Vipi JK hazungumzii ufisadi majukwaani? Kwake mimba za wanafunzi ni tatizo kubwa zaidi ya ufisadi?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233

Kwa nini JK akiwa majukwaani au kwenye hafla huwa hazungumzii ufisadi kwa namna ya kukemea na kusema ni tatizo linalohatarisha amani ya nchi?

Nakumbuka mara ya mwisho JK kuzungumzia ufisadi ni Bungeni Dodoma, mapoema August 2008 wakati wa suala la wizi wa EPA lilivyoshika kasi. Hata baada ya hiyo hajawahi kamwe kulirejea suala hilo, lilifikia wapi, iwapo kumetokea mafanikio nk. Hajawahi hata kutamka neno “EPA” katika hotuba yake yoyote baada 2008.

Leo hii JK amenukuliwa na vyombo vita habari akikemea kwa nguvu zake zote tabia ya baadhi ya wananchi kuwaoa wanafunzi wa shule, na kwamba hawa wakamatwe mara moja na kufunguliwa mashitaka ya kubaka!

Laiti JK angekuwa anakerwa sana na ufisadi kwa namna hii, tungepiga hatua kubwa katika vita hiyo.

Hata hivyo inavyonekana JK hajui tofauti kati ya kubaka na kumwingilia mwanamke chini ya umri!

Kumwingilia mwanafunzi chini ya umri kwa namna hiyo ya kumuoa mwanafunzi siyo kubaka. Hili ni kosa jingine na halihitaji ‘consent’. Na kubaka pia anaweza kufanyiwa mwanamke mwenye umri mkubwa.
 
mhhhhhhhh loading,nilidhani suala la ufisadi linahitaji utekelezaji zaidi ya maneno matupu jukwaani?
 
Kwa nini JK akiwa majukwaani au kwenye hafla huwa hazungumzii ufisadi kwa namna ya kukemea na kusema ni tatizo linalohatarisha amani ya nchi?

Nakumbuka mara ya mwisho JK kuzungumzia ufisadi ni Bungeni Dodoma, mapoema August 2008 wakati wa suala la wizi wa EPA lilivyoshika kasi. Hata baada ya hiyo hajawahi kamwe kulirejea suala hilo, lilifikia wapi, iwapo kumetokea mafanikio nk. Hajawahi hata kutamka neno "EPA" katika hotuba yake yoyote baada 2008.

Leo hii JK amenukuliwa na vyombo vita habari akikemea kwa nguvu zake zote tabia ya baadhi ya wananchi kuwaoa wanafunzi wa shule, na kwamba hawa wakamatwe mara moja na kufunguliwa mashitaka ya kubaka!

Laiti JK angekuwa anakerwa sana na ufisadi kwa namna hii, tungepiga hatua kubwa katika vita hiyo.

Hata hivyo inavyonekana JK hajui tofauti kati ya kubaka na kumwingilia mwanamke chini ya umri!

Kumwingilia mwanafunzi chini ya umri kwa namna hiyo ya kumuoa mwanafunzi siyo kubaka. Hili ni kosa jingine na halihitaji ‘consent'. Na kubaka pia anaweza kufanyiwa mwanamke mwenye umri mkubwa.

Kwenye red: Huyu si aliwahi kusema kwamba wanafunzi wanaopata mimba ni kutokana naviherehere vyao? Au siyo yeye aliyesema?
 
Yeye naye si tunda la mti uleule sasa atasemaje mti huo matunda yake mabaya?
 
Kwa nini JK akiwa majukwaani au kwenye hafla huwa hazungumzii ufisadi kwa namna ya kukemea na kusema ni tatizo linalohatarisha amani ya nchi?

Nakumbuka mara ya mwisho JK kuzungumzia ufisadi ni Bungeni Dodoma, mapoema August 2008 wakati wa suala la wizi wa EPA lilivyoshika kasi. Hata baada ya hiyo hajawahi kamwe kulirejea suala hilo, lilifikia wapi, iwapo kumetokea mafanikio nk. Hajawahi hata kutamka neno "EPA" katika hotuba yake yoyote baada 2008.

Leo hii JK amenukuliwa na vyombo vita habari akikemea kwa nguvu zake zote tabia ya baadhi ya wananchi kuwaoa wanafunzi wa shule, na kwamba hawa wakamatwe mara moja na kufunguliwa mashitaka ya kubaka!

Laiti JK angekuwa anakerwa sana na ufisadi kwa namna hii, tungepiga hatua kubwa katika vita hiyo.

Hata hivyo inavyonekana JK hajui tofauti kati ya kubaka na kumwingilia mwanamke chini ya umri!

