Vitu sita ambavyo si viumbe vya Mungu

Vitu sita ambavyo si viumbe vya Mungu

Kabla ya kusema mungu kaumba hiki na kile, unaweza kuthibitisha kwamba yupo at all?

Kuthibitisha uwepo wa Mungu hiyo ni akili, na nimekueleza akili haiwezi kuelewa what is God, unahitaji kitu kikubwa zaidi ya akili ili kuwa na ufahamu wa juu kukuwezesha kutambua Mungu ni nini na hata wewe ni nani? Sio kwa kutumia akili.
 
Nina neno moja tu kwa mtoa mada we ni kichwa uwezo wako kufikiria uko guru hujafungwa na imani, safi sana
 
Kuthibitisha uwepo wa Mungu hiyo ni akili, na nimekueleza akili haiwezi kuelewa what is God, unahitaji kitu kikubwa zaidi ya akili ili kuwa na ufahamu wa juu kukuwezesha kutambua Mungu ni nini na hata wewe ni nani? Sio kwa kutumia akili.
Kama akili haiwezi kuelewa what is god, utajuaje kwamba yupo na si hadithi tu?

Utatumia nini kujua mungu yupo na utajuaje kwamba unachofikiri ni sawa na si wishful thinking tu?
 
Na ukweli ni kwamba hio contradiction haiwezi kutatuliwa kitu ambacho kinatupeleka kwenye hitimisho kuwa hayupo

Wewe unauhakika gani kwamba Mungu ameumba hivyo vitu vyote ulivyovitaja? Je ulikuwepo? Uliona? How do you prove it?
 
Hayo ni mawazo yako tena ni tone tu kwa uwezo wa uumbaji wa Mungu.tena Mungu wa Eliya.Mungu ni zaidi ya fikra zako sema Imekuwa
 
Kama akili haiwezi kuelewa what is god, utajuaje kwamba yupo na si hadithi tu?

Utatumia nini kujua mungu yupo na utajuaje kwamba unachofikiri ni sawa na si wishful thinking tu?

Unahitaji kutumia kitu zaidi ya akili ili kukuza ufahamu wako kuweza kuelewa what is God and what is not, kama upo Dar inabidi ufike Chang'ombe Maduka Mawili ili ufundishwe Meditation ni mbinu ambayo itakusaidia kukuza ufahamu wako kwa hatua mbalimbali na utaanza kuelewa vitu vilivyo zaidi ya akili yako. Kwa sababu binadamu ndani yake anauwezo mkubwa kuliko anvyoweza kujifikiria ila kwa sababu amejazwa hofu nyingi , amenyimwa au amepewa taarifa ambazo si sahihi kuhusu Mungu amekuwa na contradictions nyingi then ule uwezo wake pia umekuwa suppressed kwa sababu hajui namna ya kuamsha kwa sababu hakufundishwa.
 
Hayo ni mawazo yako tena ni tone tu kwa uwezo wa uumbaji wa Mungu.tena Mungu wa Eliya.Mungu ni zaidi ya fikra zako sema Imekuwa

Wewe usiweke limit katika Mungu! Mungu hana Mipaka. God is not a person as you can think.
 
Wewe usiweke limit katika Mungu! Mungu hana Mipaka. God is not a person as you can think.
Mi sijasema neno mipaka.nimekwambia hayo ni mawazo yako tena ni kidogo sana juu ya uwezo wa uumbaji wa Mungu.sema Amen
 
Vitu vingine vinamajibu rahisi lkn watu wanasumbuka cjui nn.
Ukisema kwa nini Mungu asingeumba ulimwengu usio na dhambi wakti yy ndo anamamlaka yote unakosea.
Ukisoma Yeremia 29:11 mungu anasema mipango yake nikutuwazia mema wakati wote. Mwanzo kabisa Mungu aliumba Ulimwengu ulio perfect usio na dhambi ambamo aliishi Adam na Hawa. Ila kuna siri moja kubwa Mungu alimuumbia Adam na Hawa.....UWEZO WA KUJICHAGULIA MEMA NA MABAYA.... na tunaona Hawa alitumia uwezo huu akachagua kusikiliza nyoka na ikaletea maasi kwa kizazi chake chote. Pia Lucifer alitumia huu uwezo na akaasi mbinguni akiwa na malaika zake. Hta leo kila mtu ana hii nguvu bado.
Waweza kuniuliza ni kwa nini Mungu asingeondoa hii nguvu ya uhuru wakujichagualia mema na mabaya na akatuwekea moja tuu yakuchagua mema ili tusitende dhambi tena?
Jibu la swali hili linapatikana Warumi 9.
Mfinyanzi anapoandaa udongo kwa kutengeneza chombo huwa anatengeneza chombo akiwa na makusudi maalum na akizingatia matumizi ya chombo hicho.
Anaweza akatengeneza cha kikombe,chungu,kinu na kadhilika...huo ni uamuzi wake. Pia anaweza akatengeneza kingine kwa ajili ya matumizi yakawaida na kingine kwa matumizi ya kifalme. Je hicho chombo kina mamlaka gano ya kumuuliza mfinyanzi kwa nini umenitengeneza hivi?
Wanadamu ni kazi ya ifinyanzi ya Mungu....wew ni nani na unamamlaka gani kumuuliza Mungu kwa nini ameumba ulimwengu jinsi ulivyo na akaweka hiyo nguvu ya kujiamulia(willing power) ndani yetu????


1 Nasema ukweli mtupu; nimeungana na Kristo nami sisemi uongo. Dhamiri yangu ikiongozwa na Roho Mtakatifu inanithibitishia jambo hili pia. 2 Nataka kusema hivi: nina huzuni kubwa na maumivu yasiyopimika moyoni mwangu 3 kwa ajili ya watu wangu, walio damu moja nami! Kama ingekuwa kwa faida yao, ningekuwa radhi kulaaniwa na kutengwa na Kristo. 4 Hao ndio watu wa Israeli ambao Mungu aliwateua wawe watoto wake, akawashirikisha utukufu wake; aliagana nao, akawapa Sheria yake, imani ya kweli na ahadi zake. 5 Wao ni wajukuu wa mababu, naye Kristo, kadiri ya ubinadamu wake, ametoka katika ukoo wao. Mungu atawalaye juu ya yote, na atukuzwe milele! Amina.

6 Sisemi kwamba ahadi ya Mungu imebatilika; maana si watu wote wa Israeli ni wateule wa Mungu. 7 Wala, si wazawa wote wa Abrahamu ni watoto wake wa kweli. Ila, kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Wazao wake watatokana na Isaka." 8 Nido kusema, wale waliozaliwa kimaumbile ndio watoto wa Mungu, bali wale waliozaliwa kutokana na ahadi ya Mungu ndio watakaoitwa watoto wake. 9 Maana ahadi yenyewe ni hii: "Nitakujia wakati maalum, naye Sara atapata mtoto." 10 Tena si hayo tu ila pia Rebeka naye alipata mapacha kwa baba mmoja, yaani Isaka, babu yetu. 11 Lakini, ili Mungu aonekane kwamba anao uhuru wa kuchagua, hata kabla wale ndugu hawajazaliwa na kabla hawajaweza kupambanua jema na baya, 12 Rebeka aliambiwa kwamba yule mtoto wa kwanza atamtumikia yule wa nyuma. Hivyo uchaguzi wa Mungu unategemea jinsi anavyoita mwenyewe, na si matendo ya binadamu.13 Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: "Yakobo nilimpenda, lakini Esau nilimchukia."

14 Basi, tuseme nini? Je, Mungu amekosa haki? Hata kidogo! 15 Maana alimwambia Mose: "Nitamhurumia mtu yeyote ninayetaka kumhurumia; nitamwonea huruma mtu yeyote ninayetaka." 16 Kwa hiyo, yote hutegemea huruma ya Mungu, na si bidii au mapenzi ya mtu. 17 Maana Maandiko Matakatifu yasema hivi kwa Farao: "Nilikufanya mfalme ili kwa njia yako, uwezo wangu ujulikane, na jina langu litangazwe popote duniani." 18 Ni wazi, basi, kwamba Mungu humhurumia yeyote anayetaka kumhurumia, na akipenda kumfanya mtu awe mkaidi, hufanya hivyo.

