Visa Card Vs Master Card | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Visa Card Vs Master Card

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Viper, Jul 26, 2011.

 1. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Wakuu ....

  naomba mwenye uwelewa wa hivyo vitu viwili anieleze Tofauti yake ni nini hasa ?!


  sssssssssssssssssssss[​IMG]
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Zote ni kadi za benki zinazorahisisha matumizi ya fedha. Zote ni kampuni za Kimarekani. Unaweza ukazipata katika namna mbili; kama debit card au kama credit card.

  Debit card inachukua nafasi ya pesa taslimu. Yaani badala ya kubeba hela na kuzitumia ktk malipo yako, unaweza ukatumia debit card iliyounganisha moja kwa moja na checking account yako. Ukinunua kitu au huduma basi unaichanja tu hiyo debit card yako na hela zinatoka moja kwa moja kwenye akaunti yako kwenda kwa huyo unayemlipa. Hii inahitaji kimashine cha kuchanjia. Pia unaweza kulipia hivyo kwa njia ya simu au mtandao.

  Credi card ni kama mkopo. Badala ya kupewa mkopo wa pesa taslimu unapewa ki-card hicho badala yake. Na chenyewe unakitumia kama ilivyo debit card lakini tofauti ni kwamba hela itokayo kwenye credit card si yako. Ni mkopo na hivyo itabidi uulipe kwa kadri utumiavyo (ukopavyo).

  Nimeeleweka?
   
 3. muwaha

  muwaha JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 743
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Excellent N.N
   
 4. c

  changman JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Jamaa hapo juu ameongea vizuri sana. Sasa ikija suala la kulipia vitu kwenye internet, unatumia credit card, huwezi tumia debt card mpaka uende kwenye benki yako waiwezeshe kufanya hivyo. Ciao!
   
 5. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  nimekualewa 100% mkuu

  ahsante
   
 6. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Master Card ni kadi ya benki inayokuwezesha kuchukua pesa kwenye ATM yeyote duniani iliyopo katika mfumo huo wa MASTER. Kwa mfano kama unayo master card ya CRDB unaweza kuchukua pesa kwenye ATM ya Exim, NBC au Backlays etc ...


  Visa Card ni kadi ya benki inayokuwezesha kuchukua pesa kwenye ATM za benki yako peke yake. Kama unayo visa card ya CRDB huwezi kuitumia kuchukua pesa kwenye ATM ya NBC, Exim au Backlays
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Jul 26, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Huo ni uongo! Mimi ninazo zote, Mastercard na Visa (check card and platinum check card, respectively). Na nina uwezo wa kuchukua hela katika ATM yoyote ile. Hata zile ATM zisizo za benki yangu. Nikichukua hela kwenye ATM ambazo si za benki yangu natozwa ada ndogo.
   
 8. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Safi sana. Kuna wana JF wanadhani kwamba ni lazima wachangie hata kama hawajui kitu.
   
 9. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  sio kweli mpendwa.

  mimi kuna wakati natumia tembo card visa na nachukua hela kwenye ATM za mabenki yote ndani na hata nikisafiri nje!

  majibu ya NN na changman kwa pamoja yanatosheleza mia kwa mia.

  ubarikiwe sana
   
 10. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye red umesema uongo. Kama ilivyo master card ndivyo ilivyo Visa card. Kazi zake ni zile zile. Unaweza kuitumia Visa kadi kupata cash kutoka kwenye ATM yoyote ila utapata local currency za sehemu ulipo. Kama account yako iliyounganishwa na Visa card yako iko kwenye Euro, ukija Tanzania unaweza kwenda kwenye ATM za international banks na kuchukua pesa lakini kwa Tshs.

  Tiba
   
 11. Mchizi

  Mchizi JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 683
  Likes Received: 860
  Trophy Points: 180
  Tofauti ya hizo kadi mbili ni kampuni tu ,lakini zote zinafanya kazi sawa
   
 12. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,819
  Trophy Points: 280
  Je kama nina AMEX na Discovery Cards nawezafanya cash withdrawals ktk ATM za bongo?
  Je naweza-swipe AMEX na Discovery kwenye pumps za gas stations, registers za super markets au malls za hapo Dar, Arusha, Mwanza etc?
   
 13. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #13
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Naona lile wazo lako la kutaka kurudi uko serious... Na huwezi Swipe AMEX na Discovery kwenye pumps za gas stations, registers za Super markets wala malls... Kwanza kwa mfano Dar kwenyewe mall ipo moja tu!!...lol... Hata hivo welcome back Sherriff....
   
 14. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Different Brands..., Same Job...
  credit/debit (it does what is says) debit (using what you have) credit (loan according to your limit and you will pay interest)

  Usage.... (swipe, online, ATMS...)
  Thats means you will have a card

  Virtual Credit / Debit Cards (Prepaid One Time Cards)
  Hapa unanunua Kadi ambazo zimejazwa pesa tayari (kwa wale wenye credit score mbovu au hawawezi kupata credit/debit card) na unaweza ukazitumia kununulia vitu online (ebay, amazon, n.k) au kufungua account ya paypal au Google Account au kulipia Google Adwords..

  Kumbuka kinachohitajika kwenye Credit card ni Jina la Mwenye Kadi, Credit Card Number na CVS number ambazo ni number tatu za mwisho kwenye kadi yako.... (kwahiyo kampuni za virtual credit cards zinakupa hizo information hence unaweza kununua vitu online)
   
 15. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #15
  Jul 27, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Nyani wacha uongo kwa Tanzania inaweza kuwa tofauti hata nchi nyingine kuna cards ambazo huwezi kuchukua mpunga kwenye benki nyingine. Inategemea na mtoa card kakupa masharti gani. unless unapalilia yaliyopo USA.

  BTW Tanzania unaweza kuchukua pesa kutoka kwenye mashine za Barclays tu kama una card kutoka nchi za magharibi na hivi vibenki vingine hupati kitu.
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Jul 27, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Huna hata uhakika na unachokiongea halafu unadiriki kuniita mimi muongo.
   
 17. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #17
  Jul 27, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa Tanzania last week sikuweza kupata pesa kwa kadi kwenye bank zisizo Barclays, na hata ile cash back sahau ...... .... khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeee uhakika 100% soma BTW .... .....
   
 18. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #18
  Jul 27, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,819
  Trophy Points: 280
  ADii umeshaanza....ha ha ha!
  Ahsante kwa kunijulisha hilo la kuhusu AMEX na Discovery cards.
  Kurudi bado kidogo nitapiga box mpaka kibanda changu kiishe kwanza kule maeneo ya Bunju then ndio hesabu za kurudi. Box tamu na halimtupi mtu banaa
   
 19. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #19
  Jul 27, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,819
  Trophy Points: 280
  Mkuu as long as una logo ya visa ama mastercard kwenye debit/credit card yako unachukua mkwanja popote na ndio nimekuwa nikifanya hivyo miaka nenda miaka rudi miji tofauti, states tofauti, ATM's tofauti na benk tofauti. Sijaona mahali wamesema Visa only ama MC only. Labda bongo
   
 20. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #20
  Jul 27, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Not True! Maestro za UBS zinatumika kwenye ATM za CRDB!
   
Loading...