Vitu sita ambavyo si viumbe vya Mungu

Vitu sita ambavyo si viumbe vya Mungu

Tatizo lako hukunielewa niliporejea juu ya suala la theory ninamaanisha kuwa kwa kuwa wewe mwenyewe huamini uwepo wa mungu kwa kutokana na theory basi ndo maana wajibiwa kwa theory kuthibitishiwa uwepo wake na hata imani zetu juu ya uwepo wa mungu umetokana na theory lakini ndani theory hizo tukawekewa vivid examples ili kuverify hizo theories kwa mwenye shaka
Na mwenyezi mungu akasema hiki ni kitabu kisicho na shaka ndani take (Surat baqara)
Hii ni kuonesha kuwa kuna uthibitisho juu ya theories zenye kujenga imani zetu ili kuondoa shaka zitakazojitokeza
Hivyo basi kwa wale wasioamini uwepo wa Mungu kama wewe bwana kiranga (hili jina kiranga lina tafsiri ya hali ya kulaaniwa au mtu mwenye kuandamwa na mabalaa kwa tafsiri ya lugha ya kikwetu) samahani kama nitakua nimefanya personal offending) ni wenye kujawa na nadharia tu pasi na uthibitisho wowote wenye kuondoa shaka juu ya kile wanachokisimamia
Basi sema nyinyi mliokufuru kamwe sitaabudu kile mnachokiabudu na wala sitaamini kile mnachokiamini........
Mzee huyu ameshasema hataki kuamini unajisumbua tu, mwisho utaniambia kama atakuelewa,..
 
Hiyo vivid example ipi? Na kitu gani kinaifanya kuwa vivid?

Hicho kitabu kisicho na shaka ndani yake kinasema mungu atawafanya watu wengine kuwa na mioyo migumu, atawafunga macho na masikio ili wasimjue hata wakijitahidi vipi.

Kisha atawahukumu kwa kutomjua.

Hiki kitabu kweli cha mungu au kimeandikwa na binadamu aliyeona maruweruwe tu?

Hata binadamu akimnyima mwanawe kwenda shule, halafu mwanawe akashindwa kusoma, halafu huyo binadamu akamuadhibu mwanawe kwa kutojua kusoma, tutamuita baradhuli.

Sembuse mungu?
 
Mungu hakuwa na uwezo?

Sijahusisha bila swali, nimeuliza swali. Unaweza kulijibu?

Umethibitisha wapi uwepo wa mungu? Unaweza ku link au copy paste hapa?

Kwani zuri likifanywa bila kujulikana hili zuri linapungua uzuri wake?

Habari ya kwamba. Dhana hii ni potofu.

Tunajua muda unavyokwenda mbele bila hata ya kuwahi kurudi nyuma katika muda.

Unarudia kile kile. Si lazima kwa vitu kuwa pacha ili kimoja kiwe na maana.Mbona mud.

1.Usiniulize kwamba je hakuwa na uwezo, bali unatakiwa unijibu ulijuaje?huwezi kuhoji kitu kisha ukamaliza alafu usijue msingi wa kile unachokiuliza.
2.Nimeshakupa jibu kwamba binaadamu hawezi kumthibitishi binaadamu mwenzie kwa misingi ya kisayasi.
3.@Kiranga unatakiwa uonyeshe walau kwa mifano kwamba ;-
a).usingekuwepo ubaya ungeujuaje ubaya?.
b).ungepata wapi kipimo cha kulinganishia uzuri bila ubaya?.
c).wewe ungepata wapi hoja za kushambulia uwepo wa Mungu??
Tulioitambua haki hatuyumbishwi.
 
Mzee huyu ameshasema hataki kuamini unajisumbua tu, mwisho utaniambia kama atakuelewa,..
Sitaki kuamini, nataka kujua. Na kufika kwenye kujua, kuamini njiani si vibaya.

Tatizo nyinyi mnaishia kwenye kuamini wakati mnatakiwa kuendelea kuhakiki na kuondoka kwenye Imani ili mfike kwenye kujua.

Ukifikiri kwa makini utaona huyu mungu mnayemsema hayupo. Kwa sababu idea ya yeye kuwapo inajipinga yenyewe kama idea ya pembetatu duara kuwepo.
 
1.Usiniulize kwamba je hakuwa na uwezo, bali unatakiwa unijibu ulijuaje?huwezi kuhoji kitu kisha ukamaliza alafu usijue msingi wa kile unachokiuliza.

Kwa nini nisikuulize kama hakuwa na uwezo? Kwa nini natakiwa kukujibu alijuaje? Alijuaje nini?

Msingi wa swali langu ni contradiction.

Mungu wenu mzuri, mwema, ana uwezo wote, ujuzi wote, upendo wote, halafu anaruhusu mabaya wakati ana uwezo wa kuzuia mabaya yasiwepo.

Kwa nini?

Hii ni contradiction. Unaweza kuitatua?

2.Nimeshakupa jibu kwamba binaadamu hawezi kumthibitishi binaadamu mwenzie kwa misingi ya kisayasi.

Kwa kifupi unaamini kitu ambacho hakithibitishiki. Na mimi nakwambia hakithibitishiki kwa sababu hakipo.

3.@Kiranga unatakiwa uonyeshe walau kwa mifano kwamba ;-
a).usingekuwepo ubaya ungeujuaje ubaya?.

Kwa nini kuujua ubaya kuwe muhimu?

