Vitu sita ambavyo si viumbe vya Mungu

Vitu sita ambavyo si viumbe vya Mungu

Naweza kuwa nimekujibu, ila jibu hulielewi.

Ngoja nijaribu tena.

Nikikujibu kwamba, hakuna kilicho complex kinachotokea chenyewe, bila ya kuwekwa, kuumbwa, kusababisha na kingine.

Na hii ndiyo sababu Mungu hayupo.

Kwa sababu Mungu unayemsema ni complex, na kama na yeye ni complex, basi kwa kanuni yako ya "hakuna kilicho complex kinachoweza kuwapo bila ya kusababishwa na kingine", Mungu wako atahitaji kitu kingine kimsababishe, na akishahitaji kitu kingine tu kimsababishe uwepo wake, anakuwa si Mungu tena.

Kwa hivyo, kama hakuna kilicho complex ambacho kinatokea au kuwepo bila ya kusababushwa na kingine, basi kanuni hii inazuia Mungu kuwepo.

Unaelewa?
Mkuu Kiranga ndio maana mwanzo nilikuambia kama Mung hayupo maana yake ni kwamba hata wewe haupo

katika maana gani?

Nithibitishie uwepo wako mkuu

Nithibitishie uwepo wa nguvu zako

Nithibitishie uwepo wa akili yako

Nithibitishie uwepo wa pumzi inayokufanya uko hai mpaka sasa

hapo nilipobold kama ulinijbu kuwa hakuna kilicho complex kilichojitokeza chenyewe bila kuumbwa,kusababishwa na kingine ,naomba basi wewe uniambie vitu vyote ulimwenguni vilitoka wapi?nani msababishaji wake?
 
Mbona yesu mnasema alizaliwa bila mbegu za kiume je hii unaikubali??
Tunasema?Akina nani? kutokana na ujuzi wako Maria alipataje mimba bila kukutana na mwanaume?
 
VITU SITA AMBAVYO SI VIUMBE VYA MUNGU.

View attachment 331270

Tarehe Mar 2016 niliandika makala juu mahusiano kati Kiza, Mungu, Kifo, Vita, Njaa, na Maradhi. Makala ile ilizua mjadala mkubwa facebook na whatsapp nilipoiweka, na moja jambo kubwa lilotuvuruga ni uwezo na mamlaka ya Mungu katika uumbaji, na hasahasa ile nadharia ya kuwa MUNGU ni muumbaji wa viumbe vyote ilitumiwa sana na watu katika kuikosoa makala yangu.

Awali ya yote nakubali bila kigegezi chochote kuwa Mungu ni muumbaji wa viumbe vyote na ya kwamba ni Mola wa viumbe hivyo. Nakubali kuwa ulimwengu haukuzuka tu wenyewe katika tukio la lisilo ratibiwa. Bali yupo injinia wa Ulimwengu huu ambaye si mwingine bali ni MUNGU.

Misaahafu ya dini za Ibrahim, yaan uislamu, uyaudi na ukristo yote kwa pamoja bila kukhitililafiana inasema ulimwengu na vilivyomo ndani yake havikuzuka kwa bahati mbaya bali vimeumbwa na Mungu.

Kuna viumbe hai kama wanyama na mimea, lakini pia kuna viumbe ambavyo havina uhai kama mawe na mchanga. Vyote hivi Muumbaji wake ni Mungu.

"Mwenyezi Mungu ameumba mbingu na ardhi kwa Haki. Kwa hakika katika hayo ipo Ishara kwa Waumini. " Quran 29:44

"...Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Na Yeye ni Mmoja Mwenye kushinda!..." Quran 13:16

"Mbingu ni mali yako, nchi nayo ni mali yako, Ulimwengu na vyote viujazavyo Ndiwe uliyeupiga msingi wake. Kaskazini na kusini ndiwe uliyeziumba....." Zaburi 89:11-12

Hiyo quran 13:16 inatutanabaisha kuwa Mungu ameumba kila kitu, lakini tujiulize, kitu kilichoumbwa na Mungu kinaitwaje? Kwa vyovyote vile kinaitwa kiumbe. Kama ndivyo tunaweza kuwa sahihi zaidi kama tukisema kuwa Mungu ameumba viumbe vyote badala ya kusema kuwa Mungu ameumba kila kitu.

Twasema kuwa viumbe vyote vimeumbwa na Mungu, je vile ambavyo si viumbe tuna vizungumziaje? Naomba mjue Mungu ameumba viumbe vyote, lakini haimaanishi kuwa ameumba kila kitu. Kuna baadhi ya vitu ambavyo Mungu hakuviumba aidha hakutaka kuviumba au ameshindwa kuviumba.

VITU VIKUU SITA AMBAVYO MUNGU HAKUVIUMBA.

1. MUNGU
Ukisoma misahafu yote mikuu miwili quran na biblia hakuna ushahidi hata mmoja unaonesha kuwa Mungu kaumba Mungu(namaanisha Mungu kujiumba).

