Vipepeo weusi season 2: From Zurich with rules

Vipepeo weusi season 2: From Zurich with rules

tapatalk_1519472923336.jpeg


VIPEPEOWEUSI


FROM ZURICHWITH RULES



EPISODE 26



Yule binti kwa kiasi fulani alikuwa 'amerelax' tofauti na zile hasira zake za mwanzo alivyoshuka kwenye gari na kuja kutugongea kwenye kioo.
Alikuwa amenitambulisha jina lake kwamba anaitwa Winnie Akoh. Alikuwa ni mwanafunzi kutoka nchini Senegal na yuko hapa Zurich kama mwanafunzi akisomea "Banking and Finance" katika chuo kikuu cha Zurich.

"What are doing in that house?" Nakumbuka nilimuuliza.

Winnie alinieleza kwamba miaka miwili iliyopita alipowasili hapa Zurich kwa ajili ya masomo kama ilivyo kawaida ya wanafunzi wengi ughaibuni ilimlazimu kutafuta kibarua ambacho atakuwa akifanya katika muda wake wa ziada ili aweze kuingiza kipato cha kumuwezesha kujikimu.

Winnie alinieleza, kwamba aliomba kazi kadhaa mtandaoni… kuanzia uhudumu kwenye mgahawa, uhudumu kwenye kituo cha kutunza wazee, kuwa mtu wa mauzo wa kampuzi za vipodozi na kadhalika na kadhalika. Alinieleza kwamba aliomba kazi nyingi sana na kusubiri aone ipi ambayo atapata majibu. Katika mlolongo wa huo wa kuomba kazi mtandaoni aliona tangazo lenye maelezo mafupi tu likisema "Earn $ 3000/month cleaning a house".

Winnie alinieleza kwamba mwanzoni alihisi labda ni utani au tangazo la uongo kama ambavyo yamejaa huko mitandaoni. Lakini akaamua kutuma tu maombi aone kama ni kweli au la.
Anasema kwamba siku tatu baadae alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni muwakilishi wa kampuni walioweka tangazo lile ambalo yeye aliomba kazi.

"Did he tell you the company's name?" Nilimuuliza.

"Yes! REMODO HOLDINGS." Winnie alinijibu.

"Can I have their adress?" Nilimuuliza.

"I might still have their business card in my car…!" Winnie alinijibu.

Kisha akaendelea kunieleza kwamba mtu huyo alimuhoji maswali kadhaa kuhusu taarifa zake na kisha akamtaka waonane baada ya siku moja.

"Did you meet him?" Nakumbuka nilimuuliza.

"Yes! We did meet two days after the phone call."

"Where did you guys meet?"

"Freacht West Street… there is a fancy chinese restaurant there."

"Chinese restaurant??"

Nilishtuka sana aliponitajia kwanza Freacht West Street. Huu ndio mtaa ambao kuna Radison Blu Hotel ambayo nilifikia nilipoingia hapa Zurich na ndio mahala ambako siku mbili zilizopita yamefanyika mauaji ya Luke na Ivanka. Lakini nilishtuka zaidi aliponitajia mgahawa wa kichina… kwa sababu niliamini kabisa alikuwa anaongelea mgahawa ule ambao niliwahi kufika siku ya kwanza na kuchomwa sindano ya kemikali na kupoteza fahamu na baadae kujikuta nimeamka kwenye lile jengo mtaa wa Hardstrasse.

"Is everything ok?" Winnie aliniuliza baada kuona mshtuko wangu.

"Everything is ok! I was just thinking about that meeting place… it seems like an odd choice." Nilijitahidi kumzuga. Sikutaka ajue chochote kile ambacho nakifahamu kuhusu sehemu hizo.

"Why is that?" Aliniuliza

"No! Nothing… what happened next?"

Akaendelea kunieleza kwamba, mtu huyo alichukua nakala zake za hati ya kusafiria, kitambulisho cha uanafunzi chuoni pamoja na namba yake ya akaunti ya benki. Kisha akamlipa dola elfu moja tasilimu papo hapo na kumwambia kuwa anatakiwa kuanza kazi kesho yake.

"What was the job about… what where you suppose to do?" Nilimuuliza.

Alinijibu kwamba, alikuwa anatakiwa kufika kwenye ile nyumba ya mtaa wa Affolterntrassemara mbili kila wiki kwa ajili ya kufanya usafi na kupokea barua zozote ambazo zitatumwa kwenye anuani ya nyumba hiyo. Hiyo ndio ilikuwa kazi yake.

"Thats it?" Nilimuuliza.

"Yap! Thats it.." alinijibu huku anatabasamu.
 
"Did you ever got his name?"

"I dont really remember… Eddie or Edgar something like that." Winnie alinijibu.

"Don't you find it odd and curious to be paid all that money just to clean a house twice a week?" Nilimuuliza tena.

"At first I was curious… but after doing it for two years, now I am comfortable with it... I just assume may be the house belongs to some rich folks and the house hold some wonderful memories and they dont want it to get dusty… I dont I am just comfortable with it now… but that was until theree weeks ago!"

