Vipi Unatongoza

ndio gia yenu hiyo siku hizi, unamvalisha pete halafu baadaye unamtosa.

...la hasha, nilishapita huko na kuoa 'ukweli ukweli' :( (baada ya kuzidiwa)

Haha babu wewe utakuwa player si bure! Una mshindilia na msumari wa ndoa na unanunua pete ya cubic zirconia....

...:D dah, unajua mpaka 'mali ghafi' wanayotengenezea! ha ha aaa.. usikute gharama yake (uki bargain) haizidi shs 999.99/=!
 
...la hasha, nilishapita huko na kuoa 'ukweli ukweli' :( (baada ya kuzidiwa)

Hongera sana mkuu ila kama bado uko kwenye ndoa!.

... :D dah, unajua mpaka 'mali ghafi' wanayotengenezea! ha ha aaa.. usikute gharama yake (uki bargain) haizidi shs 999.99/=![/COLOR][/B]

Babu kabla ya kuingia kwenye kimbunga inabidi ujue upepo unaelekea wapi.Ila sijawahi kutoa pete, lakini info ndogo kama hizo lazima ziwe karibu karibu maana huwezi kujua.
 
Hongera sana mkuu ila kama bado uko kwenye ndoa!.

...tungo tata! :D

"Getting married is a lot like getting into a tub of hot water. After you get used to it, it ain't so hot."


...am so addicted kwenye ndoa yangu, siwezi hata kutoka!
 
Mimi mamsapu wangu nilipomuona nilimungalia sana nikajifanya namkagua kwa macho na kwa karibu sana, akaniuliza " vipi kulikoni" nikajibu "naangalia mahali ulipoumia ulipoanguka kutoka mbinguni, kwa sababu lazima utakuwa malaika" Nikapata namba, the rest is history.
 
'Nilivyokuona nikajihisi niko na mtu niliyemzoea. Sikujisikia kama niko na mtu nisiyemjua na kusema kweli najihisi furaha. Nadhani wewe ni rafiki yangu asilia na sihitaji kujieleza sana ili ujue kuwa mimi ni rafiki yako. Napenda kampani yako na nahisi hata wewe unaipenda kampani yangu. Nakukaribisha lunch leo na ukikubali nahisi hii itakuwa lunch special sana kwangu'......

Mtongozwa.... ..... .. Enhee, asante. Ila maneno yako kiboko.

Mtongozaji .... .... ... Achana na maneno, hayo yapo tuu, nitakupitia wakati naenda lunch.

Mtongozwa ..... .... Haya asante ..

Mtongozaji .. ... ... Sasa nitakupataje ofisini kwenu wapi? au nipe namba ya simu nitakupigia nitakuelekeza sehemu, uje.

........................

Mwanzoni unatakiwa uonyeshe ishara kuwa kuna kitu unataka, ila ghafla hamishia mazungumzo kwenye kitu kingine kitakacho fanya muwe karibu zaidi. Baadaye unakomelea msumari. Usiwe fasta sana, lakini vile vile usiwe longo longo sana. Unataka shoka we unaenda kuongea masaa matano. Wenzio wanakuwahi.

Amini usiamini huyo wa mazungumzo hayo hapo juu ilikuwa mara ya kwanza kuonana tena kwenye dala dala. Katika kipindi cha wiki mbili alishafungwa gori.

Ofcourse inategemeana na mwanamke. Kutongoza ni kitu natural na kwa kweli ukijaribu kanuni utashindwa kwa sababu wanawake wanatofautiana. Wapo wanaopenda longo longo, wapo wanaopenda moja kwa moja ila zingatia yafuatayo;

1/ Mwanzoni kabisa lazima uoneshe nia yako nini hasa (kufunga bao) na endelea kugonga mlango kila unapopata fursa.
2/ Ukiona anataka kuchomoa fasta, badilisha mazungumzo lete ishu nyingine kabisa
3/ Onesha kuwa unamjali, si kuwa unamtaka
4/ Usizidishe chochote. Hata kwenye mshiko onesha kuwa una limits
5/ Wiki moja kama hujaona mwelekeo ... chomoa, tafuta mwingine
6/ Usiogope kutongoza wanawake watatu, wanne, kabla ya kufanikiwa. Mwanaume umeumbwa ili utongoze. Usizame saana kabla hujapata!
7/ Kila unaposhindwa, chukua somo .. kwa nini hakuingia laini. rekebisha kitu unachohisi ulikosea

Mara nyingi kama ameingia laini, ukichomoa utaona yeye sasa anakufuatilia. Huo ndo wakati wa kutikisa nyavu. Ukichomoa na yeye asijali, ujue hapo sipo.

Ndani ya wiki moja lazima uwe na mwelekeo.
 
Wana JF ebu tuwe wakweli siku hizi hakuna mtaalam wa kutongoza,wanawake sikuhizi hawaitaji watalaam wa kupanga maneno bali wataalam wa kupanga minoti na starehe za kila mara. kila mschana anakiwango chake cha fedha na starehe anazostaili.Kama kuna demu anakusumbua mdanganye na kwenda-out utaona matokeo.
 
Duh, kwa mtaji huu wenye wake zetu wanao 'interact maofisini, vyuoni nk. tutasalimika kweli? Au tutumie arts gani ili wake zetu wawe hawalainiki kirahisi mbele ya chatu?
Mi kweli kuna mdada mmoja wa nguvu hapa ofisini ,baada ya kula nae lile zoezi la kumkazia macho na kutobadilisha tageti ya kwenye macho yake aliniambia ana mwenyewe ,ila nikamwambia huyo mwenyewe huwa anakuletea ,samaki,ndizi na vyakula kibao lakini hatokuletea mimi ? nikachezea mshonyo si wakawaida . Nikaona kizunguzungu lakini nikakumbuka kuwa ni mteja wa mtu mwengine.
Unafikiri baada ya mshonyo unaweza kuendelea ?
 
ahahahaha...bonge la mada hili ...mbona mie huwangoa fasta tuu..ukimwona unampa ma-beibe-beibe-beibe...i luv you soo much...hawa ni washkaji zangu wee waache....fasta bila kuchelewa naomba namba ..akizuga hana nampa simu ya mchina..si unajua hizi za laki 2 za line 2...nikimpa wala hakatai...kesho yake namwendea hewani.....akileta longo hana usafiri namtia ki-harrier cha kutembelea...mind you hatuongi gari...tunatoa funguo tuu..yafuatayo ni kumpa ma-high performance...ndani ya wiki lazma uwe usha mla mauroda....longolongo kwenye kutongoza ipo pale unapotaka namba yake ya simu..mengineyo watu wangu ni cash-rules na speed ya kumperform mtu
 
Enzi hizo kama hujamwambia demu
Silali kwa ajili yako
Nikilala nakuota wewe
Sili chakula
nikila nakuona kwenye kijiko
Nikinywa maji nakuona kwenye glasiiiiiiiiiii.

Basi ukimwona wimbo ndo huo huo mpaka analainika. Za siku hizi ndo hizo,,Red cars na nini cjui.
 
Sikubaliani na mnaosema kuwa siku hizi ni gari na fedha tu ,mbona kuna watu ambao hawamiliki hata baiskeli lakini kila wikiendi unamkuta ana kitu si cha kawaida anafaidika nae ?
 
Mi nafikiri hakuna fomula ya kutongoza ,inategemea na response ya demu uliyemtokea siku hiyo maneno yatakayotoka leo sijui kama ukitumia hayo utampata demu mwingine
 
Mi kweli kuna mdada mmoja wa nguvu hapa ofisini ,baada ya kula nae lile zoezi la kumkazia macho na kutobadilisha tageti ya kwenye macho yake aliniambia ana mwenyewe ,ila nikamwambia huyo mwenyewe huwa anakuletea ,samaki,ndizi na vyakula kibao lakini hatokuletea mimi ? nikachezea mshonyo si wakawaida . Nikaona kizunguzungu lakini nikakumbuka kuwa ni mteja wa mtu mwengine.
Unafikiri baada ya mshonyo unaweza kuendelea ?

Hapo kwenye red ushaharibu tayari, ebo wewe unamtaka mwanamke alafu unamzungumzia mwanaume wake? ungekaa kimya kama hujamsikia ukaendeleza story zingine, i.e kumsifia kapendeza, au ananukia vizuri au umependa nguo yake.

Haya ya msonyo na kubinuliwa mdomo wewe yasikutishe kwa mara nyingine wanadada wengi wanapenda wanaume wanaojiamini na wasiotetereka.
 
Uwe na confidence kivipi wakati vipimo vyote vinaonyesha unaweza ukachezea msonyo wa nguvu utafikiri kaona shetwani. Msichana unamuuliza hali anruka kwa sauti unikome mwanawamwenzio ,kuna wengine washaenda kunisemea kwao na kufika hadi nyumbani kwa vishindo eti nawadoea. Muda ka miezi mitatu mtaani wakawa wananiita doezi ,yaani ilikuwa noma ile mbaya ,hivyo ndio nimeingia na kuja hapa kutafuta elimu ,wewe unaniambia uwe na confidence ,hiyo confidence ndio ninayoizinga.

Nimewasomaaa, ila kitu kimoja nataka nikuulize. mvuto unao? Isije ikawa ndio sababu. Au tafuta hela za kuwachota akili
 
Asalamu alaykum.

Hilo ni somo kubwa ambalo sio rahisi mtu kuweza kufahamu ghafla kutokana na mapenzi na namna ya kunasa katika mapenzi kwa sababu kuna mambo mawili ambayo kwa urahisi uanweza kuyaona yoye ni sawa lakini ukiingia kwa undani ndipo utakapogundua kuwa hayo mambo mawili ni tofauti lakini yanashabihiana sana.

kuna kupenda na kutaka, mtu anaweza kupenda lakini asimtake mwanamke au mwanamke na pia anaweza kumtaka lakini asimpende mwanamke au mwanamme.tayari nimeshaeleza kuwa hili ni somo kubwa na linahitaji tafakuri ya kutosha ingawa wengi wetu hamtakubaliana na mimi katika suala hili lakini huo ndio ukweli na ninaweza kutoa mifano kadhaa lakini mfano mmoja tu nadhani utatosha kwa hapa.

tutaanza na mfano wa mwanamke kwa sababu mazowea yalijengeka katiak ulimwengu wetu ni kuonekana mwanamke ndiye anayetakiwa yaani kama vile mwanamke hana haki ya kumtongoza mwanamme wakati haki hiyo ni ya pande mbili lakini inaonekana mwanamke akimtongoza mwanamme anaweza kuitwa malaya.

leo nitaanza na mfano huu mtu mtu mmoja anaweza kwenda sehemu akamuona mwanamke akampenda sana lakini akasema huyu mwanamke ninampenda lakini simtaki kwa mana ya kuwa rafiki yake au mke wake na hii sio kwa kumuona mara moja pengine kwa muda anamfuatilia na hilo linaweza kuwa na sababu lukuki ikiwemo pengine anampenda lakini kuna mambo yanamkwamisha kuwa mwenza wake pamoja na kumpenda kote huko.

lakini pia mtu anaweza akamtaka mtu na akawa rafiki yake bila ya kumpenda na akathubutu hata kufanya naye mapenzi mfano mdogo .samahanini lakini kama vile unapokuwa na fedha na tamaa ya maovu imekushika ukamchukua dada poa ukalala naye jambo kwa siku moja au ukaendelea naye kwa siku kadhaa na unapoulizwa kwa nini huyu mtoto wa watu unakaa naye humuoi ukasema aaah simpendi lakini unaweza kuulizwa vipi mbona umekaa naye muda mrefu na umeshazaa naye jibi lako mimi ninafanya mashauri a kuwa na mwenza lakini sio huyu, hilo lipo na linatokezea aktika jamii yetu. na bila ya shaka miongoni mwetu tunalo lakini kawaida binaadamu hatutaki kukubali makosa lakini naamini humu humu tumo watu amabo tabia hiyo tunayo tunakaa na wenza bila ya kuwataka na wengine tunakaa na wenza bila ya kuwapenda.
 
Apo juu umekuja na somo ambalo kutokana na jina lako Stonetown naona mawe yameniangukia na kunivuruga kichwa kabisa hivi nimekaa nina kiwiliwili tu bila ya kichwa.

Umenivuruga kichwa kwa sababu suali limenirudia upya kabisa na kupoteza muelekeo wa kule ambako nilianza kujifunza ,ni kutokuwepo kwa mistari ya kumueleza huyo ,unaemtaka utamueleza vipi na unaempenda utamuanzia vipi ili ufanikishe lengo kuu la kusonga ugali ,mistari tu ndio inayonikwamisha kuendeleza libeneke la kuunga unga.

Naweza kuanza na mstari mzuri na baada ya kujibiwa ndio nimemaliza nabaki kukaa kimya tu kama hakujatokea kitu ,na nikiendeza utawasikia wakijibu shika adabu yako.hapo ndio wananiwacha hoi bin taaban ,yaani hizo shortcut zao wanazopita ni lazima zinahitaji kaujuzi flani kuzivuka ,la si hivyo anaweza akakuweka uchi mbele za watu mzee mzima ukaadhirika. Kule Zenji utasikia akikunadi yaani anakunadia kwa kukwita mchinvii kwa sauti mtu alieko mita hamsini atasikia.
 
Back
Top Bottom