Mtu kaibiwa. Halafu analalamika ubaya wa kuibiwa. Wewe unamwambia "kusingekuwepo kuibiwa ungejua kuibiwa?" kama vile kujua kuibiwa ni kitu kizuri sana ambacho kinakuwa kinastahili kulipa bei ya kuibiwa.

This is absurd thinking.

b).ungepata wapi kipimo cha kulinganishia uzuri bila ubaya?.

Nishaeleza hapo juu kwamba dhana ya kwamba ni lazima kuwe na ubaya ili ujue uzuri ni potofu.

Mtu anaweza kulinganisha uzuri mdogo na mkubwa bila kuhitaji ubaya.

Nishaeleza kwamba haturudi nyuma katika muda, ila ukweli kwamba haturudi nyuma katika muda hautuzuii kupima muda unaoenda mbele kwa siku, saa na dakika. Unachosema wewe hapa ni kama mtu anayesema "kwa kuwa haturudi nyuma katika muda, basi hatuwezi kupima muda unaokwenda mbele tu kwa siku, saa na dakika".

This is absurd thinking.

c).wewe ungepata wapi hoja za kushambulia uwepo wa Mungu??

Kwa nini unafikiri kwamba mimi kupata hoja ya kumshambulia mungu katika ulimwengu ambao hauna contradiction ni kitu muhimu? Did you even think this through?

Tulioitambua haki hatuyumbishwi.

Haki gani?

Ya mungu anayewafunga watu mioyo ili wasimjue halafu kuwahukumu kwa sababu hawajamjua?
 
hiyo jamaa ni mpotoshaji mkubwa, nahisi anatumika na watu/viumbe anvyovijua.. Mungu ni MUUMBAJI WA KILA UNACHOKIONA na usivyoviona...

rejea mwanzo 1;1-3, Mungu alitenga Nuru na giza, tatzo lako mkuu unajua kuwa Mungu aliumba hii dunia tu, jambo ambalo si kweli, soma vyema utajua kuwa kuna zaidi ya galaxy 100 ambazo Mungu aliziumba, bahati mbaya dunia yetu pekee ndo iliasi, na Mungu kwa mjib wa biblia alimtuma Yesu kuja kuukomboa huu ulimwengu..

.
Nuru tunaona aliiumba Mungu. giza je?. It means GIZA alikuwepo kabla ya NURU
 
Kiranga
1).Unatakiwa ueleze hoja za Mungu umezitoa wapi???
Kwamba alikuwa anauwezo wa kuumba mabaya yasiwepo chanzo chako cha hoja hii ni kipi au REF: yake ni ipi??

2).Mimi nimeamini kile ambacho nimekithibitisha ndani ya moyo wangu.kitu ambacho huwezi kupeleka maabara kuchunguzwa ni kwamba hakichunguziki na kiumbe.
3).Ni muhimu sana kuujua ubaya na ubaya umuhimu wake ili uweze kujipima na kujikosoa.hata wewe hoja ya kutaka mazuri matupu bila mabaya haina mashiko;
a}.kama mazuri yangekuwepo bila mabaya kungekuwa na haja gani ya Mungu kutuleta duniani ili atupime???.
b}watu waovu na wapingaji wa uwepo wa Mungu akina Kiranga wangepatikanaje????
c}watu wema wenye kushukuru wangetengwaje na watu waovu wenye kukufuru and
d}malipo ya pepo kwa wale watakao vumilia mpaka mwisho isingekuwepo,hata kama ingekuwepo hao watakaolipwa watalipwa kwa lipi?? na moto usingekuwepo na hata kama ungekuwepo hao watakaoingiza wataingizwa kwa kosa lipi wakati mabaya hayakuwepo???.
 
Kiranga
1).Unatakiwa ueleze hoja za Mungu umezitoa wapi???

Nimezitoa kwa waamini mungu.

Kwamba alikuwa anauwezo wa kuumba mabaya yasiwepo chanzo chako cha hoja hii ni kipi au REF: yake ni ipi??

Vitabu vya waamini kama Biblia na Quran. Hukubali kwamba mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote?

2).Mimi nimeamini kile ambacho nimekithibitisha ndani ya moyo wangu.kitu ambacho huwezi kupeleka maabara kuchunguzwa ni kwamba hakichunguziki na kiumbe.

Huelewi kuthibitisha wala kuamini. Unachothibitisha huamini, unachoamini, huthibitishi.

3).Ni muhimu sana kuujua ubaya na ubaya umuhimu wake ili uweze kujipima na kujikosoa.

Kama hakuna ubaya, haja ya kujikosoa itatoka wapi? Kwa nini ni muhimu kujikosoa kama hakuna ubaya?

hata wewe hoja ya kutaka mazuri matupu bila mabaya haina mashiko;

Sijataka mazuri matupu bila mabaya, nimetaka logical consistency. Unaelewa maana yake?

Maana yake, mngesema mungu yupo, ila ana roho mbaya, nisingeshangaa dunia kuwa na ubaya, kwa sababu mungu ana roho mbaya.

Mmesema mungu yupo, ana nguvu zote, ana ujuzi wote ana upendo wote, lakini kaumba ulimwengu ambao unawezekana mabaya licha ya kuwa na kila sababu, uwezo, upendo na ujuzi wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

This is an unresolved contradiction.
a}.kama mazuri yangekuwepo bila mabaya kungekuwa na haja gani ya Mungu kutuleta duniani ili atupime???.

Kwa nini mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote aone haja ya kutupima? Atupime ili iweje wakati yeye anajua kila kitu?

b}watu waovu na wapingaji wa uwepo wa Mungu akina Kiranga wangepatikanaje????

Kwa nini ni muhimu kuwepo na watu waovu kama mungu yupo, ni mwenye upendo wote na ana uwezo wa kuumba dunia isiyo na mabaya?

c}watu wema wenye kushukuru wangetengwaje na watu waovu wenye kukufuru and

Kwa nini ni muhimu kutenga watu wema na waovu kama mungu angeumba ulimwengu ambao uovu hauwezekani na kila mtu ni mwema?

d}malipo ya pepo kwa wale watakao vumilia mpaka mwisho isingekuwepo,hata kama ingekuwepo hao watakaolipwa watalipwa kwa lipi??

Kwa nini pepo iwe malipo wakati mungu alikuwa na uwezo wa kufanya pepo ni kitu cha kawaida kwa viumbe wote katika dunia ambayo mabaya hayawezekani?

na moto usingekuwepo na hata kama ungekuwepo hao watakaoingiza wataingizwa kwa kosa lipi wakati mabaya hayakuwepo???.

Kwa nini ni muhimu kuwe na moto katika dunia ambayo mabaya hayawezekani?

Umezunguka sana lakini swali langu la msingi hujalijibu.

Mnasema mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

Alipokuwa anaumba ulimwengu, alikuwa na uwezo wa kuuumba vyovyote.

Hilo lina maana kwamba aliweza kuuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani. Kama ambavyo hatuwezi kurudi nyuma katika muda.

Kwa nini mungu hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Hujanipa sababu.
 
Naam bwana Kiranga hebu tuwekane sawa katika haya:
1. Je wewe unaamini dunia ipo? Je hiyo dunia imefananaje? Ni nani mmiliki wa dunia?
2. Hivi unaamini kama wewe mwenyewe binafsi ni kiumbe? Hebu thibitisha uwepo wako kwa mifano halisi. Niambie wewe umepatikanaje? Ni nani aliyeweka mfumo wa wewe kupatikana mpk ukawa hivyo ulivyo.
3. Unauliza swali kama Mungu ni mjuzi wa yote kwanini atujaribu. Hivi umejiuliza kwa nini mwalimu anatoa mtihani kwa wanafunzi wake ikiwa yeye anajua majibu ya kile anachowauliza watoto wake??
 
hapa mwandishi anaonekana,anachanganya hoja kati ya VIUMBE,NA DUNIA.Maandiko yanasema MUNGU ameumba DUNIA NA VYOOOTE VIUJAZAVYO ULIMENGU.pia ANATUMIA "LOGIC"katika kufafanua concept.DIFINITION YA "LOGIC" ni ability of reasoning,NA PIA kuna individual difference kwahiyo hata capacity of reasoning lazima itofautiane.mfano watu watano ukawapa maandiko hayohayo na ukataka watoe ufafanuzi lazima kila mtu aeleze kwa na namna yake.ila tusisahau kuwa kuna kitu kinaitwa FACT.hii haihitaji uwezo wa mtu wa kufikiri ila nahitaji ichukuliwe kama ilivyo.ila kama ni HISTORIOGRAPHY.we are not study event in such but interpretation of event.NA NDOMANA """MJIMAJI WAR"" Nikweli ilitokea na hakuna wa kutoa maelezo tofauti,,,lakini ufafanuzi kuhusu hilo tukio kila mmoja anasema kutokana na CAPACITY OF REASONING.Mfano,wenine wanasema WALIOPIGNANA WALIKUWA WACHACHE TU WENYE KIU YA DAMU ZA WATU,WAKATI WENGINE WANASEMA,ILIKUWA NIMAPINDUZI DHIDI YA UDHARIMU,,,,,,,biblia inasema MAANDIKO HAYATAFSIRIWI KAMA APENDAVYO MTU.bali hadi kufunuliwa na mungu mwenyewe.MAELEZO MENGINE UNAWEZA UKAJIKUTA UNAKUFURU.Heri uamini mungu yupo hata ukifika usipo mkuta si neno kuliko UMKUTE,itakuwa shida.kumbuka MAWANDISHI HAKUANZA YEYE KU QUESTION UWEZO WA MUNGU WALIKUWEPO WATU KAMA HAO KAMA marxis.nietchzek wa ufaransa anathubutu kusema mungu amekufa,,,,IDEALISM,THEOLOGY NI PANA SANA KULIKO MATERIALISM
 
Mungu ameuumba Viumbe vyooteee, na kuhusu Mungu kuumba Mungu ndio nini jamani, Kwenye Qur'an Mungu sio kitu wala sio kiumbe, si mwanaume wala mwanamke, hajazaa wala hajazaliwa, sasa kazi kwako. NA KUNA VITU NI KWELI MUNGU HAJAVIUMBA MOJA KWA MOJA BALI ALIWAPA VIUMBE VYAKE MAARIFA YA KUVITENGENEZA, Kwa maslah yao wenyewe binadamu. Na pia akatupa MAARIFA AU UTARATIBU WA KUENDELEA KUVIONGEZA VIUMBE VYENGINE NA MAARIFA HAYO MPAKA KWA WANYAMA WANAYO.
 
