mwezi unao ng'ara."
Quran 25:61

"Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota."
Quran 37:6

Quran na biblia zote zinasema nyota ziko mbinguni, kama nyota ziko mbinguni kwa mujibu wa Mungu, na kama nyota pia ziko angani kwa mujibu wa sayansi, je nikisema kuwa MBINGU na ANGA ni kitu kimoja nitakosea? Kwa vyovyote vile sitakosea.

Kwahivyo naomba muelewe, mwanzo 1:1 iliposema Mungu aliziumba mbingu ili maanisha Mungu aliuumba ULIMWENGU. Sababu tumeona mbingu ni mkusanyiko wa matirioni ya nyota na mifumo yake ambayo kwa pamoja hufanya ulimwengu.

Ukisoma astronomy jinsi inavyo zielezea nyota, hasa vile zilivyo undwa, utagundua hazikuanza tu kuwa na Nuru(Mwanga) na Joto kali, bali kuna mambo na michakato ilikuwa inafanyika, na matokeo ya mambo hayo ndio yakapelekea nyota kuwa na mwanga. Kwa hivyo Mungu aliposema iwe Nuru ndio aliruhusu michakato hiyo kuanza kufanya kazi na hatimaye tukapata jua. Lakini kabla ya NURU kuja kulikuwa na nini? jibu KIZA.

Nchi maana yake Dunia, lakini lazima tujue na kukubali kuwa kila nyota ina mfumo wake, na katika kila mfumo wa nyota una sayari zake, na kila sayari ina usiku na machana. Kwa hivyo Mungu aliposema iwe NURU, basi hapo hapo nyota zote ulimwenguni zikatoa Nuru au zikawa na uwezo wa kuwa na mwanga.

Kuna baadhi ya mambo yalifanyika maalum kwaajili ya sayari moja moja, lakini kuna baadhi ya mambo yalifanyika kwa sayari zote kwa ujumla. Kwa hivyo siku iliyoumbwa "mchana" katika sayari ya dunia, ndio siku iliyo umbwa mchana katika sayari zote za ulimwengu. Ninasema hili kutokana na sababu kubwa ifuatayo.

Mfumo wa Nyota Jua una jumla ya sayari nane, na dunia ni moja katia ya sayari hizo nane. Kwa hivyo kipindi Jua lilipopewa NURU, ile Nuru yake ilifika katika sayari zote nane. Pale Mungu aliposema Nuru ijitenge na giza, na giza liwe usiku na Nuru iwe mchana, tukio hilo lilitokea kwa Sayari zote. Kwasababu hiyo si kweli hata kidogo kuwa NURU na MCHANA uliotajwa katika mwanzo 1:3-5 ulikuwa makhususi kwaajili ya Sayari Dunia pekee.

Ili useme ile NURU ni makhususi kwaajili ya dunia tu, ni lazima utuambie Nuru hiyo imetoka katika Nyota gani tafauti na nyota jua. Sababu Nyota Jua ndio huangazia sayari zote katika mfumo wa Jua. Hivyo ni dhahiri kuwa wakati Jua lilipoanza kuangazia dunia ndio wakati huohuo lilipoangazia sayari zingine pia.

Mambo mkhususi ya Dunia katika mwanzo sura ya kwanza ni uumbaji wa mito, bahari, miti, wanyama, nk. Haya ndio yalikuwa makhususi kwaajili ya Dunia, na kila sayari ilikuwa na mambo yake makhususi kadiri ya Mungu mwenyewe alivyoona vema, ndio maana tabia na sifa za dunia ziko tafauti na Zuhura, lakini zote zinategemea NURU ya Jua na zote zina usiku na mchana.

Kwa hivyo bado niko katika hoja yangu, kuwa Mungu aliposema kaumba mbingu alimaanisha kaumba ulimwengu. Akaumba Nuru kwa kulifanya jua litoe mwanga, lakini Mungu hakuumba Kiza, bali aliumba Nuru ili kukipiga KIZA, na kwasababu hiyo hakuna ushahidi Mungu akisema ameumba Kiza.

