Vitu gani vya kufanya vya uzalishaji ili usiboreke kukaa kwenye ofisi isiyo na schedule

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,587
44,832
Niliwahi kusikia baadhi ya watumishi katika taasisi au mashirika fulani fulani hawana cha kufanya ofisini ni kama kula tu mshahara wa Bure na kula umeme tu wa serikali. Kama ni mtu mzima anayekaribia kustaafu Sawa maana alitumika amechoka acha akakae tu ofisini apulizwe feni na AC, anywe Chai asubuhi ikifika mchana aagize chakula saa tisa arudi nyumbani au aende bar.

ILa Kwa kijana huwa inaboa sana ni kweli umesoma fani fulani hasa zile ambazo unahitajika zaidi uende field kweli ukabahatika kupata ajira, of course Kwa nguvu za ujana unatamani ufanye activities nyingi huko site za kukujenga uwe mbobezi sometimes hata usilipwe posho kamili ila unafurahi kufanya kazi ili kujifunza mengi kuisadia pia serikali wananchi wapate huduma.

Ila unakutana na sentensi kwamba hakuna program yoyote Kwa kuwa hakuna Hela licha ya kusikia bajeti ikiongezeka kila kukicha katika mawizara ila kiuhalisia ukija taasisini unakuta kumekauka hata OC za kuendesha office zinatoka Kwa shida yaani uwapigie pigie simu wakuu na wahasibu zaidi ya Mara 10.

Kwa situation kama Hizo unashauri kijana ujifunze skill gani rahisi ambayo kipindi umekaa kwenye kiti ofisini unaweza kuendelea kuifanyia kazi na ikakuzalishia kipato na isiwe na athari ofisini.

Maana huwezi kusema ubebe cherehani ukakae nayo ofisini uwe unashona huo utakuwa ni uongo nataman kujua vitu fulani simple kama vile kutengeneza culture za shanga,n. K.. Kawe hata kama ni kamashine fulani kadogo ila kanazalisha bidhaa ndogo ndogo Hivi ili masaa haya tisa ya siku za kazi yasipotee Bure kama kwenye michoro yao hawakuiti we uendelee na Michongo yako.

Na kama utanishauri vitu vya mtandaoni sijui content creator, blog, freelance basi unifafanulie deep unipe na ideas kamili. Natanguliza shukrani.
 
Kuna watu muna bahati, naombaga Mungu nipate hio package ya kuwa na pesa na muda at the same time alafu free office space
Pesa gani Kaka watumish hatunaga Hela mshahara huo unakauka ndani ya siku mbili.. Ponea yetu ni vi per diem kidogo ili kufukia mashimo katikati ya mwezi sasa hivo usipobahatika ndo lazima uwaze nje ya box.
 
Inategemeana na mazingira ya ofisi ulipo. Maeneo mengine hata mtandao wa simu hamna labda uchukue jembe ukalime
Assume ofisi kwanza mko wachache maybe watano na kila mtu Ana chumba chake full access, fen,computer nzuri yenye uwezo kasoro Wi-Fi tu. Ila mtandao sio shida.
 
Pesa gani Kaka watumish hatunaga Hela mshahara huo unakauka ndani ya siku mbili.. Ponea yetu ni vi per diem kidogo ili kufukia mashimo katikati ya mwezi sasa hivo usipobahatika ndo lazima uwaze nje ya box.
Nikisema pesa simaanishi utajiri mzee pesa hiohio laki tatu tatu, kitaalamu formula ni mtu ukiwa Free unakuwa huna pesa (Jobless) na ukiwa na pesa unakuwa haupo free (Employed).

Kupata hio combo ya kuwa na kazi na unamuda angalau wakufanya kitu ni baraka nayomuomba Mungu, nina vingi vya kufanya mfano kwasasa nipo tatizo pesa sina yakuwa hata na vifaa vya kufanyia navyotaka na pesa ya kuendesha utekelezaji.
 
Ndo nishauri sea beast mimi ningeweza mambo ya blog n. K ila Sina idea Kaka
For me ningefanya Blogging na Mobile Applications.

Blog naangaliaga kama njia rahisi zaidi ya mtandao na inayoeleweka na haina konakona, muda ambao unakuwa free unaweka headphone zako sauti ya chini unaandaa makala zako tu bila haraka.

Sasa suala la passion ya mtu kama mimi nina passion ya kutumia Computer tu na masuala ya Afya niliweza kuandika makala ziaid ya 130 zenye zaidi ya maneno 800 kila moja hapo uku nikatafuta pesa ya kulipia WordPress nk

Niliishia njiank sababu za kiuchumi na hapo sikuwa huo muda mqingi free kazini most makala niliandika weekend sasa nikiwa na kazi ya mshahara mzuri, free time ya kutosha, WiFi na office space nzuri I'll change this world.
 
Mkuu naona unakuja kuja kama nakupata Hivi aisee madini zaidi ya haya naweza kuyajuaje zaidi.
 
Kaka. Kutengenezewa blog kali kabisa isiyosumbua shilingi ngapi ikaunganishwa kabisa na mambo za malipo?
 
Mkuu naona unakuja kuja kama nakupata Hivi aisee madini zaidi ya haya naweza kuyajuaje zaidi.
Blagging
1)Uwe na vifaa kama Laptop, Smartphone, Internet na Cash atleast 150,000 kwa kulioia WordPress hio ita cover malipo ya domain, templates nk wataalamu watamaliza izo ishu wewe unahitaji kuwa na hio amount tu.

2)Kwanza utilities anza kuwa na bidhaa za kuoeleka sokoni (Contents/Makala), chagua Niche unayoona unaiweza na kuipenda. Niche kama ya Mazoezi, online businesses na Mapenzi ndio zinapendwa Duniani.

3)Ukishachagua Niche mfano Mapenzi, andaa list ya mada/makala zako Mfano:-
Jinsi ya kutongoza
Jinsi ya kumfanya mpenzi akupende
Saikolojia ya mwanamke na maoenzi
Nk

Ukishakuwa na hizo Heading tu unaweza kuiandikia mada ndefu ya maneno kibao those content unaandika from head na zengine zipo online una paraphrase tu just una flow ukiwa unapenda kuandika

Heading unaweza buni from scratch na kwa ku search Mfano ukiandika Google "Jinsi ya kutongo..." kabla ujamaliza unaletewa predicted sentensi zaidi ya 20 hizo zote unachukua zinakuwa Heading tiali 20 unazitengenezea mada, so unajikuta una mada zaidi ya 300 za kuandika kwenye list.

4)Ukishaandika mada zaidi ya 50 naku regard kama mtu ambae ushakuqa seriously na unachofanya, lipia Domain WordPress uanze kupakia makala zako kwa utaratibu maalum kilasiku uwe unapakia mada hata moja

5)Mada zikiwa kwa kiingereza safi zaidi maana utalenga population ya Dunia, pia hautasumbuliwa ba Google.

Mengine search ishu za technical nk kuna mambo mengi ukiwa na passion ya ku type unaflow
 
Huwzi pata vyote ukipata pesa hupati mda ukipata mda hupati pesa.
Mfano vijijini watumishi Wana muda na sio pesa ni kujiongeza tu shughuli binafsi
Ndio ilivyo hivyo, ila kuna aina ya kazi inakupa alumni kidogo ya muda kama alivyosema mtoa mada ila kupata jumla jumla umelala geto una millions zinaingia kwa account ngumu
 
150,000 inatosha malipo unaunga baadae kwanza Trafficking
Asante sana kwa maelezo yako mazuri sana Nina hoja mbili nifafanulie..

Mimi napenda kukaa sana na walevi hasa wa pombe za kienyeji tukiwa nao kwenye kikao naona katika stori wanaongelea mambo mchanganyiko so yale ndo ningependa kuyawasilisha ila kuwachukua video sio jambo zuri. So ningependa iwe content mixer iwe kama ile ya miladi ayo ilivyo..

LA pili ni Wataalamu gani wa IT wenye kampuni nzuri ya kutengeneza blog ila pia kuilink vizuri na mitandao yako mengine.
 
Back
Top Bottom