Duru za Siasa Special: Mgogoro kambi ya Upinzani (CHADEMA)

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
15,389
31,335
MKAKATI WA MABADILIKO 2013

UTANGULIZI:
Taasisi tunayoizungumzia ilisajiliwa rasmi mwezi January 1993 na tokea wakati huo imeongozwa na wakuu wa taasisi wapatao wawili na aliyepo kwa sasa ni wa tatu. Wa kwanza aliongoza kwa miaka mitano tangu wakati huo 1993 hadi 1998 na kumwachia aliyefuata ambaye naye aliongoza kwa miaka mitano hadi mwanzoni mwa 2004 na kumwachia aliyepo sasa. Huyu aliyepo aliongoza kwa miaka mitano tangu mwaka 2004 hadi 2009 na kisha akachaguliwa tena mwaka 2009 kwa kipindi cha pili. Tunapenda kwa hatua ya mwanzo kabisa kutambua juhudi za wakuu wetu wote waliopita walizozifanya katika kuhakikisha taasisi yetu inakua kwa kutumia uwezo wote waliokuwa nao na katika mazingira yaliyowakabili.

Mwaka 1995 chini ya mkuu wa kwanza tulipata wawakilishi watatu kwenye chombo chetu kikuu cha uwakilishi.
Mwaka 2000 chini ya mkuu wa pili tukapata wawakilishi wanne pamoja na wa nyongeza mmoja na kufanya idadi kuwa watano.

Mwaka 2005 chini ya mkuu wa tatu ambaye ndiye aliyepo hivi sasa, tulipata wawakilishi watano na wa nyongeza sita jumla wakawa 11. 2010 chini ya mkuu huyu huyu wawakilishi wakaongezeka na kuwa 23 na wa nyongeza 25 na kufanya idadi kuwa 48 kabla ya kupata mwingine mwaka jana na kufanya sasa wawe 49.

Tunapopongeza juhudi zao hizi tunahitaji pia kuwapongeza wakuu wetu wawili wa kwanza ambao kimsingi waliweka msingi mzuri sana wa kutong'ang'ania madaraka na badala yake kuachia mapema na kumwachia mwingine kidemokrasia bila vurugu.

Hawakuwa madikteta na tunawapongeza sana. Walijitahidi sana kutokuwa wapenda madaraka na kimsingi walituwekea utamaduni ambao walitaka wote tuufuate na kujenga taasisi imara inayojali demokrasia na haki ya kila mwana taasisi.

Ni kwa msingi huo waliamua kuandika kabisa katika mwongozo wetu kwamba kiongozi yeyote katika ngazi yoyote ya kuchaguliwa atakapogombea na kushinda ataongoza kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na kisha ataweza kugombea na kuongoza kwa kipindi cha pili cha miaka mitano baada yapo hawezi kugombea tena katika nafasi ile ile aliyoitumikia kwa vipindi viwili.

Ili kuonyesha kwamba walimaanisha kile walichokisema, wote wawili hawakuwahi kukaa madarakani kwa vipindi viwili vilivyoruhusiwa katika mwongozo bali wote wawili walikaa kipindi kimoja kimoja tu.

Lakini kuna matatizo yameanza kujitokeza na tusipochukua hatua haraka huko mbele tunaweza kupata shida kubwa.
Tunapenda kuainisha matatizo hayo kwa uchache kama ifuatavyo:

Wakati tukiufanyia mwongozo wetu mabadiliko mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano mitano.

Lakini wakati mwongozo unachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela.
Mambo yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwa makusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa. Hiki kinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanaweza kutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika na wanaweza kufanya mambo mengine makubwa na yenye athari zisizomithirika kwa taasisi yetu.

Ni dhahiri kwamba uongozi uliopo umeishiwa mbinu na kuakisi jambo la msingi sana ambalo waasisi wetu waliliona tangu mwanzo na kuamua kuweka kipengele cha ukomo wa uongozi kwenye mwongozo wetu. Kuchoka kwa uongozi wetu kunaonekana dhahiri katika mipango na mikakati ya taasisi ya miaka kadhaa. Mfano mwaka 2008 uongozi ulianzisha mkakati wa operesheni samaki mkubwa (maarufu kama Oparesheni Sangara).
Huo ulifanyiwa kazi katika mikoa kadhaa na hatimaye ikafa kimya kimya. Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kulianzishwa matembezi ya maandamano ambayo nayo yalikuwa yakipeleka ujumbe kwa watu na yalipangwa kufanyika mikoa yote na wilaya zote.

Kumbukumbu zetu zinaonyesha kwamba yalikuwa yakianzia makao makuu ya mkoa na kwenda kwenye wilaya zote.
Lakini kumbukumbu hizo zinaonyesha kwamba yalifanyika Mwanza, Musoma, Shinyanga, Kagera na mikoa ya Nyanda za Juu kusini (Mbeya, Iringa, Njombe na Rukwa) kisha nayo yakafa kifo cha mende.

Kisha mwaka 2012 ikaanzishwa operation ya mabadiliko maarufu kama Movement for Change (M4C).
Hiyo ilikuwa inakwenda kwenye mikoa na timu kama nne hivi ambazo kwa ujumla zilitathmini hali ya mtandao na uongozi wa taasisi, kuhamasisha umma kwa njia ya mikutano ya hadhara, kuingiza wanachama na kusimika uongozi na hatimaye kufanya mafunzo kwa viongozi.

Hiyo ikafanyika Mtwara na Lindi, Morogoro na kisha ikaenda kufia Iringa. Mwaka huu viongozi wetu wamekuja na ugatuaji madaraka kutoka makao makuu ya taasisi na kupeleka madaraka kwenye kanda mbalimbali.

Mkakati huu ulikufa kabla ya kuanza pale viongozi wakuu walipobadilisha maazimio ya kikao kikuu na kutekeleza matakwa yao ikiwa ni pamoja na kuleta suala la viongozi wa muda kwa muda mrefu badala ya kuajiri maofisa na wakahakikisha wanaweka watu wao kwenye uongozi wa muda. Kitendo hiki kwa peke yake, cha kufeli kwa kila mkakati unaoletwa na viongozi wetu katika hatua za utekelezaji unaofanywa na wao wenyewe waleta mkakati, ni kiashiria tosha kwamba uongozi uliopo umechoka.

Performance yetu kwenye chaguzi ndogo nayo ni ishara kwamba mabadiliko yanahitajika.
Tangu uongozi huu uingie madarakani, kumefanyika chaguzi ndogo 8 za wawakilishi kwenye chombo kikuu, kati ya hizo tumeshinda 2 tu sawa na asilimia 25. Aidha baada ya mwaka 2010 kumefanyika chaguzi kadhaa za wawakilishi kwenye halmashauri. Mwezi Oktoba 2011, mwezi wa4 2012, mwezi Septemba 2012 na mwezi Juni 2013. Kote performance yetu imekuwa poor kupindukia. Mfano mwezi wa Juni 2013 tumepata viti 6 kati ya 22 (27%) na mwezi Septemba 2012 tulipata viti 7 kati ya 29 (24%).

Ni dhahiri mabadiliko yanahitajika kwa kuwa wakuu waliopo wanatumia mbinu zile zile na kupata matokeo yale yale.
Tunahitaji mbinu mpya. Kwa kifupi, ushindi ambao tumekuwa tukiupata katika chaguzi ndogo haulingani na ukubwa wa hamasa kwa taasisi yetu iliyopo mitaani. Hii ni kwa sababu tumekuwa tukitumia mbinu hizohizo katika kila chaguzi. Aidha, tu wepesi mno wa kuridhika na kujisifu kwa mafanikio madogo badala ya kukaa chini na kutafakari kwa kina mahala tunapojikwaa.

Matumizi ya fedha za taasisi.
Hakuna mtu anayejua hivi sasa fedha za chama zinatumikaje zaidi ya kakikundi ka watu watatu yaani mkuu kabisa, mtendaji mkuu na mkuu wa fedha kwenye taasisi yetu. Maamuzi ya vikao hayaheshimiki tena na mabwana hawa.

Baada ya uchaguzi wa 2010 vikao halali vilielekeza kiasi na aina ya fedha ambazo hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Lakini leo si tu akaunti hiyo haina fedha bali hakuna akaunti yoyote yenye fedha.

Watu watatu ndo wanaamua fedha zitumikeje. Mfano mwingine ni maamuzi ya kikao cha juu mno cha hivi karibuni kilichoamua kwamba kiasi cha fedha inayotoka serikalini kipelekwe kwenye mikoa na wilaya na kiasi kingine kipelekwe kwenye kanda.

Leo ni mwezi wa tano maamuzi hayo hayajatekelezwa.
Lakini kuna michango ya watu binafsi kama yule mtanzania mwenye asili ya kihindi, hizo nazo hazijulikani zimechukuliwa lini kwa mfumo gani, zikatunzwa wapi na hatimaye zimetumikaje. Hapo hatujataja fedha zinazopatikana kutoka kwenye fundraising events mbalimbali kama ile ya Dar es salaam na Mwanza. Hizo nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha hizo fundraising, uaminifu wao kwenye masuala ya fedha ni questionable.

Taarifa za fedha. Tokea baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna kikao chochote kilichowahi kupokea na kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na matumizi ya fedha za taasisi. Kila kikao agenda hiyo inarushwa kiaina.

Wanaojua mchezo huo ni watu watatu tu tuliowataja hapo juu na malengo ya kurusha hiyo agenda kila wakati na kukwepesha isijadiliwe pia wanayajua wao. Ni dhahiri tukiendelea na hawa watu tutafika 2015 tukiwa hatuna pesa hata ya kuweka mawakala kwenye vituo na tutapigwa tukiwa tumesimama. Kwa kiasi kikubwa mkuu aliyepo anatengeneza mazingira yaleyale ya mwaka 2005 na 2010 ya kutaka chama kiwe hakina hela ili ikifika wakati wa uchaguzi kimpigie magoti. Kisha atatoa pesa bila kumbukumbu zozote na mara baada ya uchaguzi anapeleka lundo la deni na kudai alipwe hela aliyekikopesha chama wakati wa uchaguzi. Alifanya hivyo katika chaguzi za 2005 na 2010. Wakati wote wa kampeni za mwaka 2010, kwa mfano, taasisi yetu ilihangaika sana kwa kukosa hata hela ya kununua maji kwa wajumbe wa ngome. Lakini ajabu ni kwamba baada ya uchaguzi mkuu wa taasisi na baadhi wa wapambe wake walilete deni kubwa la takribani shililingi milioni mia tano akiadi kuwa walikikopesha chama. Taasisi imewalipa pesa zote hizi kwa muda mwaka mmoja. Sasa anatengeneza mazingira hayohayo kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2015.

Mipango ya kukipatia chama mapato ya ziada kutoka nje ya chama. Wakuu waliopo hawana hata ndoto ya namna ya kupata fedha za ziada. Wanachokijua ni kukusanya ‘sadaka' kwenye mikutano ya hadhara na kuwapatia kazi watu wanaoonekana kuwa matapeli eti waendeshe harambee za kuchangisha fedha kwa njia ya matukio. Mawazo mazuri kama lile la kuanzisha kampuni la uwekezaji la taasisi yetu litakalowekeza kwenye miradi mbalimbali, halijawahi kufanyiwa kazi, na hivyo uanzishaji wa miradi mbalimbali ya kuiingizia taasisi fedha imebaki ndoto ya mchana. Hatuwezi kufika hata siku moja bila fedha. Hata uchaguzi wa wenzetu wa hapa jirani juzi juzi wakuu wetu ingawa walishiriki lakini hawaonekani kama wamejifunza chochote.

Njia haramu za kubaki madarakani.
Ili kuhakikisha wakuu wanabaki madarakani, wameanzisha vikundi vikundi ndani ya taasisi yetu. Siku hizi ni rahisi sana kuambiwa kwenye taasisi yetu eti huyu ni wa boss na huyu ni wa dogo. Na wale walio wa boss kwa kuwa boss ndo anashikilia raslimali za taasisi anatumia mfumo haramu kuwaneemesha watu wake kwa kutumia raslimali za taasisi na kuwakandamiza wote wanaoonekana wanapishana naye kimtazamo. Jambo hili limewaibua wachumia tumbo, wapenda madaraka, na vibaraka lukuki wanaokwenda kujipendekeza kwa wakuu wa taasisi kwa malengo ya kujinufaisha binafsi. Katika kufanya hivyo vibaraka hao wamekuwa wakiwaendea wakuu wa taasisi na kuwajaza maneno mabaya dhidi ya viongozi wenzao na kuzidi kuwafarakanisha viongozi wa juu.

Kuna mchezo umeanzishwa na wakuu wa taasisi unaitwa ulinzi wa chama uliogawanyika katika makundi mawili yaani visible na invisible. Visible ni ule unaoonekana ambao uko chini ya kikosi chetu chekundu ambacho kinajulikana kwa kila mtu lakini invisible wanajulikana kwa mkuu wa taasisi na mtendaji mkuu peke yake. Wanafanya kazi kwa maelekezo ya wakubwa hao wawili na hawajulikani kwa viongozi wengine wa juu. Ni hawa hawa ambao wanatumika vibaya pale wanapoleta taarifa za kiintelijensia ambazo zinawahusisha viongozi wasiopendwa na wakuu na usaliti dhidi ya taasisi. Hakuna kamati maalum inayowathibitisha maaintelijensia hao bali wakuu wenyewe wanawachukua wanaowataka.

Ni katika mfumo huu wa kipuuzi mida eight amekuwa akitumika vibaya kwa kumshambulia mtendaji mkuu msaidizi hadharani kwa kutumia mitandao ya kijamii na wakuu wanafurahia na kumlipa pesa.

Udhaifu wa utendaji wa mtendaji mkuu.
Mtendaji mkuu ni dhaifu mno na ni mara nyingi sana tumeshuhudia mkuu wa taasisi akifanya mambo ya kiutendaji kinyume na utaratibu kama vile yeye mwenyewe kuja kwenye kamati ya makatibu na wakurugenzi na kupangua mipango yao na ku-inject ya kwake na mtendaji mkuu kuadopt tu kana kwamba yeye hawezi kupanga mambo ya kiutendaji, hata tunapokuwa kwenye operesheni maalum tumeshuhudia mkuu wa taasisi ndo akipanga watendaji, posho zao na hata kusimamia matumizi ya pesa na shughuli mbalimbali za kiutendaji.

Udhaifu wa mtendaji mkuu ni udhaifu wa mkuu wa taasisi kwa kuwa amemteua yeye mara mbili tena mara ya pili alileta jina moja mbele ya Baraza la juu kuonyesha kwamba aliridhika na utendaji wake kiasi cha kutotaka kumpambanisha na mwingine. Lakini baada ya kumpendekeza mara ya pili ndipo tumeshuhudia yeye kuingilia kati mara nyingi sana mambo ya kiutendaji kana kwamba anamfichia aibu mtendaji wake. Swali kwa nini alimteua tena? Jibu lake litakuwa rahisi tu kwamba ni kwa sababu mtendaji huyu ni passivekwa kila takwa la mkuu wake.

Matumizi mabaya ya madaraka yanayoweza kuhusishwa na ufisadi.
Taasisi yetu inayo kamati ya tenda ambayo iko chini ya kamati ya makatibu na wakurugenzi. Lakini uzoefu unaonyesha kwamba kamati hii haifanyi kazi imezimwa kimya kimya na wajumbe wote wa kamati ya tenda kwa kuwa ni wachumia tumbo wanaojigonga kwa wakuu, wamekubali kuzimwa. Leo ikidaiwa kamati hiyo ilete nyaraka za mchakato wa manunuzi ya magari, pikipiki, vifaa vya kueneza taasisi, set ya televisheni iliyofungwa ofisini kwa mtendaji mkuu, hawana. Manunuzi haya yote yote yanafanywa na wakuu hasa hasa mkuu wa taasisi bila utaratibu wowote jambo ambalo ni hatari na linarahisisha matendo ya kifisadi.

Bila aibu, mkuu wa taasisi ndio amekuwa mnunuzi wa vifaa vyote vya chama nje ya nchi kwa bei anayoijua mwenyewe na ambaye haihojiwi popote. Huu ni mfano wa wazi wa mgongano wa kimaslahi jambo ambalo ni hatari kwa kiongozi mkubwa wa taasisi kama yetu inayojitambulisha katika kupinga vitendo vya ufisadi na uvunjifu wa maadili ya uongozi kwa ujumla.

Makubaliano ya kifisadi na mtu binafsi anayeuza vifaa vya kueneza taasisi.
Hakuna kikao chochote cha juu kilichojadili ama kilichowahi hata kupewa taarifa tu kwamba sasa kuna mtu binafsi kapewa tenda ya kuuza vifaa vya taasisi na taasisi inanufaika vipi na mauzo hayo na kwa nini vifaa muhimu vya taasisi vinauzwa. Jambo hili linajulikana kwa wakuu tu.

Mifumo ya uteuzi wa maofisa wa makao makuu ya taasisi imevurugwa na siku hizi wakuu wa taasisi hasa mtendaji mkuu anateua na kutimua ofisa anavyotaka na mara nyingi bila hata kamati ya makatibu na wakurugenzi kujua.
Mambo haya yanafanyika mbele ya macho na masikio ya mkuu wa taasisi jambo ambalo linazidi kuthibitisha kwamba mkuu na mtendaji mkuu wanajuana na wanafanya kwa kulindana.

NANI TUMUUNGE MKONO KUCHUKUA NAFASI YA MKUU:
Baada ya utangulizi huo unaoonyesha kinagaubaga kwamba tunahitaji mabadiliko, hatua iliyofuata ilikuwa ni kuangalia nani anaweza kuleta mabadiliko tunayohitaji. Ni vema ikazingatiwa kwamba mtu ambaye tungemuunga mkono lazima awe ni mtu mwenye uwezo mkubwa kuliko tunayetaka kumtoa. Awe ana qualities za kiuongozi na zaidi sana awe na uwezo wa kupambana na mkuu aliyeko.

Tukileta mtu asiyefahamika sana kwenye mifumo ya taasisi yetu hata kama angekuwa mzuri kiasi gani hatachagulika na mkuu aliyeko atarudi kwa urahisi na kuendelea kuididimiza taasisi.

Katika kuchunguza ndani ya taasisi tuliridhika kwamba mtendaji mkuu msaidizi ana sifa zote tulizozitaja hapo juu ingawa kila mwanadamu ana udhaifu wake. Ni dhahiri pia kwamba udhaifu wa mtendaji mkuu msaidizi unarekebika kuliko wa mkuu aliyepo. Kwa ujumla mtendaji mkuu:

Ni kiongozi anayeweza kuongoza taasisi bila kujenga makundi akijali zaidi kazi ya taasisi kuliko maslahi binafsi.
Ameonyesha kwa vitendo kwamba hana maslahi binafsi kwa kuwa tumeshuhudia akifanya kazi nyingi za taasisi bila kudai malipo kwa njia ya posho ama vinginevyo.

Anaheshimika na viongozi wa ndani na nje ya taasisi jambo ambalo ni la muhimu sana kwa ustawi wa taasisi na kwa yeye kuwa mkuu wa taasisi tunatarajia wakubwa wengi sana kutoka nje ya taasisi yetu kuiamini na hata kujiunga nasi katika kuhakikisha tunafanikisha lengo la taasisi.

Ni msomi wa kiwango cha juu na mwenye uwezo mkubwa katika kuchanganua mambo ya kiuchumi, kisiasa, kijamii, kimichezo, nk jambo ambalo ni muhimu sana kwa kuwa ni hatari kuwa na kiongozi asiye na ujuzi wa kutosha kwenye masuala kama hayo.
Ndani ya taasisi anakubalika kwa makundi yote ya vijana, wazee na akina mama.

Uongozi wa sasa wa taasisi yetu umefanya tuonekana kwamba taasisi yetu ipo kwa ajili ya kuvuruga amani ya nchi.
Yote hii ni kwa sababu tumekuwa hatuna mbinu mpya za mapambano zinabadilikabadilika zaidi ya maandamano ya kila mara.
Kwa kuzingatia utamaduni wa watanzania wa kupenda amani, kuna haja ya kufuta hii taswira na njia rahisi ni kubadilisha uongozi wa taasisi haraka iwezekanavyo.

Uelewa wake wa mambo ya kiuchumi ni muhimu sana kwa taasisi kwa sasa. Tunahitaji kuja na vyanzo vipya vya mapato ikiwa tunahitaji kufanikiwa. Mkuu aliyepo si kwamba ameishiwa bali hana mbinu za maana za kuiimarisha taasisi kimapato kwa ajili ya malengo yake ya mbele.

Exposure kubwa na kukubalika katika siasa za kimataifa. Tunahitaji kiongozi ambaye anazifahamu siasa za kimataifa na anayeweza kuungwa mkono na viongozi wengi wa kimataifa. Ni hatari kutegemea utaweza kufanikisha malengo kama ya taasisi yetu bila mpango kabambe wa kuungwa mkono na jumuia ya kimataifa. Mpaka hivi sasa hakuna mpango wowote wala hata mchakato wa maana kuwa connected na jumuia ya kimataifa. Kiongozi wetu mkuu wa sasa yupo ‘too local' na hana mawasiliano yeyote ya maana na viongozi wengine katika kanda na kimataifa. Ndio maana mkuu huyo na mtendaji wake mkuu wamekuwa hawaonekani katika matukio makubwa ya kimataifa. Hata katika kutoa maoni katika mambo makubwa ya kitaifa na kimataifa viongozi hawa hawapo. Kwa kifupi kwa sababu ya aina ya viongozi tulio nao, nafasi ya taasisi yetu katika nyanja za kimataifa haipo!

Aina na staili ya uongozi wa sasa wa taasisi yetu ni kina kwamba nchi hii haipo hadi taasisi yetu itakapochukua dola.
Yaani tunafanya mambo kama kwamba tutaanza upya kabisa tukichukua dola. Ni kwa sababu tumegombana na kila mtu katika utawala wan chi, vikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama. Ukweli ni kwamba tutavihitaji vyombo hivi kabla na baada ya kuingia madarakani na ni ndoto kudhani kwamba tutakabidhiwa nchi kwa kugombana na kila mtu. Ni kwa sababu ya mtazamo kama huu ndio maana wakuu wetu wa sasa hawaonekani kabisa katika shughuli za kitaifa kama vile sherehe za uhuru wan chi, n.k.

Uwezo wa kuwaunganisha wasomi wa kada mbalimbali, wafanyabiashara wakubwa, watumishi wa umma na sekta binafsi, nk katika kupata muunganiko wa mawazo na kutoka na sera murua zinazogusa kila sekta. Hili la kuwashirikisha litaenda sambamba na kutoa elimu kwa wote waelewe na watuunge mkono. Tunasema hivi kwa kuwa watu wa kada mbalimbali hawajaelewa sera zetu juu ya mambo yanayowahusu mfano wafanyabiashara wakubwa, wawekezaji, wakulima, watumishi, wanafunzi,nk na hivyo hawajawa tayari kutuunga mkono. Kile kinachofanywa wakati wa uchaguzi kwa njia ya ilani ya uchaguzi na elimu kutolewa kwa njia ya kampeni majukwaani hakitoshi. Tunahitaji watu wajue tumeunda think tank kwa ajili hiyo na baadaye wajue nini kimetokana na think tank hiyo ili wajadili na kutoa maoni na hatimaye tutoke na kitu kinachokubalikwa na wananchi wote. Na tuna imani hilo tunayempendekeza ana uwezo nalo.

Kubwa zaidi ni kwamba alishaiangalia taasisi yetu na kuona mambo yanayohitaji mabadiliko na kujiangalia yeye na kuridhika kwamba ataweza kuleta mabadiliko tunayoyahitaji na ndipo mwaka 2009 aliamua kujitosa kuutafuta ukuu wa taasisi yetu kabla ya kuombwa kumwachia aliyepo.

SWOT ANALYSIS:
Kwa kutumia uchambuzi huu hapa chini wa uimara, udhaifu, fursa na vitisho ama vikwazo dhidi ya mtu tunayempendekeza, utaweza kutuonyesha kama tunayempendekeza ataweza kushinda vita iliyo mbele yetu.

Kama SWOT inavyotaka, tutaangalia sifa njema alizonazo tunayemtaka ambao ndio uimara wake, tutaangalia pia udhaifu wake, tutaangalia fursa alizonazo na mwisho tutazingatia vitisho ama vikwazo vilivyopo. Ni muhimu tukaeleza kwamba katika SWOT analysis tunajikita kwa mambo yanayohusika moja kwa moja na uwezekano wa tunayemtaka, kuchaguliwa. Kwa hiyo kwa mfano utakuta kwamba katika sehemu hii hatutazungumzia sifa njema alizonazo tunayemtaka kama kiongozi lakini sifa hizo zikawa hazina ushawishi wa kuwafanya wajumbe wa kikao cha uchaguzi kumchagua.

Uimara wa tunayemtaka:
Ingawa si mmoja wa waasisi wa taasisi yetu, lakini ni mwana taasisi mkongwe akiwa amejiunga na taasisi yetu miaka miwili tu tangu ianzishwe na mwaka mmoja tangu isajiliwe rasmi na serikali.

Zaidi ya kuwa mwanataasisi mkongwe, hajawahi kujiunga na taasisi nyingine hapo kabla. Alijiunga na taasisi hii kabla hata haijajulikana kwa watu na alibaki kuwa mwana taasisi mwaminifu hata pale taasisi zingine zilipoonekana kuwa imara na maarufu zaidi ya hii.

Kutokana na vipengele ‘a' na ‘b' hapo juu, hakuna mtu hata mmoja anayeweza kusema mtu huyu alikuja kwenye taasisi yetu kwa ajili ya kutafuta maslahi kama vile uwakilishi kwenye chombo chetu kikuu cha uwakilishi hapa nchini.

Ni mvumilivu sana. Katika jitahada za wakuu waliopo kuhakikisha wanaendelea kukalia viti vyao, wamejitahidi sana kumpaka matope lakini amevumilia. Mahali ambapo wengine wangeshakata tamaa na kuhama taasisi, yeye alibaki kuvumilia mpaka imefikia wana taasisi wa ngazi za chini waliokuwa wanadanganywa kwamba mtu huyu ni msaliti, wameanza sasa kushtuka.
Ana historia nzuri ya utendaji uliotukuka ndani na nje ya chombo cha uwakilishi.

Ana uwezo mkubwa wa uelewa wa mambo mbalimbali ya uchumi, jamii, utamaduni, michezo, nk. Uwezo wake unachagizwa si tu na elimu yake ya darasani bali pia vipaji na akili ya kuzaliwa.

Ni mzalendo wa hali ya juu anayeipenda nchi yake kwa moyo wa dhati. Amethibitisha hilo kwa namna anavyolitetea taifa letu katika medani za kimataifa na jinsi anavyolipigania ndani dhidi ya mafisadi na wasiolitakia mema taifa letu. Ni mwakilishi pekee aliyekuwa tayari kukosa mishahara ya miezi kadhaa kwa kuamua kusimamia ukweli kwamba kuna ufisadi ulifanyika mpaka akasimamishwa uwakilishi wake kwa mikutano kadhaa ya chombo chetu cha uwakilishi.

Katika kuzidi kuonyesha alivyo mzalendo tunaweza kusema hapa kwamba ni kiongozi pekee kutoka upande huu ambaye ameonekana sana kwenye mambo ya kitaifa kwa mfano kulipigania taifa letu katika mambo ya kimchezo, kutumia gharama zake kwenda nje ya nchi na kujifunza mambo mbalimbali yanayoweza kulisaidia taifa katika sekta nyeti kama mafuta, gesi na madini, nk bila kusahau kwamba amekuwa ndiye mwakilishi pekee aliyeongoza katika kuibua kashfa nyingi na nzito za ubadhirifu ndani ya serikali hata kufikia mawaziri kadhaa kufukuzwa kazi.

Mambo hayo tuliyoyataja kwenye vipengele ‘e', ‘f', ‘g' na ‘h' yamemfanya kuwa kiongozi wa kwanza kuwa maarufu sana katika taasisi yetu aliyewapiku hata viongozi wa serikali kwa umaarufu. Hii ya umaarufu ni sifa muhimu sana linapokuja suala la uchaguzi.

Uwezo wake wa kujieleza kwa kujenga hoja pale anapopewa nafasi. Hata pale anapokuwa amepakwa sana matope na wenzake, anapopewa nafasi ya kujieleza huweza kuwashawishi watu wengi wanaomsikiliza. Hii itamsaidia sana siku ya kujieleza mbele ya kikao cha uchaguzi ambapo ataweza kupangua hoja zote dhaifu za kumpaka matope.

Ana uwezo wa kuchangamana na makundi yote ambapo vijana humwona kama mwenzao, wanawake humwona kama mtetezi wao wakati wazee humwona kama kijana mwenye busara anayeweza kuelekeza kama kiongozi.

Ana mahusiano mema na mazuri na viongozi wa ngazi za chini kutokana na ziara nyingi alizozifanya na kukutana na viongozi wa ngazi za chini akiwa katika kuijenga taasisi hii. Mahusiano haya mazuri yanachagizwa na jinsi anavyotumia muda wa kuongea na viongozi wa ngazi za chini kuzungumza kwa lugha ya upole na kuelekeza viongozi wenzake bila kuwaonyesha dharau.

Si mtu wa kujipenda nafsi na katika kupambana umaskini wa watu badala ya umaskini wake, alifikia kuzikataa posho wanazolipwa wawakilishi wakati wakitekeleza majukumu ambayo kwayo wanalipwa na kuiomba ofisi ya chombo hicho kuzipeleka posho hizo kwa watu maskini.

Ana limu nzuri sana aliyoipata katika vyuo vinavyoeleweka kitaifa na kimataifa
Ni kijana na hii ni taswira njema kwa sababu taasisi yetu inaungwa mkono sana na vijana

Udhaifu wa tunayemtaka:
Maneno yake mara nyingine hayazingatii anayazungumza katika mazingira gani na hivyo kuwasha masikio ya wanataasisi jambo linalompunguzia kukubalika kwake taratibu.

Kama ilivyo kwa maneno, kuna matendo pia ambayo mara nyingine huyafanya bila kuzingatia mazingira na wasikilizaji wake na hivyo kupunguza imani ya wana taasisi kwake.

Hali ya ndoa ya tunayemtaka kutoeleweka msimamo wake

Kuna wakati tunayemtaka hu-respondkwa taharuki kubwa dhidi ya mashambulizi yanayoelekezwa kwake jambo linalomfanya achukue maamuzi yasiyo sahihi kwa wakati huo. Kwa kifupi kuna wakati tunayemtaka huonekana kufanya maamuzi kwaemotion zaidi badala ya kutulia kwanza na kutafakari kwa kina ikiwa ni pamoja na kutafuta ushauri kwa wenzake kabla ya kurespond.

Jambo lililoelezwa katika ‘d' hapo juu humfanya tunayemtaka wakati mwingine kuonekana ana jazba sana kwa sababu akishataharuki na kuchukua maamuzi akingali kwenye taharuki huwa ni rahisi sana kuonekana anajibu mapigo kwa jazba sana.

Ustahimilivu: yaliyotajwa katika ‘d' na ‘e' hapo juu yanaashiria tunayemtaka si mstahimilivu sana sifa ambayo inahitajika sana kwa kiongozi.

Uwazi: Katika taasisi zetu hizi ni muhimu sana kuepuka kufanya mambo yote wazi wazi hata kama ni mema ama ni haki ya mhusika ama si makosa katika jamii tuliyomo. Kuna mambo ambayo ni haki ya mtu mfano mahusiano binafsi ya kimapenzi, kuwa na marafiki wa damu kutoka upande mwingine wa utawala, nk. Lakini mambo hayo ni muhimu wakati mwingine ama kwa kiwango fulani yakafanywa kwa siri kuepuka mitazamo potofu kwa unaowaongoza.

Fursa alizonazo tunayemtaka:
Utamaduni wa taasisi yetu wa kubadilisha wakuu wa taasisi kila baada ya vipindi vifupi ili kuleta maono mapya kwenye taasisi unampendelea tunayemtaka.

Udhaifu ulioonyeshwa na uongozi uliopo chini ya mpinzani wetu katika kutekeleza program mbalimbali za taasisi nyingi zikiwa zimebuniwa na wao wenyewe, pia ni fursa kwa tunayemtaka.

Udhaifu mkubwa ulioonyeshwa na uongozi uliopo kwenye ugawanyaji wa raslimali za taasisi kama vile fedha za ruzuku, michango mbalimbali ya wahisani na hata vifaa vya uenezi.

Kujitokeza kwa tunayemtaka kutaonekana kama fursa kwa wanataasisi kufanya mabadiliko makubwa na kuua kabisa ile propaganda ya kwamba taasisi yetu ni ya kabila fulani ama eneo fulani kwa kufanya reference kwa uongozi wa taasisi.

Hoja ya uongozi uliopo kushindwa kabisa kusoma taarifa za fedha tokea 2010 ikifahamika kwa wapiga kura inaweza kuwa machinjio kabisa ya uongozi uliopo na kumpa fursa kubwa tunayemtaka.

Imani ambayo wana taasisi wengi wanayo kwake. Utafiti mdogo unaonyesha kwamba bado jina la tunayemtaka linatamkika sana midomoni mwa wanataasisi pale wanapotajwa viongozi wa juu wa taasisi yetu. Hii inaonyesha bado wana taasisi wanayo imani kubwa kwake na kwa hiyo atakapopata fursa ya kupangua matope aliyopakwa atakuwa na nafasi kubwa ya kuchaguliwa.

Mpinzani wetu hana historia nzuri ya utendaji uliotukuka ndani na nje ya chombo cha uwakilishi. Hakuonyesha utendaji wowote wa pekee alipokuwepo kwenye chombo mwaka 2000 -2005 na hata alipopewa uongozi wa upande wetu ndani ya chombo tokea 2010 hadi leo 2013 hajafanya lolote la kutukuka ndani ya chombo hicho.

Mpinzani wetu hana uwezo mkubwa wa uelewa wa mambo mbalimbali ya uchumi, jamii, utamaduni, michezo, nk. Si tuelimu yake ya darasani ni ya magumashi bali pia vipaji na akili ya kuzaliwa havijaonekana katika maisha yake.

Uzalendowampinzani wetu unatia shaka akiwa hajaonyesha lolote la maana katika kulitetea taifa letu kimataifa. Ingawa ameshapata nafasi lukuki ya kwenda nje ya nchi lakini mara zote akifika huko ni kuiponda tu nchi yake. Ingawa anayo majukwaa ya kufanya hivyo akiwa ameshakuwa mwakilishi mara mbili kwenye chombo chetu lakini hatujawahi kumsikia akiibua kashfa mahsusi ya ufisadi na kuisimamia zaidi ya yeye mwenyewe wakati fulani fulani kutuhumiwa kwa ufisadi mfano pale alipokopa kwenye shirika la umma na kugoma kulipa mkopo.

Katika kuzidi kuonyesha uzalendo hafifu wa mpinzani wetu tunaweza kuangalia jinsi ambavyo mpinzani haonekani kwenye mambo ya kitaifa. Hii ni fursa kwa tunayemtaka. Mpinzani wetu si maarufu akilinganishwa na tunayemtaka na hivyo kumpa fursa zaidi tunayemtaka kumshindani mpinzani wetu kwenye uchaguzi. Uwezo wa mpinzani wetu wa kujieleza kwa kujenga hoja pale anapopewa nafasi ni mdogo sana.

Mpinzani wetu hajazoea ushindani na changamoto. Ni mtu aliyezaliwa kwenye utajiri na anadhani pesa ni kila kitu. Ukimnyang'anya pesa ukamwambia ashindane kwa hoja hawezi na ndo maana anajaribu sana kuhakikisha anaingia mwenyewe ulingoni bila kupingwa.

Kutokana na tuliyoyasema hapo juu kwenye ‘m' ni dhahiri kwambapale mpinzani wetu anaporushiwa kombora la kashfa anakuwa mzito kujieleza hata kama anapewa nafasi ya kufanya hivyo na hii ni fursa muhimu kwa tunayemtaka.

Mpinzani wetu ni mgumu sana katika kuchangamana na makundi yote ambapo vijana humwona kama si mwenzao kiumri na kifedha, wanawake humwona kama malaya anayependa kutumia miili yao kujistarehesha wakati wazee humwona kama mtu anayedhalilisha hata nafasi aliyopewa kwa kufanya uhuni waziwazi hata kuvunja ndoa si ya kwake tu bali hata za watu wengine.

Mpinzani wetu hana mahusiano mema na mazuri na viongozi wa ngazi za chini kutokana na dharau nyingi anazozionyesha pale anapokukutana na viongozi wa ngazi za chini akiwa katika kuijenga taasisi hii. Hutumia muda mwingi kuwaponda viongozi wenzake hata kufikia kutamka mara nyingi kwamba kama kiongozi hawezi kujigharamia nauli na malazi ya kutoka mahali fulani kwenda mahali fulani kwa siku kadhaa hafai kuwa kiongozi bila kujali kwamba kuna viongozi wetu wana moyo na taasisi hii na ndo wameifikisha hapa ilipo lakini hawana uwezo wa kifedha na hivyo kauli kama hizo za mkuu huyu huona kama anawadharau kwa kuwa yeye ni tajiri.

Hii imemfanya kutopendwa na viongozi wengi wa ngazi ya chini hivi sasa na kutoa fursa ya pekee kwa tunayemtaka.
Mkuu aliyepo amekuwa na mkakati unaoitwa kuondoa watu wa zamani. Jambo hili linawaudhi sana viongozi wa ngazi za chini ambao wanaona kama baada ya kuifikisha taasisi mahali ilipo kwa sasa wanaonekana hawana maana tena. Wengi wamefikia kuapa kwamba kama mwendo ni wa kuwaondoa watu wa zamani basi na yeye ni wa zamani lazima aondoke.

Mpinzani wetu amejionyesha dhahiri kujipenda na kujijali nafsi bila kujali watu wa hali ya chini. Matukio mawili yanamwacha uchi katika hili pale alipolitangazia taifa kwamba wawakilishi wetu wote hawatachukua posho za vikao halafu yeye na wengine wote wanazichukua hadi leo na kumwacha mtendaji msaidizi peke yake. Na la pili linalofanana na hilo ni pale alipotangaza kutotumia gari la serikali ambalo ni la kifahari kisha akalirudia kimya kimya.

Kuwepo muhtasari wa kikao cha wazee ambacho mwaka 2009 kilimshauri tunayemtaka ajitoe na kumwachia mkuu aliyepo na kumtaka mkuu aliyepo kumwachia tunayemtaka katika uchaguzi ujao na wote wakasaini makubaliano hayo, nayo ni fursa muhimu sana kwa tunayemtaka.

Mkuu aliyepo anaamini kwamba ameshamsambaratisha tunayemtaka na hivyo kwa sasa amebweteka na hiyo inatupatia sisi fursa kuendelea kuimarisha mtandao wetu.

Kwa kuwa ni mwislamu. Hii ni fursa katika kupata kuungwa mkono na wanachama waislamu ambao wamekuwa na kigugumizi wakidhani waislamu hawatakiwi katika uongozi wa taasisi yetu.

Elimu ndogo na duni aliyenayo mpinzani wetu ambaye ndiye mkuu wa taasisi yetu kwa sasa. Kwa sasa ni kiongozi pekee katika nchi yetu anayeongoza taasisi kubwa asiye na elimu ya shahada huku taasisi yetu ikiwa inaongoza kwa kuwa na wasomi waliobobea katika kila nyanja.
Hii ni kejeli hasa kwetu sisi ambao tumekuwa tukiwasema wenzetu kwamba ‘akili ndogo' inaongoza akili kubwa. Kimsingi tumekuwa tukijisema kwa kukubali kuongozwa na mtu mwenye akili ndogo.

Mkuu wa sasa kutokuwa na msimamo thabiti katika mambo ya msingi. Rejea swala la maandamano ya kumshinikiza Kawambwa ajiuzulu na kujitoa katika mchakato wa katiba.

Vikwazo dhidi ya tunayemtaka:
Sisi wenyewe tunaoandaa mkakati huu hatuna uhakika kama tunayemtaka yuko tayari na yuko serious na business hii, na kwa hiyo huenda tusifanye kwa nguvu zetu zote ikiwa hatutapata nafasi mapema ya kukutana na mhusika na akatuhakikishia kwamba yuko serious.

Utayari wa mhusika mkuu kutekeleza yale tunayokubaliana. Inapotokea baada ya kukubaliana sisi na yeye akapata ushauri tofauti na ukauona uko more genuine, basi tuwasiliane kwamba nimeshawishika kufanya hivi badala ya vile tulivyokubaliana kwa sababu hizi ama zile.

Hii haitatukatisha tamaa tofauti na kama tutakuwa tunapanga hivi halafu yeye anafanya vile bila maelezo yoyote
Kitendo cha mkuu aliyepo kung'ang'ania kuendelea nayo ni kikwazo kwa kuwa baada ya kuwa madarakani kwa miaka yote hiyo lazima amejipatia watu wanaomhusudu ama kumpenda ama kumkubali na kuwepo wengine wanaoogopa tu kwamba mkuu aliyepo akitoka taasisi itakufa hata kama hawana sababu yoyote.

Tunatazamia mkuu aliyepo atafanya vitendo vingi zaidi vya haramu katika kumdhibiti tunayemtaka pale tunapoelekea kwenye uchaguzi wenyewe.
Raslimali za taasisi kutumiwa na viongozi waliopo katika kumsaidia mkuu aliyepo wakati wa kwetu anatumia raslimali zake za mfukoni.

Propaganda chafu zilizokwishapigwa dhidi ya tunayemtaka zimepunguza imani ya wanataasisi kwa tunayemtaka kwa kiasi fulani
Baadhi ya mambo ambayo amekwishayasema ama kuyatenda nayo yameshawapunguzia imani kiasi fulani wanataasisi mbalimbali.
Kutoonekana sana kwenye operations za taasisi yetu pia kumewapa wasiwasi baadhi ya wanataasisi.

Muhtasari wa SWOT analysis unaonyesha kwamba strength na opportunities za tunayemtaka ni nyingi sana zikilinganishwa na weaknesses zake na threats dhidi yake. Aidha ukichambua zaidi utaona kwamba weaknesses za tunayemtaka nirepairable na vikwazo dhidi yake pia ni rahisi kuvikabili na kuvisambaratisha. Tukishamaliza maandalizi ya mkakati huu tukaonana na mhusika mkuu na kumpa ushauri akatulia na kufanya kazi, mkuu aliyepo hatafua dafu.

Tunahitaji kutekeleza mkakati huu kwa siri kubwa ili mkuu aliyepo aendelee kubweteka na ndiyo maana hata lugha iliyotumika ni ndani hapa ni ya pekee. Tunahitaji tunayemtaka asionekane kama kuna kitu anafanya na tunafurahi kwamba kuna wakati alitangaza kwamba hana nia ya kugombea tena waliopo wanatosha. Ikitokea vyombo vya habari vikamuuliza tena hiyo ndiyo iwe kauli yake ili kuendelea kumfanya mkuu aliyepo asihangaike na hivyo kuja kummaliza kirahisi. Aidha katika utekelezaji wa mkakati kama tutakavyoeleza hapo baadaye, tunayemtaka atajitenga mbali asionekane hata kuwa karibu na sisi. Vikao vyetu na yeye vitafanyika mara chache sana na mahali pa faragha kupita kiasi ikiwezekana hata nchi jirani.

Mkakati huu hautatakiwa kupatikana kwenye komputa zaidi ya tatu yaani ya mchapaji ambaye ni M3, ya M3 na ya MK mwenyewe. Hata hivyo email zitakazotumika kusafirisha mkakati huu kutoka kwa M3 kwenda kwa M1 hadi kwa MK hazitakuwa zile za kawaida za hao watu bali mpya kabisa zilizofunguliwa kwa makusudi haya tu na kwa majina fictitious. Aidha kila atakayekuwa na mkakati huu kwenye computer yake anatakiwa kuliwekea file hilo password ili hata mtu wa karibu naye anayeweza kufungua computer yake asiweze kulifungua file hilo. Pia email address hazitatolewa kwa sms bali kwa kupiga na kuambiana spelling za address.

MTANDAO WA USHINDI:
Mtandao wa ushindi utakuwa kama ifuatavyo. Kwenye ngazi ya kitaifa tutakuwa na kamati yenye members watatu tu. M1 ndiye atakayekuwa anawasiliana na tunayemtaka ambaye ataitwa MM (Mhusika Mkuu).

Tumepanga kwamba kusiwe na mawasiliano mengi kati ya kamati na mhusika mkuu kuepuka tracking ya wapinzani wetu. M1 ni mtu wa karibu na MM kwa hiyo mawasiliano yao hayataweza kutiliwa shaka na mtu yeyote hata wangewasiliana mara nyingi kiasi gani. Hata hivyo, linapokuja suala la mkakati huu tunasihi mawasiliano yawe kwa kuonana uso kwa uso ama kwa simu na si sms. M1 ndiye atakayewasilisha mambo yote yanayotoka kwenye kamati ya kitaifa na endapo kuna haja ya MM kukutana na kamati ya kitaifa, mipango yote ya kikao itafanywa na M1 kwa usiri mkubwa. M2 ni mtu ambaye yuko kwenye ofisi kuu za taasisi yetu wakati M3 ndiye mchapaji wa mkakati huu.

Kamati hii imefanywa kuwa na members wachache sana wenye uelewa mpana wa mambo na wenye elimu nzuri ili kuhakikisha kazi inafanyika kitaalam na kwa uhakika sana. Kamati ya kitaifa itapeleka mapendekezo yake kwaMM na yeye pia ataleta ushauri wake kwa kamati kama mishale inavyoonyesha. Chini ya kamati ya kitaifa kutakuwepo waratibu wa kanda zote kumi watakaojulikana kama MK1 – MK10. Hawa watatafutwa na kusimikwa na kamati ya kitaifa kwa kushauriana na MM kwa utaratibu utakaokubalika na pande zote yaani MM na kamati ya kitaifa. Chini ya waratibu wa kanda kutakuwapo waratibu wa mikoa yote 30 (MMK1 – MMK30) ambao watapatikana kwa utaratibu ule ule wa kuwapata waratibu wa kanda. Isipokuwa pale ambapo inakuwa ngumu, itabidi kamati ya taifa isaidiane na waratibu wa kanda kuwapata waratibu wa mikoa lakini kamati itashauriana na MM kabla ya kuwasimika rasmi hao waratibu wa mikoa.Mtandao utakuwa kama inavyoonyeshwa kwenye mchoro ufuatao:


NAMNA YA KUFANIKISHA MKAKATI:

Kazi itagawanywa katika awamu tatu:
Awamu ya kwanza ni kuanzia sasa mpaka uchaguzi wa ngazi ya matawi utakapoanza. Katika awamu hii kazi ni kuhakikisha kwamba mtandao mzima umekamilika mpaka kwenye ngazi ya mkoa. Kazi nyingine itakayofanyika ni kwa waratibu wa mikoa kuendelea kuspot makada kwenye wilaya na mikoa ambao tayari wana mtazamo tulio nao ama ambao wanaweza kuingiziwa kirahisi mbegu hii ya mabadiliko na wakawa tayari na wana uwezo na sifa za kushinda uongozi kwenye wilaya na mikoa yao bila kusahau sifa ya kuwa waaminifu wenye uwezo wa kutunza siri. Kulingana na muda hii ni kazi inayotakiwa kufanyika sasa lakini kwa uangalifu mkubwa. Ni muhimu kukumbushana hapa kwamba katika awamu hii hakuna anayetakiwa kujua mpango mzima zaidi ya kamati ya kitaifa na MMili kuhakikisha uwezekano wa mkakati wetu mapema kwa wapinzani wetu unakuwa minimized to almost zero.

Awamu ya pili ni kipindi kuanzia uchaguzi wa matawi mpaka uchaguzi wa mikoa unapokamilika. Katika awamu hii tutasaidiana na waratibu wa kanda na mikoa kuhakikisha makada tuliowaspot kwenye wilaya wanapanga safu zao kwenye kata ili kuhakikisha watakaochaguliwa kwenye kata ni watu wao ili waje wawachague kwenye wilaya.Vivyo hivyo kwa makada tuliowaspot kwenye mikoa wahakikishe wanaochaguliwa kwenye wilaya ni wale makada wetu ili nao waje wawachague kwenye mikoa yao. Hapa ndipo kwenye kazi kubwa ya mkakati wetu na hapa ndipo tutakapohitaji kuingia gharama zaidi kwa ajili ya kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa asilimia angalau 80.

Awamu ya tatu ni kuanzia baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa mikoa hadi uchaguzi wa kitaifa utakapoitishwa. Katika kipindi hiki kwa ustadi mkubwa tutakuwa tukiwaandaa makada wetu waliochaguliwa tayari kuja kufanya mabadiliko makubwa kitaifa. Ni wakati huu ambapo tutawaingizia mkakati taratibu lakini kwa ustadi mkubwa tukijikita hasa kwenye kuonyesha kwa nini tunahitaji mabadiliko. Ni katika kipindi hiki ambapo kwa ustadi mkubwa tunaweza kuwaspot wale waliochaguliwa ambao hatukuwaandaa na kuwaingizia pia mbegu ya mabadiliko ili kuwawin na kuwarecruit kwenye mkakati.

Aidha katika awamu zote tatu kazi ya kuianalyze ofisi kuu itakuwa non stop kwa kuzingatia kwamba mabadiliko ya wakurugenzi na maofisa yatakuwa yanatokea na watu nao watakuwa wanabadilika kimtazamo. Analysis ya ofisi kuu ni kuhakikisha tunajua nani na nani wako na sisi na nani na nani wako against na pia nani na nani wanaweza kupandikiziwa mbegu kwa ustadi na wakaungana nasi.


MAHITAJI YA KUFANIKISHA MKAKATI:
Raslimali watu. Tunahitaji watu waaminifu watatu kwenye ngazi ya kitaifa ambao tayari wapo. Tunahitaji watu waaminifu kumi kwenye kanda ambao tutawatafuta na pia waaminifu wengine 30 kwenye mikoa yote thelathini.

Fedha. Tunahitaji fedha kwa ajili ya mawasiliano kati ya wanakamati na wale wa ngazi ya chini. Aidha tunahitaji fedha kwa ajili ya gharama za usafiri pale tutakapohitaji kwenda kwenye kanda na mikoa husika kwa ajili ya kusimika watu hao tunaowahitaji.

MAPENDEKEZO MAHSUSI NA HITIMISHO:

Katika kuhitimisha tunapendekeza mambo mahsusi yafuatayo:

Kuhusu Bajeti:
Tunapendekeza kwamba bajeti ya mkakati huu isipangwe hivi sasa. Ni muhimu tu sote kuelewa kwamba wakati wenzetu wanatumia raslimali za taasisi kujijenga na kutekeleza mkakati wao wa ushindi, sisi tunapaswa kuingia mifukoni. Kwa kila kila mmoja wetu atakuwa budget conscious ili kuepuka matumizi makubwa ya pesa. Hata hivyo, kwa kuzingatia kwamba lazima pesa inahitajika ni muhimu M1 na MM kujaribu kuangalia namna ya kuraise pesa na kushauri. Otherwise, tutakapokuwa tunahitaji kufanya hatua yoyote ama jambo lolote tutakuwa ndo tunapiga hesabu za funds tunazohitaji kwa jambo husika na kuingia katika utekelezaji.

Kuhusu mwenendo wa MM kuanzia sasa:
Ni maoni yetu pia kwamba kuanzia sasa MM aenende katika mwenendo ambao utarahisisha ushindi. Mfano tunapendekeza afanye yafuatayo kuanzia sasa:

Apunguze ukaribu na viongozi wa serikali na wa chama tawala na awe crical zaidi na utendaji wa serikali nje na ndani ya bunge.
Ashiriki kikamilifu katika shughuli za taasisi yetu zikiwamo vikao vyote vinavyomhusu, operesheni mbalimbali, chaguzi ndogo, nk.
Aendelee kushusha ‘nondo' ndani ya chombo chetu cha uwakilishi na kuendelea kuwa juu ya wawakilishi wengine katika hoja mbalimbali zenye maslahi ya kitaifa.

Ajitahidi kudhibiti jazba hata pale anapokuwa amebambikiziwa tuhuma nzito namna gani. Atulie, ashauriane na wazee ili kuona namna nzuri ya kujibu tuhuma zinazomkera. Tukumbuke kwamba wakati mwingine kukaa kimya ni jibu zuri zaidi kuliko hoja nzito.
Sambamba na ‘iv' hapo juu, adhibiti sana emotion ili kuhakikisha kila kitu kinachofanywa ama kuzungumzwa kinachomgusa asikimbilie kuongea na vyombo vya habari ama kwenye mitandao ya kijamii bali afuate kile tulichokizungumza kwenye kipengele cha ‘iv' hapo juu.

Kuhusu mapambano ya kuchafuana kwenye mitandao ya kijamii:

Katika hili sisi hatukuona haja ya kufanya hivyo kwa sababu mbili:
Imani yetu kwamba taasisi yetu ni kubwa kuliko watu kwa hiyo ni muhimu kuzingatia kwamba hatuiui taasisi katika mapambano haya. Tukiendekeza mashambulizi kwa njia ya mitandao ya kijamii hatutakuwa na ngao ya kuwakinga watu wa kawaida (wanataasisi na wasio wanataasisi) dhidi ya kujikuta wakiamini kwamba taasisi hii nayo haina jipya ni sawa tu na ile tunayotaka kuitoa.

Tutakuwa tumeiua taasisi na mkakati huu hautakuwa na maana sana kama lengo ni kufanya mabadiliko ya uongozi wa taasisi tu lakini malengo ya taasisi ya mwaka 2015 yasitimie!

Kujikita kwenye mashambulizi kupitia mitandao ni kuzidi kuwashtua wakuu waliopo kwamba bado tuko serious na mkakati wa kuwatoa na kuwafanya wafanye kazi zaidi huku wakiendelea kumpaka matope MM kwamba ndiye anayerusha makombora hayo kwenye mitandao kwa kusudi la kuhujumu taasisi maana hiyo ndo lugha yao. Hatukatai kwamba wakuu wanajua kabisa kwamba bado MM ana nia ya kumvaa mkuu aliyepo lakini tunajua kwamba kwa sasa wanaamini wamemdhoofisha na hana madhara tena. Ndiyo maana tunataka kutekeleza mkakati wetu kwa siri sana ili wafikiri MM amekata tamaa kumbe ndo anakuja na mkakati mzito zaidi.

Hata hivyo, ni muhimu kukumbushana kwamba wenzetu hawatanyamaza kwa sababu eti sisi tumeacha kuwashambulia kwenye mitandao ya kijamii. Lazima wataendelea! Wataendelea kumchafua MM kwa kupitia wapuuzi kama yule kichaa wa ‘ars' na kundi lake. Nini tutakuwa tunakifanya sasa? Tutahakikisha tuko busy kupost mambo mema na mazuri yatakayokuwa yakifanywa na MM kila wakati na kuzidi kusambaza sifa zake njema kila inapotokea nafasi. Atakayefanya kazi hiyo ni sisi wengine wala si yeye! Pia tutahakikisha kila post ya kumchafua inapatiwa majibu bila kutumia ID yake inayojulikana. Ni vema aidha akatupatia majibu na sisi kuyapost ama afungue ID mpya kabisa ambazo hazijawahi kuwepo kwenye mitandao halafu ndo awe anazitumia kujibu lakini kwa kuzingatia tuliyokwishayazungumza hapo juu yaani kutofanya kwa emotion na kuepuka jazba lakini pia kushauriana na watu wa karibu kabla ya kutoa majibu kwa jambo lolote linalomhusu.

Kuhusu kamati ya kitaifa (hususan M2 & M3):
Tulikubaliana kwa kauli moja kwamba katika kutekeleza mkakati huu tunahitaji members hawa wawe wametulia kimaisha. Inakuwa vigumu kwa mfano kumtaka member aende mahali fulani kwa makusudi ya mkakati huu wakati hajui familia yake nyumbani anaiacha inakula nini. Tuliona kwamba M3 tayari hana kazi kwa sasa tena kwa kufanyiziwa na wakuu waliopo. Ni katika mwendelezo huo huo tunamwona M2 naye akiwa ukingoni kupigwa nje na kuachwa mtupu na wakuu waliopo katika kile wanachokiita wao reshuffle ya ofisi kuu. Kwa sababu hiyo tukapendekeza kwamba MM kwa kushirikiana na M1 kwa hatua ya kwanza wanaweza kutafuta kiasi cha sh. 2m kila mmoja tukijua kwamba kama members hawa wawili wakisaidiwa milioni mbili mbili wanaweza kuanzisha projects ambazo zitawasustain hata kama hawana ajira. Kwa hatua ya baadaye tutasaidiana kuona kama hawa members wanaweza kusecure good employments mahali, provided hazitawazuia kufanya siasa.
Ndugu wana jamvi na duru za siasa.
Kwanza taarifa hii haijakanushwa na uongozi wa CDM au idara yoyotE na inabaki
ilivyosambazwa katika .
Pili, Chadema wamesema wazi wahusika wamekiri kuhusika na habari hii
Tatu, tunafahamu kuwa watuhumiwa watakuwa na kikao kujibu yaliyoelekezwa kwao na wanahaki ya kusikilizwa ili kupata ‘habari iliyo na uwiano'

Itakapodhihirika kuwa taarifa hii haina ukweli, wahusika kuikana ,uongozi wa CDM utapaswa kujiuzulu kwa sababu ni kosa la kukosa imani, kuvunja uaminifu, kudanganya, kuhadaa na kupaka watu matope.

Kwa wakati huu tutaijadili habari hii kama ilivyoletwa.

Tunafahamu baadhi ya maoni yataweza kutumika katika kujenga au kujibu hoja kwa mikutano kati ya watuhumiwa na wana habari, hilo halitaondoa ukweli kuhusu tunachokiona hakikufanyika, kimefanyika, kina ukweli, kina udanganyifu au upotoshaji.

Tusimame katika ukweli tukiongozwa na fikra wala si hisia, chuki kwakuelewa kuwa upinzani ni sehemu muhimu`ya ustawi wa demokrasia na maendeleo ya nchi yetu.

Post inayofuata tutaanza kuchambua hoja moja baada ya nyingine bila upendeleo au uonevu lakini pia bila huruma au ushawishi wa namna yoyote.

Wana duru lets get strated

Other links
https://www.jamiiforums.com/great-t...ba-ya-jk-kuzindua-bunge-maalum-la-katiba.html

https://www.jamiiforums.com/great-t...shaji-na-kiwewe-cha-kuzinduka-tanganyika.html
 
Marejeo: Kwa muda mrefu tumetahadhirisha sana kuhusu mgogoro ndani ya CDM. Mwezi wa 6 mwaka jana'sakata la Juliana Shonzo' tuliandika kwa undani kuwa nguvu yake ilikuwa na msukumo mkubwa ndani ya chama.

Tulionya mgogoro wa Kafulila kuwa kuna nguvu zaidi isiyoonekana na hivyo kuna tatizo
Mgogoro wa Masalia, tulionyesha ufa mkubwa zaidi uliopo unaohitaji ufumbuzi wa haraka.

Wiki moja iliyopita tuliandika kule duru za siasa kuhusu chanzo cha mgogoro, wahusika kwa kuwataja, na nini CDM wafanyae.
Tulionya kuwa mgogoro huo ni mkubwa unaoweza kukivuruga chama kama ilivyokuwa kwa NCCR na CUF.
Yote yaliyowahi kujadiliwa leo ni marudio tu, kinachotokea sasa ni 'movie' tuliyoiona wakati inaandaliwa tukiwa watazamaji.

Wiki iliyopita tulisema haya
1. Mgogoro unahitaji suluhu ya haraka. Mpambano wa Lema, Zitto, Mwigamba ni dalili, tatizo lilikuwa kubwa.
2. Tulionya kuwa mgogoro huu unachochowe kutoka nje wahusika wakubwa wakiwa ndani ya CDM
3. Tukashauri kikao cha haraka ili kushughulikia tatizo kwasababu litakapofumuka lenyewe itakuwa ni balaa wala si tatizo
4. Tukasema ili kuleta uwiano mzuri na utengamano lazima awepo msuluhishi nje ya uongozi na kundi la watuhumiwa

5. Tukashauri baraza la wadhamini wa CDM waliangalie tatizo na kulichukua mikononi mwao
Sababu zilikuwa kama ifuatavyo
a) Kuepuka maamuzi ya jazba au yenye namna isiyotenda haki kwasababu tayari kuna pande mbili na moja haiwezi kuwa inatuhumu, ikasima upande mwingine na kuendesha mashataka, ikageuga na kutoa hukumu
b)Maamuzi nje ya uongozi uliopo yataleta muafaka miongoni mwa wanachama waliogawanyika katika makundi kwa itikadi na mapenzi tu ya viongozi

6. Tukashauri kuwa ni muhimu ukwepo uchaguzi kabla muda tete haujawadia ili kuleta utengamano kabla ya mwaka 2015

7. CDM izingatie masuala ya kijamii katika kulishugulikia tatizo kwasababu ni kubwa na lina mizizi na washiriki wengi.

Kikao cha kamati kuu kimetoa maamuzi ya kuwavua uanachama na kutaka wajielezekatika siku 14 kwanini wasifukuzwe

Hatua hizo zinaweza kuwa za kidemokrasia, zilizofuata taratibu, sheria nakanuni.
Lakini je, zilizingatia factors nyingine zinazoweza kujitokeza ambazosi lazima ziwe za kanuni , sheria au maadili?
Je, hatua zilifuata kwa kuangalia nyakati, jamii au mazingira ya suala lenyewe?

Uwepo wa makundi ya ushindani ndani ya chama cha siasa ni jambo zuri sana.
Makundi hutoa viongozi bora kama chekecheo na ndivyo ilivyo duniani kote.
Kinachotakiwa ni kushindanisha sera, maono na mipango.
Tenamakundi hayo ni ya ushindani na wala si upinzani

CCM ilikuwa na ushindani wa ndani uliojenga chama, baada ya kuuachakilichofuata ni makundi na maana nzima ya chama tawala imepotea. Kilichobaki nikuviziana katika 'glasi za maji ya kunywa'

Mag3 hoja yako ina msingi na mantiki. Hebu tuvute subira kidogo ili tupate kuona silingi pande zote

Tutaendelea baada ya mkutano tarajiwa kesho
 
Mkuu nadhani tunatakiwa kujua kuwa migongano ndani ya chama ni jambo la kawaida, na kimisngi kama ikiwa hadled vizuri basi inaweza kujenga chama na sio kukibomoa. Nadhani tunaweza kujifunza kutokana na experience ya NCCR.

KUna watu walijazwa NCCR na kufanya kila hila kuijuhumu hadi ilipokuifa, na wale waliojazwa wakaneda TLP na Mremba na kummaliza huko huko TLP.

Kueleka 2013 ni wazi kabisa kuwa sasa hivi CDMinawekwa kwenye defence mode ili isihindwe kuishambulia CCM, na kinachotokea ndani ya chama, kama kweli ni genuine mgogoro naona ni jambo zuri, as longo as linalenga kuifanya CDM iwe na posture ya offense.

Tunatakiwa kuiangalia CDM as a an institution and its ability to deal with internal troubles, i do not think it is of any good start looking into individuals.
 
Mkuu nadhani tunatakiwa kujua kuwa migongano ndani ya chama ni jambo la kawaida, na kimisngi kama ikiwa hadled vizuri basi inaweza kujenga chama na sio kukibomoa. Nadhani tunaweza kujifunza kutokana na experience ya NCCR.

KUna watu walijazwa NCCR na kufanya kila hila kuijuhumu hadi ilipokuifa, na wale waliojazwa wakaneda TLP na Mremba na kummaliza huko huko TLP.

Kueleka 2013 ni wazi kabisa kuwa sasa hivi CDMinawekwa kwenye defence mode ili isihindwe kuishambulia CCM, na kinachotokea ndani ya chama, kama kweli ni genuine mgogoro naona ni jambo zuri, as longo as linalenga kuifanya CDM iwe na posture ya offense.

Tunatakiwa kuiangalia CDM as a an institution and its ability to deal with internal troubles, i do not think it is of any good start looking into individuals.
Well said Bongolander
Katika bandiko 3 nimezungumzia hili la ushindani nikasema ni jambo zuri sana katika kuimarisha demokrasia.
Ninachokiona ndani ya cdm ni upinzani na wala si ushindani. Upinzani hauwezi kutokea ndani ya chama kimoja lakini upinzani unatokea miongoni mwa vyama.

Chadema kama insitution ambayo imebeba matarajio ya sehemu ya jamii inapaswa kuoneysha utayari wa kushughulikia migogoro ndani ya chama kwanza ili kuonyesha utayari wa kushughulikia migogoro katika dola.

Kwa viashirio, maoni, maonyo n.k. haikuonekana kama insitution inayoweza kufanyia kazi habari. Ndio maana nilieleza kuwa tatizo halikuanza juzi Arusha, lilianza kuanzia wakati wa Kafulila, Juliana na Masalia kwa ujumla.
Kwanini tatizo lenye miaka zaidi ya 5 liendelee kuitafuna institution kubwa kama hiyo? Kuna utayari kwa hilo.

Ni kweli lazima tuiangalie kama institution lakini pia ikumbukwe kuwa institution inatangenezwa na watu na hakuna institution inayoishi bila watu. Ni watu wanaojenga au kubomoa na hao ndio wanaangaliwa.
CDM kama chama sioni kama kuna tatizo, lakini CDM kama uongozi naona lipo tatizo.
Je, hilo lifumbiwe macho tukitumaini kuwa institution itajirekebisha yenyewe?

Ni kweli kuwa kuna mbinu za kuihujumu kutoka kwa CCM. Hii ni baada ya CCM kukosa nguvu za hoja kama insstitution iliyotokana na watu kuacha misingi yake ya awali, kuruhusu watu kuingilia institution n.k.
Lakini pia majaribio kama ya kuwagawa watu kwa kutumia ukabila na udini yalionekana kugonga mwamba na pengine kuirudi CCM kwa namna moja au nyingine.

Kinachoonekana sasa hivi ndani ya cdm ni kuruhusu au kutoa udhaifu ambao CCM wanautumia kuimaliza.
CCM sidhani kama ina makosa kwasababu ndicho inachotaka, makosa yapo CDM kwa kuruhusu udhaifu unaowezesha CCM kutimiza matakwa yake.
 
wakuu matamko yameshatolewa,
TAARIFA YA ZITTO ZUBERI KABWE (MB) KUHUSU KUVULIWA NAFASI ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA CHANGU CHA CHADEMA

1. Utangulizi


Katika kikao chake cha siku mbili kilichofanyika tarehe 20 - 22 Novemba 2013, Kamati Kuu ya CHADEMA, pamoja na mambo mengine, iliazimia kunivua nafasi zangu zote za uongozi ndani ya chama. Kwa mujibu wa taarifa ya chama iliyotolewa katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa tarehe 22 Novemba 2013, ilielezwa kwamba sababu za kuvuliwa uongozi mimi na Dk Kitila Mkumbo ni uhaini na hujuma kwa chama kutokana na waraka unaojulikana kama mkakati wa uchaguzi 2013. Ukweli ni kwamba waraka uliotajwa si sababu ya mimi kuvuliwa nafasi zangu za uongozi kama ilivyojadiliwa katika Kikao cha Kamati Kuu.

Sababu za kufukuzwa kwangu kama zilizojadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu ni tuhuma lukuki ambazo si mara yangu ya kwanza kuzisikia zikijadiliwa ndani na nje ya vikao vya chama. Hitimisho la tuhuma hizi ni kwamba mimi nimekuwa nikikisaliti chama kwa kutumika na CCM na Usalama wa Taifa. Nitazianisha tuhuma hizi na kuzijibu kama ambavyo nimekuwa nikizijibu katika vikao mbalimbali vyama.

Ninatambua kwamba chama changu kinapita katika wakati mgumu sana sasa hivi. Nataka nitamke mapema sana kwamba mimi Zitto Zuberi Kabwe sitokuwa chanzo cha CHADEMA kuvunjika. Hiki ndicho chama kilichonilea na kunifikisha hivi nilivyo. Ningependa chama hiki mtoto wangu atakapokuwa mtu mzima na atakapoamua kujiunga na siasa aingie CHADEMA. Bado nina imani kubwa na chama changu na ninaamini ndicho kinachostahili kuendesha nchi jana, leo na kesho.

2. Kuhusu tuhuma mbalimbali zinazo elekezwa kwangu

Zipo tuhuma nyingi ambazo zimekuwa zikirudiwarudiwa katika vikao vya chama na nje ya vikao na baadhi ya viongozi wenzangu. Tuhuma hizi zinalenga kuonyesha kwamba mimi ni mbinafsi na kwamba ninapokea rushwa ili kukihujumu chama changu. Nitazianisha tuhuma kwa kifupi na kuzijibu kama ambavyo nimekuwa nikizijibu katika vikao mbalimbali vya chama.

i) Tuhuma kwamba sikushiriki kumpigia kampeni mgombea wetu wa urais katika uchaguzi wa mwaka 2010. Ningependa kueleza yafuatayo kuhusu jambo hili:


  • Mimi nilikuwa mgombea wa ubunge katika Jimbo la Kaskazini huko Kigoma.
  • Pamoja na kuwa mgombea wa ubunge, nilifanya kampeni katika majimbo mengine 16 katika mikoa mbalimbali, ikiwemo Dar es Salaam, Mtwara, Pwani, Shinyanga, Mara na Rukwa. Hakuna kiongozi yeyote wa juu aliyefanya kampeni katika majimbo mengi kama mimi, ukiacha mgombea urais.
  • Kote nilipopita nilimpigia kampeni wagombea wetu wa udiwani, ubunge na Rais.
  • Katika Mkoa wa Kigoma nilizunguka na mgombea urais katika kata zote za Kigoma Kaskazini na majimbo yote manane ya Mkoa wa Kigoma.

ii) Tuhuma kwamba katika Mkoa wa Kigoma nilishindwa kuwapigia kampeni wagombea wetu kiasi kwamba peke yangu ndiye niliyeshinda katika uchaguzi huo. Ukweli ni kwamba niliwapigia sana kampeni wagombea wetu, na hivyo ndivyo wapiga kura wa Kigoma walivyoamua.

iii) Tuhuma kwamba nilishiriki kuwashawishi wagombea wetu katika baadhi ya majimbo kujitoa katika uchaguzi wa mwaka 2010 ili kuwapisha wagombea wa CCM wapite bila kupingwa kwa njia ya rushwa. Majimbo yanayotajwa ni pamoja na Sumbawanga, Musoma Vijijini na Singida Mjini. Kama nilivyokwisha kueleza katika vikao mbalimbali vya chama jambo hili si la kweli na hakuna popote ambapo watoa tuhuma hizi wamewahi kutoa ushahidi kwamba nilifanya jambo hili. Nipo tayari kwa uchunguzi ndani ya chama na watoa tuhuma waje na ushahidi bayana wa jambo hili. Si afya kwa chama kuendelea kurudiarudia tuhuma hizi kila mara tangu mwaka 2010 bila uchunguzi wowote kufanyika na jambo hili lifikie mwisho.

iv) Tuhuma kwamba nimekuwa sishiriki katika operesheni mbalimbali za chama: Ukweli ni kwamba nimeshiriki sana katika operesheni mbalimbali za chama ndani na nje ya nchi. Kwa mfano, mwaka 2011 tulikuwa na operesheni kubwa katika mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na nilikwenda katika mikoa yote tuliyotembelea. Mwaka 2012 baada ya hoja ya mkonge bungeni nilifanya ziara Mkoa wa Tanga. Mwaka 2012 kulikuwa na operesheni kubwa moja katika mikoa ya kusini ya Mtwara na Lindi. Operesheni hii sikushiriki kwa sababu nilikuwa nchini Marekani kufungua matawi kwa mwaliko wa Watanzania wanaoishi huko.

v) Tuhuma kwamba nimekidhalilisha chama kwa tamko la PAC kwamba Hesabu za Vyama hazijakaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG): Katika jambo hili ninatuhumiwa kwamba mimi kama Naibu Katibu nilipaswa kuwasiliana kwanza na viongozi wa chama 'kuwatonya' ili wajiandae. Kwamba kutokuwatonya kumekidhalilisha chama na kukiweka kundi moja na CCM na nastahili kuadhibiwa vikali kwa kuwa katika taarifa yangu nilikuwa na nia mbaya na chama chetu. Maelezo yangu niliyoyatoa na ambayo ningependa kuyakariri hapa kuhusu jambo hili ni kama ifuatavyo:


  • Utawala bora hautaki mimi kutumia nafasi yangu ya uenyekiti wa PAC kulinda chama changu na kuonea vyama vingine. Kufanya hivyo ni kuendeleza tabia zile zile ambazo tunazipinga na ambazo tunapigania kuzibadilisha
  • Napenda kusisitiza kwamba hakuna chama ambacho kimewahi kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG). Natambua kwamba mahesabu ya chama changu yamekuwa yakikaguliwa na wakaguzi wa nje kwa utaratibu tuliojiwekea. Lakini matakwa ya kisheria ni kwamba mahesabu ya vyama vya siasa hayajakaguliwa na CAG, na hili ni kosa la kisheria, bila kujali kosa hili ni la nani.

vi) Tuhuma kwamba mimi ni mnafiki katika kukataa kwangu kuchukua Posho za Vikao
Mtakumbuka kwamba mimi nilikataa kuchukua posho tangu mwaka 2011 kama ishara ya kuonyesha kwa vitendo msimamo wa chama chetu wa kupinga posho za kukaa na matumizi mengine yasiyofaa katika fedha za umma kama ilivyoanishwa kwenye Ilani yetu ya mwaka 2010-2015. Mtakumbuka kwamba hivi karibuni Mheshimiwa Lema amenishutumu kwamba kukataa kwangu kuchukua posho ni unafiki kwa sababu ninapokea posho kubwa zaidi katika mashirika ya umma ambapo mimi ni mwenyekiti wa kamati husika. Ninapenda kueleza yafuatayo kuhusu jambo hili:


  • Sipokei posho yeyote ya vikao (sitting allowance) ndani na nje ya Bunge tangu mwaka 2011. Hii ni pamoja na vikao vyote katika Kamati za Bunge ninavyohudhuria. Mtu yeyote mwenye ushahidi vinginevyo auweke hadharani.
  • Swala la kukataa posho (sitting allowance) ni swala la kiilani katika chama chetu, na kwangu ni swala la kimisingi zaidi. Katika Wilaya yangu vifo vya kina mama wajawazito ni 1900 kati ya wanawake 100,000 wenye ujauzito. Vifo hivi vinatokana na ukosefu wa huduma kwa sababu ya bajeti finyu. Ndiyo maana nilifurahi sana kwa chama chetu kuliweka swala la kupunguza matumizi ya Serikali katika Ilani, na kuondoa posho za wabunge, ambao tayari wanapokea mishahara mikubwa, kungesaidia sana kupatikana fedha ambazo zingeokoa vifo vingi vya kina mama.
  • Jambo hili si suala la ugomvi baina yangu na Mheshimiwa Lema. Ni suala la msingi katika chama chetu.


3. Usambazaji wa Ripoti ya Siri kuhusu Zitto Kabwe
Hivi karibuni kulisambazwa waraka unaoitwa ripoti ya siri kuhusu mimi ukibeba lundo la tuhuma kwamba nimehongwa fedha nyingi ili kukihujumu chama changu. Waraka huu ulidaiwa kuwa umechomolewa kutoka makao makuu ya CHADEMA. Jambo hili pia lilijadiliwa katika kikao cha juzi kwa kifupi, na majibu ya viongozi wa chama ilikuwa ni kwamba waraka huu haukuandaliwa wala kusambazwa na makao makuu. Katika mchango wangu nililalamikia mambo matatu yafuatayo:


  1. Kwamba baadhi ya waliokuwa wanasambaza waraka ule walikuwa ni viongozi wa chama chetu. Bahati mbaya hadi leo hakuna hata mmoja ambaye amekwishachukuliwa hatua za kinidhamu. Ninaamini kwamba kuna siku watu hao watachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za chama chetu.
  2. Kwa kuwa chama kimekana rasmi kuhusika na waraka huu, nitaendelea na taratibu za kisheria ili kuhakikisha kwamba wote waliohusika kutengeneza hekaya ile wanachukuliwa hatua stahiki za kisheria.


4. Hitimisho
Ninatambua kwamba kuna watu walitegemea leo ningejibu mapigo na ningewazodoa watu kwa majina kama ilivyo kawaida katika siasa za Tanzania. Natambua pia kwamba, kama ilivyo kawaida wakati wa migogoro katika vyama vya siasa hapa Tanzania, kuna watu walitegemea leo ningetangaza 'maamuzi magumu'. Natambua kwamba wapo ambao wangependa kupata nafasi ya kuendelea kutumia suala hili katika harakati zao za kudhoofisha mapambano ya demokrasia na uthabiti wa siasa za ushindani nchini mwetu. Napenda wanachama wa CHADEMA na wapenda demokrasia na siasa safi wote nchini watambue kwamba mimi bado ni mwanachama mwaminifu wa chama hiki na nitakuwa wa mwisho kutoka kwenye chama hiki kwa hiari yangu. Nitafuata taratibu zote ndani ya chama katika kuhitimisha jambo hili.

Naomba wanachama waelewe kwamba mimi kama binadamu ninaumia ninapopigwa. Tuhuma ninazorushiwa ni kubwa na zinanikwaza. Tuache siasa za uzushi ili tujenge chama chetu na nchi yetu, ili hatimaye tuwakomboe Watanzania wenye matarajio na imani kubwa kwa chama chetu.

Kama mwanasiasa kijana niliyekaa katika siasa kwa muda sasa yapo mengi mazuri nimeyafanya. Lakini kuna maeneo nilipojikwaa na yapo makosa niliyofanya kisiasa katika maisha yangu ya siasa.

Kinachoendelea ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia. Ni mapambano baina ya wapenda demokrasia dhidi ya wahafidhina, waumini wa uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu na wapenda siasa safi dhidi ya watukuzao siasa majitaka. Hii ni changamoto kubwa ndani ya chama chetu inayohitaji uongozi shupavu kuikabili. Nitasimama daima upande wa demokrasia. Kama alivyopata kunena mmoja ya wanasiasa maarufu, 'kiwango cha juu kabisa cha uzalendo katika nchi ni kukubali kutofautiana kimawazo', na ninatamani huu ndio uwe utamaduni wa chama chetu.


Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Dar es Salaam.
24 Novemba, 2013
Taarifa ya Dk. Kitila Mkumbo kwa Umma kuhusu Kuvuliwa nafasi za mamlaka ndani ya CHADEMA

1. Katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kilichofanyika tarehe 20-22 Novemba 2013, pamoja na mambo mengine, kulijadiliwa waraka wa siri unaojulikana kama Mkakati wa Mabadiliko 2013. Waraka huu ulilenga kujenga hoja ya kufanya mabadiliko ya uongozi na kuanisha mikakati ya ushindi kwa mgombea mlengwa katika uchaguzi mkuu ndani ya CHADEMA. Nilikiri kuwa nilikuwa naufahamu waraka huu, na kwamba nilishiriki kuuandaa na kuuhariri, na kwamba mimi ni mmoja wa wanachama wanaoamini kwamba kuna haja ya kubadilisha uongozi wa juu wa chama katika uchaguzi ujao ndani ya chama.

2. Katika mjadala, maudhui ya waraka huu yalionekana kwa wajumbe kwamba yalikuwa na mapungufu na yalikiuka misingi na kanuni zilizoanishwa katika Katiba ya Chama. Kwa kuwa katika chama cha siasa hoja za watu wengi ndizo hupewa uzito, na kwa kuwa dhamira na nia yangu ndani ya chama hiki imekuwa ni kusukuma mabadiliko ambayo watanzania wanayatazamia nje ya mfumo wa sasa wa utawala, nilikiri makosa yangu na kuwaomba msamaha wajumbe wa Kamati Kuu na viongozi wakuu wa chama, na kueleza kwamba nilikuwa tayari kujiuzulu na kubaki kuwa mwanachama wa kawaida. Wajumbe walikataa kukubali ombi langu la kujizulu bali walipitisha azimio la kunivua mimi na Mhe. Zitto Zuberi Kabwe nafasi zetu za uongozi. Nilipokea kwa unyenyekevu adhabu ya kuvuliwa nafasi zote za mamlaka nilizokuwa nazo ndani ya chama hiki na kueleza kuwa nitaendelea kutoa mchango wangu kama mwanachama wa kawaida hadi hapo chama kitakapoona ninafaa kukitumikia katika nafasi yeyote.

3. Kufuatia mkutano wa waandishi wa habari siku ya Ijumaa tarehe 22 Novemba 2013 ambapo, pamoja na mambo mengine, ilielezwa na viongozi wa CHADEMA kwamba mimi na wenzangu (Samson Mwigamba na Zitto Kabwe) tumehujumu chama na tumefanya uhaini kwa kuandaa mkakati wa ushindi kwa mgombea tunayemtaka, ningependa nieleza mambo yafuatayo:

a. Siamini hata kidogo kwamba kugombea nafasi yeyote iliyo wazi ndani ya chama cha siasa ni uhaini na hujuma. Msingi namba moja wa CHADEMA ni demokrasia na hakuna namna ya kudhihirisha mapenzi kwa demokrasia zaidi ya kuruhusu ushindani katika nafasi za uongozi na hasa uongozi wa juu kabisa. Hiki kinachoitwa uhaini ni wasiwasi wa siasa za ushindani katika chama chetu.

b. Sijawahi na sitarajii kushiriki vitendo vyovyote vya kuhujumu chama changu cha CHADEMA na harakati za mabadiliko hapa nchini. Chama hiki kiliniamini katika nafasi nyingi nyeti sana na kama mie ningekuwa mhujumu nilikuwa na fursa nzuri za kufanya uhujumu huo. Nimeshiriki kuandaa ilani ya chama ya 2010-2015, kuratibu kampeni za mwaka 2010 nikiwa makamu mwenyekiti wa kampeni chini ya Profesa Baregu na nilishiriki kutengeneza na kusimamia utaratibu mzuri wa kupata wabunge wa viti maalumu katika chama chetu. Zote hizi ni nafasi nyeti mno ambazo kamwe huwezi kumkabidhi mtu ambaye ni ‘mhaini' na ‘mhujumu'. Nilishiriki katika shughuli za chama kwa kiwango ambacho nilijisababishia matatizo makubwa katika familia yangu na kazini, lakini sijawahi kutetereka na sijaterereka. Nilifanya yote haya kwa mapenzi yangu ya dhati na imani yangu kwa CHADEMA kwamba ndicho chama kinachostahili kuongoza harakati za mabadiliko hapa nchini kwa sasa.

c. Nasikitika kwamba nimesababisha usumbufu kwa viongozi wangu wa CHADEMA kutokana na dhamira yangu ya kutaka mabadiliko ya uongozi ndani ya chama chetu kwa njia halali za kidemokrasia. Nilifanya hivi kwa imani niliyo nayo kwa misingi ambayo CHADEMA inasimamia, ikiwemo demokrasia, na imani yangu kwamba chama hiki kinahitaji kufanya mabadiliko makubwa katika uongozi wa juu wa chama, ikiwa ni maandalizi muhimu kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Nasisitiza tena kwamba siamini hata kidogo kwamba matamanio ya mabadiliko ya uongozi ndani ya chama, na kuandaa mikakati ya kufikia matamanio hayo kwa njia za kidemokrasia ni uhaini.

d. Tunaweza kujifunza kutokana na historia. Siasa za ushindani ndani ya vyama katika nchi hii sio kitu kigeni. Enzi za TAA na kabla TANU haijazaliwa wanachama walikuwa wanagawana nafasi za uongozi mezani. Lakini mwaka TANU ilipozaliwa (mwaka 1954) kulikuwa na uchaguzi mkali sana kwa nafasi ya uenyekiti. Mwalimu Nyerere alimshinda Mzee Skyes kwa kura chache sana. Rais Obama wa Marekani alianza mkakati wa kushinda uteuzi wa kugombea nafasi ya urais kupitia chama chake cha Democrat mapema kabisa mwaka 2006 kupitia waraka maalumu wa siri ulioainisha mikakati yake. Waraka huu uliandaliwa na watu wanne tu bila yeye mwenyewe kujua. Waandaji wa mkakati huu walikuja kumshirikisha baadaye mwaka 2007 na kumshawishi yeye ajitokeze kugombea dhidi ya Hillary Clinton aliyekuwa anachukuliwa kama mrithi halali wa kiti cha urais. Yaliyobaki ni historia. Hivi ndivyo ambavyo siasa za ushindani ndani ya vyama hatimaye huzaa wagombea na viongozi imara katika nchi.

e. Zitto Zuberi Kabwe hajafukuzwa kwa sababu ya waraka huu kwa sababu yeye hakuhusika kwa namna yoyote kuuandaa, ingawa alikuwa ni mlengwa mkuu. Yeye amefukuzwa kwa sababu ambazo yeye atazieleza na ambazo viongozi wa CHADEMA hawakuzieleza katika mkutano na waandishi wa habari.

f. Napenda ijulikane kwamba sikuomba kujiuzulu kwa sababu ya kuogopa aibu ya kufukuzwa. Niliomba kujiuzulu kwa sababu nilitambua kwamba wenzangu katika Kamati Kuu walikuwa hawana imani nami tena, na ni uungwana kujiuzulu mkifika mahala hamuaminiani. Nilitambua vilevile kwamba, kwa mujibu wa Katiba yetu, Kamati Kuu ilikuwa haina uwezo wa kunivua nafasi yangu moja kwa moja.

Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, Sura ya Sita, Ibara ya 6.3.6 (b), inasomeka hivi "Kiongozi aliyeteuliwa na vikao vya uongozi ataweza kusimamishwa au kuachishwa uongozi na kikao kilichomteua". Mimi nilichaguliwa na Baraza Kuu na ni kikao hiki pekee chenye uwezo wa kunivua nafasi niliyokuwa nayo. Ninaamini wajumbe wa Kamati Kuu walipitiwa katika hili kwa sababu siamini kwamba hawajui takwa hili la kikatiba ukizingatia kwamba ndani yake kuna wajumbe waliobobea kabisa katika tasnia ya sheria.

4. Hiki kilichotokea ndani ya chama sio kitu kibaya. Vyama vingi imara hupitia katika migogoro na misukosuko kama hii na zaidi. Naamini tutavuka na tutakuwa imara zaidi. Muhimu ni kwamba ni lazima tuaminiane. Katika kuaminiana sio lazima tufanane kimawazo na kimtazamo kwa sababu hili ni jambo lisilowezekana kibinadamu na zaidi katika siasa.

5. Ninapohitimisha, ninawasihi wanachama wa CHADEMA na wapenzi wa mabadiliko popote walipo wapiganie kwa dhati MISINGI mama ya CHADEMA ikiwemo demokrasia ndani ya chama. Hakuna namna ambavyo chama chochote kinaweza kushawishi umma kwamba kitapigania demokrasia katika nchi wakati kinayahainisha mapambano ya kidemokrasia ndani ya chama chenyewe.

Kukataa siasa za ushindani ndani ya chama ni kuhujumu demokrasia na ni usaliti kwa misingi mama ya chama ambayo ni uhuru wa kweli na mabadiliko ya kweli. Hisia za usaliti na umamluki zilitumika enzi za ukomunisti katika kunyamazisha wapinzani ndani ya vyama vya siasa na katika nchi. Zilikuwa ni njia haramu zilizozoeleka ambazo hatimaye zilizaa udikteta wa kutisha katika mataifa ya kikomunisti. Tusikubali utamaduni wa kuhisiana usaliti na umamluki ukaota mizizi katika chama chetu na katika nchi kwa sababu utaua demokrasia na mfumo wa vyama vingi utakuwa hauna maana tena.

6. Nitafuata taratibu zote za chama kama zilivyoelekezwa na Kamati Kuu na kwa mujibu wa katiba yetu, na nitashiriki kikamilifu katika kutuliza hali ya kisiasa ndani ya chama ili kuhakikisha kwamba tunabaki imara, na CHADEMA inaendelea kuwa tumaini la watanzania.

Mungu ibariki Tanzania.

Dkt. Kitila Mkumbo
Dar es Salaam
Jumapili, 24 Novemba 2013.
sijui mnasemaje? binafsi ntashangaa kama hawa watu hawatofukuzwa uanachama, ntarudi badae kutoa maoni yangu.
 
wakuu matamko yameshatolewa, sijui mnasemaje? binafsi ntashangaa kama hawa watu hawatofukuzwa uanachama, ntarudi badae kutoa maoni yangu.
Ahsante sana zumbemkuu kuhamisha uzi wa taarifa na kuuleta hapa.

Tumesoma taarifa hizo kwa kina. Kilichoonekana ni siasa na wala si majibu kuhusu tuhuma za usalaiti zinazowakabili.
Nadhani wamekubali kuwa wanahusika na waraka na sasa ni wakati tuuchambue kwa kina.
Mkuu Mag3 kitendawili kimeshateguliwa na sasa tunaweza kuongelea kwa ukubwa na upana wake.
 
Last edited by a moderator:
Ningependa kutoa baadhi ya vifupisho vilivyotumika katika waraka huo ili kuuelewa kwa undani.

Mtendaji mkuu- Dr Slaa
Kiongozi aliyepo, mpinzani wetu- Mh Mbowe
Mtendaji msaidizi- Zitto Kabwe
mida eight (mida= saa, eight nane) saa nane
kichaa wa 'ars'-Lema
MM= Zitto
MI= Kitila mkumbo
M3 =Mwigamba

Marejeo: Kwa muda mrefu tumetahadhirisha kuhusu mgogoro ndani ya CDM.
Mwezi wa 6 2012 'sakata la Juliana Shonzo' tuliandika kwa undani kuhusu nguvu aliyokuwa nayo na mshukumo mkubwa ndani ya chama.

Tulionya mgogoro wa Kafulila kuwa kuna nguvu zaidi isiyoonekana na hivyo kuna tatizo
Mgogoro wa Masalia, tulionyesha ufa mkubwa unaohitaji ufumbuzi wa haraka.

Wiki iliyopita tuliandika duru za siasa kuhusu chanzo cha mgogoro, wahusika kwa kuwataja, na nini CDM wafanye.Tulisema mgogoro ni mkubwa unaoweza kukivuruga chama kama ilivyokuwa NCCR na CUF.
Yote yaliyodiliwa leo ni marudio tu, kinachotokea ni 'movie' tuliyoiona wakati inaandaliwa tukiwa watazamaji.

Wiki iliyopita tulisema haya
1. Mgogoro unahitaji suluhu ya haraka. Mpambano wa Lema, Zitto, Mwigamba ni dalili za tatizo kubwa.
2. Mgogoro huu unachochewa kutoka nje lakini wahusika wakubwa wamo ndani ya CDM
3. kikao cha haraka ili kushughulikia tatizo kwasababu litakapofumuka lenyewe itakuwa ni balaa wala si tatizo
4. Tukasema ili kuleta uwiano mzuri na utengamano lazima awepo msuluhishi nje ya uongozi na kundi la watuhumiwa

5.Tukashauri baraza la wadhamini wa CDM waliangalie tatizo na kulichukua mikononi mwao

Sababu zilikuwa kama ifuatavyo
a) Kuepuka maamuzi ya jazba au yenye namna isiyotenda haki kwasababu tayari kuna pande mbili
b)Maamuzi nje ya uongozi uliopo yataleta muafaka miongoni mwa wanachama waliogawanyika
6.Tukashauri ni muhimu ukwepo uchaguzi kabla muda tete(2015) haujawadia ili kuleta utengamano

7. CDM izingatie masuala ya kijamii katika kulishugulikia tatizo,ni kubwa na lina mizizi na washiriki wengi na wakubwa.

Kikao cha kamati kuu kimetoa maamuzi ya kuwavua uongozi na kutaka wajieleze katika siku 14 kwanini wasitimuliwe

Hatua hizo zinaweza kuwa za kidemokrasia, zilizofuata taratibu, sheria na kanuni.
Lakini je, zilizingatia factors nyingine zinazoweza kujitokeza ambazo si lazima ziwe za kanuni , sheria au maadili.
Je, hatua zilifuata na kuangalia nyakati, jamii au mazingira ya suala lenyewe?

Uwepo wa makundi ya ushindani ndani ya chama cha siasa ni jambo zuri.
Makundi hutoa viongozi bora kama chekecheo na ndivyo ilivyo duniani kote.
Kinachotakiwa ni kushindanisha sera, maono na mipango. Tena makundi hayo ni ya USHINDANI na wala si UPINZANI.

CCM ilikuwa na ushindani wa ndani uliojenga chama, baada ya kuuacha kilichofuata ni makundi na maana nzima ya chama tawala imepotea. Kilichobaki ni kuviziana katika 'glasi za maji ya kunywa'

Kuna swali linajitokeza endapo waraka huo una tatizo lolote.
Jibu la haraka ni ndiyo. Lipo tatizo kubwa sana katika waraka huo.

Laiti matatizo tutakayoyaonyesha yasingekuwepo waraka usingekuwa na tatizo.
Tungebaki kuuita waraka wa mipango ya ushindani ambayo tumekubali ni njia halali ya kuimarisha chama.

Kwanini waraka huo una matatizo.
1. Umeandikwa ukihusisha viongozi wa chama. Zitto ni naibu katibu mkuu, mtendaji wa pili wa chama ngazi ya kitaifa.
Kitila ni mjumbe wa kamati kuu na mshauri wa chama aliyeaminiwa hata kuja na formula ya kupta wabunge wa kuteuliwa. Kitila amehusishwa sana katika shughuli za chama kwa wadhifa huo.

Mwigamba ambaye ametajwa pia katika waraka ni mwenyekiti wa mkoa wa CDM.
Mtu muhimu sana katika shughuli za chama kimkoa na kitaifa.

Hawa walikuwa na nafasi ya kuleta mabadiliko waliyokusudia bila kupandikiza mbegu za chuki, udini na uhasama.
Bila kuwagawa wanachama kwa njia za chuki badala ya sera.

Kwa kuweka tuhuma dhidi ya uongozi hadharani bila kujificha au kujiuzulu nafasi zao kama kitendo cha kutoridhika. Kuendelea na nafasi zao wakitengeneza kundi ni usaliti katika maamuzi yale yale wanayoyafanya wakiwa viongozi ndio usaliti na wala si lazima uwe wa kutumiwa na CCM.

2,. Waraka umepotosha umma au kupaka matope viongozi waanzilishi na wa sasa.
Soma hapa ''.....wakuu wetu wawili wa kwanza ambao kimsingi waliweka msingi mzuri sana wa kutong'ang'ania madaraka na badala yake kuachia mapema na kumwachia mwingine kidemokrasia bila vurugu. Hawakuwa madikteta na tunawapongeza sana''

Mbowe alichaguliwa kidemkorasia na hivyo kumsema ni dikteta ni upotoshaji.
Pili, utaratibu wa kuachiana madaraka ni vipindi viwili,kama watangulizi waifanya kwa kipindi kimoja ni matakwa yao na si kanuni au sheria za chama. Kudai Mbowe ang'ang'ania madaraka ni upotoshaji.

3. Waraka umetumia maneno makali kuonyesha vita kati ya wanachama na wala si washindani.
Mfano '' mtu mwenye uwezo kubwa kuliko tunayetaka kumtoa, Mkuu aliyepo kung'ang'ania kuendelea ni kikwazo, Kukubali kuongozwa na mtu mwenye akili ndogo, Mpinzani wetu anaporushiwa kombora,mpinzani wetu hana uwezo ABC, ...akili yake ni ya magumashi darasini na hana vipaji,... kushinda vita iliyopo mbele yetu n.k.''
Kauli hizi hazionyeshi watu waliokuwa wanajenga ushindani bali waliotaka kuleta mapinduzi nje ya demokrasia.

4. Waraka ulikusudia kuvunja misingi ya demokrasia ya chama kinachojinasibu kuwa cha kidemokrasia.
Viongozi wanachuguliwa na watu na si kundi la watu wachache tena wasiofika 10.

Hiyo hufanyika katika Vanguard party kama Politubuoro ya Urusi au communist part ya China.
soma walichokusudia ''Sisi wenyewe tunaoandaa mkakati huu hatuna hakika kama tunayemtaka yu tayari, ...nayo ni fursa muhimu kwa tunayemtaka, ...aliyepo ni lazima ang'olewe,....tukileta mtu asiyefahamika n.k.'

Lengo lilikuwa kung'oa uongozi uliopo kidemkrasia na kuweka watu wanaowataka wao na wala siyo waliowanadi wakatakiwa na wanachama. Huku ni kubinya demokrasia na lengo la waraka si zuri

5. Waraka umepingana na maneno ya chama, umethibitisha tatizo la chama na umepingana na maneno ya viongozi.
CDM siku zote imetuhumiwa kwa udini na wapinzani wao.

Hata kama si kweli leo tunaona mkakati wa kuweka viongozi kwa kutumia vigezo vya dini.
Maneno yao '' ......ni mwislam..'

Hili halionyeshi nia njema ya walioandaa waraka kwa mustakabali wa chama au taifa kwa ujumla.
Waraka umekusidia kuchoche hisia zilizokuwepo na pengine kuaminisha watu kuhusu hisia zao.Ni usaliti na hujumu

6. Waraka ulikusudia hujuma katika CDM, soma ''mkakati huu hautakiwa kujulikana...,tunahitaji watu watatu waaminifu katika ngazi ya taifa ambao tayari tuna, lazima ang'olewe'

Haya yalifanywa na watu waliokuwa wanaingia katika maamuzi makubwa ya chama kitu ambacho ni kama ushushu wa kukihujumu chama kwani kila walilofanya lililenga tofauti na kule walikofikiria

Kwa kuangalia hayo ni ngumu kuamini waraka huu ulilenga ushindani wa kisiasa. Ni wazi kabisa kulikuwa na hujuma.

Lakini, je kila kilichoelezwa kilikuwa uzushi?
Je kuna ukweli au upotoshaji?

Tunaendelea na sehemu ya tatu.......
 
Huyu M2 anastahili kuwa wa kwanza kufukuzwa, kwanza ni mwajiriwa wa chama huyu! utetezi wa Dr. Mkumbo unaeleweka ila chaguo lao yaani MM wamebugi kabisa.
 
Inaendelea

UPOTOSHAJI KUTOKA KATIKA WARAKA

1.
Waraka unasema haya ''Tunapopongeza juhudi zao hizi tunahitaji pia kuwapongeza wakuu wetu wawili wa kwanza ambao kimsingi waliweka msingi mzuri sana wa kutong'ang'ania madaraka na badala yake kuachia mapema na kumwachia mwingine kidemokrasia bila vurugu''

Kusema Mbowe kang'angania madaraka si sahihi.Katiba inasema vipindi viwili. Si lazima viwe viwili kama alivyofanya Mtei na Mkani. Hilo haifanyi ung'ang'anizi kwa yule atakateimiza vipindi viwili.
Endapo muda umepita ni suala la kufuata taratibu kwa kuzungumza ndani ya chama na si vikundi tena vikitoa kashfa na kejeli wakati watu hao wakiwa wajumbe vikao muhimu vya chama.

2.
''Mwaka 1995 chini ya mkuu wa kwanza(Mtei) tulipata wawakilishi watatu kwenye chombo chetu kikuu cha uwakilishi.
Mwaka 2000 chini ya mkuu wa pili(Makani) tukapata wawakilishi wanne pamoja na wa nyongeza mmoja na kuwa watano.
Mwaka 2005 chini ya mkuu wa tatu(Mbowe), tulipata wawakilishi watano na wa nyongeza sita jumla wakawa 11.
2010 (Mbowe) wawakilishi wakaongezeka kuwa 23 na wa nyongeza 25idadi kuwa 48 na mwingine mwaka jana wawe 49''

Waraka umewapongeza viongozi wawili wa mwanzo na kuacha ukweli kuwa idadi imezidi kuongezeka hata alipokuja mkuu wa tatu. N kweli kuwa matokeo ya serikali za mitaa hayakuwa mazuri, lakini waraka hauonyeshi ikilinganishwa na nini.
Matarajio kutokana na hamasa yanaeleza kwanini matokeo si mazuri. Kwa kutumia takwimu idadi ya viti katika serikali za mitaa imeongezeka kutoka 0 had 6%, 0 hadi 24%. Kutosema ukweli kwa kuficha takwimu ni upotoshaji.

3.''Makubaliano ya kifisadi na mtu binafsi anayeuza vifaa vya kueneza taasisi.
Hakuna kikao chochote cha juu kilichojadili ama kilichowahi hata kupewa taarifa tu kwamba sasa kuna mtu binafsi kapewa tenda ya kuuza vifaa vya taasisi na taasisi inanufaika vipi na mauzo hayo na kwa nini vifaa muhimu vya taasisi vinauzwa. Jambo hili linajulikana kwa wakuu tu''

Wakina Mkumbo na Zitto ni wajumbe wa kamati kuu. Hakuna kumbu kumbu walizoonyesha kuhusu kujadili suala hilo ndani ya vikao. Endapo kulikuwa na kufunika agenda bado walikuwa na nafasi ya kuuliza katika AOB ili iwe katika kumbu kumbu. Hawakuonyesha hilo kutokea. Walipaswa wapaze sauti zao zaidi ya watu watatu hawakufanya hivyo.
Huku ni kupotosha umma kwa kujifanya hawakuwa sehemu ya uongozi ule ule wanaoutuhumu.

4.''Uongozi wa sasa wa taasisi yetu umefanya tuonekana kwamba taasisi yetu ipo kwa ajili ya kuvuruga amani ya nchi.
Yote hii ni kwa sababu tumekuwa hatuna mbinu mpya za mapambano zinabadilikabadilika zaidi ya maandamano ya kila mara. Kwa kuzingatia utamaduni wa watanzania wa kupenda amani, kuna haja ya kufuta hii taswira na njia rahisi ni kubadilisha uongozi wa taasisi haraka iwezekanavyo''

Vyombo vya dola vimetumika katika kuvuruga mikutano ya CDM. Pale CDM walipoombwa kusitisha maandamano walifanya hivyo. Mkutano uliochukua roho za watu Arusha haukuwa maandamano bali kampeni. Ndivyo ilivyokuwa maeneo kama Iringa watu walipovamiwa ndani ya kikao. Hivyo kusema suala zima ni maandamano na ni kuvunja amani ni upotoshaji.

Hakuna kumbu kumbu Kitila Mkumbo kama mshauri wa chama chao kuelezea athari hizo za maandamano.
Zitto ameshiriki katika maandamano kama yale yaliyopita Tazara, na juzi alikuwa katika mkutano kanda ya magaharibi.
Endapo mikutano ni kuvunja amani basi Zitto alishiriki kikamilifu, kama siyo basi alifanya hivyo kwa unafiki.
Huu ni upotoshaji.

5.. Mpaka hivi sasahakuna mpango wowote wala hata mchakato wa maana kuwa connected na jumuia yakimataifa. 'Mbowe' yupo ‘too local' na hana mawasilianoyeyote ya maana na viongozi wengine katika kanda na kimataifa.
Ndio maana mkuuhuyo na mtendaji wake mkuu wamekuwa hawaonekani katika matukio makubwa yakimataifa. Hata katika kutoa maoni katika mambo makubwa ya kitaifa nakimataifa viongozi hawa hawapo. Kwa kifupi kwa sababu ya aina ya viongozitulio nao, nafasi ya taasisi yetu katika nyanja za kimataifa haipo!'

Waraka umeonyesha sehemu ambayo Mbowe alikuwa Nairobi katika uchaguzi. Tunakumbu kumbu kuwa Mbowe alifiwa na dada yake akiwa Denmark, Dr Slaa alikuwa US hivi karibuni. Slaa ametoa kauli kuhusu tatizo la Rwanda ambayo tuliipinga. Jinsi kauli ilivyowekwa kuna aina ya upotoshaji ili kujenga hoja na si kujenga hoja kwa kuepuka upotoshaji.

6.''Nikwa sababu tumegombana na kila mtu katika utawala wan chi, vikiwemo vyombovya ulinzi na usalama. Ukweli ni kwamba tutavihitaji vyombo hivi kabla nabaada ya kuingia madarakani na ni ndoto kudhani kwamba tutakabidhiwa nchi kwakugombana na kila mtu. Ni kwa sababu ya mtazamo kama huu ndio maana wakuu wetuwa sasa hawaonekani kabisa katika shughuli za kitaifa kama vile sherehe zauhuru wan chi, n.k''

Sidhani CDM inahitaji kupendwa na watawala. Kuna kauli za kina Wasira zisizoitakia mema na hata za mkuu wa nchi kuhusu kutuhumu baadhi ya viongozi kuwa wazandiki. Akina Kitila na Mkumbo wanaamini kuwa uwepo wa ukaribu na viongozi wa CCM utasaidia Chadema kuingia madarakani. Wanaamini kuwa vyombo vya dola vinaweza kufanya haki kama CDM wataacha mikutano. Wanaamini damu za watu ni kwasababu ya viongozi watatu.
Si kweli, chama tawala kinatumia vyombo vya dola na hilo linajulikana kwa kila mtu.
Upotoshaji kusema CDM inahitaji mapenzi na watu walioshindwa kusema chanzo cha bomu Arusha.

Waraka na kashfa ndani yake

Itaendelea

 
7. ''Tunayemataka (Zitto) ni kiongozi anayeweza kuongoza taasisi bila kujenga makundi akijali zaidi kaziya taasisi kuliko maslahi binafsi''

Zitto amehusishwa na makundi mara nyingi. Alikuwa kiongozi wa kundi Kafulila. Ametajwa katika masalia(M7) na sasa ametajwa katika waraka kukiwa na ushahidi wa kimazingira kuwa alishaanza kazi aliyopewa kwa kufuata ushauri kama waraka unavyosema.Kusema kuwa si mtu wa makundi ni upotoshaji.

8.''
Katika kuonyesha mzalendo Zitto ni kiongozi ....amekuwa ndiyemwakilishi pekee aliyeongoza katika kuibua kashfa nyingi na nzito za ubadhirifundani ya serikali hata kufikia mawaziri kadhaa kufukuzwa kazi''

Tuna ushahidi kuwa Zitto aliuza uzalendo kwa Barrick ili wamjengee shule.
Baada ya kupokea milioni 10 suala la Barrick likawa limefikia kikomo.
Kuonyesha uzalendo kwa kuibua kashfa na kuficha unyonge kwa makampuni yanayoumiza wananchi wa chini ni upotoshaji.

9.''
Uwazi: Katika taasisi zetuhizi ni muhimu sana kuepuka kufanya mambo yote wazi wazi hata kama ni mema amani haki ya mhusika ama si makosa katika jamii tuliyomo. Kuna mambo ambayo nihaki ya mtu mfano mahusiano binafsi ya kimapenzi, kuwa na marafiki wa damukutoka upande mwingine wa utawala, nk. Lakini mambo hayo ni muhimu wakatimwingine ama kwa kiwango fulani yakafanywa kwa siri kuepuka mitazamo potofu kwaunaowaongoza''

Kama wanakubali uwepo wa mambo binafsi kama mapenzi kwanini basi katika waraka huu uonyeshe kuwa Slaa ni mhuni kama jamii inavyoona. Hapa wanapotosha umma kuwa kuna mambo yana mipaka wakati waraka wao unamsumanga Slaa kwa mambo yale yale wanaosema yana mipaka. Kupotosha umma kwa hali ya juu

Lakini ukisoma hapo juu utagundua kuwa kuna elements za undugu, ufamilia na marafiki wa damu kitu wanachokiona ni sawa. Wakati huo huo wanaeneza tuhuma dhidi ya ukabila.
Hizi ni double standard tunazoita upotoshaji maana hazina ukweli bali kuwa fabricated ili kuchangaya umma.

10 ''
Mpinzaniwetu hana uwezo mkubwa wa uelewa wa mambo mbalimbali ya uchumi, jamii,utamaduni, michezo, nk. Si tuelimu yake ya darasani ni ya magumashi bali piavipaji na akili ya kuzaliwa havijaonekana katika maisha yake''

Kipaji ni uwezo kwa kutenda jambo katika hali bora kuliko sehemu kubwa ya jamii. Mzee Moris Nyunyusa alikuwa na uwezo wa kipiga ngoma kumi akiwa kipofu, hicho ni kipaji. Si lazima mtu aibue kashfa za ufisadi ili awe na kipaji.
Na wala kipaji hakitegemei elimu ingawa mwenye elimu na kipaji ana nafasi kubwa.

11.''Mpinzaniwetu ni mgumu sana katika kuchangamana na makundi yote ambapo vijana humwonakama si mwenzao kiumri na kifedha, wanawake humwona kama malaya anayependakutumia miili yao kujistarehesha wakati wazee humwona kama mtu anayedhalilishahata nafasi aliyopewa kwa kufanya uhuni waziwazi hata kuvunja ndoa si ya kwaketu bali hata za watu wengine

Ukisoma nukuu #9 hapo juu utaona wanakubali kuwa mambo ya mapenzi ni binafsi. Mbele ya safari wanazusha tuhuma zile zile walizosema ni binafsi. Hii si upotoshaji tu bali unafiki uliopinduukia.

Labda niwakubushe wana duru kuwa kumekua na malumbano mengi hapa jamii forum wengi. Wengi wakisema tuhuma dhidi ya viongozi wa CDM zinatolewa na vijana wa Lumumba.
Ni kweli kuna hilo suala lakini ukisoma waraka wa Kitila na Zitto utaona kuwa tuhuma nyingi zinatoka hapa.

Mfano hili suala la mapenzi limekuwa katika midomo sana kumbe nyuma yake wapo wajumbe wa kamati kuu ya CDM. Tuhuma kuhusu fedha zimekuwa zinatolewa kumbe nyuma yake kuna kundi la wana kamati kuu ya CDM.
Tuhuma za ubadhirifu na ufujaji wa mali zimekuwa nyingi, ukisoma waraka ni wazi zimetoka hapa.

Hatusemi tuhuma hizo hazina ukweli au ni za kweli. Duru za siasa tunaonyesha kile kinachoitafuna CDM.
Badala ya kuelekeza macho yao nje lazima wajisafishe kwanza.

Leo tunafahamu kuwa Zitto kama mwenyekiti wa PAC ameibua tuhuma kuhusu hesabu za vyama vya siasa. Wengi walidhani ni sehemu ya uzalendo.
Na kwa mujibu wa majibu yake ni kweli alichokisema.
Hata hivyo duru tunahoji kama ulikuwepo uzalendo wa pesa za umma.

Ukisoma waraka moja ya tuhuma ni hesabu kutokaguliwa. Kama ni hivyo na ni kosa hesabu kutowekwa wazi na ni kosa kutokagauliwa lakini basi tunafahmu kumbe Zitto alitumia nafasi hiyo kwa uzalendo ili akwee ngazi za chama kwa kumutuhumu mwingine.
Hizi ni siasa mufilisi sana.

Zito na Kitila kama wajumbe wa kamati kuu ya chama walikuwa na nafasi nzuri ya kueleza uozo huo ndani ya chama badala ya kutumia ofisi za PAC huku wakiwa na malengo yao. Hapa ni unafiki na upotoshaji wa umma

Itaendelea....

 
Huyu M2 anastahili kuwa wa kwanza kufukuzwa, kwanza ni mwajiriwa wa chama huyu! utetezi wa Dr. Mkumbo unaeleweka ila chaguo lao yaani MM wamebugi kabisa.
Mdau wakati tunaendelea kuufanyia kazi waraka nikuonyeshe tuhuma za akina Zitto na Kitila
''Mifumoya uteuzi wa maofisa wa makao makuu ya taasisi imevurugwa na siku hizi wakuu wataasisi hasa mtendaji mkuu anateua na kutimua ofisa anavyotaka na mara nyingibila hata kamati ya makatibu na wakurugenzi kujua

Walichokusudia ni kutaka uongozi uache ili waweke watu wao kuibua kile wanachokitaka.
Ukisoma hapo juu wanamtuhumu mtendaji kwa kufukuza watu, lakini waraka huo unahusisha watu kutoka katika ofisi zile zile wanazodai zinafukuza watu hovyo. Hii ni hasira ya watu wao kuondolewa ndio maana tunauangalia waraka kwa kina kabisa bila kumuonea mtu au kumhurumia.

Kadri tunavyosonga mbele tutaaangali upande unaotuhumiwa na 'shea' yao katika mjadala
 
Uroho wa madaraka na mali ndio unaosababisha Tanzania tuendelee katika hali ya ufukara tulio nao. Kila mtu anafikiria ya kwake tu; hata watu tuliodhani wanatutetea kama akina Zito kumbe nao wanatutetea kwa sababu ya maslahi yao binafsi.

Kitila anaonyesha ana akili sana na anajua sana kupanga maneno yake kwa makini kuliko Zitto ila nadhani naye alishindwa kujua njia nzuri ya kupamabana.

Ni kwa bahati mbaya sana kuwa watu hawa, kama ilivyokuwa kwa wafuasi wao akina Shonza (something like that) nao watahamia CCM na na kupewa ukumbi mkubwa sana wa kutangaza kuwa matatazio ya Tanzania yanatokana na CHADEMA. CCM siyo chama imara ila kina raslimali nyingi sana zitokanazo na utaratibu mbovu wa serikali yetu, halafu kinapowapata watu wenye uchu wa madaraka na tamaa kubwa kama hawa basi wanatumiwa kwa nguvu sana kuibakisha CCM madarakani. Angalia Tambwe Hiza leo sijui yuko wapi, na wapo wengi sana katika historia: Nzanzugwaku, Lamwai, Kaburu, Jidulamabambasi (something like that), na wengine wengi sana. Ni kweli kuwa wanatumia haki zao za kikatiba lakini hawazitumii haki hizo kwa manufaa ya nchi.

Migogoro ya uongozi CDM ilikuwa na njia nyingi za kuitatua kitaasisi, lakini timu hii ilipoamua kuwa confrotational basi inawezekana sana kuwa ilichangia sana kutibua kila kitu kwani ni hulka ya binadamu kutotaka kushindwa. Waraka wao ulikokuwa na observations nzuri lakini ni observations ambazo hawakuonyesha kuzichannel vizuri, kwani ningekuwa katika positions zao nisingefanya hivyo na huenda ningefanikiwa sana. CDM wamekuwa wanatumia sana public opinion kumsimamisha mgombea wao. Hakukuwa na ulazima wa kusema hatumtaki huyu tunamtaka yule, wangetumia vigezo vile vile walivyotumia kumsimamisha Slaa mwaka 2010 wangeweza kufanikiwa malengo bila kuvuruga chama chao

Hata hivyo ya ngoswe tumwachie ngoswe, ila ngoswe huyo akikata mti ukaangukia nyumba yetu inabidi tulalamike. Mgogoro huu umeirahisishia sana CCM kurudi madarakani kwa kutumia mtu yeyote watakayemsimamisha hata kama ana uchafu wa namna gani.
 
Inaendelea....

Katika waraka tumeona sehemu zenye tuhuma dhidi ya uongozi uliopo madarakani.
Tuhuma hizo ni nzito na zinapaswa kutolewa ufafanuzi.

1. Kuhusu kipengele cha uongozi kufanyiwa mbinu, je ni kweli kuhusu hilo?
Kwanini uongozi haukurekebisha ulipobaini kulikuwa na tatizo katika uchapaji.
Na kwanini kila mara kumekuwa na mang'uniko juu ya suala hili bila kupatiwa jibu la maana

2. Tuhuma za Mbowe kukopesha chama bila kumbu kumbu
Je, Mbowe anaweza kujitokeza na kuonyesha kumbu kumbu zinazohusiana na madai yake ya fedha kwa uthibitisho?

3.Je, ni utaratibu gani unaotumika katika kutoa tenda na akina nani wanahusika.
Kuna kumbu kumbu zozote za kuthibitisha kuwa tenda zinatolewa kwa kufuata taratibu zilizowekwa na chama?

4. Je, Mbowe ni kweli kuwa una mtu anaye supply vifaa vya chama ambaye hakuteuliwa na chama na kwamba wewe na wenzako wawili ndio mnaofahamu hilo

5. Dr Slaa kwanini hakuna ukaguzi wa fedha kutoka kwa CAG. Je, mwenyekiti wa POAC mh Zitto ambaye pia ni msaidiz wako ameshawahi kukueleza kuhusu hilo, kama ndio kwanini hujafanya kama ilivyotarajiwa, kama hapana ni kwanini.

6. Dr Slaa, utaratibu wa kuajiri na kufukuza ndani ya chama upoje. Nani anayeajiri na nani anayefukuza mfanyakazi.

7. Dr Slaa, ni ipi ratiba ya uchaguzi ndani ya chama ikizingatia kuwa muda wa uongozi uliopo unakaribia kufikia hatima

8. Mbowe, ni upi utaratibu wa kupata viongozi wasiochaguliwa katika chama kama katibu mkuu, katibu mkuu msaidizi

9. Katika madai ya waraka ipo sehemu inayosema kikao kiliamua kuajiri watendaji wa kanda.
Dr Slaa kuna sababu gani za msingi za kufikia miezi 5 hilo halijatendeka

10. Mbowe na Slaa, je kuna utaratibu gani zaidi ya kuchangisha pesa wa kuleta mapato ndani ya chama.


Wana duru tunauliza maswali hayo kwasababu yanaonekana kujirudia rudia katika mitandao kukiwa hakuna majibu ya kuridhisha. Tunaamini kuwa ili tuwe na 'fair trial' ni lazima tufanye 'cross examination'.

Yale tunayoyajua tutayaeleza kwa ukamilifu, yale yenye mashaka yatahitaji ufafanuzi na hii ni sehemu ya fursa hiyo ili kuondoa sintofahamu ndani ya chama.

Tunawakaribisha viongozi, wasemaji au idara za CDM kuweka uwazi.


cc @Dr W.Slaa HAMY-D sixgate Mungi Ben Saanane Ritz Tumaini Makene

Itaendelea....
 
Uroho wa madaraka na mali ndio unaosababisha Tanzania tuendelee katika hali ya ufukara tulio nao. Kila mtu anafikiria ya kwake tu; hata watu tuliodhani wanatutetea kama akina Zito kumbe nao wanatutetea kwa sababu ya maslahi yao binafsi.

Kitila anaonyesha ana akili sana na anajua sana kupanga maneno yake kwa makini kuliko Zito ila nadhani naye alishindwa kujua njia nzuri ya kupamabana. Ni kwa bahati mbaya sana kuwa watu hawa, kama ilivyokuwa kwa wafuasi wao akina Shonza (something like that) nao watahamia CCM na na kupewa ukumbi mkubwa sana wa kutangaza kuwa matatazio ya Tanzania yanatokana na CDM.

CCM siyo chama imara ila kina raslimali nyingi sana zitokanazo na utaratibu mbovu wa serikali yetu, halafu kinapowapata watu wenye uchu wa madaraka na tamaa kubwa kama hawa basi wanatumiwa kwa nguvu sana kuibakisha CCM madarakani. Angalia Tambwe Hiza leo sijui yuko wapi, na wapo wengi sana katika historia: Nzanzugwaku, Lamwai, Kaburu, Jidulamabambasi (something like that), na wengine wengi sana.

Ni kweli kuwa wanatumia haki zao za kikatiba lakini hawazitumii haki hizo kwa manufaa ya nchi. Migogoro ya uongozi CDM ilikuwa na njia nyingi za kuitatua kitaasisi, lakini timu hii ilipoamua kuwa confrotational basi inawezekana sana kuwa ilichangia sana kutibua kila kitu kwani ni hulka ya binadamu kutotaka kushindwa.

Waraka wao ulikokuwa na observations nzuri lakini ni observations ambazo hawakuonyesha kuzichannel vizuri, kwani ningekuwa katika positions zao nisingefanya hivyo na huenda ningefanikiwa sana.

CDM wamekuwa wanatumia sana public opinion kumsimamisha mgombea wao.
Hakukuwa na ulazima wa kusema hatumtaki huyu tunamtaka yule, wangetumia vigezo vile vile walivyotumia kumsimamisha Slaa mwaka 2010 wangeweza kufanikiwa malengo bila kuvuruga chama chao

Hata hivyo ya ngoswe tumwachie ngoswe, ila ngoswe huyo akikata mti ukaangukia nyumba yetu inabidi tulalamike. Mgogoro huu umeirahisishia sana CCM kurudi madarakani kwa kutumia mtu yeyote watakayemsimamisha hata kama ana uchafu wa namna gani.
Mkuu Kichuguu ahsante kwa hoja zako naomba nizichangie japo kidogo.
1. Mambo haya si ya ngoswe kwasababu yanagusa masilahi ya taifa kwa namna fulani. Hatupendi turudi kule kwa kikundi cha watu kukaa na kufanya watakavyo kwasababu hakuna 'watch dog'. Upinzani ni sehemu muhimu sana ya demokrasia na hilo hatuwezi kulikataa.

2. Observations zao zingekuwa na maana kama zingejikita katika mkakati wa hoja za kujenga chama chao.
Nilitegemea kama wanalaumu hakuna mkakati wa kuongeza mapato au mkakati wa kisiasa waonyeshe kwa mantiki.
Hawakuonyesha wakaishia matusi kama 'akili ndogo, wahuni wanaopora wake za watu n.k.'

Mkakati wao ulikuwa kupora madaraka kwa njia haramu wakiwa chama cha kidemokrasia.
Walikuwa tayari jengo lianguke ili waje kulijenga upya.

Walichotaka kufanya si kusaidia chama kupata viongozi bora bali viongozi waliowataka wao.
Wakati wanaandika hayo wanalaani taratibu zinazotumiwa sasa hivi.

Nakubaliana mkakati wao hauna tofauti na ule wa Juliana Shonzo. Niwahi kuandika kuwa maneno ya Kitila ya kutaka 'Akina Juliana waachwe ili wabalehe' yalikuwa na maana. Nilisema Juliana alikuwa na nguvu kubwa ambayo leo tunaijua wazi. Ingawa wanasema hawakutaka kutumia mitandao kuhujumu chama ukweli ni kuwa wametumia

Tuhuma dhidi ya Slaa na mkewe zimekuwepo katika jamvi kila siku. Tuhuma za akina Mbowe kupewa tenda, mapiki piki zimekuwepo kila siku. Tuhuma za kufukuza watu makao makuu zimekuwepo. Tuhuma za matumizi ya fedha bila mahesabu tumezisoma sana. Kila mara watu walidhani ni LB7 kwamba CCM wanachokonoa.
Yote hayo yapo katika warakaMbinu za kuwa na multiple ID ndizo zimetumika katika kuleta tuhuma kutoka ndani ya chama. Leo wanaposema hawakutaka kutumia mtando ni ulaghai, wameutumia sana wawe wakweli tu

3. Wanasema Mbowe ana akili ndogo na elimu yake ni magumashi. Nilitarajia wao wakiwa wasomi waone mambo tofauti.
Mtei hakuwahi kugombea urais kwavile alikuwa anajenga chama. Bob Makani alikuwa anaimarisha chama.
Mbowe aligombea akijua ni kutangaza chama na wala si kushinda. Dr Slaa aliingia kama mshindani.

Ni Mbowe mwenye akili ndogo ndiye alikwenda kuwa recruit akina Zitto. Kwa 'akili yake ndog' alifahamu chama kinahitaji viongozi wa baadaye tena wasomi. Sijui hiyo ni akili ndogo zaidi ya ile ya kuzungumzia mahusiano binafsi ya Dr Slaa!!

4. CDM walikuwa na utaratibu mzuri wa kupata hata wagombea wao kutokana na public opinion. Sina shaka kabisa kuwa kilichotokea kwa Dr Slaa kingeweza kutokea kwa Zitto kwasababu ya public opinion.
Hili ni kosa ambalo halikhitaji hata certificate kulitambua. It was just a matter of time wangefika kule walikotaraji.

5. Tumewahi kuzungumzia sana na Mchambuzi kuwa CDM inajengwa na personality na hilo lazima walikomeshe.
Ukisoma waraka kuna sehemu wanasema 'tulete mtu maarufu tukileta siyejulikana itakuwa ni ngumu'

Mbowe alikwenda kuwaibua wasiojulinkana akina Zitto. Vipi hawa wasomi waseme wanahitaji mtu maarufu na si mtu mwenye quality za uongozi? Nani mwenye akili ndogo, yule aliyeibua vipaji au hawa wanaovizia watu maarufu?

Haya tunayoandika si maoni kutoka vichwani au hisia zetu, ni kwa mujibu wa waraka uliopo.
Wamejitahidi kupiga siasa lakini hawakujibu maswali muhimu sana yanayotokana na waraka.

Wao wamekuwa sehemu ya kuchochea mtafaruku na si kupata suluhu.
Ndio maana tunasema huo waraka una makosa na asiyeona ausome kwa uangalifu.
 
Last edited by a moderator:
MAKUNDI NDANI YA CHAMA

Wiki iliyopita tulisema chadema ina makundi yafuatayo
1. Kundi linalowania madaraka (power) ambalo sasa tunalijua ni la Kitila na Zitto
2. Kundi la Wasaliti ndani ya chama
3. kundi la CDM kama ilivyokuwa (Hili ni la akina Mbowe)
4. Kundi Neutral (Lisilofungamana na upande wowote)

Katika makundi hayo tulisema kundi la neutral linaonekana kuumizwa na migogoro. Mchambuzi akasema lipo bordeline.Leo tumeliona likiondoka katika borderline na kuchukua upande

Kundi la kuwania madaraka tulisema ndilo linachochea mitafaraku, halina subira kufika kileleni kwa mikakati yoyote.
Leo tunalijua

Kundi la CDM kama ilivyokuwa;
Hili ni la viongozi wa sasa wasiokubaliana na mabadiliko ya kijamii na kisiasa .
Linapenda consensus kuliko kufuata principles au kubadilika.
Ni kundi la wahafidhina kwa kiasi fulani.Ni kutokana na hilo kundi hili linapenda kupanga na wala si kushindana.

Kundi la wasaliti: Tukasema wapo watu ambao ni sehemu ya usaliti wakitumia na maadui wa CDM. Kwa bahati nzuri kundi hili limejinasibisha sana na 'kundi la madaraka' likiamini kuvunja nguvu za sasa ni kazi kubwa kuliko nguvu zijazo.

Tuliandika huko nyuma kuwa suluhu ya CDM ni kutafuta dawa ya kudumu na wala si kutumia asprin kutuliza maumivu. Uongozi uliopo umezembea katika suala hili kwa hofu ya kuudhi personality.

Kulikuwa na kila aina ya viashiria kuwa hali si shwari, tahadhari hazikuchukuliwa.
Leo zinachukuliwa hatua katika wakati mgumu na nyeti sana.

Uongozi umechukua hatua na kusahau factor(s) nyingine muhimu na hivyo kuwa vulnerable zaidi kwa 'maadui' wao wa nje.Ilipaswa uongozi utafute chombo neutral ili upate nguvu ya kusimamia maamuzi kwa uadilifu, uangalifu na weledi.

Endapo uongozi ulikuwa na waraka huu ambao ni ushahidi unaojitosheleza kwanini kisIundwe chombo neutral au kutumia baraza la wadhamini ili kupata suluhu. Hili lingeambatana na hatua ambazo zisingeweza kuwaacha vulnerable zaidi.

Pamoja na matatizo yaliyojiyokeza ukweli unabaki kuwa kuna kila sababu ya kufanya reform. Njia njema ya kufanya reform ni kufanya uchaguzi. Kupitia uchaguzi wa wazi na kidemokrasia CDM inaweza kupata viongozi watakaoamsha hamasa ambayo sasa imegawanyika katika political base yao.

Kwasasa hivi hakuna kitakachofanyika kama mageuzi ya haraka ya kidemokrasia hayatafanyika.
CDM ipo vulnerable kwa maadui wa nje na wa ndani wenye sentiments kutokana na viongozi wao kueneguliwa.
Hivyo wasibweteke kuwa kazi imekwisha, in fact ndio imeanza na itawavuruga kama hawatakuwa makini.
 
Last edited by a moderator:
Wanajamvi
Kuna swali nimeulizwa pembeni na pengine tuliangalie wote kwa pamoja.

Swali: Je hatua ya CDM kuwakatalia Zitto na Mkumbo kujiuzulu ilikuwa sahihi? Je haikulenga kuwadhalilisha au kukiumbua chama kama waraka huo ambao sasa umetoa habari za ndani za chama?

Jibu:
Hatua ya uongozi kuwakatalia kujiuzulu ilikuwa muafaka kabisa. Tunakumbu kumbu kuwa mgogoro umekuwa unafukuta kwa kwa muda mrefu. Tunasema wale waliokuwa wanashambulia CDM mitandaoni kwa habari za ndani ndio hawa wenye waraka. Madai yao yapo katika waraka na hata waraka umethibitisha kuwa waliamua kutumia ID feki katika shughuli zao.

Endapo wangeachiwa wajiuzulu hilo lingekuwa kosa kubwa sana.
Hakuna ambaye angeweza kutoka hadharani na kueleza kiini na sababu za kujiuzulu kwao.

Zingebaki hisia miongoni mwa watu. Kuna uwezekano mahasimu wa CDM wakachukua habari hiyo na kuifanyia spinning katika ukanda au ukabila na hilo lingeleta 'mantiki'hata kama si kweli.

Pili, viongozi waliotuhumiwa wangeweza kabisa kuendeleza mbinu zao kwa remote kwa kueleweka kama watu walioamua kuepuka majungu, ubaguzi n.k.

Hilo lingewapa nafasi ya kujijenga upya tena kwa nguvu kubwa isiyo na gharama.
Huo ndio ulikuwa mkakati wao kukimbilia kujiuzulu.

Tatu, hilo lingewaondoa katika kashfa ya Mwigamba. Ingeonekana kama Mwigamba alikuwa 'solo'

Maamuzi ya kuwakataza wasijiuzulu ni sahihi kabisa.
Maamuzi niliyo na shaka nayo hasa uelewa wa washabiki, manazi na wapenzi ni pale ambapo spinning itafanyika ili uongozi uliotoa adhabu uonekane onevu.

Kuna atakayesema kama Mbowe na Slaa ni watuhumiwa, haki ilitendekaje wakati wao ndio walioshtaki, wakaendesha mashtaka na kutoa hukumu?

Well, ndio maana tuliwaambia CDM watafute chombo neutral ili kuondoa hisia hizo.
Kwa bahati mbaya hawakufanya na hilo litabaki kama donda wakati huu wakiuguza mengine makubwa.

Nadhani hasira, jazba na kukosa mbinu kulipelekea baadhi ya maamuzi bila kuzingatia hali ya kisiasa ikiwa ni pamoja na weledi wa sehemu ya wanachama.
Na wala sikuona sababu za kufanya uteuzi kujaza nafasi ambazo hazina dharura kwa wakati huu

CDM walitakiwa wachukue muda ili kutuliza hali, kusoma mazingira na kutafuta njia mbadala itakayowaondoa katika vulnerability ambayo itaanza muda si mrefu.
 
Naam,

Sijachelewa kuingia ukumbuni,japo sijakaribishwa kwa ukamilifu lakini natia timu hivyo hivyo,

Nguruvi3,with all of my due respect hapo juuu mwanzo wakati unaianzisha hoja hii umesema wazi kabisa kwamba hapa watu tuwe huru,tueleze uhalisia wa kile kilichopo na bila woga na hofu yoyote,SHUKRANI KWA HILO..

Lakini niuleze swali,katika al mujadla huu ruksa kuchagua upande??kwani napokusoma kwa ndan sana nakuona unauma na kupulizia huku ukichagua upande wa mbowe na slaa kuutetea na kuchagua upande wa zitto na kitila KUUKANDIA,why??


Well,may be wewe tayar umeshachagua upande,ila hata hivyo sina haja,kama wewe umechagua upande ama haujachagua,mimi nasema wazi wazi kwamba mimi upande wangu ni UPANDE WA WALE WANAOPIGANIA MABADILIKO NDAN YA CHAMA BY ANY MEANS NECESSARY,MADAM WAO WANAPIGANIA MABADILIKO YATAKAYOONDOA UUNGU MTU,SIASA ZA KUOGOPANA NA DEMOKRASIA MAGHILINI NDAN YA CHAMA CHA CHADEMA,BASI MIMI NA AKILA MTANZANI MWENYE KUTAKA MABADILIKO LAZIMA ATALIAFIKI HILO (TEAM ZITTO)

Nguruvi3,si kweli kwamba ndan ya chama hiko watu hawajatumia njia za kidemokrasia kuonesha nia yao ya kutaka kupewa na fasi ya wao m kukitumikia chama hiko,siyo kweli hata kidogo,ili mtu uweze kupata picha ya kukifanya kitu flan let say kuomba ridhaa ya kuongoza,lazima kwanza uoneshe nia hiyo wazi wazi ikiwemo na kuitangaza nia hiyo na kuangalia mrejesho wa wale unaowatangazia nia hiyo ukoje,

Zitto alishaonesha nia hiyo tokea muda mrefu sana,kwa kutamka wazi wazi na kwenye viwanja halali kabisa,lakin unakumbuka kilitokea kitu gani??mara baada ya yeye kuonesha nia ya kuitumia haki nyake hiyo kikatiba na kidemokrasia basi ikawa ni zengwe mtindo mmoja,simu zilipigwa kutoka kila sehemu za watu mbali mbali kulaani kitendo kile,simu zilipigwa hadi kutoka TENGERU KWA MZEE MTEI, ziklaani kitendo hiko na kusema muda bado na zitto aache uroho na kukigawa chama..!!,kukigawa chama tena??yan kwa mtu kuonesha nia ya kutumia haki yake kidemokrasia ndan ya CHAMACHA DEMOKRASIA NA MENDELEO INAKUWA TENA LAWAMA NA KUSEMA KWAMBA ANAKIGAWA CHAMA??KIVIPI SASA??

Hapo hoja iko wazi kabisa,hoja mama dhidi ya haya yote ni kwa wahafidhina ndan ya chama hiko kutokuwa tayari kuwa challanged kwa namna yoyote ile hasa ukizingatia muda wa kufanyika kwa uchaguz umeshawadia,na wao wanahisi kwamba bado wana nafasi ya kuendela kuwatumika watanzania,inshort MBOWE & SLAA NA WAHAFIDHINA WENGINE THEY HAVE UNFINISHED BUSSNESS TOWARD 2015,SASA WANAPOONA KUNA HATI HATI YA MTU KAMA ZITTO(INTRUDER)ANATAKA KUINGIA KATI NA KUHARIBU PLAN HIYO WANA KUWA WAKALI NA KUTAFUTA KILANAMNA YA KUMJERUHI KWA KUTUMIA CHARACTER ASSISSNATION NA KUAMINISHA UMMA WA WATANZANIA KWA PROPAGANDA UCHWARA ETI KWAMBA ZITTO ANATUMIWA NA CCM PAMOJA NA USLAMA WA TAIFA,,HILO HALIPO NA WAHAFIDHINA IFIKIE HATUA KWA SASA WAUKUBALI UKWELI NA WAPISHE MABADILIKO,WAWE WAUMINI WA KWELI WA DEMOKRASIA,

Wilbroad Slaa(KAMBI YAKO),ambae kwangu mimi kwa sasa namuona kama ni kiongoz MPUUZI NA ALIEKOSA MAONO NA MWENYE UCHOVU WA KIFIKRA NI TATIZO KUBWA SANA NDAN YA CHAMA,
samahani natumia lugha kali dhidi yake lakini naweza kuthibitisha kwa nin namuita kiongoz huyo ni mpuuzi na mwenye kupaswa kupumzka,

Mara kwa mara humu jukwaani tumeona yanatokea magroup ya watu wasio fahamika ndan ya chama hiko kwamba hao ni kina nan,wana uongoz gan ndan ya chama,wanatumwa na nani na kadhalika kama Yerikcko Mdandia nasaba ya nyerere na Ben Masaa manane kuja kueleza mambo chungu tele yenye ukakasi na kumtukana zitto na watu wengine wanaonekna kwenda kinyume na mawazo yao huku WILBROAD SLAA AKITOKELEZEA NA KUJA KUWASHANGILIA WATU KAMA HAO??ZIPO TETESI AMBAZO TUNAZISKIA YA KWAMBA WATU HAO AMBAO KWA SASA HUMU JF HUONEKANA KAMA NI MATAPELI WANATUMWA NA WILBROAD SLAA.

Sasa Wilbroad Slaa naibu wake anatukanwa na kudhalilishwa mitandaoni bila ya ushahid bila ya kufuata PROTOKALI kisha yeye anatokezea kuja kushangilia je NIKISEMA WILBROAD SLAANI MPUUZI NA M.PU.MBA.VU NAKOSEA??Usichukie Nguruvi3 upumbavu na upuuzi sio tusi,RAFIKI YANGU NINAEMUHESHIMU SANA Invisible analitumia neno hilo na kusema kwamba "FICHA UPUMBAVU WAKO NA UONESHE WEREVU WAKO NA BUSARA ZAKO",,
Sasa najiuliza kwa nin Slaa hafichi u.p.umba.vu wake na kuonesha busara zake yeye kama KATIBU MKUU WA CHAMA??kwasababu haiwezekani wewe naibu wako anatukanwa kisha wewe uje ushangilie,kwani yeye zitto haumii???yeye ni binadamu na ana nyongo,Slaaalikua anadhani vipi??huo ni mfano mmoja kukuonesha kwamba kulikuwa kuna Mpango wa kufanya Character Assissnation ili lengo la wahafidhina na waungui watu ndan ya chama litimie kuelkea kwenye uchaguz huu unaokuja..


Either Kuhusu huo unaosemekana kama waraka wa siri,zitto amekanusha kuwa hausiki nao,na hata hao viongoz wa kamati k,uu hawajamvua vyeo vyake zitto kwa kuhusika na waraka huo..

Sababu walizomvua nazo uongoz ni zile zile za kunyoosheana vidole vinayvofanywa siku zote ndan ya chama hiko,

Ni vigumu sana kuonesha nia ya kutaka kuleta demokrasia ndan ya chadema kwa kuwa wao wenywe sio waumin wa hiyo demokrasia,

Chadema wanapata wapi MORAL AUTHORITY YA KUSEMA KWAMBA WAO NI WANA DEMOKRASIA ILI HALI NDAN YA KATIBA YAO KIPENGELE CHA UKOMO WA VIPINDI VYA MADARAKA HAKIPO??WANA TOFAUTI GANI SASA NA MUGABE AU MUSEVENI??UKOMO WA MADARAKA HAUPO,KISHA WATU WAKIONESHA NIA YA KUTAKA KUITUMIA HAKI YAO YA KIKATIBA HUONEKANA MAMLUKI NA WASALITI KWAN NIN??AU KWA KUWA HAWANA NUMBER ONE QUALIFICATION YA KWAMBA LAZIMA BARAKA ZITOKE TENGERU KWA MZEE MTEI??HAYA MANENO YANAWAUMIZA BAADHI YA WATU,LAKIN SASA TUFANYAJE??BORA TUSEME TUH NA KILA MTU ASIKIE,YAN MTEI AMEKUWA KAMA AYATOLLAH ALKHEMENEI??

Madam wamesema kuwa hiki ni chama cha demokrasia basi waoneshe uhalisia wa hayo wanayoyasema,WATANZANIA WA SASA SIO WALE WA 2010,HILO LIFAHAMIKE WAZI,HILI SUALA LA ZITTO KABWE(TEAM YANGU) NI ZITO NA CHADEMA WASIPOKUWA MAKINI LITAWAGHARIMU MILELE,
 
Last edited by a moderator:
The Big show
Kwanza narudia kauli yangu kuwa tusimame katika ukweli na nasimama na neno hilo.Mwanzo wa bandiko nimesema tujadili waraka kama ulivyo na waraka uliopo ni wa Kitila na Zitto. Nilisita kuendelea kama alivyoshauri Mag3 ili tupate upande wa pili wa utetezi, ambao nao umewekwa hapa. Hatujadili hisia tunajadili waraka ndio maana nimekuwa nawanukuu ili kuonyesha sichomeki hisia bali najadili kile kilichopo mbele yetu.
Sababu kubwa ni kuufanyia kazi huo waraka ambao wamekiri upo na wamekiri makosa wao wenyewe.
Hakuna njia nyingine ya kuujadili waraka huo kwa namna tofauti tutaujadili kama ulivyo.

Kikubwa zaidi nimejaribu kueleza nafasi yangu kuhusu maswali tunayoulizwa.
Ndugu Torch kauliza je waraka una ubaya gani? Nimeonyesha kwa mtazamo wangu makosa ya waraka huo na katika kufanya hivyo itaonekana kuchukua upande, waraka ni wa Kitila ni makosa kumhusisha Mbowe kama mwandikaji.

Kuhusu mbinu za watu kujaribu kuleta mabadiliko, mara nyingi nimeunga mkono ushindani ndani ya chama.
Nimewahi kuandika kuwa utamaduni wa kupita uchaguzi bila mpinzani ni ujinga na sasa ufike mwisho kwa vyama vyote.

Lazima kuwe na chechecheo. The Big sjow hivi kweli chekecheo tunalolitaka ndio waraka huo tunaousoma!
Yaani sera za chama zinaandikwa na wasomi kuhusu mapenzi ya Dr Slaa, tena kuna kipengele wanakubali ni mambo binafsi.Utaona ni waraka ulio dhalili kiasi siamini aliyeandika ni Kitila, nahisi ni Juliana ! Honestly

Mbinu za kuleta mabadiliko hazifanywi kitoto namna hiyo kwa kuzua uongo na kudhalilisha watu.
Nimesoma waraka na wewe umeusoma naomba unionyeshe wapi kuna substance inayoweza kuamsha fikra zako kama mpenda mabadiliko, please the big hebu tujadiliane.

Tatu, nimeonyesha kuwa wale wanaochafua CDM mtandaoni na pengine kudhoofisha jitihada ni hawa hawa unaosema wanaka mabadiliko.Nimeorodhesha tuhuma zote ambazo zinaletwa na watu ambao wanajifanya ni CCM kumbe ni akina Kitila na Zitto ambao wamekjiri waraka ule usio na chembe ya mabadiliko.

Nimeonyesha kuwa Juliana na wenzake ambao Kitila aliwaandika makala Raia mwema kuwa 'waachwe wabalehe' walikuwa wanatumika kuvuruga chama. Rejea post za nyuma na za duru za siasa tumeweka wazi kila kitu kabla hakijatokea.Tumeweka kiti moto akina Salaa na Mbowe bila huruma lakini hili la waraka ni aibu sana.

Kama Kitila na Mkumbo hawakuridhika na mwenendo walikuwa na nafasi nyingine za kukisaidia chama.
Hawa ni watu maarufu ambao wanachama wangewahitaji kwa namna yoyote bila kuwa na kikwazo.
Wangejiuzulu nafasi zao wakiendelea na mikakati positive ya kujenga chama si waraka huu hafifu.

Hatukuwasikia hata siku moja bali walikuwa wanachochea maasi ya kuondoa viongozi kwa njia ya ufitini knyume na misingi ya kidemokrasia ya chama chao.Kampeni za CDM zimekufa kumbe ni hawa watu na nashangaa unawatetea.

Nimewauliza akina Slaa na Mbowe kuwa tuhuma dhidi yao ni nzito na zenye kufikirisha ndio maana tumewataka wajibu.
Haina maana waraka wote ni null and void, no thank you! lakini hauna substance za mabadiliko na wala hauwakilishi kundi la wasomi kama wanavyojinasibu.

Nikupe challenge mkuu, hebu nionyeshe wapi ambapo unadhani nimechukua upande kwa kuangalia waraka huo.
Nukuu zipo na maoni yangu yapo, waspi sikutenda haki.

Nimalizie kusema, hata kama jambo lililokusudiwa lilikuwa jema ukweli ni kuwa halikufanyika katika njia njema na hakukuwa na mantiki zaidi ya kiu na uchu wa madaraka. Kutoa takwimu zaupande mmoja ni majungu na hilo nabaki kulisema hivyo.

Hebu tujadiliane
 
Last edited by a moderator:
Arguably, wapo watakaodai kuwavua nyadhifa wahusika wa sakata ni maamuzi sahihi. Bado nasimama hoja uamuzi unaweza kuwa sahihi lakini njia zilizotumika hazikuwa sahihi, zinaacha loophole, ni pande mbili husika kulitakiwa kuwe na chombo kingine.

Kwa uapnde mwingine maamuzi yalikuwa ya jazba kuliko busara.

Kuwavua uongozi watu maarufu ni jambo zito na lilihitaji ‘cooling effect''

kwamba uongozi ujipe muda wa kutathmini nini cha kufanya kuhusu nafasi mbali mbali.


Kitendo cha kuteua kuziba nafasi kililenga kupeleka ujumbe kuwa nafasi ya katibu mkuu msaidizi imeshazibwa na hakuna atakachofanya kuhusu hilo.

Ni ujumbe kwa wafuasi kuwa hatua zitachukuliwa tena kali kama harakati zitaendelea.


Hii ni jazba, haikuzingatia mazingira mengine yanayoweza kuambatana au kuambatanishwa na teuzi hizo. Ilikuwa muhimu kuwa na muda wa kutafakari na kupambanua zaidi ya kukurupuka.


Kwa sasa CDM ipo katika crisis, inaonekana kuwagawa wanachama katika makundi.

Hilo si jambo jema kwa wakati walio nao .


Hakuna shughuli za chama zitakazoendelea huku kukiwa na manung'uniko na maswali ambayo hayajajibiwa.Wapo watakaoamini katika mitazamo tofauti na hilo lita paralyze shughuli za chama.


Katika nchi zenye utawala wa demokrasia na utawala bora, CDM ingeitisha uchaguzi.

Crisis iliyopo ikihusisha ofisi kuu na wajumbe wa kamati kuu ni ishara ya kutokuwa na imani na uongozi .

Mataokeo ya ‘vote of no confidence' yangeshangaza endapo lingefanyika hilo.


Kimantiki tukubali kuwa CDM ipo njia panda ili kurejesha mwamko, imani na hamasa kwa wanachama lazima uongozi ujiridhishe kuwa unakubalika au la.

Njia ya kufanya hivyo ni kupitia uchaguzi ili safu ya uongozi iingie.


Chaguzi huwa ni crisis kwa vyama vyote na inachukua muda kupona(healing).

Kunapokuwepo na looming crisis kama hii, time constrains kutokana na matukio yanayokuja ya kitaifa, CDM haina muda wa kupoteza tena.


Ni vema uongozi ukafuata taratibu za kiungozi kutafuta ridhaa wakati huu muda ukitoa nafasi. Vinginevyo ni kulundika matatizo ili yashughulikiwe siku moja, ni tatizo kubwa.


Ningewashauri viongozi waitishe uchaguzi kwasababu kimantiki kuna vote of no confidence tayari. Uongozi wa CDM utafute mandate tena au wanachama waamue vinginevyo . Kwasasa hakuna kitakachofanyika.

 
Back
Top Bottom