Njano5
0622845394
Daaah we mbaya aseee
 
mkuu asante kwa majib japo umetumia maelezo marefu sana, jambo 1 ambalo tunapaswa kufahamu kuwa dunia na watu wote wakaao duniani wanauwezo ambao Mungu ameruhusu kuwa nao,

ikiwa uwezo wa akili hii ya dhambi, hauwezi kujua jema na baya je unaweza kuchunguza akili ya Mungu?

kwa mjib wa biblia shetani alitupwa humu duniani baada ya vita mbingun, na kabla ya kuja duniani alipita kwenye galaxies zingine ila alikataliwa ndipo alifanikiwa. kuwadanganya wazazi wetu,

hvyo uumbaji wa mungu haukuamzia kwetu ila mbali zaidi.. narudia Mungu aliumba giza, swali dogo nikuulize je Mungu alimuuba shetani au laa? jib lako litasaidia kujua hyo dhana ya uumbaji ya Mungu.
 
Unaweza kuthibitisha pembetatu duara haipo?

Must complexity come from even greater complexity?

Unafahamu kwamba hata ukiweza ku prove kwamba DNA haiwezi kujitengeneza yenyewe, bado hujathibitisha kwamba imetoka kwa mungu? That your enterprise is a fool's errand borne out of logical non sequitur that in the end will prve nothing?
mkuu huyu jamaa tumsaidie taratibu
 
Samahani mkuu. Mm ni miongoni kati ya watu wasioamini uwepo wa mungu. Nilianza kutoa imani yangu baada ya kujiuliza uwepo wa shetani. Naomba kushare na wewe hilo swali huenda tukapata jibu sahihi. Swali lenyewe ni hili hapa "je, uwepo wa shetani ni mpango wa mungu au ni kufeli kwa mungu? " naomba tujiulize kwa pamoja. Kama ukipata jibu usisite kunielekeza
mkuu m ntakujib ila kwa kuwa mleta mada nmemuuliza swali hilo ambalo majib yake yataleta mkanganyiko ngoja aje akijib kuhusiana na Kama Mungu alimuumba shetani au laa ntakujib vzr...
vuta subra ninamajb sahihi mkubwa..
 
Samahani mkuu. Mm ni miongoni kati ya watu wasioamini uwepo wa mungu. Nilianza kutoa imani yangu baada ya kujiuliza uwepo wa shetani. Naomba kushare na wewe hilo swali huenda tukapata jibu sahihi. Swali lenyewe ni hili hapa "je, uwepo wa shetani ni mpango wa mungu au ni kufeli kwa mungu? " naomba tujiulize kwa pamoja. Kama ukipata jibu usisite kunielekeza
Sina reference ya kitabu kukupa lakini kutokana na mapokeo niliyoyapata kutoka ukatoliki na kusoma Bible. Mungu aliumba malaika wakuu wanne, Michael, (the host prince), Lucifer, Raphael na Gabriel. Lucifer alipendwa sana na akajiona untouchable, akawa mkaidi na akafukuzwa mbinguni. Michael alitii amri ya Mungu ahakikishe Lucifer ametolewa kule na haingii tena na ndiye mlinzi wa kanisa kutoka kwa nguvu za giza.
Lucifer alikimbilia ulimwenguni. Kutoka hapo Mungu akamuumba binadamu kwa mfano wake, ukaidi wa Lucifer ulikuwa kukubali binadamu ni juu ya malaika na anatakiwa kumsujudia. Lucifer anaona wivu sana kwa binadamu, yale mazuri aliyoyaacha kule mbinguni sisi ndiyo tutayafaidi, kwahiyo ameapa kutupa figisu figisu hapa duniani mpaka tuikose raha ya mbingu.
 
Mungu alijua haya yatatokea? Au yalimshinda tu hakujua?
 
umejua kupitia THREAD hii au nyingine..!?
kama umujua kupitia THREAD hii nakushauri ujaribu kuipitia tena VIZURI ili usije ukatoka na ELIMU tofauti na aliyoikusudia MWANDISHI..!!!
Hakuna elimu ambayo sikuifahamu katika yote aliyoongea mtoa mada. Zaidi hayo niliyoyasema mapya niliyoyapata.
 
Mungu alijua haya yatatokea? Au yalimshinda tu hakujua?

Alijua yatatokea na alitaka kutupa mitihani kidogo pia. Unajua kwanini Mungu alikuumba, ili umjue, umpende, umwabudu na mwisho uweze kufika kwake mbinguni. Na hata wazazi wetu walipokosa alimtuma mwanae ili awe kafara juu ya upatanishi wetu.
 
uzushi wa jamaa ni huu kwa ufupi
mungu(sijui ni yupi) hakuumba vitu vifuatavyo
1mungu(hakujiumba)
2kifo
3maradhi
4njaa/vita
5giza

jamaa anaelim yake sijui katoa wapi anajua yy.. nmemwambia hapo juu akjipange, maana amekariri, hajui kuwa kabla ya dunia hii haijaumbwa Mungu alikwisha umba galaxies 99, na ya kwetu ni ya mia..

Dinarsoess na wenzie, other galaxes au anafikiri dunia ndo sayari pekee kwenye universe? aniPM ili nimkaribishe aone kwenye telescope yangu aina ya anga ambaozo watu hawazijui. Ila awe tayari kunilipa angalao 500 us $
 
Alijua yatatokea na alitaka kutupa mitihani kidogo pia. Unajua kwanini Mungu alikuumba, ili umjue, umpende, umwabudu na mwisho uweze kufika kwake mbinguni. Na hata wazazi wetu walipokosa alimtuma mwanae ili awe kafara juu ya upatanishi wetu.
Kwa nini mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote atake kutupa mtihani?

Kama anajua yote, si hata kabla ya kutupa mtihani atakuwa kashajua matokeo, sasa point ya kutupa mtihani ni nini?

Kwa nini mungu muweza vyote na mjuzi wa yote atake kuabudiwa? Asipoabudiwa atapungukiwa nini?

Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
 
Huu ni uongo mwingine kwamba kuna zaidi ya Mungu au afananaye na Mungu.
 
Kwa nini mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote atake kutupa mtihani?

Kama anajua yote, si hata kabla ya kutupa mtihani atakuwa kashajua matokeo, sasa point ya kutupa mtihani ni nini?

Kwa nini mungu muweza vyote na mjuzi wa yote atake kuabudiwa? Asipoabudiwa atapungukiwa nini?

Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Hata watoto wako nyumbani unawatimizia mahitaji yao yote lakini kama mzazi utapenda wakuheshimu na kukusikiliza. Na wale wanaokuheshimu watakachokuomba utawapa kwa moyo mmoja ila wale wakaidi hutawatenga kwakua ni wanao utahakikisha wana mahali pa kulala, chakula, n.k.
Mbona Yesu alipokuwa na wanafunzi wake aliwauliza kama wanafahamu yeye ni nani? Inamaana waliosma maandiko walijua kuwa Masiah anakuja.
Kitabu cha Isaya alisema kabisa ujio wa Yesu. Inamaana yalishajulikana.
 
Hujajibu maswali haya, unahubiri.

Kwa nini mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote atake kutupa mtihani?

Kama anajua yote, si hata kabla ya kutupa mtihani atakuwa kashajua matokeo, sasa point ya kutupa mtihani ni nini?

Kwa nini mungu muweza vyote na mjuzi wa yote atake kuabudiwa? Asipoabudiwa atapungukiwa nini?

Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom