Kuna hali gani hapo mtaani kwenu?

o_2

JF-Expert Member
Jul 20, 2017
348
287
Wanajamii salama? Muhali gani?

Katika hali ya kawaida kabisa kila sehemu, mahali kuna hali yake fulani ya tofauti. Inaweza kuwa hali ya hewa, hali ya kiuchumi, hali fulani hivi ya utulivu.. burudani nakadhalika.

Kila sehemu kuna mambo yake na nyakati zake. Kuna watu sasa hivi ndio wanarudi makazini wengine ndio wanatoka kwenda kutafuta... wengine hawajui wafanye nini kwa maana hawana cha kufanya.

Muda huu kuna mtu anafikiria giza liingie aende akaibe... mwingine anafikiria giza linaingia atalala wapi. Mwingine anafikiria aende kijiweni akanywe kasusu na pweza. Mwingine aende kwenye uasherati na uzinzi. Yaani kila jamii kila mtaa kuna hali fulani ya tofauti.

Hali ya mvua wapo wanafurahia. Watauza makoti, masweta na mabuti ya mvua, myamvuli. Lakini kuna watu hali ya mvua wanapata wasiwasi mafuriko yatakuwaje, itakuaje? Nyumbani patalalilika...

Sasa hebu tiririka hapa tuambie kuna hali gani hapo mtaani kwenu? Nyumbani kwenu?

Usiku wa deni.
 
Back
Top Bottom