"When someone started following you!" Nikamsadia kumaliza sentensi.

"Yap! Then I started to be curious again… why am I being followed? Do you know who they are?"

"Not really! That's what we are trying to figure out.!" Nikamjibu. "So how do you get paid?"

Winnie alinijibu kwamba kila mwisho wa mwezi anaingiziwa fedha kwenye akaunti yake kiasi cha dola elfu tatu. Nikamuomba anipe namba ya akaunti ambayo inatumika kumtumia hizo fedha.
Winnie akachukua simu yake nakuanza kubofya bofya akitafuta mahala ambako alihifadhi namba hiyo ya akaunti ya benki. Baada ya kama dakika moja hivi aliipata na kunisomea huku na mimi nikiandika kwenye simu yangu.


"AECD0210000000693123456"


"Winne I can not thank you enough! Thank you very much!"

"Its ok! I hope this is information I have given you is not going to get me into any trouble."

"Not at all!" Nilimfariji lakini moyoni nikiwa na mashaka hasa nikikumbula vifo vya Luke na Ivanka siku mbili tu zilizopita.
"Jus one last question…"

Kabla hajaondoka nikamuuliza swali la mwisho. Kwamba alinieleza kuwa mtu ambaye alionana naye alimuelezakuwa jukumu lake ni kufanya usafi kwenye ile nyumba pamoja kupokea barua. Nikamuuliza hizo barua anazifanyia nini?

"I forward them… he gave me a forwarding address." Alinijibu.

"Can I have that address?"

"Its actually their company's address… as I said, I think I still have thier business card in my car."

Nikamshukuru Winnie tena na tena kwa taarifa hizi zote ambazo alikuwa amenipatia. Sasa nilikuwa najihisi kabisa kwamba nimeanza kupiga hatua kutegua fumbo hili ambalo lilikuwa limenileta hapa Zurich.

Tukatoka pale mgahawani na kutembea kuelekea pale ambako tulikuwa tumeyaacha magari. Winnie walau sasa alikuwa anatabasamu tofauti na hasira ambazo nilimuona nazo awali alipokuja kutugongea kioo cha gari. Ni muda huu ndipo ambapo nilipata kutambua uzuri aliokuwa nao. Alikuwa ni binti mrembo haswa. Mrefu kiasi, mwenye umbo zuri haswa la kuvutia, uso mwembamba kiasi na macho mazuri ya kutamanisha mwanaume yeyote. Tukiwa tunatembea nilijaribu kufanya utani wa hapa na pale ili 'arelax' zaidi. Kila mara ambapo alitabasamu au kucheka kutoka na utani niliokuwa naufanya nilijikuta nafurahi moyoni kuona tabasamu lake la bakshasha na namna ambavyo meno yake meupe peee yalivyo pangika kwa uzuri kinywani mwake.

Gari lake alikuwa amelisimamisha mbele ya gari yetu kama, kama umbali wa mita mia moja hivi. Kwa hiyo tulilipita gari letu tukiongozana nikimsindikiza kuelekea kwenye gari lake. Jimmy bado alikuwa ndani ya gari. Alituangalia tu tulivyopita bila kusema chochote.

Tulitembea mpaka tukalifikia gari lake. Tukiaganana kutakina heri na kuahidiana kwamba tutaonana tena siku za karibuni. Kwa kiasi fulani nilihisi pia Winnie alikuwa amefurahia 'kampani' yangu kwa dakika chache zile. Sikujua kama ni kwa sababu mimi ni Mwafrika mwenzake au vipi. Maana Waafrika ikitokea mkikutana ughaibuni mnajikuta mnafurahi kama vile ndugu mliopotezana siku nyingi.
Sikujua ni kwa nini lakini ilikuwa dhahiri kabisa kwamba Winnie alifurahia muda ule tuliokuwa wote.
 
"Let me get that card!"

Alifungua mlango wa gari na kuingia ndani akianza kupekua pekua kutafuta ile business card ambayo alihisi kuwa bado anayo.

"Here you go!" Aliibuka kutoka kwenye gari akiwa ameshikilia business card na kunikabidhi.

Alipobikabidhi tu macho yangu moja kwa moja yalianza kudadisi ile kadi hasa anuani yake.


REMODO HOLDINGS
HARDSTRASSE 201
1985
ZURICH
SWITZERLAND

Nilisikia moyo unalipuka kama vile unataka kutoka kifuani. Nilijitahidi kweli kweli Winnie asigundue mshituko wangu.
Hii ilikuwa ni anuani ya lile jengo ambalo kwa sasa naishi ndani yake. Jengo lile la mtaa wa Hardstrasse.

"Are you ok?" Winnie aliniuliza kwa udadisi.

"I'm ok! So when can I see you again.." nilijaribu kuhamisha mjadala huku nikilazimisha tabasamu usoni.

"I don't know… we will see about that!" Winnie alinijibu huku anatabasamu.

Tulibadilishana namba za simu kisha akakwea kwenye gari lake na kuondoka.

Nilibakia pale nikilitazama gari likiondoka. Nililitazama mpaka ambapo lilipotea kwenye upeo wa macho yangu. Kichwani nilikuwa nawaza vitu vingi sana lakini kikubwa kikiwa ni usalama wa Winnie. Taarifa kwamba kuna watu walikuwa wanamfuatilia kabla yetu iliniumiza moyo sana na kunipa wasiwasi. Nilikuwa na mashaka juu usalama wake. Nilitamani ningekuwa na uwezo nimchukue na kurudi naye Hardstrasse.
Kwa muda mchache tu baada ya kuonana na Winnie nilikuwa nimejikuta najihisi nina jukumu la kuhakikisha yuko salama. Sikujua ni nini hasa kilikuwa kinatokea moyoni mwangu. Nimempenda?? Nikatingisha kichwa kuondoa hilo wazo kichwani mwangu.

Nikatupa macho tena mkononi kwenye ile business card ambayo ina anuani ya jengo la Hardstrasse. Moyo ukaanza tena kwenda mbio.
Nikatembea haraka kurejea kwenye gari yetu.

Jimmy alikuwa ananitazama huku anatabasamu nilipoingia ndani ya gari.

"I think you said you were married mate!"

"Yes, I am!"

"I saw the way you look at that girl… not cool mate… not cool..!" Jimmy aliongea akitingisha kichwa huku anatabasamu kwa utani.

"Shut up you idiot!" Nikajikuta nashindwa kuficha tabasamu fulani la aibu. Alichokuwa anakisema Jimmy kilikuwa na kiasi fulani cha ukweli.

"So what did your girlfriend say?" Jimmy aliniuliza huku bado akiwa na tabasamu la utani.

Nilimsimulia kila kitu kuhusu maongezi yangu na Winnie. Namna alivyopata kazi. Maagizo aliyopewa. Namna anavyolipwa. Mpaka ile anuani ya kampuni.

"What does all this mean?" Jimmy aliniuliza taharuki.

Hata yeye alishitushwa kuona anauani ya kampuni iliyomuajiri Winnie kufanya usafi kwenye ile nyumba ya mtaa wa Affolterntrasse ni anuani ile ile ya jengo ambalo kwa sasa tunakaa mtaa wa Hardstrasse.

Lakini binafsi taa ilikuwa inawaka kwa nguvu kichwani. Nilihisi nukta zinaungana. Hatua kwa hatua nang'amua hili fumbo.

"Have you ever heard of the word 'shell company'?" Nilimuuliza Jimmy.

"I might have.. I dont really know though what it means.!"

Nikaanza kumueleza Jimmy kile ambacho nilikuwa nakihisi na kwa sababu gani nilipewa lundo la zile nyaraka. Na kwa nini anuani ya hii kampuni inaonyesha ipo jengo la Hardstrasse.

Nilimueleza kuhusu shell companies. Kwamba kampuni hewa zinazoanzishwa kwa lengo la kuficha umiliki wa kampuni nyingine au kupitisha rasilimali tu kwa lengo la kuficha umiliki wa hizo rasilimali na zilikotoka. Kwamba unaweza kuanzisha msururu wa 'shell companies' ambazo kampuni moja inamiliki nyingine na nyingine na nyingine inamiliki nyingine. Vivyo hivyo kwa lengo la kuficha wamiliki halisi.

Hiki ndicho ambacho nilihisi kilikuwa kimefanyika. Na ndio sababu ya lundo la nyaraka nilizopewa kule mtaa wa Wipkeng na watu wa Hudini kuwa zimesheheni ananuani na namba za akaunti.

"So what we do now?" Jimmy aliniuliza.

"We find a loophole.!" Nilimjibu huku nimeanza kung'oa gari.

"What is that?" Jimmy aliniuliza tena.

"This bank account, this adress amd this woman, Winnie... that's our loophole!" Nikamjibu huku nikitabasamu na kuingiza gari barabarani tayari kurejea Hardstrasse.

Nilikuwa na hakika kabisa bila shaka anuani hii, yaani jengo lile ambalo tunaishi pamoja na namba ya benki account ambayo Winnie alinipatia zilikuwa zinatosha kabisa kujua ni nani ambaye yuko nyuma ya hili suala. Na nikimfahamu mtu huyo, ndio wasaa ambao nitafahamu hasa kwa nini mzee alinitaka kuja hapa Zurich. Nini ambacho alitaka nikione.



Itaendelea….


Habibu B. Anga 'TheBold'
To Infinity and Beyond
 
Si ana cheupe wake huyo ila nyie wanaume tamaa zimewazidi
Na nyie mmezidi kuwa wazuri sana
Nafsi ni shida sana inatamani kila kitu
Ukipata mweupe unataka mweusi ukipata mnene utataka mwembamba Mara mwenye chura Mara nini sijui yaani
Wanaume tumeumbwa Mateso Mateso kuhangaika [emoji443] [emoji444] [emoji442] [emoji442] [emoji443] [emoji444] [emoji445]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom