Vitambulisho vya Taifa: Maoni ya Mchungaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vitambulisho vya Taifa: Maoni ya Mchungaji

Discussion in 'Great Thinkers' started by Rev. Kishoka, Feb 26, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Wakati tunagombania ulaji wa Vitambulisho vya Taifa, ni lazima tuwe wakweli tujiulize huu uharaka wa kukamilisha hili zoezi, huku ukweli ni kuwa ni asilimia 25 (25%) au juu kidogo ndio watakuwa na manufaa na kufanikisha zoezi hili.

  Asilimia hii ndogo ni ya wale walioko mijini, wenye akaunti benki na kuajiriwa.

  Mimi najiuliza, kwa nini tusibadilishe mwondoko huu wa Vitambulisho kwa kuufanyia kazi kwa makini na kuleta matunda ya manufaa?

  Kama ni gharama, tupende tusipende, lazima tutaingia gharama. Je kufanya zoezi hilo leo ni muhimu kuliko kesho au jana? Jibu ni kuwa hakuna lililobora pamoja na kilio cha kusema tusitumie hizo pesa kutengeneza vitambulish, bali tununulie mahindi na dawa za malaria.

  Mimi nina mawazo tofauti na kwa Ukihiyo wangu, naonelea kuwa zoezi hili lina walakini si kwa ajili ya harufu ya uhujumu au ufisadi, bali limekosa umakini unaohitajika ambao unelipa zoezi zima la vitambulisho vya Taifa maana.

  1. Tunafanyaje zoezi huku hatuna mfumo bora wa kufuatilia vifo na uzazi? Je kule Dongobesh anapozaliwa Mmang'ati anapewa cheti cha kuzaliwa na nani? siku akifa ni nani anatoa hati ya kifo?

  2. Yule mmaonde wa Beira aliyehamia Tanzania na watoto wake wakakulia Newala, na kakaa vizuri na mwenyekiti wa kaya, tutahakikishaje yeye huyu mmakode au wale watusi na wacongo wa mipakani hawatajifanya ni Watanzania kwa kuidhinishwa uhalali wao na mwenyekiti wa kata na si cheti cha kuzaliwa ambacho watadai hawana kama yule Mmang'ati?

  Je sisi wengine wakimbizi wakazi wa nje ya nchi tutapewa vitambulisho hivi?

  Je suala la uraia wa nchi mbili likoje kwenye suala hili nyeti la vitambulishi vya Taifa?

  Sasa ukishayasoma maswali haya mawili, Mchungaji anasema badala ya kuleta vitambulisho, uanze zoezi la kuboresha takwimu na kumbukumbu kupitia sensa.

  Ndiyo nimesema Sensa ambayo tulishindwa kuifanya hivi karibuni kwa ukosefu wa fedha.

  Ushauri wangu ni huu: tujiandae kikamilifu kufanya zoezi la sensa ambalo:
  • kwanza litatupa idadi kamili ya Watanzania,
  • pili tuhakikishe kuwa katika zoezi hili, tunathibitisha Utaifa ama kwa watu kutoa vyeti vya kuzaliwa au kithibitisho kingine kile kinachokubalikakuwa huyu ni Mtanzania
  • tatu, wakati wa zoezi hili, namba za Taifa zitolewe kwa wananchi an zirekodiwe kwa teknolojia bora
  • nne, sensa, ibainishe yafuatayo, jinsi, umri, elimu, kipato, dini na ajira
  Tukisha maliza Sensa na kujua haya yote, tunaweza kumua sasa ni vipi uendelee na mradi mzima wa vitambulisho vya Taifa.

  Suali linakuja, jee tutapeleka teknolojia kwa kila kona ya nchi? je tutaruhusu hospitali na zahanati kutoa vyeti vya kuzaliwa na kifo na kuhakikisha kuwa vinasajiliwa na kuhifadhiwa katika mkongo wa Taifa wa kumbukumbu (database)?

  Je leo hii tunapojenga mtambo wa fibreoptic kwenye bahari, hatuwezi kuupitisha kwa kila mkoa na wilaya ili tuwezekujenga mtandao mzuri wa teknolojia amba utaweka kumukumbu hizi za watu, leseni za magari, leseni za biashara, kufuatilia kodi, kadi ya kupiga kura, kutoa pasipoti na vitu vingine ambavyo ni muhimu na tunataka kuvipatia ufumbuzi kwa kutumia vitambulisho vya Taifa?

  Hofu yangu ni kuingia gharama mara kumi, kwa kitu ambacho tungeweza kukifanya kwa umakini na mapana na hivyo kutoa suluhisho la matatizo yote.

  Ikiwa Uhamiaji, BRELA na Usalama wa Barabara na Tume za uchaguzi bado wanatumia madaftari na uthibitisho wa mwenyekiti wa kaya na tarafa, je tunategemeaje kuwa tukitoa vitambulisho vya Utaifa tutaleta hatua za kiteknolojia?
   
 2. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Asante sana Mchungaji kwa kutukumbusha hilo, nilitegemea mawaziri "vijana" ndio wangetoa mawazo kama yako hayo. Kwa sababu kama tulishindwa hata kuhesabu (sensa) watu tutawapaje vitambulisho? Yaani nina uhakika mtu ataweza kuwa na majina tofauti katika mikoa tofauti na utaratibu wao huoo. Haya mambo yanafanyika kwa kuiga tuu bila kutumia akili. Eti "smart card" hivi ina u-smart wowote? nadhani kwa teknolojia ya kwetu Bongo tungeeta "Dumb Card" kwa sababu sidhani kama itakuwa na u-smart wowote kama hata internet yenyewe ndio kwanza inajitahidi kuendelea kwenda mikoa mingine. Anyways tutafika tuu Mchungaji hata kama tukipoteza mabilioni leo na kesho yake yatatoka mengine tuu. Ila Asante kwa kuwakumbusha/kutukumbusha hili.
   
 3. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mchungani umenena kama wageni wanapata passport, kadi za kupigia kura za Tanzania kirahisi tutazuia vipi wasipate hivyo vitambulisho vya uraia.......kuna tatizo kubwa kwenye mifumo yetu na ndio ilibidi kwanza iangalie kabla ya kujiingiza kwenye huu mradi.
   
 4. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Watanzania tunapenda viraka, hili l vitambulisho kama lilivyo sasa hivi ni sawa na kiraka. Badala ya kujenga mfumo mpya na bora, tunakimbilia kuweka viraka na kukosa umakini.

  Zoezi la Sensa likipangwa vizuri, litatusaidia sana kutatua matatizo mengi na kujua kwa undani ni ninin tunataka kufanya katika kuleta mfumo bora wa kujua Mtanzania ni nani na yuko wapi!
   
 5. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu Rev. Kishoka nashukuru kwa hoja yako nzito na yenye maana sana hapo juu. Nilikuwa nikidhani utaratibu mzima wa kushughulikia Vitambulisho vya Taifa umefanyiwa kazi kwa kiasi hicho. Ila kwa kweli sioni kama hayo uliyoyasema yamefanyika (labda kwa kutokujua kwangu tu).

  Mkuu ni kweli kuwa ili vitambulisho hivyo viwe "smart" kama inavyotarajiwa, ni lazima kuwe na msingi imara wa kuviwezesha kuwa "smart". Misingi imara ingetakiwa iwe imeshafanyiwa kazi (kama bado) kabla vitambulisho hivyo havijatengenezwa na kutolewa. Misingi kama;

  1. ukusanyaji wa Record za watu (kupitia sensa, daftari la wapiga kura n.k.) wanaostahili kupewa vitambulisho hivyo; record za idadi ya watu, mahali walipo, shughuli zao n.k
  2. Miundo mbinu ya kuwezesha ufanisi wa usambazaji na utumaji wa data zote zinazohusika (ICT, n.k.)
  3. Utaratibu wa jinsi ya kuwafikia watu wenye stahili ya kupata vitambulisho hivyo
  4. Mengine yoyote yanayohitajika.

  Ni kweli kuwa kama haya na yote uliyopendekeza yasipoangaliwa vizuri na kuwekewa utaratibu wa kuyafanyia kazi, vitambulisho hivyo vitapoteza maana kabisa, na gharama kubwa itakayokuwa imetumika haitakuwa na manufaa yoyote.

  Mkuu, nashukuru tena na naomba wanaohusika wayachukulie mapendekezo ya mjadala huu kwa umuhimu unaostahili.
   
 6. A

  August JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  8th February 2009, 02:35 PM
  August
  August has no status. Edit
  JF Senior Expert Member Join Date: Mon Jun 2007
  Posts: 742
  Rep Power: 23

  Thanks: 464
  Thanked 248 Times in 169 Posts
  Credits: 32,171

  Re: National Identity Cards Information

  --------------------------------------------------------------------------------

  Quote:
  Originally Posted by MegaPyne
  1. UTANGULIZI

  Wazo la kuanzisha Vitambulisho vya Taifa kwa Raia wa Tanzania na Raia wageni waishio nchini Tanzania lilizaliwa mwaka 1968 katika Kikao cha "Interstate Intelligence Gathering" kilicho-jumuisha wajumbe kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Zambia. Kwa wakati huo nchi za Kenya na Zambia tayari zilikuwa na Vitambulisho vyao vya Taifa. Iliazimiwa kwamba ili kuimarisha mahusiano ya kiusalama yanayozingatia Utawala wa Sheria katika nchi hizo nne ni lazima nchi za Uganda na Tanzania nazo zikatoa Vitambulisho vya Taifa kwa Raia wao.

  Kumekuwa na jitihada mbalimbali za Serikali kuhakikisha Watanzania na wageni wote wanapatiwa Vitambulisho vya Taifa, lakini jitihada hizo hazikuweza kuzaa matunda yaliyotajariwa kwa kipindi kirefu kutokana na sababu mbalimbali. Mwaka 1986 Serikali ilitunga Sheria ya Vitambulisho ambayo haikutumika wala kutungiwa kanuni zake.

  Ni ukweli ulio wazi kwamba kwa wakati huu kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na Vitambulisho vya Taifa kulingana na mazingira tuliyonayo.


  Ikiwa serikali ina nia ya kutambua watu wake na wageni pia kitu cha kwanza ni kuwa na reliable Data Base, na ikiwezekana family tree, sasa kwa hilo sijui tumefikia wapi?
  na hii data base inaweza ku-update kutokana mabadiliko yanayo tokea eg kusoma, kufungwa, anuani, ajira etc etc, mimi naona tuanze na hili baada ya miaka mitatu or so tukisha jiridhisha na reliability yake ndio twende hatua ya kutoa hicho kipande kitacho kuwa , jina lako na picha zako, na taarifa zako zinazo takikana kuwepo kwenye hicho kipande, wakati taarifa zingine in detail zipo kwenye Data base. Sasa excess to the main data base inaweza kuwa restricted to different users depending na requirments zako eg Polisi, Daktari, Uhamiaji, Muajiri, Bunge , daftari la wapiga kura etc etc Once our data base ikiwa reliable kitambulisho na key to it eg finger prints au sikuhizi macho/jicho then kitambilisho cha CCM, Chadema , CUF , cha kazi si naweza kumtambulisha Mtu? maana inforamtion itakayo wekwa kutoka kwenye reliable central data base iakuwa na basi information za mtu, ukitaka zaidi utaingia kwenye hiyo data base kutokana na mahitaji yako iwe Polisi, mtu wa uchaguzi , shule , pensheni etc etc. lakini kwa sababu watu wanataka kula ndi hivyo wanaweka a cart in front of the horse badala ya a horse in front of a cart  --------------------------------------------------------------------------------
  Last edited by MegaPyne; 8th February 2009 at 04:57 PM..


  The Following User Says Thank You to August For This Useful Post:
  Zalendohalisi (8th February 2009)

  August
  View Public Profile
  Send a private message to August
  Send email to August
  Find all posts by August
  Add August to Your Contacts

  #602 (permalink) 8th February 2009, 05:49 PM
  Ogah
  Ogah is Omnipotent
  JF Premium Member
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Feb 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mchungaji.. naona kwaresma imeanza vizuri. Hapa umetoa mambo muhimu sana.

  a. Nini kitangulie? Sensa ya Taifa ambayo itatupa picha halisi ya taifa letu na kutusaidia kupanga mipango mingi ya maendeleo? Au vitambulisho vya taifa ili hatimaye tuweze kufanya sensa nzuri?

  b. Sensa ya taifa inapofanyika kwanini isitumike wakati huo huo kutoa namba za raia na wananchi waliopo na kuwaingiza kwenye database na hivyo baadaye kuwa rahisi kutoa vitambulisho kwani some vital info zitakuwa tayari kwenye database? Kwanini turudie kitu kile kile mara mbili? (yaani kukusanya taarifa za mtu yule yule)?
   
 8. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mchungaji Umezungumza Mambo ya Msingi sana! Ni Lazima kwanza tuwe na Mfumo Mzuri na wenye kuaminika wa Kutunza kumbukumbu za Raia wa Tanzania. Ni Lazima tujenge Mfumo ambao Kila KIZAZI KITAREKODIWA na kila KIFO KINAREKODIWA. Kama tukiweza kuwa na Mfumo huo ambao naamini unawezekena. Hivi kama tunafahamu kwamba sasa hivi tuna watu millioni X, na tukawa na Mfumo mzuri wa kusajili vizazi na Vifo hivi kuna haja ya kila miaka kumi kuwa tunahesabiwa. Mimi nadhani Idadi ya watu baada ya Miaka kumi inapatikana by Simple Mathematics ie X + WALIOZALIWA – WALIOKUFA. Na tukishakuwa na Mfumo kama huo ishu ya Vitambuliosho vya Taifa itakuwa EASY tu
   
 9. Companero

  Companero Platinum Member

  #9
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Vijana wakinyimwa nafasi mnalalama. Vijana wakipewa nafasi mnakejeli.
   
 10. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Compa:

  Vipi mambo huko front. Huku mabepari wanaboronga. Wakiendelea nitarudisha majeshi.

  Wako

  Lobengula, sparky, Rasputin the evil Monk.
   
 11. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #11
  Aug 17, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Wakuu hii issue inaendeleaje? Kuna zaidi?

  [​IMG]

  [​IMG]
   
 12. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Duh!!
  kuna jambo wajualo hawa jamaa nini ? Ama ni haki yao tu ya kukatakiwa wanayo itaka ?
   
 13. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  still ''under construction''!plan changed,they are going for ''PLAN B'' making sure kwamba hamtawashtukia
   
 14. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #14
  Aug 17, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Kama kuna kampuni ingine imekubaliwa badala ya hawa sijui ni kwa sababu gani.

  Hii ni kampuni kubwa sana na ya kimataifa na tawi lake Afrika lipo South Africa peke yake.

  Sasa kama kampuni hii ilianza shughuli za kutengeneza kadi tangu 80s kweli imeshindwa kupita katika mchujo au ndio inatafutwa kampuni yenye namna gani?
   
 15. K

  Keil JF-Expert Member

  #15
  Aug 17, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Walitonywa na Mkuu wa Wizara Husika na ndo maana Mzee Slaa alienda kuuliza Bungeni kwamba imekuwaje mtu kaingilia mchakato?

  Sasa nadhani jamaa walikuwa wanachokonoa tu wakijifanya hawajui lolote na kumbe walishaambiwa kila kitu.
   
 16. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #16
  Aug 18, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,122
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Tanzania nchi ya ajabu sana! Barabara ovyo, umeme ovyo, hospitali hakuna vifaa, polisi hata kwenye simu kuwapata taabu!! So tunafanya nini? Tunatengeneza ID za SMART CARD!!!! Kichwa kitalipuka nikifikiria sana.
   
 17. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #17
  Aug 18, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Mimi naammini vitambulisho au utaratibu fulani wa kuwatambua wananchi kama passport etc ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa. Tunapokosea sisi ni huu utapeli wa dhahiri kwenye hii miradi.

  Wazo lolote zuri likichanganywa na utapeli, linaonekana hovyo.
   
 18. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #18
  Aug 18, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hii ni hatari sana wadugu, naona kuna kitu kinakuja
   
 19. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #19
  Aug 18, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Bora kije...I can't wait kuona CCM inagawanyika..!!
   
 20. zacha

  zacha JF-Expert Member

  #20
  Aug 18, 2009
  Joined: Feb 28, 2009
  Messages: 495
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 60
  Freemansoon............................. Nd' zile za kuuza wala kununua kama huna chapa yao.................. Mnh!
   
Loading...