DC wa Rungwe azindua zoezi la ugawaji wa Vitambulisho vya NIDA, asema vitambulisho 69,638 vitatolewa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
cc12407d-2a17-4090-8218-1585e25fa06a.jpeg

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amezindua zoezi la ugawaji wa Vitambulisho Taifa (NIDA), leo Desemba 5, 2023 ambapo uzinduzi umefanyika katika Kata ya Kyimo, Tarafa ya Ukukwe.

DC Haniu ameeleza kuwa jumla ya vitambulisho 69,638 vitatolewa kwa Wakazi wa Wilaya ya Rungwe huku Kata ya Kyimo ikipokea jumla ya vitambulisho 2,850.

Amepongeza kwa hatua hii serikali imefanya na kuwa itarahisha utambulisho kwa Wananchi katika kupata huduma mbalimbali.

Ameeleza kuwa uwepo wa kitambulisho kwa kila mkazi utasaidia kupata huduma mbalimbali hususani Mbolea, Kibenki, Vitambulisho vya bima ya afya na hivyo kila mmoja hana budi kuvitunza kwani serikali imetumia gharama kubwa kuvitengeneza.

5e56e29c-c1c6-454b-8946-51c39b18198d.jpeg

Aidha, Haniu amekemea vitendo vya kukaribisha wageni kutoka katika mataifa ya jirani bila kufuata taratibu na kuwa kufanya hivyo kunahatarisha usalama wa watu na mali zao.

Pamoja na hayo ameagiza watendaji wote wanaofanikisha upatikanaji wa vitambulisho kutoandikisha watu kutoka mataifa ya jirani.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Mpokigwa Mwankuga amepongeza Serikali kwa kazi hiyo nzuri hatua itakayosaidia upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa Wananchi hasa katika msimu huu wa kilimo.
 
View attachment 2833883

View attachment 2833884

Machadema yatapinga
 
Hivi ni tofauti na ambavyo tunavyo huku tukikosa anayoyasema watapata!
 
Back
Top Bottom