Kumwingilia mwanafunzi chini ya umri kwa namna hiyo ya kumuoa mwanafunzi siyo kubaka. Hili ni kosa jingine na halihitaji ‘consent'. Na kubaka pia anaweza kufanyiwa mwanamke mwenye umri mkubwa.

Kasome Vizuri sheria ya Ubakaji uje kumkosoa Mh. Rais, Sio kila Mtu aanzishe Thread wengine inatosha kuchangia za wengine. Kuhusu Suala la Ufisadi pengine leo ndo umefika kwewnye Access yA HABAR.
 
vita ya ufisadi ni zaidi ya kauli ya Rais. kila mmoja wetu akikemea na kuchukua hatua, hali itabadilika. haiyumkini Dr Slaa mathalan anajikopesha milioni 180 fedha za ruzuku kujengea nyumba. haiyumkini Mbowe anaiba fedha za chama na kununua majumba ya kifahari huko Dubai halafu wafuasi wake wanampigia makofi tu. huu ni uhayawani wa hali ya juu
 
Ufisadi ni singo ya Dr Slaa iliyochuja.

Vipi tayari mmeishachakachua mahesabu ya ruzuku?
 
Siku akizungumzia ufisadi majukwaani siku ya pili yake jua litachomoza magharibi na kulelekea mashariki! Hana ubavu dogo huyo!
 
Ufisadi ni singo ya Dr Slaa iliyochuja.

Vipi tayari mmeishachakachua mahesabu ya ruzuku?

Vipi kale ka mchezo ka kujivua Gamba kaliishia wapi Mkuu. Make bila Kumtaja Dr. Slaa hulipwi Buku 7 zako. Tuambieni kuhusu:-
1. Mikataba mibovu
2. Kushuka kwa Elimu na kuongezeka kwa Division V
3. Mbio za Urais 2015
4. Utajiri wa Dogo alitishia kuwashtaki CHADEMA ndani ya siku 7 hazijaisha tu?
5. Vipi Biashara ya Menno ya Tembo na madawa ya kulevya washashtakiwa wangapi?
Unasemaje kuhamisha Twiga wetu kwenda Qatar?
6. Hivi ninyi mlishapewa ripoti ya wataalamu wa Inteligensia kuhusu sakata la Olasiti na Mkutano wa CHADEMA Arusha.
7. Vipi kauli za kuwataka watanzania kutumia koroboi na wengine wakauze Juice ili wawekezaji wapore raslimali zetu za asili ndo Maisha bora kwa kila Mtanzania hayo?
8. Je safari ingine ya majuu ni lini make naona kimya sasa Mkuu
 
Hajaambiwa bado!

Si unasikia katika hotuba zake mara nyingi anasema "nimeambiwa", "nimesikia" nk. Tuombe Mungu labda huu muda aliobakisha apate muda wa kukaa ofisini kwake na kuyaona mambo mengi ya nchi mwenyewe badala ya 'kuambiwa' na hapo ataweza kuuona ufisadi uliokithiri.
 
Kama ana uchungu sana na wanaobakwa, yeye kama steringi wa hili dola anasemaje kuhusu ubakaji wa yatima uliofanywa na Kapuya? Au ndo hivyo katoa maagizo kuwa vyombo vya hili dola vimshughulikie?
 
ufisadi wa jukwaani upo chadema ambao hufanywa na viongozi wake kwa kuchangisha hele wanachi wao wanafaidi wao na familia.
 
Kama ana uchungu sana na wanaobakwa, yeye kama steringi wa hili dola anasemaje kuhusu ubakaji wa yatima uliofanywa na Kapuya? Au ndo hivyo katoa maagizo kuwa vyombo vya hili dola vimshughulikie?

sasa ubakaji kama wa lema unafanyaje kama ingekuwa ni wewe.
 
wanafunzi wanapata mimba kwa viherehere vyao by kikwete kiongozi wa mafisadi
 
vita ya ufisadi ni zaidi ya kauli ya Rais. kila mmoja wetu akikemea na kuchukua hatua, hali itabadilika. haiyumkini Dr Slaa mathalan anajikopesha milioni 180 fedha za ruzuku kujengea nyumba. haiyumkini Mbowe anaiba fedha za chama na kununua majumba ya kifahari huko Dubai halafu wafuasi wake wanampigia makofi tu. huu ni uhayawani wa hali ya juu
na rais ni fisadi hivyo hawezi kukemea mafisadi wenzake wakamuelewa!
 
ufisadi mimi umejaa chadema sasa ni ufisadi wa madaraka na kubadili katiibA chama kwa malengo ya kutawla milele.
 
Back
Top Bottom