19 Labda utaniuliza: "Ikiwa mambo yako hivyo, Mungu anawezaje kumlaumu mtu? Nani awezaye kuyapinga mapenzi yake?" 20 Lakini, ewe binadamu, u nani hata uthubutu kumhoji Mungu? Je, chungu chaweza kumwuliza mfinyanzi wake: "Kwa nini umenitengeneza namna hii?" 21 Mfinyanzi anaweza kuutumia udongo apendavyo na kufinyanga vyungu viwili kwa udongo uleule; kimoja kwa matumizi ya heshima, na kingine kwa matumizi ya kawaida. 22 Hivyo ndivyo ilivyo kwa Mungu. Alitaka kuonyesha ghadhabu yake na kujulisha uwezo wake, Basi, alikuwa na saburi sana, akiwavumilia wale ambao walikuwa lengo la ghadhabu yake, ambao walistahili kuangamizwa. 23 Alitaka pia kudhihirisha wingi wa utukufu wake ambao alitumiminia sisi tulio lengo la huruma yake; sisi ambao alikwisha kututayarisha kuupokea utukufu wake. 24 Maana sisi ndio hao aliowaita, si tu kutoka miongoni mwa Wayahudi bali pia kutoka kwa watu wa mataifa mengine.

25 Maana ndivyo asemavyo katika kitabu cha Hosea: "Wale waliokuwa Si watu wangu nitawaita: Watu wangu! Naye Sikupendi ataitwa: Mpenzi wangu!

26 Na pale walipoambiwa: Ninyi si wangu hapo wataitwa: Watoto wa Mungu hai."

27 Naye nabii Isaya, kuhusu Israeli anapaaza sauti: "Hata kama watoto wa Israeli ni wengi kama mchanga wa pwani, ni wachache tu watakaookolewa; 28 maana, Bwana ataitekeleza upesi hukumu yake kamili juu ya ulimwengu wote."

29 Ni kama Isaya alivyosema hapo awali: "Kama Bwana Mwenye Nguvu asingalituachia baadhi ya watoto wa Israeli, tungalikwisha kuwa kama Sodoma, tungalikwisha kuwa ma Gomora."

30 Basi, tuseme nini? Ni hivi: watu wa mataifa ambao hawakutafuta kukubaliwa kuwa waadilifu, wamekubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya imani, 31 hali watu wa Israeli waliokuwa wakitafuta Sheria iletayo kukubaliwa kuwa waadilifu, hawakuipata. 32 Kwa nini? Kwa sababu walitegemea matendo yao badala ya kutegemea imani. Walijikwaa juu ya jiwe la kujikwaa

33 kama yesemavyo Maandiko Matakatifu: "Tazama! Naweka huko Sioni jiwe likwazalo, mwamba utakaowafanya watu waanguke. Mtu atakayemwamini yeye aliye hilo jiwe, hataaibishwa!"
 
Hujathibitisha, umeandika tu "Mungu yupo".

Unafahamu tofauti ya kuthibitisha mungu yupo na kuandika "Mungu yupo" ?

Unaweza kuthibitisha mungu yupo?
Kiranga takuja kuwa kama Donard Trump wa Marekani we jua kianzia leo kuwa Mungu yupo.Amen
 
Mi sijasema neno mipaka.nimekwambia hayo ni mawazo yako tena ni kidogo sana juu ya uwezo wa uumbaji wa Mungu.sema Amen

Swala la kuniambia niseme amen huo ni utumwa uliopitiliza kwa sababu niseme au nisiseme amen siongezi wala sipunguzi chochote kwa Mungu kwa sababu Mungu ni Ukamilifu. Mipaka maana yake unagawa kitu, umesema Mungu wa Eliya ambaye inawezekana akawa tofauti na mungu wa Raju, hapo umeweka mipaka mkuu
 
Kabla ya kusema mungu hana mipaka, unaweza kuthibitisha kwamba yupo?

Kuthibitisha Uwepo wa Mungu inabidi uachane na huo mwili, akili na hisia zako ndio utathibitisha uwepo wa mungu, kwa sababu mtu huwezi kujipa kitu kikubwa kuzidi uwezo wako
 
Kuthibitisha Uwepo wa Mungu inabidi uachane na huo mwili, akili na hisia zako ndio utathibitisha uwepo wa mungu, kwa sababu mtu huwezi kujipa kitu kikubwa kuzidi uwezo wako
Unajuaje kwamba mungu yupo na hii si habari ya hadithi isiyo ukweli?
 
Tufanye Mungu hayupo, sasa nieleze kwa nini wewe upo duniani. Nini lengo la uwepo wako?
Kwa nini unafikiri ni lazima kuwe na lengo?

Na hata nikikwambia sijui, hilo linathibitishaje kuwapo kwa mungu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom