Viti Maalum, CCM - Orodha ya watu 94

Viti Maalum, CCM - Orodha ya watu 94

Naapa huu ni ufisadi wa kupitiliza ni aibu kwa Taifa kufanya haya mambo ya ajabu, unaweza kidogo kusema ok tunalipa haya lakini tunapata Money for Value, hawa hawana mchango wowote wa maana ni kugonga meza tu na nilazima ugonge meza hujachaguliwa umepewa kama hisani tu.

Gharama ngapi zinatumika hapa wewe kama unajiweza gombania uwakilishi haijalishi mwanamke au mwanaume.

Huu kwangu mimi ni ufisadi au matumizi mabaya ya rasilimali kwa kiwango cha lami.
 
Wote hawa kazi yao ni ipi na wakilisha majimbo gani?? Nadhani kuna haja ya kuangalia upya hili suala la viti maalumu. Maana hao wote wana mishahara, posho, marupurupu plus pensheni. Kwani kukiwa na wabunge wachache bungeni kuna ubaya gani?? Je huo wingi wa wabunge ndio hitaji la wananchi ama ndio suluhisho la kero zao?Tutafakari..
 
Kabula ndani ya nyumbaaaaa! no. 61 hapo. Hongera mama!
Swali la ufahamu: Hivi viti maalum wanachagua kutoka mikoa yote au siyo lazima?
Kila mkoa lazima ulete mtu ikiwa mna idadi ya kutosha, kwa mfano CCM ina 94 kwahiyo kila mkoa unatoa wawili, halafu wanachukua kutoka makundi maalum mfano walemavu, vyuo vikuu aliyoingia nayo asha rose migiro
 
Viti maalumu yanini wakati wamechukua majimbo nchi nzima. Hiyo budget ingeenda kwa wananchi sasa
 
Jaman hawa watu ni wengi
Hii ni hasara hapa ni sawa na shule mpya kama hamsini
Au ajira za walimu wa primary hata 30000
Kwa mishahara wanayolipwa jumlisha na posho.

Ni sawa na walimu 500,000+ , ajabu walimu wamekalishwa benchi,
Majina yao mwezi wa pili huu tangu wameomba hayatoki, ila ya wanasiasa yanapewa kipaumbele.

So sad,
 
Hii ingefanywa na vyama venye wawakilishi wachache ingeleta ticha...sasa hao waliochukua majimbo yote maalimu ya kazi gani.... Mengine wapotezee waanze kutuletea kinacho wapasa.

Tuone Kama Chadema hawatafanya huu upuuzi, wasipofanya tutajua huu ni upuuzi.
 
Bunge ambalo haliko kikatiba wala kisheria kwa mara ya kwanza
 
Inamaana CCM imewatema wale wasanii ambao walipitishwa na wajumbe [emoji2][emoji2][emoji2]

Vetting ya CCM sio ya dezo kabisaa
 
Back
Top Bottom