Kuhusu maradhi kuna Baadhi ya Maradhi naweza kuungana na wewe kuwa Mungu hakuyaleta ila ni kutokana na jinsi Mwanadamu anavyotumia hii dunia ndipo kunapoibua maradhi, na hapo hapo viumbe walopewa ufahamu huvumbua dawa za maradhi hayo, kwa mfano Malari, kipindupindu hivi ni vitu vinatokana na uchafu wa mazingira ndo kunapatikana vizalia vya hayo maradhi, Na ndio mana baadhi ya maeneo hamna maradhi hayo kabsaa kutokana na mazingira kuyatumia vizuri

LAKIN KUNA MARADHI AMBAYO UNAWEZA SEMA NI MUNGU MWENYEWE Labda kama sisi tunaita ugonjwa/Maradhi ila sio hivyo kuna wanaozaliwa kama matahira wale ni vipi?
 
hapa mwandishi anaonekana,anachanganya hoja kati ya VIUMBE,NA DUNIA.Maandiko yanasema MUNGU ameumba DUNIA NA VYOOOTE VIUJAZAVYO ULIMENGU.pia ANATUMIA "LOGIC"katika kufafanua concept.DIFINITION YA "LOGIC" ni ability of reasoning,NA PIA kuna individual difference kwahiyo hata capacity of reasoning lazima itofautiane.mfano watu watano ukawapa maandiko hayohayo na ukataka watoe ufafanuzi lazima kila mtu aeleze kwa na namna yake.ila tusisahau kuwa kuna kitu kinaitwa FACT.hii haihitaji uwezo wa mtu wa kufikiri ila nahitaji ichukuliwe kama ilivyo.ila kama ni HISTORIOGRAPHY.we are not study event in such but interpretation of event.NA NDOMANA """MJIMAJI WAR"" Nikweli ilitokea na hakuna wa kutoa maelezo tofauti,,,lakini ufafanuzi kuhusu hilo tukio kila mmoja anasema kutokana na CAPACITY OF REASONING.Mfano,wenine wanasema WALIOPIGNANA WALIKUWA WACHACHE TU WENYE KIU YA DAMU ZA WATU,WAKATI WENGINE WANASEMA,ILIKUWA NIMAPINDUZI DHIDI YA UDHARIMU,,,,,,,biblia inasema MAANDIKO HAYATAFSIRIWI KAMA APENDAVYO MTU.bali hadi kufunuliwa na mungu mwenyewe.MAELEZO MENGINE UNAWEZA UKAJIKUTA UNAKUFURU.Heri uamini mungu yupo hata ukifika usipo mkuta si neno kuliko UMKUTE,itakuwa shida.kumbuka MAWANDISHI HAKUANZA YEYE KU QUESTION UWEZO WA MUNGU WALIKUWEPO WATU KAMA HAO KAMA marxis.nietchzek wa ufaransa anathubutu kusema mungu amekufa,,,,IDEALISM,THEOLOGY NI PANA SANA KULIKO MATERIALISM
Ukitumia logic, huyu mungu wa Abrahamic religions hayupo, kwa sababu nilizozitaja hapo juu mara lukuki.

Huwezi kuwa na mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote akaumba ulimwengu wenye kuruhusu maovu na mabaya kama huu.

That is a huge logical contradiction.
 
Kuhusu maradhi kuna Baadhi ya Maradhi naweza kuungana na wewe kuwa Mungu hakuyaleta ila ni kutokana na jinsi Mwanadamu anavyotumia hii dunia ndipo kunapoibua maradhi, na hapo hapo viumbe walopewa ufahamu huvumbua dawa za maradhi hayo, kwa mfano Malari, kipindupindu hivi ni vitu vinatokana na uchafu wa mazingira ndo kunapatikana vizalia vya hayo maradhi, Na ndio mana baadhi ya maeneo hamna maradhi hayo kabsaa kutokana na mazingira kuyatumia vizuri

LAKIN KUNA MARADHI AMBAYO UNAWEZA SEMA NI MUNGU MWENYEWE Labda kama sisi tunaita ugonjwa/Maradhi ila sio hivyo kuna wanaozaliwa kama matahira wale ni vipi?
Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao magonjwa yanawezekana kuwepo wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao magonjwa hayawezekani?
 
Nataka wasio amini uwepo wa Mungu wakidai ushahidi kama ww waniambie ni ushahidi gani wakipewa wataamini kama yupo??
Ukinitatulia contradiction hii nitaanza kukusikiliza kwa ku entertain uwepo wa mungu.

Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

This is a logical contradiction that needs to be resolved by logic.

Huhitaji kutoa picha ya mungu au fingerprints zake.

Logic tu.

Unaweza kutatua swali hili?
 
Ukitumia logic, huyu mungu wa Abrahamic religions hayupo, kwa sababu nilizozitaja hapo juu mara lukuki.

Huwezi kuwa na mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote akaumba ulimwengu wenye kuruhusu maovu na mabaya kama huu.

That is a huge logical contradiction.
KIRANGA kama lilivyo jina lako unajitahidi sana kuhangaika kutoa reason zako kwa uwezo wa akili uliyo nayo,,,speculation,,kama ulinielewa kuhusu LOGIC usingekuwa na taabu hii,,,LOGIC kama maana yake ilivyo sio njia nzuri ya kufahamu FACT.sasa kama JAMBO MOJA,ukitumia ability of resoning unapata majibu tofauti kwa kila mtu je LOGIC ni njia nzuri ya kufikia kwenye conclusion???? "your lost brother in the bush of your poor brain"una nikumbusha o level kwenye debate ya """"urban life is better than rural life""" Mpaka leo hatujawahi kufika hitimisho lakusema kuwa KIPI NI BORA KULIKO KIPI....kwa taarifa yako LOGIC is the brunch of epistemology,,,other brunches are like intuitive,authority,revelation.....sasa FUNGUKA.biblia inasema mawazo yake haya chunguziki,mawazo yake si mawazo yetu,njia zake si zetu,KAMA KWELI UNAPENDA KUELEWA SIO KUBISHA NJOO DARASANI
 
VITU SITA AMBAVYO SI VIUMBE VYA MUNGU.

View attachment 331270

Tarehe Mar 2016 niliandika makala juu mahusiano kati Kiza, Mungu, Kifo, Vita, Njaa, na Maradhi. Makala ile ilizua mjadala mkubwa facebook na whatsapp nilipoiweka, na moja jambo kubwa lilotuvuruga ni uwezo na mamlaka ya Mungu katika uumbaji, na hasahasa ile nadharia ya kuwa MUNGU ni muumbaji wa viumbe vyote ilitumiwa sana na watu katika kuikosoa makala yangu.

Awali ya yote nakubali bila kigegezi chochote kuwa Mungu ni muumbaji wa viumbe vyote na ya kwamba ni Mola wa viumbe hivyo. Nakubali kuwa ulimwengu haukuzuka tu wenyewe katika tukio la lisilo ratibiwa. Bali yupo injinia wa Ulimwengu huu ambaye si mwingine bali ni MUNGU.

Misaahafu ya dini za Ibrahim, yaan uislamu, uyaudi na ukristo yote kwa pamoja bila kukhitililafiana inasema ulimwengu na vilivyomo ndani yake havikuzuka kwa bahati mbaya bali vimeumbwa na Mungu.

Kuna viumbe hai kama wanyama na mimea, lakini pia kuna viumbe ambavyo havina uhai kama mawe na mchanga. Vyote hivi Muumbaji wake ni Mungu.

"Mwenyezi Mungu ameumba mbingu na ardhi kwa Haki. Kwa hakika katika hayo ipo Ishara kwa Waumini. " Quran 29:44

"...Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Na Yeye ni Mmoja Mwenye kushinda!..." Quran 13:16

"Mbingu ni mali yako, nchi nayo ni mali yako, Ulimwengu na vyote viujazavyo Ndiwe uliyeupiga msingi wake. Kaskazini na kusini ndiwe uliyeziumba....." Zaburi 89:11-12

Hiyo quran 13:16 inatutanabaisha kuwa Mungu ameumba kila kitu, lakini tujiulize, kitu kilichoumbwa na Mungu kinaitwaje? Kwa vyovyote vile kinaitwa kiumbe. Kama ndivyo tunaweza kuwa sahihi zaidi kama tukisema kuwa Mungu ameumba viumbe vyote badala ya kusema kuwa Mungu ameumba kila kitu.

Twasema kuwa viumbe vyote vimeumbwa na Mungu, je vile ambavyo si viumbe tuna vizungumziaje? Naomba mjue Mungu ameumba viumbe vyote, lakini haimaanishi kuwa ameumba kila kitu. Kuna baadhi ya vitu ambavyo Mungu hakuviumba aidha hakutaka kuviumba au ameshindwa kuviumba.

VITU VIKUU SITA AMBAVYO MUNGU HAKUVIUMBA.

1. MUNGU
Ukisoma misahafu yote mikuu miwili quran na biblia hakuna ushahidi hata mmoja unaonesha kuwa Mungu kaumba Mungu(namaanisha Mungu kujiumba).

Kubwa zaidi katika misahafu hiyo ambayo imeandikwa kwa matakwa yake MUNGU, inaonesha ukuu wa Mungu, uwezo wake, mamlaka yake, utukufu wake, usafi wake na kila aina ya sifa nzuri na tukufu, lakini hatuoni chanzo chake kikiandikwa humo na hatuoni mwisho wake ukiandikwa humo, zaidi ya vitabu hivyo kusema ufalme wa MUNGU na Nguvu zake hazina mwanzo wala mwisho.

"Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi" Ufunuo 1:8

"Na Mola wako Mlezi anayajua yaliyo ficha vifua vyao, na wanayo yatangaza. Naye ni Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye. Sifa zote njema ni zake Yeye, mwanzo na mwisho...." Quran 28:69-70

Kwa aya hizi, na mafundisho mengine ya kinabii kama haya, yanathibitisha bila shaka kuwa ni kweli kuna mambo au vitu ambavyo Mungu hakuviumba na kwasababu hiyo vitu hivyo haviwezi kuitwa viumbe na ingawa viko. Kitu cha kwanza MUNGU, kipo na hakija umbwa.

Wanaosema kuwa MUNGU ameumba kila kitu waje hapa watuambie "MUNGU" kaumbwa na nani? Wakishindwa kututajia basi waishie kusema Mungu kaumba viumbe vyote lakini si vitu vyote.

2. KIZA
Ukisoma hiyo quran 28:69-70 na ukisoma vizuri ufunuo 1:8 utagundua mambo yote na habari zote kabla ya uwepo wa MUNGU hayajulikani na huenda anayajua Mungu mwenyewe, lakini kwetu sisi tunaona mambo hayo kwetu ni KIZA.

