Virusi vya corona: Google yazuia mamilioni ya barua pepe za wadukuzi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Wadukuzi wa mtandaoni huwa wanatuma barua pepe milioni 18 kila siku zenye ujumbe wa uongo kuhusu ugonjwa wa Covid-19, kwa mujibu wa Google.
Mataalamu wa teknolojia anasema mlipuko wa ugonjwa huo umesababisha uhalifu wa mtandaoni kukua kwa kasi huku wakijaribu kutumia mbinu mbalimbali ili kuvamia taarifa za watu.

Kampuni hiyo ilisema kuwa iliamua kufungia barua pepe zaidi ya milioni 100 kila siku.

Wiki kadhaa zilizopita,karibu barua pepe zote ambazo zilikuwa zina ulakini zilikuwa zinahusu virusi vya corona.

Virusi vya corona ndio mada ambayo imekuwa inatumika sana na waharifu wa mtandaoni kutapeli watu, mtaalamu wa teknolojia hiyo aeleza.
Wanaotumia mtandao wa Google kupitia Gmail wanafikia watu bilioni 1.5.
A scam email impersonating the WHO. It encourages the recipient to donate money via Bitcoin.


Moja ya barua pepe ghushi inayodaiwa kutoka kwa Shirika la Afya Duniani ikiwaomba watu kutoa mchango kupitia Bitcoin
Watu binafsi wamekuwa wakitumiwa barua pepe mbalimbali kwa kiwango kikubwa, zikiwa zinajitambulisha kuwa zimetokea katika mamlaka ya Shirika la Afya Duniani (WHO), ikiwa ni jitihada za kuwadanganya watu kufungua programu zao au kutaka watu wachangie fedha kwa jambo ambalo halina umuhimu wala ukweli.

Wahalifu wa mtandaoni wamejaribu kutumia taasisi za umma na kudai kuwa serikali inahitaji kuungwa mkono.

Google imedai kuwa mashine yao inajifunza kuwa na uwezo wa kufungia barua pepe zaidi ya 99.9% kuwafikia watumiaji wao.

Barua pepe hizo zinawalenga wafanyabiashara katika mtandao wa Gmail


Ongezeko la maudhui ya virusi vya corona imerikodiwa na kampuni kadhaa za usalama wa mtandaoni.

Barracuda Networks ilisema kuwa imeona ongezeko la 67% la barua pepe za uongo wakati huu wa mlipuko wa ugonjwa wa corona.

Wahalifu mtandaoni wamekuwa wakituma barua pepe na ujumbe mfupi wa uongo wakidai kuwa wametokea serikali ya Uingereza, wengine wakidai wametoka shirika la afya duniani-WHO, kituo cha kukabiliana na kuzuia magonjwa na hata maafisa wa Marekani akiwemo rais Trump.

"Shambulio hili la uhalifu mtandaoni huwa wanatumia mbinu zinazofanana za kuweka hisia za taharuki, sababu za hatua fulani kwa wakati huo ambapo watu wanaweza kurubunika kuwa ni jambo sahihi," alisema mtafiti binafsi wa usalama wa mtandaoni Scott Helme.

"Mlipiko wa virusi vya corona, suala ambalo linawagusa watu wengi kwa sasa na wahalifu wa mtandaoni wanalitambua hilo.Wanadhani kuwa watu wanaweza kufuata muongozo wao wa uongo au kubonyeza link wanazozituma."

Watafiti wamebaini pia tovuti za uongo ambazozina programu za tovuti na simu za mkononi kwa kuweka madai kuwa wanachangia kukabiliana na virusi vya corona.

Programu katika simu ya Android inayodai kuwa inasaidia kufuatilia watu wenye virusi vya corona, badala yake inaidukua simu kwa ransomware ambayo inataka malipo ya kuweka programu hiyo kwa simu.

Wiki iliyopita kituo cha usalama wa mtandaoni nchini Uingereza (NCSC) na idara ya Marekani ya masuala ya usalama walisema , wameona ongezeko kubwa la udukuzi wa mtandaoni ambao unatumia mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 kuwa ndio mada yao kuu ya kuwaibia watu".

NCSC imechapisha maelezo kwenye mtandao wake ili kusaidia watu kujizuia wasiwe wahanga wa wadukuzi wa mtandaoni.
 
Back
Top Bottom