Kubwa zaidi katika misahafu hiyo ambayo imeandikwa kwa matakwa yake MUNGU, inaonesha ukuu wa Mungu, uwezo wake, mamlaka yake, utukufu wake, usafi wake na kila aina ya sifa nzuri na tukufu, lakini hatuoni chanzo chake kikiandikwa humo na hatuoni mwisho wake ukiandikwa humo, zaidi ya vitabu hivyo kusema ufalme wa MUNGU na Nguvu zake hazina mwanzo wala mwisho.

"Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi" Ufunuo 1:8

"Na Mola wako Mlezi anayajua yaliyo ficha vifua vyao, na wanayo yatangaza. Naye ni Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye. Sifa zote njema ni zake Yeye, mwanzo na mwisho...." Quran 28:69-70

Kwa aya hizi, na mafundisho mengine ya kinabii kama haya, yanathibitisha bila shaka kuwa ni kweli kuna mambo au vitu ambavyo Mungu hakuviumba na kwasababu hiyo vitu hivyo haviwezi kuitwa viumbe na ingawa viko. Kitu cha kwanza MUNGU, kipo na hakija umbwa.

Wanaosema kuwa MUNGU ameumba kila kitu waje hapa watuambie "MUNGU" kaumbwa na nani? Wakishindwa kututajia basi waishie kusema Mungu kaumba viumbe vyote lakini si vitu vyote.

2. KIZA
Ukisoma hiyo quran 28:69-70 na ukisoma vizuri ufunuo 1:8 utagundua mambo yote na habari zote kabla ya uwepo wa MUNGU hayajulikani na huenda anayajua Mungu mwenyewe, lakini kwetu sisi tunaona mambo hayo kwetu ni KIZA.

Kwa hivyo tunaweza kusema kabla ya Mungu hajaumba chochote alikuwako yeye na Kiza, Kiza ni mwanamke na Mungu ni mwanaume. Kwakuwa kwa kipindi hicho walikuwa wenyewe, na wanajuana wenyewe, jambo jepesi twaweza kusema hivi vitu ni ndugu. Ipo siku inshallah nitakuja kufafanua kwanini nasema Kiza mwanamke na Mungu mwanaume.

"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. 3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. 4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza."
Mwanzo 1:1-4

Katika andika hilo la juu tunajifunza yafuatayo.

A. Mbingu na nchi zimeumbwa na Mungu. Maji, ardhi na vitu vya kufananayo ni sehemu ya mbingu ya nchi.

B. Mungu aliumba NURU lakini hakuumba KIZA, tunaambiwa tu Kiza kilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji lakini hatuambiwi Mungu aliumba Kiza.
Hiyo mwanzo 1:3 "Mungu akasema, iwe Nuru; ikawa Nuru"

Alijuaje kuwa Nuru imekuwa kama kabla ya Nuru hiyo kulikuwa hakuna Kiza? Je, mbona hatuoni maandiko yakionesha Mungu akisema iwe Kiza kisha kikawa Kiza?

C. Ukisoma mwanzo 1:2 tunaona Mungu akiumba mbingu na nchi kisha Kiza alikaa juu ya uso wa vilindi vya maji, kwasababu hiyo, nikisema kuwa Kiza alikuwako kabla ya mbingu na nchi nitakosea? Kama alikuwako kabla ya mbigu na nchi, ama kabla ya ulimwengu, nikisema kuwa Kiza na Mungu waliishi wenyewe kabla ya ulimwengu pia nitakosea?

D. Baada ya Mungu kuumba Nuru, hapo ndipo alipofanikiwa, kumfungia KIZA, na athari za Kiza akaziita USIKU na athari za NURU akaziita MCHANA. Kwahivyo Mungu hakumuumba KIZA, ila Mungu kaumba Nuru, Mchana, na Usiku.

Kwahivyo kama tuko pamoja, utakubaliana na mimi kuwa KIZA ni moja ya kitu ambacho Mungu hakukiumba. KIZA si kiumbe, KIZA kimezuka tu kama alivyozuka Mungu mwenyewe. Tafauti kubwa kati ya MUNGU na KIZA ni kuwa Mungu kaumba na ni Mola wa viumbe vyote, lakini Kiza hakuumba kitu chochote kwa hivyo si MUUMBAJI.

Astronomy inatuambia kuwa ulimwemgu umeundwa na vitu vikuu vitatu, normal matter, dark matter na dark energy. Normal matter ndio hujumuisha zile atoms zilizo tumika kuumba Nyota,sayari, na vitu vingine.

Normal matter ni asilimia 5 tu ya ulimwengu wote, 25% ni dark energy na 70% dark matter. Hiyo dark energy na dark matter athari zake zinaonekana katika zenyewe hazionekane. Hii huenda ndio KIZA ambacho kimetajwa katika mwanzo 1:1

Astronomy pia yatuambia ulimwengu unatanuka kwa kasi, na ya kwamba unazidi kuongezeka kutokana ile motion iliyosababishwa na BING BANG, kutanuka kwake ina maanisha unazidi kumeza au ama kuingia katika sehemu mbele zaidi kutokea kule ulipo anzia(kipind cha dark age) Swali kule unapoelekea kuna nini kama si Kiza??

Astronomy pia yatuambia hakuna empty space, kama inavyo onekana, katika space waweza kuona ama kudhani hakuna maada yoyote, lakini kimsingi asilimia kubwa ya space ina dark energy na dark matter. Vitu hivi vinaashiria uwepo KIZA mbali na ulimwengu tunao ujua.

3. KIFO
Kwanza naomba tukumbuke wakati Mungu anafikiria kuumba ulimwengu tayari kulikuwako na KIZA. Ili Mungu awe kuumba ulimwengu ilikuwa lazima kwanza amuondoshe au amuue KIZA. Ili Kiza kiweze kufa shuruti pawe na "KIFO" Hata hivyo, kutokana na nguvu za Kiza, basi kikawa hakijakufa bali kilifungiwa.(Rejea mwanzo 1:3 Mungu akatenga giza na nuru)

Pili naomba mjue kuwa kiumbe hai cha kwanza kuumbwa na Mungu ni "NENO" kisha wakafuatia malaika wakubwa wanne(four Arc Angels) ambao ni Mikaeli, Raphaeli, Rucifer na Gabrieli. Hoja inakuja, Mungu alitumia kipimo gani kujua kwamba amefanikiwa kuumba kiumbe hai? Kwa vyovyote vile ili ajue kuwa amefanikiwa kuumba kiumbe hai ni lazima alinganishe uhai uliopo ndani ya kiumbe hai na mauti(KIFO). Kwa hivyo kilianza KIFO kabla ya UHAI, na bahati nzuri maandiko yanakubali kuwa Mungu kaumba uhai, lakini hayaoneshi kuwa Mungu kaumba KIFO.

Wachungaji wetu katika makanisa wanakataa katakata kuwa Mungu kaumba KIFO, wao wanasema KIFO kilisababishwa na shetani, bi maana shetani ndio kaumba KIFO. Huku ni kutokujua, lakini hakuna aliyeumba KIFO, KIFO sio kiumbe na alizuka tu kama alivyo zuka Mungu.

Kama nilivyosema ule muda Mungu anafikiria kuumba uhai, tayari kifo kilikuwako, na kwasababu hiyo, pia haijulikani kati ya Mungu na Kifo na mkubwa(kiumri).

Mungu aliumba uhai, na kwa kupitia huo uhai akaumba mwanadamu, lengo lake lilikuwa mwanadamu aishi milele, lakini kifo kikawa kikwazo katika lengo hili.

Sivyo tu, kwakuwa siku zote KIZA anataka atoke kifungoni, hivyo kila siku anapambana na Mungu kwa lengo la kutaka kumuua, na wakati huohuo Mungu naye anataka kumuua KIZA, mshindi wa pambano hili lazima amtumie "KIFO" na hapa ndipo tunapoona nafasi ya KIFO katika mahusiano ya NURU na KIZA.

Lakini Mungu anasema atakuja kumshinda KIZA na KIFO, na pindi atakapo shinda hakuna roho au mwili utakao kufa.

"na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. " Ufunuo 1:18

4. VITA na NJAA
KIZA baada ya kugundua Mungu ameumba malaika wakubwa wanne, KIZA alichukia na hapo yakazuka mapambano kati ya MUNGU na KIZA. Kwa mapambano hayo ndipo ilipozuka "VITA" mungu alichofanikiwa ni kumfungia KIZA, na funguo zake akakabidhiwa Rucifer. Mark of Darkness ndio Funguo na sehemu alofungiwa KIZA, chapa hii baadae iliitwa mark of cain.

Mnyama wa kwanza kuumbwa na Mungu kabla hata ya wanadamu ni Levithans, hawa ndio ile mijusi mikubwa na Magodizilla. hawa walikuwa na "NJAA" sana kiasi walane wenyewe kwa wenyewe, Hapa Mungu kwa kutumia jeshi lake la malaika waliwaondoa dunia na kuwafungua Purgatory. Hapa pia VITA alihitajika kufanikisha hili.

Tembo na vufaru wanapungua kwa kuuliwa na binadamu, hivi Magodizilla na Levithans waliuliwa na nani? Ikiwa wao walikuwako miaka mingi kabla ya wanadamu? Jibu jepesi ni upanga wa Malaika Mikael na jeshi lakd.

Wakati hayo yakitokea, Darkness akaigeuza ile mark kuwa laana, na laana ile ikasababisha hali ya uasi kwa mtunza funguo. Wakati Mungu anamuumba mwanadamu, na malaika kuambiwa wamsujudie, Rucifer akiwa kesha athiriwa na laana ya funguo akagoma kumsujidia adamu.

Kwa mara nyingine "VITA" ilihitajika katika kumdhibiti Rucifer na kundi lake.

6 MARADHI
Mungu hakuumba maradhi, na wala si lengo mungu mwanadamu aumwe na kuteseka kwa maradhi. Ila pale mwanadamu alipoumbwa na afya bora kabisa, na maradhi yakazuka hapo hapo. Baada ya Mungu kuja kumshinda KIFO, pia atakuja kuyashinda MARADHI, na hayo yakitokea katika maisha Paradiso hakutakuwa na KIFO wala MARADHI.

MWISHO.
Makala hii haina tafauti na ya juzi, ila leo baadhi ya nukta nimemua kuziongelea kwa undani zaidi ili iweze kujibu maswali na hoja zilizo jitokeza katika makala ya msingi. Hata hivyo najua siwezi kumaliza kila kitu hapa, ila mengine tutajifunza katika mjadala!

Njano5
0622845394
"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. 3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. 4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza."
Mwanzo 1:1-4

Kwahiyo Mungu hakuumba na maji pia maana yalikuwepo, na giza lilikuwepo vilindini mwa maji na Roho ua Mungu ilikuwa juu ya Uso wa maji??
 
Tunasema?Akina nani? kutokana na ujuzi wako Maria alipataje mimba bila kukutana na mwanaume?
Akina nyinyi kupitia biblia kwani unapinga?

Wewe hapo juu umesema haiwezekani mwanamke akaishi peke yake halafu akaja kuzaa mtoto bila kuhusisha mbegu za kiume

Sasa nakuuliza inamaana ile stori ya maria ilikua niya kugushi?
 
Hizi mada ukiziendekeza unaweza kuingizwa chaka ukakubaliana kwamba Mungu hayupo.
 
Akina nyinyi kupitia biblia kwani unapinga?

Wewe hapo juu umesema haiwezekani mwanamke akaishi peke yake halafu akaja kuzaa mtoto bila kuhusisha mbegu za kiume

Sasa nakuuliza inamaana ile stori ya maria ilikua niya kugushi?
na mimi ndo nikakuuliza wewe kulingana na ujuzi wako unajua maria alipata mimba kwa njia gani?

na unaweza kunipa simulizi la mwanamke tofauti na maria aliyebeba mimba bila kukutana na mwanaume?
 
na mimi ndo nikakuuliza wewe kulingana na ujuzi wako unajua maria alipata mimba kwa njia gani?

na unaweza kunipa simulizi la mwanamke tofauti na maria aliyebeba mimba bila kukutana na mwanaume?

Mbona nimekuonesha kua kitabu kimeandika kua alipata mimba bila kulalwa na mwanaume, Unakwama wapi??

Kwanini simulizi umeipa kipaumbele sana katika habari usizozijua?? Ukipewa simulizi utajihakikishiaje kua ulichosimuliwa ni kweli??

Nami nakuuliza ukipewa simulizi kuonesha mwanamke aliyebeba mimba bila mwanaume, utaikubali kwasababu simulizi haziongopi?
 
basi kupitia kitabu hicho hicho ambacho we umesema yaani maandiko matakaifu ya Mungu mimi naamini Maria alizaa bila kukutana na mwanaume kutokana na uwezo wa Mungu

simulizi ipi kaka mbona hueleweki,aliyeleta simulizi ni wewe,na katika maswali niliyomuuliza mkuu kule awali wala sikutia ndani simulizi lolote bali niliuliza ikiwa amewahi kushuhudia kuna mwanamke kabeba mimba bila kukutana na mwanaume

sio kila simulizi nitakalopewa nitakubaliana nalo mkuu itategemea na chanzo chake kwa sababu sio kila chanzo kinachoaminika
 
Inathibitika vipi kuwa jua halina Uhai wala Ufahamu?
Umetumia kigezo kipi kusema hivyo?
Mimi nathibitisha kuwa Jua lipo hai,kwa sababu ya utendaji wake kazi,pia nathibitisha kuwa Jua lina Ufahamu kwa kuwa linajiendesha kwa kanuni zile zile bila kukosea.
Labda tuache huo uwezekano wa Jua kuwa halina Uhai wala Ufahamu.
Tulipe sifa ya Uhai na Ufahamu,
Je! Unaweza kulithubitushia Uwepo wa Usiku?
Uhai ni nini na kitu kinatakiwa kiwe na sifa zipi ili ujue kipo hai?
 
Mkuu Kiranga ndio maana mwanzo nilikuambia kama Mung hayupo maana yake ni kwamba hata wewe haupo

katika maana gani?

Nithibitishie uwepo wako mkuu

Nithibitishie uwepo wa nguvu zako

Nithibitishie uwepo wa akili yako

Nithibitishie uwepo wa pumzi inayokufanya uko hai mpaka sasa

hapo nilipobold kama ulinijbu kuwa hakuna kilicho complex kilichojitokeza chenyewe bila kuumbwa,kusababishwa na kingine ,naomba basi wewe uniambie vitu vyote ulimwenguni vilitoka wapi?nani msababishaji wake?
That is a logical non sequitur.

Kushindwa kuthibitisha uwepo wa kitu hakufanyi kitu kisiwepo. Kitu kinaweza kuwepo halafu watu wakashindwa kuthibitisha kipo. Kwa sababu hawajajua kuthibitisha.

Kitu kinaweza kisiwepo, halafu watu wakashindea kuthibitisha kipo, kwa sababu hakipo.

Unalinganisha vitu viwili ambavyo havina uhusiano.

Tuseme watu wawili wanabishana kuhusu uwepo wa Dodoma. Wako Dar es salaam.

Wanajua Dar es salaam ipo, kwa sababu ni mji ambao wamo ndani yao.

Mwingine anasema kuna mji unaitwa Dodoma. Mwi gine anabisha. Anamwambia anayesema kuna mji unaitwa Dodoma athibitishe hilo. Anayesema kuna mji unaitwa Dodoma, anashindwa kuthibitisha mji huo upo.

Je, hilo linafanya mji unaoitwa Dodoma usiwepo?

Mimi sipingi uwepo wa Mungu kwa sababu tu watu hawawezi kuthibitisha uwepo wa Mungu. Mbali zaidi ya hapo, habari za kuwepo kwa Mungu zina inherent contradictiin.

Huku unaambiwa Mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, huku unaambiwa Mungu kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kutokea.

Kama Mungu yupo, ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana?

Kwa nini hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani popote, kwa vyovyote, muda wowote?
 
Uhai ni nini na kitu kinatakiwa kiwe na sifa zipi ili ujue kipo hai?
Mkuu naona unataka kulikwepa swali kwa kutaka kuthibitishiwa Uhai wa jua una sifa ZIPI!

Nimekwambia Tujaalie kuwa jua lina Uhai na ufahamu kama wako!
Je! Utalithibitishia vipi uwepo wa usiku?
 
KIZA.
******
Mwenyezi Mungu ni Nuru katika dhati yake!
Kwa hiyo Unapo zungumzia Kuwa Mwenyezi Mungu hana Mwanzo wa uwepo wake wala mwisho wake,hapo unaizungumzia Nuru katika dhati yake isiyo kuwa na Mwanzo wala mwisho,kwa sifa hiyo tu utajua kuwa KIZA si sifa ya dhati ya Mwenyezi Mungu, na kama si sifa katika dhati ya Mwenyezi Mungu basi inakuwa KIZA ni hali iliyo umbwa na Mwenyezi Mungu kwa kuwa ina Mwanzo wa uwepo wake na Mwisho wa uwepo wake,
kwa kuwa mtoa mada amejenga hoja zake kupitia maandiko ya Quran na Bibilia,nami nimeona nitoe mchango wangu wa kujibu hoja kwa kutumia vitabu hivyo.
Na hapa naanza kuthibitisha dhati ya Mwenyezi Mungu kwa maandiko hafuatayo:-

35. Mwenyezi Mungu ni Nuru ya Mbingu na Ardhi. Mfano wa Nuru yake ni kama shubaka lenye kuwekwa ndani yake taa. Taa ile imo katika tungi. Tungi lile ni kama nyota inayo meremeta, inayo washwa kwa mafuta yanayo toka katika mti ulio barikiwa, mzaituni. Si wa mashariki wala magharibi. Yanakaribia mafuta yake kung'aa wenyewe ingawa moto haujayagusa - Nuru juu ya Nuru. Mwenyezi Mungu humwongoa kwenye Nuru yake amtakaye. Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu.(24:35 AN-NUR).
*******

5 Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza lo lote hamna ndani yake.
(1 Yohana 1 :5)

Kwa kuwa Nuru haina Mwanzo wa uwepo wake wala mwisho wa uwepo wake daima milele,hivyo KIZA kwa sifa yake hakiwezi kuwa kili kuwepo palipo na Nuru.
kwa sifa hiyo ni wazi kuwa Kiza kimeumbwa na maandiko yanadhihirisha hilo.

7 Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni Bwana, niyatendaye hayo yote.
(Isaya 45 :7)

Nano Kuhuluku kuna maana hiyo hiyo ya kuumba kwa ushahidi wa aya hii.

12 Mimi nimeiumba dunia, nimemhuluku mwanadamu juu yake; Mimi, naam, mikono yangu mimi, imezitanda mbingu, na jeshi lake lote nimeliamuru.
(Isaya 45 :12)
*******

72. Sema: Mwaonaje, Mwenyezi Mungu angeli ufanya mchana umekukalieni moja kwa moja mpaka Siku ya Kiyama, mungu gani asiye kuwa Mwenyezi Mungu ataye kuleteeni usiku mkapumzika humo? Basi je, hamwoni?
(28:72 Al qasas)

Kwa hiyo Mwenyezi Mungu kaumba Kiza kwa ushahidi wa Maandiko hayo.

kwa hivyo hoja ya kudai kuwa Mwenyezi Mungu hakuumba KIZA inafia hapo.

KIFO.
********
Uhai ni dhati ya Mwenyezi Mungu,kwa kuwa Mwenyezi Mungu hana Mwanzo wa uwepo wake wala mwisho wa uwepo wake na Uhai ni katika dhati yake basi kifo hakikuwepo na wala hakina nafasi,
Na kwa kuwa Mwenyezi Mungu hana sifa ya kuto kuwepo kabla ya kuweko kwake,hivyo sifa ya kifo au kitu kisicho na Uhai hakina sifa ya kuwa kilikuwepo,
Hivyo basi kwa kukosekana sifa ya kifo katika dhati ya Mwenyezi Mungu ni wazi kuwa KIFO kiliumbwa na Mwenyezi Mungu kwa sababu maalum.
Aya zifuatazo zinaonyesha kuwa KIFO kimeumbwa kwa ajili ya viumbe hai na ni kwa sababu maalum:-

1. AMETUKUKA ambaye mkononi mwake umo Ufalme wote; na Yeye ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.

2. Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenye nguvu na Mwenye msamaha.(Qur:67:1-2 AL MULK)
****
21 akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe.
(Ayubu 1 :21).

Aya hizo zinathibitisha kuwa Kifo ni katika mpango wa Mungu.

Mtoa mada alibainisha kuwa kabla ya Mwenyezi Mungu hakuumba chochote kulikuwa hakuna kitu kinacho itwa Uhai,hivyo ametafsiri kuwa kuto kuwepo Uhai kuna maanisha kifo!.
Mtazamo huu hauna maana kwa sababu unazungumzia Uhai wa viumbe hai ambavyo kabla ya kupewa kwao Uhai havikuwa viumbe hai.
Adamu aliumbwa kutokana na udongo,Kisha akapuliziwa pumzi ya Uhai akawa nafsi hai,
Kabla hata udongo ambao haukuwa na Uhai kuwepo,Mwenyezi Mungu ambaye ni Uhai alikuwako!
Mwenyezi Mungu ambaye ni Uhai daima milele,aliumba vitu vyenye Uhai na visivyo na Uhai.
kisha katika vile alivyo viumba ambavyo havikuwa hai,aliumba Uhai wa viumbe kupitia vitu hivyo,

Sifa ya kifo inakuwa kwa kitu ambacho kilikuwa kina Uhai kisha kikatokwa na Uhai!
kile kitendo cha kutokwa na Uhai kwa kitu kilicho kuwa hai ndipo inapo patikana sifa ya Umauti.
Angalia mmea una kanuni mbili ukitunzwa vizuri na kumwagiwa maji unakuwa hai ,
usipo tunzwa na kupewa maji Unakufa,
Kama mmea umeumbwa kupoke kanuni mbili kanuni yenye matokeo chanya na kanuni yenye matokeo hasi,
basi Ujue kanuni hizo zimo ndani ya Maumbile ya mmea.
Na mmea haukujiumba hivyo ulivyo wenyewe bali Mwenyezi Mungu ameuumba kupokea hali ya Uhai na umauti.

Kwa hiyo hoja ya kusema kuwa Mwenyezi Mungu hakuumba kifo inafia hapo.

NJAA
*********
Mwenyezi Mungu kamuumba Mtu Katika Umbile ambalo linahitajia kula na kunywa ili liendelee kuwa hai.
Mtu kuhisi njaa na kiu ni sehemu ya maumbile yake.
kwa kupitia rasilimali njaa na rasilimali kiu mwili unalazimika kula na kunywa kwa faida ya Uhai wa mwili.
Tunaweza kusema mahitajio ni Hasi na Kumiliki ni chanya!
Kama mwanaadamu asinge umbwa katika hali ya mahitajio, dunia ingelisimama!
hakuna kitu kingefanyika,
Maendeleo yote unayo yaona ya kielimu,kiuchumi,kiteknolojia, yote yameletwa na Mahitajio aliyo umbiwa mwanaadamu ikiwemo rasilimali njaa!.

Unapo zungumzia majanga ya kibinaadamu,Njaa kwa maana ya Ukosefu wa chakula,Mafuriko,Majanga ya Moto,vita, Magonjwa,
hayo ni Matoke ya njia tatu!.
Njia mbili ni pacha ambazo Mwenyezi Mungu kaziumbia matokeo.
Nazo ni kanuni mbili!.
Kanuni hasi na kanuni Chanya.

Mwanaadamu kawekwa duniani kwa Muda mfupi ili kufanyiwa mtihani wa Utii kwa akili huru, Mungu kampa elimu ya kujua Jema na baya katika maumbile yake,
Kisha baada ya mwanaadamu kuumbika kwa kutambua jema na baya, Mwenyezi Mungu akamletea Muongozo ambao kwa sifa alizo nazo ataupokea!
akamletea mitume na vitabu vya kumuelekeza nini cha kufanya na nini cha kuachwa!.
Kisha akamuonyesha matokeo ya kutii Muongozo na Matokeo ya kuto tii,
Kutii Muongozo wa Mungu kunampeleka Mtu Katika Matokeo Mazuri ambayo Mungu ameyaandaa!
Na kuto tii Muongozo wa Mungu kunampeleka Mtu kupata Matokeo mabaya ambayo Mungu ameyaandaa.

Kutunza Mazingira, kuhifadhi misitu,vyanzo Maji,kufanya uadilifu katika kila jambo kama Mungu alivyo agiza,basi Mungu kaweka matokeo Mazuri kwa kutii Muongozo wake! anae tii atayapata.

Kuchafua mazingira,Kukata miti hovyo,kuharibu vyanzo vya maji,na kufanya ufisadi katika Ardhi ni kukiuka Maagizo ya Mungu hivyo kunatupeleka kwenye matokeo mabaya ambayo Mungu ameyaandaa.
Na mfanyaji atayapata.

Kwa hiyo Mwenyezi Mungu kaweka kanuni mbili,moja ni njema na Moja ni mbaya,
Anatutaka tufuate kwa akili huru ile kanuni iliyo njema,
ametuletea msaada wa mitume na vitabu ili kutuongoza kuziendea kanuni zenye kuleta matoke mema kwa akili huru.
Kisha ametupa maonyo na tusiende katika kuzifuata kanuni ziletazo matokeo mabaya.

KWA HIYO MAGONJWA! MAJANGA YA MAFURIKO,UKAME,VITA,NI MATOKEO YA SISI WENYEWE KUZIFUTA KANUNI ZENYE KULETA MATOKEO MABAYA AMBAZO MUNGU AMEZIWEKA NA KUTUONYA TUSIZIFUATE.

Njia ya Tatu ambayo haina Mafungamano na uchaguzi huru wa Mwanaadamu,
Ni wakati Mungu anapomrudi mja wake katika kupima imani yake.

155. Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri,

156. Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.

157. Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao Mlezi na rehema. Nao ndio wenye kuongoka.
(Quran:1:155-157 Al-baqara)

KWA HIYO HAKUNA JAMBO LOLOTE AMBALO LIPO NJE YA MWENYEZI MUNGU
 
basi kupitia kitabu hicho hicho ambacho we umesema yaani maandiko matakaifu ya Mungu mimi naamini Maria alizaa bila kukutana na mwanaume kutokana na uwezo wa Mungu

simulizi ipi kaka mbona hueleweki,aliyeleta simulizi ni wewe,na katika maswali niliyomuuliza mkuu kule awali wala sikutia ndani simulizi lolote bali niliuliza ikiwa amewahi kushuhudia kuna mwanamke kabeba mimba bila kukutana na mwanaume

sio kila simulizi nitakalopewa nitakubaliana nalo mkuu itategemea na chanzo chake kwa sababu sio kila chanzo kinachoaminika

Ngoja kwanza usiwe na haraka ya kwenda mbali wakati hapa hujapamaliza

Ulivyosoma ile habari wewe ulijuaje kua habari ile ni yakweli??

Hapa nategemea kuona circular logic
 
That is a logical non sequitur.

Kushindwa kuthibitisha uwepo wa kitu hakufanyi kitu kisiwepo. Kitu kinaweza kuwepo halafu watu wakashindwa kuthibitisha kipo. Kwa sababu hawajajua kuthibitisha.

Kitu kinaweza kisiwepo, halafu watu wakashindea kuthibitisha kipo, kwa sababu hakipo.

Unalinganisha vitu viwili ambavyo havina uhusiano.

Tuseme watu wawili wanabishana kuhusu uwepo wa Dodoma. Wako Dar es salaam.

Wanajua Dar es salaam ipo, kwa sababu ni mji ambao wamo ndani yao.

Mwingine anasema kuna mji unaitwa Dodoma. Mwi gine anabisha. Anamwambia anayesema kuna mji unaitwa Dodoma athibitishe hilo. Anayesema kuna mji unaitwa Dodoma, anashindwa kuthibitisha mji huo upo.

Je, hilo linafanya mji unaoitwa Dodoma usiwepo?

Mimi sipingi uwepo wa Mungu kwa sababu tu watu hawawezi kuthibitisha uwepo wa Mungu. Mbali zaidi ya hapo, habari za kuwepo kwa Mungu zina inherent contradictiin.

Huku unaambiwa Mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, huku unaambiwa Mungu kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kutokea.

Kama Mungu yupo, ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana?

Kwa nini hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani popote, kwa vyovyote, muda wowote?
kwanza mkuu Kiranga nikiri unareason vizuri sana am so pleased with the way unareason mkuu,asante kwa maswali na majibu yako mujarabu

back to the topic mkuu nitakujibu kama tu ulivyonijibu kwa mtiririko wa majibu yako

maneno ya kwanza kuwa bolded umeongea sawa kabisa mkuu kitu kinaweza kuwepo na watu wakashindwa kuthibitisha uwepo wake ni kweli na hiyo iko applied kwenye uwepo wa Mungu mkuu,wanasayansi wengi wameshindwa kuthibisha uwepo wa Mungu kutokana na elimu yao ya kisayansi na ndio maana wanafikia mkataa kuwa Muungu hayupo.lakini je ni kweli kwamba hayupo kwa sababu wameshindwa kuthibisha jambo hilo?Uwepo wa Mungu?,je hilo linapaswa kutufanya hata sisi wengine tukubaliane nao kuwa Mungu hayupo just kwa sababu wao wameshindwa kuthibitisha kuwa yupo?

Ni inherent contradiction zipi unazoziongelea wewe kuhusu uwepo wa Mungu mkuu?

kuhusu maneno ya mwisho yaliyokuwa bolded hiyo ni ishu nyingine kabisa mkuu tena inayo majibu ya kutosha na yenye kuridhisha,ishu ya msingi ni uwepo wake huyu Mungu

Uwepo wa Mungu ni too obvious,

Fikiria mfano huu mdogo mkuu kila kitu unachokiona humu duniani kuna mtu kakifanya au kakitengeneza tena katumia muda wake mwingi na akili zake zote kutengeneza kitu hicho,tena kaka yangu naona una upeo mkubwa sana wa mambo kwa hiyo naamini unajua historia nyingi za namna wataalamu mbali mbali walivhohangaika kutengeneza vitu mbali mbali kama camera,ndege,magari,meli n.k hata kuna wengine walijaribu kutengeneza vitu na kutofanikiwa kuvimalizia kabisa na kuwaachia wengine waendeleze

Je ianwezekana kabisa kuwa kila kitu kina mtengenezaji halafu,dunia,bahari viumbe vyote angani hewani na duniani viwe vimejitokeza?pasiwepo na mtu ambaye kavitokeza? how is even that possible?

kila kitu kilichopo duniani leo kimeigwa kutokana na vitu vya asili

Mfano camera ni matokeo ya mfumo mzima wa utendaji wa jicho la mwanadamu
Ndege ni matokeo ya kuiga utendaji wa mabawa ya ndege shakwe bila kumsahau nyangumi mwenye nundu
mifano ni mingi sana mkuu
Tena wote wanaokaa na kutizama na kujifunza kutoka kwenye kitu cha asili ni watu ambao tunawaita magenious innovators,wanatumia muda mwingi sana kukisoma kiumbe hicho cha asili waelewe kiundani kabisa utendaji wake wa kazi na ndipo wanapotengeneza kitu kinachofanana na kiumbe hicho

copy ya kitu cha asili imetengenezwa na jopo la watu wenye akili,walioketi na kuumiza kichwa na kutunga theory mbali mbali ya namna ya kukitumia kitu hicho,je kitu hicho cha asili kilichoigwa kinaweza kuwa kimejitokeza chenyewe?How is even that possible?
 
Ngoja kwanza usiwe na haraka ya kwenda mbali wakati hapa hujapamaliza

Ulivyosoma ile habari wewe ulijuaje kua habari ile ni yakweli??

Hapa nategemea kuona circular logic
circular logic ndo nini mkuu,twende kwa lugha nyepesi nyepesi mi sio Msomi kama wewe kaka am just a layman,

back to swali lako nisiwe na haraka ya kwenda wapi?nimeenda wapi mpaka unaniambia nisiwe na haraka ya kwenda mbali wakati hapa sijapamaliza,hapo ambapo sijapamaliza ni wapi?

kwani mkuu wewe hizo circular logic zako unajuaje kama ni za kweli?
 
Unaelewa kwamba kila kilichopo kuwa na muumba si lazima muumba awe Mungu?

Unaelewa kwamba ukisema kila kilichopo ni lazima kina muumba, hapo ujesema Mungu hawezi kuwepo, kwa sababu na yeye atahitaji muumba, na akiwa na muumba si Mungu tena?
 
circular logic ndo nini mkuu,twende kwa lugha nyepesi nyepesi mi sio Msomi kama wewe kaka am just a layman,

back to swali lako nisiwe na haraka ya kwenda wapi?nimeenda wapi mpaka unaniambia nisiwe na haraka ya kwenda mbali wakati hapa sijapamaliza,hapo ambapo sijapamaliza ni wapi?

kwani mkuu wewe hizo circular logic zako unajuaje kama ni za kweli?

Nanukuu
basi kupitia kitabu hicho hicho ambacho we umesema yaani maandiko matakaifu ya Mungu mimi naamini Maria alizaa bila kukutana na mwanaume kutokana na uwezo wa Mungu

hapa ndipo nilipokuambia kua hujapamaliza

Unajuaje kua hayo maandishi ni matakatifu na yamesema ukweli?? Ulitumia vigezo gani kuhotimisha kua hicho ni kitabu kitakatifu na nimaneno ya mungu??

Unahakika gani kua hicho kitabu ni kitabu cha mungu na siyo projects za watu ili kushika watu kama nyinyi??
 
circular logic ndo nini mkuu,twende kwa lugha nyepesi nyepesi mi sio Msomi kama wewe kaka am just a layman,

back to swali lako nisiwe na haraka ya kwenda wapi?nimeenda wapi mpaka unaniambia nisiwe na haraka ya kwenda mbali wakati hapa sijapamaliza,hapo ambapo sijapamaliza ni wapi?

kwani mkuu wewe hizo circular logic zako unajuaje kama ni za kweli?
Kama kila kilicho complex kimeumbwa, hilo kinamaanisha unayemuita Mungu naye kaumbwa.

Na kama kaumbwa, basi si Mungu.

Unakubali?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom