Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Kwa nini JK akiwa majukwaani au kwenye hafla huwa hazungumzii ufisadi kwa namna ya kukemea na kusema ni tatizo linalohatarisha amani ya nchi?
Nakumbuka mara ya mwisho JK kuzungumzia ufisadi ni Bungeni Dodoma, mapoema August 2008 wakati wa suala la wizi wa EPA lilivyoshika kasi. Hata baada ya hiyo hajawahi kamwe kulirejea suala hilo, lilifikia wapi, iwapo kumetokea mafanikio nk. Hajawahi hata kutamka neno EPA katika hotuba yake yoyote baada 2008.
Leo hii JK amenukuliwa na vyombo vita habari akikemea kwa nguvu zake zote tabia ya baadhi ya wananchi kuwaoa wanafunzi wa shule, na kwamba hawa wakamatwe mara moja na kufunguliwa mashitaka ya kubaka!
Laiti JK angekuwa anakerwa sana na ufisadi kwa namna hii, tungepiga hatua kubwa katika vita hiyo.
Hata hivyo inavyonekana JK hajui tofauti kati ya kubaka na kumwingilia mwanamke chini ya umri!
Kumwingilia mwanafunzi chini ya umri kwa namna hiyo ya kumuoa mwanafunzi siyo kubaka. Hili ni kosa jingine na halihitaji consent. Na kubaka pia anaweza kufanyiwa mwanamke mwenye umri mkubwa.