Vitu gani vinamfanya Mwanamme "anyemelee" nyumba yake mwenyewe?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Baada ya furaha za mwanzo za maisha ya pamoja kuna baadhi ya wanaume huanza kunyemelea nyumba zao wenyewe. Mtu toka anatoka kazini anapiga mahesabu ya jinsi gani ataingia nyumbani bila kusababisha mfarakano. Wengine huja na giza za 'uchovu' wengine huja na giza 'kukasirishwa' na mtu huko na wengine huja na hata gia za 'unyonge'. Lengo la gia hizo zote na nyingine nyingi ni kutuliza hasira za mwenza wake pale nyumbani. Lakini wakati mwingine, mwanamme anaingia nyumbani kwa kunyemelea kwa sababu ya hofu ya kile atakachokikuta nyumbani siku hiyo.

Ni vitu gani hasa vinaweza kumfanya mwanamme apaone nyumbani pake pa chungu na hivyo kutafuta kila sababu ya kuchelewa au hata kukwepa kulala nyumbani siku fulani fulani?
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Mwenza kutoa makucha yake na kuonesha rangi zake halisi kisha home panakuwa jehanam.... Nimesahau kuna aya moja kwenye kitabu cha Methali inasema ni heri kukaa katika pembe ya dari kuliko kuishi na mwanamke mgomvi ndani....
 
mkewake kumtendea kinyume na matarajio ya mtima wake,mfano:mwanamke kuwa na ulimi mchungu zaidi ya shubiri kwa mumewe.

Kuwa na matendo yanayomfanya mume apaone nyumbani kwake ni TARIME ndogo.

Yote ya yote ni Ni Maudhi ya jumlajumla kwa mwenza wake ndo chazo kikuu.
 
Lakini tunaweza tukajiuliza kwanini hawa wanawake wamekuwa wagomvi na wakorofi???!! Lakini kuna chanzo ambacho nafikiri mume hakuweza kukishughulikia mapema mpaka ikafika hakuna amani ndani ya nyumba. Binafsi, nafikiri pia kutokuwa na mawasiliano kati ya mume na mke inachangia sana kuvuruga amani.
 
kuna wanawake wanabadilika sana baada ya kuingia kwenye ndoa na ndo hapo mwanaume anapoanza kunyata kuingia kwake.
 
Kwa kawaida katika ndoa wanaume ndiyo wanauza (wananyang'anywa) uhuru wao zaidi ya wanawake (kutokana na mila na desturi zetu),
Kipindi cha upya wa ndoa, wanaume huwa wana pretend au wa act tabia ambazo kimsingi sio tabia zao asilia, kwa hiyo inapotokea ndoa imekomaa kidogo, wanaume hurudi katika ile tabia ya awali, yaani kutokuzoea kuchungwa, kurudi usiku, kulewa, umalaya na kadhalika.
Sasa hapo ndo zinaanza songombingo, risala na magomvi yasiyo isha na nyumbani kuonekana kama jehanamu ndogo.
Ili kujihami wanaume wanaanza kunyatia, maana moyoni wanajua wamewatendea wenzi wao ndivyo sivyo.
 
Hii mada imenifanya nicheke sana. Nahisi kama vile Mwanakijiji huwaga anaanzisha mada kutokana na experiences zake mwenyewe teh teh teh.

Wee Mwanakijiji, bibi umemfanya nini tena?
 
Baada ya furaha za mwanzo za maisha ya pamoja kuna baadhi ya wanaume huanza kunyemelea nyumba zao wenyewe. Mtu toka anatoka kazini anapiga mahesabu ya jinsi gani ataingia nyumbani bila kusababisha mfarakano. Wengine huja na giza za 'uchovu' wengine huja na giza 'kukasirishwa' na mtu huko na wengine huja na hata gia za 'unyonge'. Lengo la gia hizo zote na nyingine nyingi ni kutuliza hasira za mwenza wake pale nyumbani. Lakini wakati mwingine, mwanamme anaingia nyumbani kwa kunyemelea kwa sababu ya hofu ya kile atakachokikuta nyumbani siku hiyo. <br /> wanawake wa siku hizi wababe mno! fanya mzaha unaota manundu!!!!!!!!!
<br />
Ni vitu gani hasa vinaweza kumfanya mwanamme apaone nyumbani pake pa chungu na hivyo kutafuta kila sababu ya kuchelewa au hata kukwepa kulala nyumbani siku fulani fulani?
<br />
<br />
 
1. Kama mkeo ni vuvuzela
2. Kama umechakachua bila kijiamini ( mwenyewe unajistukia)
3. Kama mke ulie naye ulimpenda kwa sababu, na ile sababu haipo tena
4. Kama hukuacha hela ya matumizi home (uchumi mbovu) huna hata uhakika kama pamelika msosi siku hiyo ......... n.k n.k
 
sipendi kelele na sipendi kumpigia mtu kelele, usipochunga ulimi wako hasa wanawake, utamkimbiza mpenzi wako hivihivi unaona
 
huna mshiko na list of demands ya mwanamke inazid kukua.
 
Huyo anayenyata na visingizio vingine kama kachoka lazima ametoka kufanya uzinzi nyumba ndogo hivyo anafanya makusudi kuharibu mazingira ya kuombwa tena ndani maana reading through posts most men hawana nguvu za kupiga mara mbili though unakuta huyo huyo ana nyumba ndogo tatu na anaziudumia once a week each siku zilizobaki anasaidiwa na wenzie .

1. Kama mkeo ni vuvuzela
2. Kama umechakachua bila kijiamini ( mwenyewe unajistukia)
3. Kama mke ulie naye ulimpenda kwa sababu, na ile sababu haipo tena
4. Kama hukuacha hela ya matumizi home (uchumi mbovu) huna hata uhakika kama pamelika msosi siku hiyo ......... n.k n.k
 
masuala ya pesa ndio nambari wani....

mengine ni gubu tu.....la wanawake
 
Back
Top Bottom