mangikule
JF-Expert Member
- Jun 11, 2012
- 6,054
- 5,432
Waje watuambie kisa Cha kusisitza kuvaa kondom baada ya maambukizi. Hivi kufungia ndege kutoka nje baada ya wengine wote siyo Sasa na mfano huo ?halafu kwa jeuri tunapewa ukweli kuwa Sasa tumeingia community infectionsWanabodi,
Vita dhidi ya janga la ugonjwa wa Corona, COVID-19, Mapambano yanaendelea, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas na Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndungulile, kesho asubuhi, watakuwa live ndani ya kipindi cha JLNH (Jicho Letu Ndani ya Habari) kinachorushwa na Star TV, kila siku za Jumamosi asubuhi kuanzia Saa 1:30 hadi saa 3:00 asubuhi.
Nchi yetu Tanzania, kama zilivyo nchi nyingine zote duniani, iko kwenye mapambano ya vita dhidi ya janga la ugonjwa wa Corona, COVID-19, kwa vile janga hili ni kubwa na zilikumba karibu nchi zote duniani, hivyo kila nchi iko vitani katika mapambano ya kujiokoa.
Ili Tanzania tuweze kushinda vita hii, tunahitaji juhudi za pamoja za kila Mtanzania tukiwemo sisi wanahabari collectively as media fraternity as a team na susi waandishi individually kujitolea kusaidia kwa kujituma zaidi na kujitolea zaidi, na kwa vyombo vya habari vya utangazaji kujitoa airtime ya bure kwa vipindi vya uelimishaji umma, production houses kuiitolea kufanya production bure na TV na redio zirushe bure, magazeti yaandike makala za uelimishaji umma kwa media ku play role yake ya kuwa ni kiungo muhimu kati ya serikali na wananchi hivyo kwa upande wa Star TV kupitia kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, tunawapa fursa wanahabari na wananchi kwa ujumla kuuliza maswali yao, kutoa maoni yao na mapendekezo yao kwa serikali na jamii.
Kwa vile hii ni vita, mafanikio ya vita yoyote hutegemea mbinu unazotumia, majeshi yako na silaha ulizonazo ukilinganisha na adui yako, ila silaha kubwa kabisa ni morali ya askari wako na kufanya juhudi za pamoja, moral support kwa kupigana as one.
Hivyo katika vita hii ya Corona kila Mtanzania ni mpiganaji, tukisimama pamoja, kupambana bega kwa bega as one, tutashinda.
Mapambano kwa Tanzania yanaongozwa na Kamanda wetu Mkuu na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, Rais, Dr. John Pombe Joseph Magufuli aliyetuanzishia kwa moral buster kubwa kabisa kuhusu Corona kwa kututa Watanzania tusitishike, tuendelee kuchapa kazi huku tukizingatia maelekezo ya kitaalamu ya jinsi ya kujikinga.
Wasemaji wakuu wa Corona kwa Tanzania ni:
Katika kipindi cha kesho, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas na Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndungulile watajibu maswali yenu in one way, lakini kwa vile hawa ni waserekali, na tangu kutokea kwa janga hili, wananchi tunapewa tuu taarifa kutoka juu kuja chini, one way traffic, hivyo kipindi hiki pia kina fursa ya two way traffic, kwa nyinyi kutoa maoni yanu.
- Rais Magufuli mwenyewe
- Makamo wa Rais
- Waziri Mkuu
- Waziri wa Afya
- Msemaji Mkuu wa Serikali
Kipindi hiki pia kitakuwa live kupitia mitandao ya kijamii, ya YouTube, Facebook, Instagram na Twitter za Star TV, hivyo naomba ushiriki wako, kwa kutuma maswali, maoni au mapendekezo kwa serikali yetu ili tuweze kushinda vita hii.
Kwa wana jf, unaweza kutupia swali lako humu, kwenye uzi huu, nami nitamtupia Dr Abbas na Dr. Ndungulile.
Karibu.
Paskali
Nawatakia Ijumaa Kuu Njema
Background Info.
Kwa Dr. Abbas hiki kitakuwa ni kipindi mwendelezo, kilianza last week
Star TV: Msemaji Mkuu wa Serekali, Dr. Hassan Abbas, azungumzia wajibu wa vyombo vya habari kuripoti janga la Corona - JamiiForums
Janga hili liasababishwa na kirusi cha COVID-19 na kusababisha ugonjwa wa homa kali ya mapafu kwa mtu kushindwa kupumus hivyo kufa.
Kirusi hiki kama vilivyo virusi vingine vyote, hujibadili badili kila sekunde kutokana na mazingira tofauti tofauti, hivyo kuna maeneo vimeleta mlipuko mkubwa kwa kushambulia mamia kwa maelfu watu na kuketa maafa makubwa kama China, Italy, Marekani na nchi za ulaya ambazo zina vivaa tiba vya kutosha, na wataalamu wa afya wa kutosha lakini zikaelemewa kwa idadi ya vifo kufikia zaidi ya 1000 kwa siku hivyo kufanya kitu kinachoitwa, Total Lockdown kwa kufunga shughuli zote na watu kutakiwa kujifungia ndani.
Kwa bara la Africa ambalo hatuna vifaa tiba, mahospitali wala wahudumu wa Afya wa kutosha, mpaka haoa tulipofikia ni Mungu tuu mwenyewe anayetulinda, japo tunachukua hatua mbalimbali za kuzuia maambukizi.
Kila nchi inapambana kivyake kwa mbinu zake, wengine wameiga nchi za ulaya kwa kulazimisha lockdown kwa watu wao, hadi wa kipato cha chini wanaotegemea kuishi kwa kufanya vibarua.
Sisi Tanzania, bado Mungu anasimama na sisi, mpaka sasa kumetokea kifo kimoja tu.
Maswali Kwa Dr. Abbas
Maswali Kwa Dr. Ndungulile-