Kwa hivyo tunaweza kusema kabla ya Mungu hajaumba chochote alikuwako yeye na Kiza, Kiza ni mwanamke na Mungu ni mwanaume. Kwakuwa kwa kipindi hicho walikuwa wenyewe, na wanajuana wenyewe, jambo jepesi twaweza kusema hivi vitu ni ndugu. Ipo siku inshallah nitakuja kufafanua kwanini nasema Kiza mwanamke na Mungu mwanaume.

"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. 3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. 4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza."
Mwanzo 1:1-4

Katika andika hilo la juu tunajifunza yafuatayo.

A. Mbingu na nchi zimeumbwa na Mungu. Maji, ardhi na vitu vya kufananayo ni sehemu ya mbingu ya nchi.

B. Mungu aliumba NURU lakini hakuumba KIZA, tunaambiwa tu Kiza kilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji lakini hatuambiwi Mungu aliumba Kiza.
Hiyo mwanzo 1:3 "Mungu akasema, iwe Nuru; ikawa Nuru"

Alijuaje kuwa Nuru imekuwa kama kabla ya Nuru hiyo kulikuwa hakuna Kiza? Je, mbona hatuoni maandiko yakionesha Mungu akisema iwe Kiza kisha kikawa Kiza?

C. Ukisoma mwanzo 1:2 tunaona Mungu akiumba mbingu na nchi kisha Kiza alikaa juu ya uso wa vilindi vya maji, kwasababu hiyo, nikisema kuwa Kiza alikuwako kabla ya mbingu na nchi nitakosea? Kama alikuwako kabla ya mbigu na nchi, ama kabla ya ulimwengu, nikisema kuwa Kiza na Mungu waliishi wenyewe kabla ya ulimwengu pia nitakosea?

D. Baada ya Mungu kuumba Nuru, hapo ndipo alipofanikiwa, kumfungia KIZA, na athari za Kiza akaziita USIKU na athari za NURU akaziita MCHANA. Kwahivyo Mungu hakumuumba KIZA, ila Mungu kaumba Nuru, Mchana, na Usiku.

Kwahivyo kama tuko pamoja, utakubaliana na mimi kuwa KIZA ni moja ya kitu ambacho Mungu hakukiumba. KIZA si kiumbe, KIZA kimezuka tu kama alivyozuka Mungu mwenyewe. Tafauti kubwa kati ya MUNGU na KIZA ni kuwa Mungu kaumba na ni Mola wa viumbe vyote, lakini Kiza hakuumba kitu chochote kwa hivyo si MUUMBAJI.

Astronomy inatuambia kuwa ulimwemgu umeundwa na vitu vikuu vitatu, normal matter, dark matter na dark energy. Normal matter ndio hujumuisha zile atoms zilizo tumika kuumba Nyota,sayari, na vitu vingine.

Normal matter ni asilimia 5 tu ya ulimwengu wote, 25% ni dark energy na 70% dark matter. Hiyo dark energy na dark matter athari zake zinaonekana katika zenyewe hazionekane. Hii huenda ndio KIZA ambacho kimetajwa katika mwanzo 1:1

Astronomy pia yatuambia ulimwengu unatanuka kwa kasi, na ya kwamba unazidi kuongezeka kutokana ile motion iliyosababishwa na BING BANG, kutanuka kwake ina maanisha unazidi kumeza au ama kuingia katika sehemu mbele zaidi kutokea kule ulipo anzia(kipind cha dark age) Swali kule unapoelekea kuna nini kama si Kiza??

Astronomy pia yatuambia hakuna empty space, kama inavyo onekana, katika space waweza kuona ama kudhani hakuna maada yoyote, lakini kimsingi asilimia kubwa ya space ina dark energy na dark matter. Vitu hivi vinaashiria uwepo KIZA mbali na ulimwengu tunao ujua.

3. KIFO
Kwanza naomba tukumbuke wakati Mungu anafikiria kuumba ulimwengu tayari kulikuwako na KIZA. Ili Mungu awe kuumba ulimwengu ilikuwa lazima kwanza amuondoshe au amuue KIZA. Ili Kiza kiweze kufa shuruti pawe na "KIFO" Hata hivyo, kutokana na nguvu za Kiza, basi kikawa hakijakufa bali kilifungiwa.(Rejea mwanzo 1:3 Mungu akatenga giza na nuru)

Pili naomba mjue kuwa kiumbe hai cha kwanza kuumbwa na Mungu ni "NENO" kisha wakafuatia malaika wakubwa wanne(four Arc Angels) ambao ni Mikaeli, Raphaeli, Rucifer na Gabrieli. Hoja inakuja, Mungu alitumia kipimo gani kujua kwamba amefanikiwa kuumba kiumbe hai? Kwa vyovyote vile ili ajue kuwa amefanikiwa kuumba kiumbe hai ni lazima alinganishe uhai uliopo ndani ya kiumbe hai na mauti(KIFO). Kwa hivyo kilianza KIFO kabla ya UHAI, na bahati nzuri maandiko yanakubali kuwa Mungu kaumba uhai, lakini hayaoneshi kuwa Mungu kaumba KIFO.

Wachungaji wetu katika makanisa wanakataa katakata kuwa Mungu kaumba KIFO, wao wanasema KIFO kilisababishwa na shetani, bi maana shetani ndio kaumba KIFO. Huku ni kutokujua, lakini hakuna aliyeumba KIFO, KIFO sio kiumbe na alizuka tu kama alivyo zuka Mungu.

Kama nilivyosema ule muda Mungu anafikiria kuumba uhai, tayari kifo kilikuwako, na kwasababu hiyo, pia haijulikani kati ya Mungu na Kifo na mkubwa(kiumri).

Mungu aliumba uhai, na kwa kupitia huo uhai akaumba mwanadamu, lengo lake lilikuwa mwanadamu aishi milele, lakini kifo kikawa kikwazo katika lengo hili.

Sivyo tu, kwakuwa siku zote KIZA anataka atoke kifungoni, hivyo kila siku anapambana na Mungu kwa lengo la kutaka kumuua, na wakati huohuo Mungu naye anataka kumuua KIZA, mshindi wa pambano hili lazima amtumie "KIFO" na hapa ndipo tunapoona nafasi ya KIFO katika mahusiano ya NURU na KIZA.

Lakini Mungu anasema atakuja kumshinda KIZA na KIFO, na pindi atakapo shinda hakuna roho au mwili utakao kufa.

"na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. " Ufunuo 1:18

4. VITA na NJAA
KIZA baada ya kugundua Mungu ameumba malaika wakubwa wanne, KIZA alichukia na hapo yakazuka mapambano kati ya MUNGU na KIZA. Kwa mapambano hayo ndipo ilipozuka "VITA" mungu alichofanikiwa ni kumfungia KIZA, na funguo zake akakabidhiwa Rucifer. Mark of Darkness ndio Funguo na sehemu alofungiwa KIZA, chapa hii baadae iliitwa mark of cain.

Mnyama wa kwanza kuumbwa na Mungu kabla hata ya wanadamu ni Levithans, hawa ndio ile mijusi mikubwa na Magodizilla. hawa walikuwa na "NJAA" sana kiasi walane wenyewe kwa wenyewe, Hapa Mungu kwa kutumia jeshi lake la malaika waliwaondoa dunia na kuwafungua Purgatory. Hapa pia VITA alihitajika kufanikisha hili.

Tembo na vufaru wanapungua kwa kuuliwa na binadamu, hivi Magodizilla na Levithans waliuliwa na nani? Ikiwa wao walikuwako miaka mingi kabla ya wanadamu? Jibu jepesi ni upanga wa Malaika Mikael na jeshi lakd.

Wakati hayo yakitokea, Darkness akaigeuza ile mark kuwa laana, na laana ile ikasababisha hali ya uasi kwa mtunza funguo. Wakati Mungu anamuumba mwanadamu, na malaika kuambiwa wamsujudie, Rucifer akiwa kesha athiriwa na laana ya funguo akagoma kumsujidia adamu.

Kwa mara nyingine "VITA" ilihitajika katika kumdhibiti Rucifer na kundi lake.

6 MARADHI
mungu hakuumba maradhi, na wala si lengo mungu mwanadamu aumwe na kuteseka kwa maradhi. Ila pale mwanadamu alipoumbwa na afya bora kabisa, na maradhi yakazuka hapo hapo. Baada ya Mungu kuja kumshinda KIFO, pia atakuja kuyashinda MARADHI, na hayo yakitokea katika maisha Paradiso hakutakuwa na KIFO wala MARADHI.

MWISHO.
makala hii haina tafauti na ya juzi, ila leo baadhi ya nukta nimemua kuziongelea kwa undani zaidi ili iweze kujibu maswali na hoja zilizo jitokeza katika makala ya msingi. Hata hivyo najua siwezi kumaliza kila kitu hapa, ila mengine tutajifunza katika mjadala!

Njano5
0622845394
Safi bana doto kwa kushare knowledge ila kuna mambo mawili nikuweke sawa kuhusu utafsiri wako wa viumbe...kwa muujibu wa hali ya kibinadamu viumbe vipo vya aina mbili hai au sio hai ILA KWA MUNGU KWAKE VYOTE NI HAI NA VYOTE VINAMUABUDU MAANA VINAMFATA VILE ATAKAVYO NA HADI KUONGEA NAVYO..vinavyoonekana na visivyoonekana..vinavyoweza kuhisika au visivyoweza..sasa ukisema neno KIUMBE akili ya mwenye lugha kwa haraka itamleta kwenye hivi vinavyoshikika bila ya kudhania kuwa kuna baadhi ya vitu alivyoviumba mungu haviwezi shikika au hata kufikirika kuwa ni viumbe bali mwanadamu ataita kama ni halifulani tuu ambayo ipo..mfano wa viumbe hivyo ni
1.KIFO... kifo ni kiumbe ambacho ni chakwanza kuumbwa kabla ya uhai..ktk qurani mungu anaeleza kuwa aliumba kifo baadae ndo akaumba uhai anatueleza sisi sasa hapo kwa hali ya kiubinaadamu ili tumuelewe ila jua kuwa kwake vyote ni hai.
2.MARADHI..qurani na hadithi zinasema mungu kaumba maradhi na dawa zake..ndo mana sheikh yoyote msomi ukimwambia ukimwi hauna dawa anakataa.
3.KIZA..qurani na hadithi zasema mungu aliumba mchana na usiku kwa kiarabu ilmeandikwa aliumba nuru yaani mwanga na kiza..kiswahili tumetafsiri usiku na mchana..so kiza ni kiumbe cha mwenyezimungu kinacho mtii vizuri tuu kila siku kiza lazima kijioneshe na kuondoka kama kilivyoagizwa na muumba.
4.VITA NA NJAA..nimeona unasema kuwa mwingi wa rehema muumba mbingu na ardhi alikuwa na vita na lusifer??? SO nkaona ukatumia mwanya huo ya kueleza kuwa vita ilitokea bila wiling ya mungu so nikiumbe ambacho hakikuumbwa na mungu????Hiyo ni misconception ya kitabu ulichokitumia..HAKUNA KIUMBE ANAEWEZA KUFANYA VITA NA MUNGU ALIEUMBA mbingu ardhi galaxy na kumpa akilimwanadamu kutengeza smartphone[emoji2] na mengineyo mengii sana by intuition.
Kuhusu shetani lusifer na mungu ilikuwa hivi
"Kabla ya mwanadamu palikuwa na viumbe wengine wakiwemo majini na malaika katika ufalme wa mungu ..tofauti iliopo ni kuwa malaika aliumbwa na nuru na walikuwa ni wenye kutii kile wanachoagizwa ila majini waliumbwa kwa moto na waliumbwa kuwa na uhuru yaani choice kuwa wafwate maagizo au wasifuate kama vile mwanadamu ananjia mbili awe muumini au kafiri...majini wakawa makafiri exept mmoja ambaye ni ibilisi mungu akaangamiza wete akamwacha ibilisi....kwa muda tusioujua mungu akaanza kuumba kiumbe kwa kutumia udogo ulovunda ..mungu atoa amri juu ya kiumbe alichoumba ..malaika wakakubali ila ibilisi akasema MIMI NI MMBORA KULIKO HUYU MIMI NIMEUMBWA KWA MOTO YEYE AMEUMBWA KWA UDOGO ULOVUNDA mungu akasema mbora ni yule anaenifata nitakachosema so ibilisi akapewa laana na mungu then akapewa nafasi ya kujitetea akasema ANAOMBA AWE NA PAWA YA KUWAPOTEZA WATU KWA KUWASHAURI VIBAYA ILI NAO WALANIWE KAMA YEYE..mungu akampa hiyo pawa ila akamwambia hutoweza kumpoteza mtu mpaka mungu yeye atake...kiunyonge ibilisi akapokea laana hiyo naw tuponae huku duniani tunakulanae shida za magufuli KIUNYONGEE BILA HATA VURUGU..kama ungebaatika kuona sura ya ibilisi ungemuonea huruma anahaha...alafu ndo useme alileta VITA NA MUNGU??

KWA POINT YA KWANZA KUHUSU MUNGU VIPI AMEJIUMBA YAANI MUNGU KUUMBA MUNGU...hii nakueleza kimfano ..ushawahi pita sehemu ng'ombe akawa anakutazamaaa mpaka unamalizikia au umepewa hesabu unashindwa hata pakuanzia kiufanya(CALUKULAS) hivyo nilivyosema hapo vinaashiria kuwa mwanadamu kunabaadhi ya vitu hawezi kufikiria ..ukiambiwa mungu hana mwanzo wala mwisho huwezi kuelewa hata kidogo ukikaaukafikiria kuhusu mwanzo wake utashindwa tuu...so kunabaadhi ya vitu mungu kaweka siri kwa mwanadamu kuvitambua
SO KUSEMA MUNGU HAJAUMBA MUNGU inakosa mantiki kwa sababu mungu hakuzaa wa hakuzaliwa na afanani na vitu au viumbe alivyoumba..hana mwanzo wala mwisho.

CONCLUSION
Soma kwa umakini vitabu vya dini uvielewe usichukue mstari mmoja mmoja na pia angalia kitabu kipi unatumia kufanya reference ukichanganya utakosa majibu..vingine vinasema kuna mungu watatu vingine mmoja..na vingine vinachanganya kweli akiliza watu na ndo maana madhebu yamejitokeza mengi sana kwa sababu ya udhaifu wa baadhi ya vitabu vya dini...nimetumia qurani kukujibu ambayo ina zaburi njili ya isa bin mariam na taurati ya musa.
 
KIRANGA kama lilivyo jina lako unajitahidi sana kuhangaika kutoa reason zako kwa uwezo wa akili uliyo nayo,,,speculation,,kama ulinielewa kuhusu LOGIC usingekuwa na taabu hii,,,LOGIC kama maana yake ilivyo sio njia nzuri ya kufahamu FACT.sasa kama JAMBO MOJA,ukitumia ability of resoning unapata majibu tofauti kwa kila mtu je LOGIC ni njia nzuri ya kufikia kwenye conclusion???? "your lost brother in the bush of your poor brain"una nikumbusha o level kwenye debate ya """"urban life is better than rural life""" Mpaka leo hatujawahi kufika hitimisho lakusema kuwa KIPI NI BORA KULIKO KIPI....kwa taarifa yako LOGIC is the brunch of epistemology,,,other brunches are like intuitive,authority,revelation.....sasa FUNGUKA.biblia inasema mawazo yake haya chunguziki,mawazo yake si mawazo yetu,njia zake si zetu,KAMA KWELI UNAPENDA KUELEWA SIO KUBISHA NJOO DARASANI
Unajuaje kwamba mungu yupo na mawazo yake hayachunguziki kweli, na kwamba hii si story tu ambayo imetungwa na watu waliotaka kuuelezea ulimwengu ambao hawauelewi?

Nimeuliza swali, kwa nini mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati ana uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Ukiniambia mawazo yake hayachunguziki kimsingi unaniambia unaamini katika mungu usiyemuelewa na ambaye hawezi kueleweka.

Na kama unaamini katika mungu ambaye humuelewi na wala haeleweki, utajuaje kwamba yupo na si hadithi tu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom