Vitu sita ambavyo si viumbe vya Mungu

Vitu sita ambavyo si viumbe vya Mungu

VITU SITA AMBAVYO SI VIUMBE VYA MUNGU.

View attachment 331270

Tarehe Mar 2016 niliandika makala juu mahusiano kati Kiza, Mungu, Kifo, Vita, Njaa, na Maradhi. Makala ile ilizua mjadala mkubwa facebook na whatsapp nilipoiweka, na moja jambo kubwa lilotuvuruga ni uwezo na mamlaka ya Mungu katika uumbaji, na hasahasa ile nadharia ya kuwa MUNGU ni muumbaji wa viumbe vyote ilitumiwa sana na watu katika kuikosoa makala yangu.

Awali ya yote nakubali bila kigegezi chochote kuwa Mungu ni muumbaji wa viumbe vyote na ya kwamba ni Mola wa viumbe hivyo. Nakubali kuwa ulimwengu haukuzuka tu wenyewe katika tukio la lisilo ratibiwa. Bali yupo injinia wa Ulimwengu huu ambaye si mwingine bali ni MUNGU.

Misaahafu ya dini za Ibrahim, yaan uislamu, uyaudi na ukristo yote kwa pamoja bila kukhitililafiana inasema ulimwengu na vilivyomo ndani yake havikuzuka kwa bahati mbaya bali vimeumbwa na Mungu.

Kuna viumbe hai kama wanyama na mimea, lakini pia kuna viumbe ambavyo havina uhai kama mawe na mchanga. Vyote hivi Muumbaji wake ni Mungu.

"Mwenyezi Mungu ameumba mbingu na ardhi kwa Haki. Kwa hakika katika hayo ipo Ishara kwa Waumini. " Quran 29:44

"...Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Na Yeye ni Mmoja Mwenye kushinda!..." Quran 13:16

"Mbingu ni mali yako, nchi nayo ni mali yako, Ulimwengu na vyote viujazavyo Ndiwe uliyeupiga msingi wake. Kaskazini na kusini ndiwe uliyeziumba....." Zaburi 89:11-12

Hiyo quran 13:16 inatutanabaisha kuwa Mungu ameumba kila kitu, lakini tujiulize, kitu kilichoumbwa na Mungu kinaitwaje? Kwa vyovyote vile kinaitwa kiumbe. Kama ndivyo tunaweza kuwa sahihi zaidi kama tukisema kuwa Mungu ameumba viumbe vyote badala ya kusema kuwa Mungu ameumba kila kitu.

Twasema kuwa viumbe vyote vimeumbwa na Mungu, je vile ambavyo si viumbe tuna vizungumziaje? Naomba mjue Mungu ameumba viumbe vyote, lakini haimaanishi kuwa ameumba kila kitu. Kuna baadhi ya vitu ambavyo Mungu hakuviumba aidha hakutaka kuviumba au ameshindwa kuviumba.

VITU VIKUU SITA AMBAVYO MUNGU HAKUVIUMBA.

1. MUNGU
Ukisoma misahafu yote mikuu miwili quran na biblia hakuna ushahidi hata mmoja unaonesha kuwa Mungu kaumba Mungu(namaanisha Mungu kujiumba).

Kubwa zaidi katika misahafu hiyo ambayo imeandikwa kwa matakwa yake MUNGU, inaonesha ukuu wa Mungu, uwezo wake, mamlaka yake, utukufu wake, usafi wake na kila aina ya sifa nzuri na tukufu, lakini hatuoni chanzo chake kikiandikwa humo na hatuoni mwisho wake ukiandikwa humo, zaidi ya vitabu hivyo kusema ufalme wa MUNGU na Nguvu zake hazina mwanzo wala mwisho.

"Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi" Ufunuo 1:8

"Na Mola wako Mlezi anayajua yaliyo ficha vifua vyao, na wanayo yatangaza. Naye ni Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye. Sifa zote njema ni zake Yeye, mwanzo na mwisho...." Quran 28:69-70

Kwa aya hizi, na mafundisho mengine ya kinabii kama haya, yanathibitisha bila shaka kuwa ni kweli kuna mambo au vitu ambavyo Mungu hakuviumba na kwasababu hiyo vitu hivyo haviwezi kuitwa viumbe na ingawa viko. Kitu cha kwanza MUNGU, kipo na hakija umbwa.

Wanaosema kuwa MUNGU ameumba kila kitu waje hapa watuambie "MUNGU" kaumbwa na nani? Wakishindwa kututajia basi waishie kusema Mungu kaumba viumbe vyote lakini si vitu vyote.

2. KIZA
Ukisoma hiyo quran 28:69-70 na ukisoma vizuri ufunuo 1:8 utagundua mambo yote na habari zote kabla ya uwepo wa MUNGU hayajulikani na huenda anayajua Mungu mwenyewe, lakini kwetu sisi tunaona mambo hayo kwetu ni KIZA.

Kwa hivyo tunaweza kusema kabla ya Mungu hajaumba chochote alikuwako yeye na Kiza, Kiza ni mwanamke na Mungu ni mwanaume. Kwakuwa kwa kipindi hicho walikuwa wenyewe, na wanajuana wenyewe, jambo jepesi twaweza kusema hivi vitu ni ndugu. Ipo siku inshallah nitakuja kufafanua kwanini nasema Kiza mwanamke na Mungu mwanaume.

"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. 3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. 4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza."
Mwanzo 1:1-4

Katika andika hilo la juu tunajifunza yafuatayo.

A. Mbingu na nchi zimeumbwa na Mungu. Maji, ardhi na vitu vya kufananayo ni sehemu ya mbingu ya nchi.

B. Mungu aliumba NURU lakini hakuumba KIZA, tunaambiwa tu Kiza kilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji lakini hatuambiwi Mungu aliumba Kiza.
Hiyo mwanzo 1:3 "Mungu akasema, iwe Nuru; ikawa Nuru"

Alijuaje kuwa Nuru imekuwa kama kabla ya Nuru hiyo kulikuwa hakuna Kiza? Je, mbona hatuoni maandiko yakionesha Mungu akisema iwe Kiza kisha kikawa Kiza?

C. Ukisoma mwanzo 1:2 tunaona Mungu akiumba mbingu na nchi kisha Kiza alikaa juu ya uso wa vilindi vya maji, kwasababu hiyo, nikisema kuwa Kiza alikuwako kabla ya mbingu na nchi nitakosea? Kama alikuwako kabla ya mbigu na nchi, ama kabla ya ulimwengu, nikisema kuwa Kiza na Mungu waliishi wenyewe kabla ya ulimwengu pia nitakosea?

D. Baada ya Mungu kuumba Nuru, hapo ndipo alipofanikiwa, kumfungia KIZA, na athari za Kiza akaziita USIKU na athari za NURU akaziita MCHANA. Kwahivyo Mungu hakumuumba KIZA, ila Mungu kaumba Nuru, Mchana, na Usiku.

Kwahivyo kama tuko pamoja, utakubaliana na mimi kuwa KIZA ni moja ya kitu ambacho Mungu hakukiumba. KIZA si kiumbe, KIZA kimezuka tu kama alivyozuka Mungu mwenyewe. Tafauti kubwa kati ya MUNGU na KIZA ni kuwa Mungu kaumba na ni Mola wa viumbe vyote, lakini Kiza hakuumba kitu chochote kwa hivyo si MUUMBAJI.

Astronomy inatuambia kuwa ulimwemgu umeundwa na vitu vikuu vitatu, normal matter, dark matter na dark energy. Normal matter ndio hujumuisha zile atoms zilizo tumika kuumba Nyota,sayari, na vitu vingine.

Normal matter ni asilimia 5 tu ya ulimwengu wote, 25% ni dark energy na 70% dark matter. Hiyo dark energy na dark matter athari zake zinaonekana katika zenyewe hazionekane. Hii huenda ndio KIZA ambacho kimetajwa katika mwanzo 1:1

Astronomy pia yatuambia ulimwengu unatanuka kwa kasi, na ya kwamba unazidi kuongezeka kutokana ile motion iliyosababishwa na BING BANG, kutanuka kwake ina maanisha unazidi kumeza au ama kuingia katika sehemu mbele zaidi kutokea kule ulipo anzia(kipind cha dark age) Swali kule unapoelekea kuna nini kama si Kiza??

Astronomy pia yatuambia hakuna empty space, kama inavyo onekana, katika space waweza kuona ama kudhani hakuna maada yoyote, lakini kimsingi asilimia kubwa ya space ina dark energy na dark matter. Vitu hivi vinaashiria uwepo KIZA mbali na ulimwengu tunao ujua.

3. KIFO
Kwanza naomba tukumbuke wakati Mungu anafikiria kuumba ulimwengu tayari kulikuwako na KIZA. Ili Mungu awe kuumba ulimwengu ilikuwa lazima kwanza amuondoshe au amuue KIZA. Ili Kiza kiweze kufa shuruti pawe na "KIFO" Hata hivyo, kutokana na nguvu za Kiza, basi kikawa hakijakufa bali kilifungiwa.(Rejea mwanzo 1:3 Mungu akatenga giza na nuru)

Pili naomba mjue kuwa kiumbe hai cha kwanza kuumbwa na Mungu ni "NENO" kisha wakafuatia malaika wakubwa wanne(four Arc Angels) ambao ni Mikaeli, Raphaeli, Rucifer na Gabrieli. Hoja inakuja, Mungu alitumia kipimo gani kujua kwamba amefanikiwa kuumba kiumbe hai? Kwa vyovyote vile ili ajue kuwa amefanikiwa kuumba kiumbe hai ni lazima alinganishe uhai uliopo ndani ya kiumbe hai na mauti(KIFO). Kwa hivyo kilianza KIFO kabla ya UHAI, na bahati nzuri maandiko yanakubali kuwa Mungu kaumba uhai, lakini hayaoneshi kuwa Mungu kaumba KIFO.

Wachungaji wetu katika makanisa wanakataa katakata kuwa Mungu kaumba KIFO, wao wanasema KIFO kilisababishwa na shetani, bi maana shetani ndio kaumba KIFO. Huku ni kutokujua, lakini hakuna aliyeumba KIFO, KIFO sio kiumbe na alizuka tu kama alivyo zuka Mungu.

Kama nilivyosema ule muda Mungu anafikiria kuumba uhai, tayari kifo kilikuwako, na kwasababu hiyo, pia haijulikani kati ya Mungu na Kifo na mkubwa(kiumri).

Mungu aliumba uhai, na kwa kupitia huo uhai akaumba mwanadamu, lengo lake lilikuwa mwanadamu aishi milele, lakini kifo kikawa kikwazo katika lengo hili.

Sivyo tu, kwakuwa siku zote KIZA anataka atoke kifungoni, hivyo kila siku anapambana na Mungu kwa lengo la kutaka kumuua, na wakati huohuo Mungu naye anataka kumuua KIZA, mshindi wa pambano hili lazima amtumie "KIFO" na hapa ndipo tunapoona nafasi ya KIFO katika mahusiano ya NURU na KIZA.

Lakini Mungu anasema atakuja kumshinda KIZA na KIFO, na pindi atakapo shinda hakuna roho au mwili utakao kufa.

"na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. " Ufunuo 1:18

4. VITA na NJAA
KIZA baada ya kugundua Mungu ameumba malaika wakubwa wanne, KIZA alichukia na hapo yakazuka mapambano kati ya MUNGU na KIZA. Kwa mapambano hayo ndipo ilipozuka "VITA" mungu alichofanikiwa ni kumfungia KIZA, na funguo zake akakabidhiwa Rucifer. Mark of Darkness ndio Funguo na sehemu alofungiwa KIZA, chapa hii baadae iliitwa mark of cain.

Mnyama wa kwanza kuumbwa na Mungu kabla hata ya wanadamu ni Levithans, hawa ndio ile mijusi mikubwa na Magodizilla. hawa walikuwa na "NJAA" sana kiasi walane wenyewe kwa wenyewe, Hapa Mungu kwa kutumia jeshi lake la malaika waliwaondoa dunia na kuwafungua Purgatory. Hapa pia VITA alihitajika kufanikisha hili.

Tembo na vufaru wanapungua kwa kuuliwa na binadamu, hivi Magodizilla na Levithans waliuliwa na nani? Ikiwa wao walikuwako miaka mingi kabla ya wanadamu? Jibu jepesi ni upanga wa Malaika Mikael na jeshi lakd.

Wakati hayo yakitokea, Darkness akaigeuza ile mark kuwa laana, na laana ile ikasababisha hali ya uasi kwa mtunza funguo. Wakati Mungu anamuumba mwanadamu, na malaika kuambiwa wamsujudie, Rucifer akiwa kesha athiriwa na laana ya funguo akagoma kumsujidia adamu.

Kwa mara nyingine "VITA" ilihitajika katika kumdhibiti Rucifer na kundi lake.

6 MARADHI
Mungu hakuumba maradhi, na wala si lengo mungu mwanadamu aumwe na kuteseka kwa maradhi. Ila pale mwanadamu alipoumbwa na afya bora kabisa, na maradhi yakazuka hapo hapo. Baada ya Mungu kuja kumshinda KIFO, pia atakuja kuyashinda MARADHI, na hayo yakitokea katika maisha Paradiso hakutakuwa na KIFO wala MARADHI.

MWISHO.
Makala hii haina tafauti na ya juzi, ila leo baadhi ya nukta nimemua kuziongelea kwa undani zaidi ili iweze kujibu maswali na hoja zilizo jitokeza katika makala ya msingi. Hata hivyo najua siwezi kumaliza kila kitu hapa, ila mengine tutajifunza katika mjadala!

Njano5
0622845394
Kama Post hii imetoka katika kichwa chako basi unacho kichwa kizuri na hazina kubwa ambayo ni ya kuitunza, vinginevyo acha kabisa kwasababu hayo ni mafundisho ya mapepo. Bwana Mungu alijua kuwa kutatokea mawazo kama haya ndio maana akasema kuwa yeye ameumba vitu vinavyoonekana na vile visivyoonekana, akasema pia yeye anajua na anaweza yote, akaongeza kuwa usikubali mafundisho ya wanikolai (hawa watu walijihusisha na mafundisho ya unajimu), akakutahadharisha kuwa pia unaye adui ambaye humwoni kwa macho ambaye anaitwa Shetani, mwishoni akasema mauti na kuzimu zitatupwa katika lile ziwa liwakalo moto kwa kibiriti.
Chanzo cha Mungu anakijua yeye mwenyewe kama ilivyo anavyojua kuwa wewe ulikuwa wapi kabla ya kuja duniani. Akili ya mwanadamu ipo limited yaani ni ya kiasi chake tu kwahiyo kwa namna yeyote ile hawez kujibu maswali mengi sana yanayomsibu.

Kuna msemo unasema: Mwisho wa kufikiri wa mwanadamu ndio mwanzo wa maajabu ya Mungu.
kwasasa ni hayo tu!!!!!!!
 
mkuu asante kwa majib japo umetumia maelezo marefu sana, jambo 1 ambalo tunapaswa kufahamu kuwa dunia na watu wote wakaao duniani wanauwezo ambao Mungu ameruhusu kuwa nao,

ikiwa uwezo wa akili hii ya dhambi, hauwezi kujua jema na baya je unaweza kuchunguza akili ya Mungu?

kwa mjib wa biblia shetani alitupwa humu duniani baada ya vita mbingun, na kabla ya kuja duniani alipita kwenye galaxies zingine ila alikataliwa ndipo alifanikiwa. kuwadanganya wazazi wetu,

hvyo uumbaji wa mungu haukuamzia kwetu ila mbali zaidi.. narudia Mungu aliumba giza, swali dogo nikuulize je Mungu alimuuba shetani au laa? jib lako litasaidia kujua hyo dhana ya uumbaji ya Mungu.
Nipe andiko lolote linalothibitisha kauli yako kwamba... shetani alipotupwa kuyoka mbinguni alipitia katika galaxies nyingine lakini alikataliwa akaja duniani.. Kisha thibitisha kwamba mbinguni ni wapi exactly
 
Unaelewa kwamba kila kilichopo kuwa na muumba si lazima muumba awe Mungu?

Unaelewa kwamba ukisema kila kilichopo ni lazima kina muumba, hapo ujesema Mungu hawezi kuwepo, kwa sababu na yeye atahitaji muumba, na akiwa na muumba si Mungu tena?
iko hivi mkuu kwa mifano kadha wa kadha niliyotoa ni wazi kuwa kila kitu kimeumbwa hakijajitokeza tu chenyewe,sasa okay say nikubaliane na wewe mkuu Kiranga kwamba sawa kila kitu kina muumba ila sio lazima awe Mungu,then atakuwa nani muumba wa vitu vyote ?

Mungu unamdefine vipi mkuu? hivi kwamba the fact that ni lazima awe na muumba na kwamba kuwa kwake na muumba that means si Mungu tena? Definition yako ya Mungu ni nini?
 
Kama kila kilicho complex kimeumbwa, hilo kinamaanisha unayemuita Mungu naye kaumbwa.

Na kama kaumbwa, basi si Mungu.

Unakubali?
mkuu point kubwa kwanza ni kujua na kukubali kwamba kila kitu kimeumbwa na kiumbe chenye nguvu nyingi na akili nyingi sana kuzipitia hizi akili zetu duni za kibinadamu,

kuna kiumbe ambacho kina uwezo mkubwa sana kuweza kututokeza sisi wenye akili za kutengeza complicated machines like hizo ndege,submarines,na vingine vingi

Mungu katoka wapi hilo ni swala jengine mkuu
 
Nanukuu

hapa ndipo nilipokuambia kua hujapamaliza

Unajuaje kua hayo maandishi ni matakatifu na yamesema ukweli?? Ulitumia vigezo gani kuhotimisha kua hicho ni kitabu kitakatifu na nimaneno ya mungu??

Unahakika gani kua hicho kitabu ni kitabu cha mungu na siyo projects za watu ili kushika watu kama nyinyi??
mkuu kuhusu mahala unaposema sijamaliza sijapaona mkuu,maneno yangu uliyobold yako very clear,kwa nini nasema vile the fact that wewe huiamini bibilia kuwa kitabu cha kweli hilo sio tatizo langu mkuu.

unajuaje kama hizo facts ulizofundishwa huko chuoni sijui wapi za kuhoji utakatifu au uhakika wa biblia ni maneno sahihi na yenye uhakika?

una uhakika gani kuwa hayo maneno uliyoaminishwa ya kuhoji uhakika na ukweli wa biblia sio projects za kuwaangamiza watu kama ninyi?

unaniambia nitumie circular logic?ni nini hicho?umekitoa wapi?nani alikufundisha?una uhakika gani na chanzo cha hizo cicular logic zako? nini kimekupa uhakika wa Kamba chanzo cha hayo mafundisho yako ya cilrcular logic ni sawia na hayapo kwa ajili ya kuwapotosha watu kama ninyi?
 
na ishu kubwa hapa sio kuamini, kwasababu imani ingekua njia pekee ya kujua ukweli wa jambo basi kila kitu kingekua sahihi as long as kuna imani

Hapa tunahoji kujua ukweli kupitia uthibitisho, sasa tuambie wewe ulijuaje kua biblia imesema ukweli katika habari ya maria kuzaa bila kuingiliwa?? Unauthibitisho gani kua kitabu hicho ni cha mungu na sio projects za watu tu??

unajuaje kama hizo facts ulizofundishwa huko chuoni sijui wapi za kuhoji utakatifu au uhakika wa biblia ni maneno sahihi na yenye uhakika?
kwanza "utakatifu" unaupima kupitia vigezo gani??

Pili ishu ya kujua uongo wa kitu wala haihitaji elimu ya chuoni, naweza kujua uongo kwa njia nyingi ikiwemo kujipinga kwa hilo jambo. Ukisema wewe umemzidi umri baba yako, je hiyo itshitaji elimu ya chuo kugundua kua ni uongo??

una uhakika gani kuwa hayo maneno uliyoaminishwa ya kuhoji uhakika na ukweli wa biblia sio projects za kuwaangamiza watu kama ninyi?
Maneno gani niliyoaminishwa??

Hapa unavurunda, mimi sijihusishi na imani mzee

Halafu sijafundishwa kukataa kitu eti ila nimejifunza kuhoji kitu kwa kupewa uthibitisho niweze kujua kwa hakika.

Kwaiyo wewe utakubali kila kitu unachoambiwa kua ni sahihi kwasababu kila utachoambiwa kwako kitakua ni sahihi??

unaniambia nitumie circular logic?ni nini hicho?umekitoa wapi?nani alikufundisha?una uhakika gani na chanzo cha hizo cicular logic zako? nini kimekupa uhakika wa Kamba chanzo cha hayo mafundisho yako ya cilrcular logic ni sawia na hayapo kwa ajili ya kuwapotosha watu kama ninyi?
Circular logic utaiona hapa hapa ukijibu swali hili

Unahakika gani kua kilichoandikwa kwenye biblia ni kweli??
 
Mungu hayupo, ni hadithi ya kufikirika tu. Kama unadai yupo, thibitisha.
Mungu hayupo, ni hadithi ya kufikirika tu. Kama unadai yupo, thibitisha.

Kiranga: Je, ikiwa Mungu yupo na kwa bahati mbaya huyu uliyemuomba akuthibitishie kuwa yupo, akawa hawezi kuthibitisha kuwa yupo, je kushindwa kwake kuthibitisha juu ya uwepo wa Mungu kunamfanya Mungu asiwepo? Mfano mwingine. Mimi hapa nilipo kabisa sijawahi kufika Ulaya au hata Rwanda tu, ila NAAMINI kuwa Ulaya ipo na Rwanda ipo, na Rais wake ni Mh. Paul Kagame. Still, mimi mwenyewe ukinitaka nikuthibitishie kuwa Rwanda ipo au Ulaya, siwezi, ila naamini kuwa Dola hizi zipo hapa duniani. Je, kushindwa kwangu kuthibitisha kuwa Rwanda au Ulaya vipo, kunazifanya dola hizi zisiwepo wakati ukweli ni kwamba zipo? Ni nini basi kinachopelekea niseme kuwa Rwanda ipo? Ni kitu kinachoitwa authoritative knowledge. Waliosoma ualimu, yaani Professional Teachers, wamesoma kitu hiki kwenye ualimu kwenye kozi inaitwa Philosophy of Education, kwamba mojawapo ya sources of knowledge, ni authoritative knowledge. Sasa wewe ndugu yangu Kiranga, unataka kila kitu kitokane na Emperical Knowledge. Ni mzuri sana kwenye argument isipokuwa kuna vitu fulani fulani vya msingi ambavyo bado una gapes, tena gapes za msingi. Wewe ukijitahidi ukarudi kusoma degree nyingine kama ya ualimu hivi, you can make among the most knowlegaeable people in the world. Siyo Tanzania au Africa, hapana utakuwa kati ya watu wazuri sana duniani!
 
Mwanadamu amechota siri chache sana kuhusu Uumbaji.... hizi amechota kutoka kwa Malaika aliyeasi yaani Ibilisi - Kwa kutumia siri hizo chache ndipo mwanadamu alijifunza namna ya kutenganisha Nafsi na Mwili pia akajifunza namna ya kuita Kudra bila kufuata HAKI yaani Kuroga nk

Kwa wale walikwenda KUZIMU wanajua namna ufalme wa Ibilisi ulivyo na nguvu kule, ila nguvu zile hazifui dafu kwa Nguvu za Mungu yaani nguvu za HAKI.
 
na ishu kubwa hapa sio kuamini, kwasababu imani ingekua njia pekee ya kujua ukweli wa jambo basi kila kitu kingekua sahihi as long as kuna imani

Hapa tunahoji kujua ukweli kupitia uthibitisho, sasa tuambie wewe ulijuaje kua biblia imesema ukweli katika habari ya maria kuzaa bila kuingiliwa?? Unauthibitisho gani kua kitabu hicho ni cha mungu na sio projects za watu tu??

kwanza "utakatifu" unaupima kupitia vigezo gani??

Pili ishu ya kujua uongo wa kitu wala haihitaji elimu ya chuoni, naweza kujua uongo kwa njia nyingi ikiwemo kujipinga kwa hilo jambo. Ukisema wewe umemzidi umri baba yako, je hiyo itshitaji elimu ya chuo kugundua kua ni uongo??

Maneno gani niliyoaminishwa??

Hapa unavurunda, mimi sijihusishi na imani mzee

Halafu sijafundishwa kukataa kitu eti ila nimejifunza kuhoji kitu kwa kupewa uthibitisho niweze kujua kwa hakika.

Kwaiyo wewe utakubali kila kitu unachoambiwa kua ni sahihi kwasababu kila utachoambiwa kwako kitakua ni sahihi??

Circular logic utaiona hapa hapa ukijibu swali hili

Unahakika gani kua kilichoandikwa kwenye biblia ni kweli
??
nilipobold sehemu ya kwanza ulijuaje kuwa biblia inasema uwongo? ni uthibitisho gani ulionao kuwa bilbilia inasema uwongo kuhushu habari ya kuzaa kwa maria bila kuingiliwa? una uthibitisho gani kuwa biblia si kitabu cha Mungu ila projects za watu tu?

wewe unaupimaje utakatifu?

maneno unayokuja kuniuliza hapo ndo hayo uliyoaminishwa yanayofanya upate sababu za kuhoji ukweli sijui uhakika and so on

unajihusisha na nini mkuu, nini maana ya Imani?

okay hujafundishwa sawa kabisa ila umejifunza kuhoji kitu kupewa uthibitisho uweze kujua kwa hakika,sawa niambie umejifunza kuptitia nini? una uhakika gani kuwa hicho chanzo unachojifunzia wewe ni cha kweli?nipe uthibitisho wa kwamba chanzo chako cha maarifa ni cha kweli na cha kuaminika

apo kwenye maneno niliyoweka rangi nyekundu,narudia tena kama nilivyokuambia hapo awali,siamini kila kitu,naamini kitu ikitegemeana na chanzo chake ningekua wa kuamini kila kitu ningekuwa nishakubaliana na hoja zako za kuhoji uhakika na ukweli wa biblia

wewe uone majibu yangu yana hizo circular logic au lah hilo ni tatizo lako,najibu kulingana na kile kinacholeta logic kwa akili ya kawaida kabisa ya binadamu ,maana sina uhakika na chanzo chako ulichojifunzia hizo issue zako za circular logic mkuu
 
nilipobold sehemu ya kwanza ulijuaje kuwa biblia inasema uwongo? ni uthibitisho gani ulionao kuwa bilbilia inasema uwongo kuhushu habari ya kuzaa kwa maria bila kuingiliwa? una uthibitisho gani kuwa biblia si kitabu cha Mungu ila projects za watu tu?
Kabla ya yakuangaika kujua usahihi wa hiyo habari kwanza unatakiwa uwe umekwisha jua usahihi wa hicho kitabu kilicho andika hizo habari. Ikiwa kama hujaweza kupata jibu la uhakika kuthibitisha kama ni kitabu cha kweli basi kuhoji kwako kuhusu habari zilizo ndani yake kutakua hakuna mashiko

Je kitabu hicho unahakika gani kua cha mungu?? Thibitisha kwanza hili kwasababu jibu utalopata hapa litathibitisha hiyo habari kirahisi tu. Sasa wewe hujathibitisha kua hicho ni kitabu cha mungu achilia mbali kuthibitisha mungu mwenyewe kama yupo unarukia kutaka kujua ukweli wa hiyo habari

Nikikupa kitabu cha Spiderman usome utakubali kua habari zilizo ndani yake ni za kweli kwasababu kimeandikwa??

wewe unaupimaje utakatifu?

maneno unayokuja kuniuliza hapo ndo hayo uliyoaminishwa yanayofanya upate sababu za kuhoji ukweli sijui uhakika and so on
hujaeleza utakatifu maana yake ni nini na ili jambo liwe talatifu linatakiwa liwe na nini.

unajihusisha na nini mkuu, nini maana ya Imani?
niambie wewe unaye dili na mambo ya imani kwako neno imani unalielewaje??

okay hujafundishwa sawa kabisa ila umejifunza kuhoji kitu kupewa uthibitisho uweze kujua kwa hakika,sawa niambie umejifunza kuptitia nini?
Kwanza sijafunzwa bali nimejifunza, kwaiyo hili ni jambo binafsi bila kuhusisha mtu mwingine

Nimejifunza kuhoji kwasababu kuna uongo ambao unaweza kufichwa kwa sura ya ukweli hivyo pasipo kuhoji huwezi kujua. Hii ni sawa na kuuziwa simu ambayo ni clone ukiangalia inamuonekano kama simu halisi yani original lakini kwa ndani ni fake. Anayependa kuhoji na kudadisi mambo hawezi kuuziwa hii simu ila kwa wewe ambaye huwezi kuoji kwasababu kila utakachokiona kwako ni sahihi basi uko katika asilimia kubwa ya kuuziwa gaka.

una uhakika gani kuwa hicho chanzo unachojifunzia wewe ni cha kweli?nipe uthibitisho wa kwamba chanzo chako cha maarifa ni cha kweli na cha kuaminika
Chanzo cha maarifa ni ubongo, ila tatizo linakuja kwenye utumiaji. Wewe unatumia ubongo wako kukubali kila kitu uanchoambiwa wakati mimi nautumia kuhoji ili kujua vitu kwa hakika.

Nakuuliza swali, nikikupa kitabu kilichoandika habari za mtu aitwae pazi kua alibebwa kichwa chini miguu juu na jogoo utakubali kua habari hiyo ni ya kweli na ilishawahi kutokea?? utatumia vigezo gani kupima kua sio kweli au ni kweli???

apo kwenye maneno niliyoweka rangi nyekundu,narudia tena kama nilivyokuambia hapo awali,siamini kila kitu,naamini kitu ikitegemeana na chanzo chake ningekua wa kuamini kila kitu ningekuwa nishakubaliana na hoja zako za kuhoji uhakika na ukweli wa biblia
ishu ya imani hua haina mipaka, unaweza kuamini chochote kile as long as huna ushahidi. Ukiweka mipaka inakua sio imani tena hapo unakua umevuka boda

Kwaiyo kusema kwako kua huamini chochote kile hapo unatengeneza swali kua unatumia vigezo gani kukataa imani zingine??

Ukisema unaamini biblia na imani yako ni sahihi nitakuuliza usahihi wa imani yako umeujuaje?? Umejuaje kua biblia imeandika habari za kweli na si uongo??

wewe uone majibu yangu yana hizo circular logic au lah hilo ni tatizo lako,najibu kulingana na kile kinacholeta logic kwa akili ya kawaida kabisa ya binadamu ,maana sina uhakika na chanzo chako ulichojifunzia hizo issue zako za circular logic mkuu
tatizo swali la maana hujibu

Umejenga hoja huku ukizungumzia ukweli wa habari zilizo ndani ya biblia, nimekuuliza unajuaje kua kitabu hicho kimeandika habari za kweli? hujajibu
 
Kabla ya yakuangaika kujua usahihi wa hiyo habari kwanza unatakiwa uwe umekwisha jua usahihi wa hicho kitabu kilicho andika hizo habari. Ikiwa kama hujaweza kupata jibu la uhakika kuthibitisha kama ni kitabu cha kweli basi kuhoji kwako kuhusu habari zilizo ndani yake kutakua hakuna mashiko

Je kitabu hicho unahakika gani kua cha mungu?? Thibitisha kwanza hili kwasababu jibu utalopata hapa litathibitisha hiyo habari kirahisi tu. Sasa wewe hujathibitisha kua hicho ni kitabu cha mungu achilia mbali kuthibitisha mungu mwenyewe kama yupo unarukia kutaka kujua ukweli wa hiyo habari

Nikikupa kitabu cha Spiderman usome utakubali kua habari zilizo ndani yake ni za kweli kwasababu kimeandikwa??

hujaeleza utakatifu maana yake ni nini na ili jambo liwe talatifu linatakiwa liwe na nini.

niambie wewe unaye dili na mambo ya imani kwako neno imani unalielewaje??

Kwanza sijafunzwa bali nimejifunza, kwaiyo hili ni jambo binafsi bila kuhusisha mtu mwingine

Nimejifunza kuhoji kwasababu kuna uongo ambao unaweza kufichwa kwa sura ya ukweli hivyo pasipo kuhoji huwezi kujua. Hii ni sawa na kuuziwa simu ambayo ni clone ukiangalia inamuonekano kama simu halisi yani original lakini kwa ndani ni fake. Anayependa kuhoji na kudadisi mambo hawezi kuuziwa hii simu ila kwa wewe ambaye huwezi kuoji kwasababu kila utakachokiona kwako ni sahihi basi uko katika asilimia kubwa ya kuuziwa gaka.

Chanzo cha maarifa ni ubongo, ila tatizo linakuja kwenye utumiaji. Wewe unatumia ubongo wako kukubali kila kitu uanchoambiwa wakati mimi nautumia kuhoji ili kujua vitu kwa hakika.

Nakuuliza swali, nikikupa kitabu kilichoandika habari za mtu aitwae pazi kua alibebwa kichwa chini miguu juu na jogoo utakubali kua habari hiyo ni ya kweli na ilishawahi kutokea?? utatumia vigezo gani kupima kua sio kweli au ni kweli???

ishu ya imani hua haina mipaka, unaweza kuamini chochote kile as long as huna ushahidi. Ukiweka mipaka inakua sio imani tena hapo unakua umevuka boda

Kwaiyo kusema kwako kua huamini chochote kile hapo unatengeneza swali kua unatumia vigezo gani kukataa imani zingine??

Ukisema unaamini biblia na imani yako ni sahihi nitakuuliza usahihi wa imani yako umeujuaje?? Umejuaje kua biblia imeandika habari za kweli na si uongo??

tatizo swali la maana hujibu

Umejenga hoja huku ukizungumzia ukweli wa habari zilizo ndani ya biblia, nimekuuliza unajuaje kua kitabu hicho kimeandika habari za kweli? hujajibu
Endelea na mtazamo wako ndugu
 
Ulianza vizuri kunukuu misahafu yote Agano la kale na injili na Qur'an Kareem, ila huko mbele ukagundua kwamba kuna vitabu Ni fiction ukajikuta unakwama na kuamua kubase kwenye fiction ukaacha original scripture Qur'an na kuharibu kila ulilokua ukisimamia.

Mfano.
Qur'an inasema Lucifer sio malaika bali alikua kwenye kundi la majini Surat Baqara 186.

KIFO
Qur'an inasema Qul nafsi dhaikal tul maut, atazungumziaje kifo wakati hakikua kwenye mpango wake?

MARADHI
Qur'an Ayubu aleyh Salaam aliruhusiwa kujaribiwa na shetani kwa maradhi hivyo maradhi Ni moja kati ya mtihani kwa mwanadamu Kama jaribu dhidi ya Imani take juu ya muumba wake.

VITA NA NJAA
Hapa nimeshindwa kuelewa kwamba uliandika sana kiasi point zikaisha ukaamua kutuchomekea ma vitu yako.
 
Kabla ya yakuangaika kujua usahihi wa hiyo habari kwanza unatakiwa uwe umekwisha jua usahihi wa hicho kitabu kilicho andika hizo habari. Ikiwa kama hujaweza kupata jibu la uhakika kuthibitisha kama ni kitabu cha kweli basi kuhoji kwako kuhusu habari zilizo ndani yake kutakua hakuna mashiko

Je kitabu hicho unahakika gani kua cha mungu?? Thibitisha kwanza hili kwasababu jibu utalopata hapa litathibitisha hiyo habari kirahisi tu. Sasa wewe hujathibitisha kua hicho ni kitabu cha mungu achilia mbali kuthibitisha mungu mwenyewe kama yupo unarukia kutaka kujua ukweli wa hiyo habari

Nikikupa kitabu cha Spiderman usome utakubali kua habari zilizo ndani yake ni za kweli kwasababu kimeandikwa??

hujaeleza utakatifu maana yake ni nini na ili jambo liwe talatifu linatakiwa liwe na nini.

niambie wewe unaye dili na mambo ya imani kwako neno imani unalielewaje??

Kwanza sijafunzwa bali nimejifunza, kwaiyo hili ni jambo binafsi bila kuhusisha mtu mwingine

Nimejifunza kuhoji kwasababu kuna uongo ambao unaweza kufichwa kwa sura ya ukweli hivyo pasipo kuhoji huwezi kujua. Hii ni sawa na kuuziwa simu ambayo ni clone ukiangalia inamuonekano kama simu halisi yani original lakini kwa ndani ni fake. Anayependa kuhoji na kudadisi mambo hawezi kuuziwa hii simu ila kwa wewe ambaye huwezi kuoji kwasababu kila utakachokiona kwako ni sahihi basi uko katika asilimia kubwa ya kuuziwa gaka.

Chanzo cha maarifa ni ubongo, ila tatizo linakuja kwenye utumiaji. Wewe unatumia ubongo wako kukubali kila kitu uanchoambiwa wakati mimi nautumia kuhoji ili kujua vitu kwa hakika.

Nakuuliza swali, nikikupa kitabu kilichoandika habari za mtu aitwae pazi kua alibebwa kichwa chini miguu juu na jogoo utakubali kua habari hiyo ni ya kweli na ilishawahi kutokea?? utatumia vigezo gani kupima kua sio kweli au ni kweli???

ishu ya imani hua haina mipaka, unaweza kuamini chochote kile as long as huna ushahidi. Ukiweka mipaka inakua sio imani tena hapo unakua umevuka boda

Kwaiyo kusema kwako kua huamini chochote kile hapo unatengeneza swali kua unatumia vigezo gani kukataa imani zingine??

Ukisema unaamini biblia na imani yako ni sahihi nitakuuliza usahihi wa imani yako umeujuaje?? Umejuaje kua biblia imeandika habari za kweli na si uongo??

tatizo swali la maana hujibu

Umejenga hoja huku ukizungumzia ukweli wa habari zilizo ndani ya biblia, nimekuuliza unajuaje kua kitabu hicho kimeandika habari za kweli? hujajibu

nilitaka nikujibu ila naona napoteza muda na nguvu zangu nyingi kujadiliana na mtu ambaye anayapa maarifa kwenye chanzo kisichoeleweka na kisicho na uhakika

sasa ni hivi suit yourself mkuu ,maanake nakuuliza maswali mengine hata hujibu unalazimisha tu kuniuliza maswali yako yasiyo na kichwa wala miguu,nimekuuliza Imani ni nini unanigeuzia swali,afu unasema hujihusishi na Imani wakati mpaka sasa na kwa maelezo yako ni kwamba una Imani au unaamini biblia sio kitabu cha Mungu (kazi kweli kweli) yet unadai hujihusishi na maswala ya Imani wakati hata maana ya Imani umeshindwa kuniambia maana yake

nasimamia nilichokisema hapo awali naamini kitu kutokana na chanzo chake,so hata mambo ambayo wewe umejifunza na ambayo unataka hata mimi nifikiri kama unvyofikiri kutokana na hayo maarifa yako sioni kama yana mantiki kwa sababu sijui kama chanzo chake ni cha uhakika na kinaaminika na hata wewe huna namna ya kuthibitsha hilo

hivyo hii ni conlucion yangu,save energy yako kwa ajili ya kuzidi kujipatia maarifa ya kuhoji uhakika na ukweli wa biblia,na mi nasave energy yangu ya kuzidi kujipatia maarifa na ujuzi kwenye kitabu kitakatifu,maandiko matakatifu ya Mungu biblia.
 
Kiranga: Je, ikiwa Mungu yupo na kwa bahati mbaya huyu uliyemuomba akuthibitishie kuwa yupo, akawa hawezi kuthibitisha kuwa yupo, je kushindwa kwake kuthibitisha juu ya uwepo wa Mungu kunamfanya Mungu asiwepo? Mfano mwingine. Mimi hapa nilipo kabisa sijawahi kufika Ulaya au hata Rwanda tu, ila NAAMINI kuwa Ulaya ipo na Rwanda ipo, na Rais wake ni Mh. Paul Kagame. Still, mimi mwenyewe ukinitaka nikuthibitishie kuwa Rwanda ipo au Ulaya, siwezi, ila naamini kuwa Dola hizi zipo hapa duniani. Je, kushindwa kwangu kuthibitisha kuwa Rwanda au Ulaya vipo, kunazifanya dola hizi zisiwepo wakati ukweli ni kwamba zipo? Ni nini basi kinachopelekea niseme kuwa Rwanda ipo? Ni kitu kinachoitwa authoritative knowledge. Waliosoma ualimu, yaani Professional Teachers, wamesoma kitu hiki kwenye ualimu kwenye kozi inaitwa Philosophy of Education, kwamba mojawapo ya sources of knowledge, ni authoritative knowledge. Sasa wewe ndugu yangu Kiranga, unataka kila kitu kitokane na Emperical Knowledge. Ni mzuri sana kwenye argument isipokuwa kuna vitu fulani fulani vya msingi ambavyo bado una gapes, tena gapes za msingi. Wewe ukijitahidi ukarudi kusoma degree nyingine kama ya ualimu hivi, you can make among the most knowlegaeable people in the world. Siyo Tanzania au Africa, hapana utakuwa kati ya watu wazuri sana duniani!
Sikatai uwepo wa Mungu kwa sababu tu watu hawawezi kuthibitisha uwepo wa Mungu.

Kwa sababu, kama unavyosema, inawezekana kitu kipo, halafu watu hawajui kukithibitisha tu.

Zaidi ya watu kushindwa kuthibitisha uwepo wa Mungu, habari za Mungu kuwepo zinajipinga zenyewe. Zina contradiction.

Kwa mfano.

Tunaambiwa Mungu ni mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.

Sasa imekuwaje Mungu huyo aumbe ulimwengu ambao mabaya, njaa, maafa, ujambazi, majanga ya kiasili etc yanaweza kutokea, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao hayo hayawezi kutokea?

This is a contradiction.

Ukisema nataka kila kitu kijulikane kwa empirical knowledge (basically using the senses), unakuwa hujaelewa kwamba pingamizi langu halijataka picha ya Mungu, halijataka fingerprints za Mungu, halijataka sauti ya Mungu, halijataka kumgusa Mungu, halijataka kumnusa Mungu.

Nimepinga kwa kutumia a logical contradiction, a philosophical abstract.

Sasa utasema vipi nataka empirical evidence?

Hili ni pingamizi dhidi yangu ambalo naona linajirudia. Watu hawaelewi kwamba "the problem of evil" is not about empirical evidence, it is about an inherent philosophical and logical contradiction.

Inaonekana unakosoa kitu ambacho hujakielewa, unafikiri nataka empirical evidence wakati naongelea logical contradiction.
 
nilitaka nikujibu ila naona napoteza muda na nguvu zangu nyingi kujadiliana na mtu ambaye anayapa maarifa kwenye chanzo kisichoeleweka na kisicho na uhakika
sio chanzo kisichoeleweka sema chanzo ambacho akili yako haijaweza kukielewa. Nimesisitiza hapo juu kua natumia ubongo kutafakari na kupima ukweli wa mambo

Sasa ni hivi suit yourself mkuu ,maanake nakuuliza maswali mengine hata hujibu unalazimisha tu kuniuliza maswali yako yasiyo na kichwa wala miguu,nimekuuliza Imani ni nini unanigeuzia swali,afu unasema hujihusishi na Imani
Hujajibiwa au akili yako haijaweza kuona jibu?? Nakupa nukuu ya post yangu hapo juu "ishu ya imani hua haina mipaka, unaweza kuamini chochote kile as long as huna ushahidi. Ukiweka mipaka inakua sio imani tena hapo unakua umevuka boda"

Nataka unipe maana ya imani kwa jinsi unavyoelewa wewe

Wakati mpaka sasa na kwa maelezo yako ni kwamba una Imani au unaamini biblia sio kitabu cha Mungu (kazi kweli kweli) yet unadai hujihusishi na maswala ya Imani wakati hata maana ya Imani umeshindwa kuniambia maana yake
Hivi mtu ambaye haamini biblia anakuaje tena katika kundi la waamini? Kwamba kipara nacho ni rangi ya nywele??

nasimamia nilichokisema hapo awali naamini kitu kutokana na chanzo chake
hapa tayari umeshasema mungu hayupo, kwasababu Ili umuamini huyo mungu atahitaji naye awe nachanzo chake.

so hata mambo ambayo wewe umejifunza na ambayo unataka hata mimi nifikiri kama unvyofikiri kutokana na hayo maarifa yako sioni kama yana mantiki kwa sababu sijui kama chanzo chake ni cha uhakika na kinaaminika na hata wewe huna namna ya kuthibitsha hilo

kama huoni mantiki ya kuwa na ubongo huwezi kuona hata mantiki ya hoja zangu

hivyo hii ni conlucion yangu,save energy yako kwa ajili ya kuzidi kujipatia maarifa ya kuhoji uhakika na ukweli wa biblia,na mi nasave energy yangu ya kuzidi kujipatia maarifa na ujuzi kwenye kitabu kitakatifu,maandiko matakatifu ya Mungu biblia.
Energy ulianza kupoteza tangu huko mwanzo kwa kukwepa maswali

Ulisema
au umewahi kusikia au kushuhudia tokea uzaliwe kwamba kuna mwanamke anaishi peke yake hana mume wala mpenzi ila kakaaa tu kisha baada ya muda kapata mimba,hajawahi kusex wala kuingiziwa mbegu za kiume ila ana mimba?
Nikakuiliza: inamaana zile habari zinazosema kuna mwanamke aitwae maria alizaa bila mwanaume nizauongo?? Hukujibu zaidi ukaendelea kupoteza energy kwa kukwepa maswali
 
uzushi wa jamaa ni huu kwa ufupi
mungu(sijui ni yupi) hakuumba vitu vifuatavyo
1mungu(hakujiumba)
2kifo
3maradhi
4njaa/vita
5giza

jamaa anaelim yake sijui katoa wapi anajua yy.. nmemwambia hapo juu akjipange, maana amekariri, hajui kuwa kabla ya dunia hii haijaumbwa Mungu alikwisha umba galaxies 99, na ya kwetu ni ya mia..
Umamtuhumu mleta Mada kuwa amekariri. Aya ebu wewe tuambie ni maandiko gani au ni wapi Mungu anaposema ameeumba hizo unazoita galaxy
 
Sikatai uwepo wa Mungu kwa sababu tu watu hawawezi kuthibitisha uwepo wa Mungu.

Kwa sababu, kama unavyosema, inawezekana kitu kipo, halafu watu hawajui kukithibitisha tu.

Zaidi ya watu kushindwa kuthibitisha uwepo wa Mungu, habari za Mungu kuwepo zinajipinga zenyewe. Zina contradiction.

Kwa mfano.

Tunaambiwa Mungu ni mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.

Sasa imekuwaje Mungu huyo aumbe ulimwengu ambao mabaya, njaa, maafa, ujambazi, majanga ya kiasili etc yanaweza kutokea, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao hayo hayawezi kutokea?

This is a contradiction.

Ukisema nataka kila kitu kijulikane kwa empirical knowledge (basically using the senses), unakuwa hujaelewa kwamba pingamizi langu halijataka picha ya Mungu, halijataka fingerprints za Mungu, halijataka sauti ya Mungu, halijataka kumgusa Mungu, halijataka kumnusa Mungu.

Nimepinga kwa kutumia a logical contradiction, a philosophical abstract.

Sasa utasema vipi nataka empirical evidence?

Hili ni pingamizi dhidi yangu ambalo naona linajirudia. Watu hawaelewi kwamba "the problem of evil" is not about empirical evidence, it is about an inherent philosophical and logical contradiction.

Inaonekana unakosoa kitu ambacho hujakielewa, unafikiri nataka empirical evidence wakati naongelea logical contradiction.

"Tunaambiwa Mungu ni mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote."

Unless na wewe ni mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, ndiyo unaweza ukawa kwenye nafasi ya kuhoji juu ya qualities hizo za Mungu, vinginevyo much far huwezi. Na kama basi hauko hivyo, hakuna namna ambayo unaweza ukajua ni wapi unakosea na wapi uko sahihi katika kutoa hoja zako juu yake. Zaidi ni kuwa Mungu ni Roho, hana mwili na haonekani kwa macho, na hivyo sikuwa namaanisha kuwa ulitaka athibitishwe kwako physically. Pamoja na hayo, kuna emperical evidence nyingi tu zinazoweza kuthibitisha kuwa Mungu yupo lakini zinakuwa ni za kiroho zaidi na ni unique experiences ambazo ukimdai mmoja azithibitishe kwako, inakuwa ni kazi ngumu kidogo unless na wewe uwe kwenye line sawa na yeye katika ulimwengu wa roho. Kwa hiyo mambo ya kiroho si ya kuibuka tu halafu unamwambia mtu akuthibitishie wakati hata hauko aligned naye kiroho au hauko kwenye imani moja naye. Kama wewe ni atheist au non believer, hakuna namna NZURI zaidi ambayo mtu ambaye anamwamini Mungu anaweza akamthibitisha Mungu kwako. Wanaomwamini Mungu wanatumia standards zao ambazo zinatokana na Maandiko Matakatifu, wewe usiyemwamini, hutumii hayo na wala haukubaliani nayo. Hii tayari ni discrepancy kubwa kabisa ambayo haiwezi kuwafanya arguments zenu zikaja kukubaliana mbele ya safari hata siku moja.

Mfano wa emperical evidence ambayo ni ya kiroho ni ndoto. Kuna watu wengi tu huwa wanaongea na Mungu kupitia kwenye ndoto au hata maono mengine yanayofanana na hayo. Sasa mtu kama huyu akikupa shuhuda zake juu ya uwepo wa Mungu, kwa mtu kama wewe ukimwambia kuwa anakudanganya utakuwa uko sahihi 100%, ila hata ukimkubalia pia utakuwa uko sahihi 100%.

Still, uelewa wangu wa siku nyingi tangu huko nyuma, nilikuwa najua kuwa wewe huamini kama Mungu yupo kwa sababu wanaomini kuwa yupo, hawajaweza kukuthibitishia hilo!

Mwisho, je kutokana na maelezo yako hapo juu, unataka sasa wanaomwamini Mungu wamthibitishije kwako? Watumie standards zipi, za kwao za kwako? Kumbuka kuwa hapa lazima standard mojawapo tu ndiyo inatakiwa itumike, ya kwako au ya kwao ila si zote mbili. Nauliza maswali haya kwa sababu leo nimegundua kuwa wanaomwamini Mungu wanao uwezo huo wa kukuthibitishia kuwa Mungu yupo isipokuwa tu walikuwa hawajawahi kulielewa swali lako la siku nyingi!

NB: Kumbuka pia kuwa hoja yangu kubwa hapa ni kwamba, arguments za uwepo wa Mungu kuwa illogical kwako, bado hakumfanyi Mungu asiwepo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom