Vipepeo weusi season 2: From Zurich with rules

Vipepeo weusi season 2: From Zurich with rules

tapatalk_1519472923336.jpeg


VIPEPEO WEUSI


SEASON 2 – FROM ZURICH WITH RULES



EPISODE 27

Majengo ya chuo kikuu cha Zurich yalikuwa yanapendeza haswa. Yalikuwa yanaakisi kwa uzuri kabisa umahiri wa stadi za uhandisi wa majengo wa karne ya kumi na tisa. Muda mchache uliopita nilikuwa nimemtumia Winnie ujumbe mfupi wa maandishi kumfahamisha kwamba nimeshafika hapo chuoni na alinijibu kwamba nimsubiri kwenye eneo la kuingilia kwenye Campus ya chuo ambayo lina sanamu maarufu sana la kutambulisha chuo hiki. Ilikuwa ni sanamu ya mwanamke aliyekaa juu ya jiwe huku akiwa amejitanda kwa shuka upande mmoja huku upande mwingine wa kifua ukiwa wazi titi moja likionekana. Mkono wa kulia kulikuwa na sanamu nyingine ya mwanaume ambaye naye pia alikuwa amekaa juu ya jiwe akiwa kifua wazi na huku amejifunika na shuka kuanzia kiunoni. Sanamu hizi zilikuwa zina umaridadi wa kuvutia mno kwa macho kutokana na kudhihirisha ustadi wa sanaa ya ufinyanzi ambayo ilitamalaki mno kwenye nchi za ulaya kwenye karne ya kumi na saba, kumi na nane na karne ya kumi na tisa.

Chini ya viambaza vyenye kushikilia sanamu hizi kulikuwa na maneno yaliyoandikwa kwa herufi kubwa katika lugha ya kijerumni, “UNIVERSITAT ZURICH ZENTRIUM” yakimaanisha “Zurich University Center” kwa umombo.

Nilisogea mpaka kwenye benchi dogo la kumpumzika ambalo lilikuwa karibu na sanamu hizi. Nilikuwa nimeomba kuonana na Winnie ili nimuhoji maswali kadhaa ambayo nilihisi kuwa yanaweza kunisaidia. Kwa siku mbili zilizopita nilikuwa nimekesha kuchambua nyaraka nilizonazo nikijaribu kutafuta uhusiano kati ya zile nyaraka nilizonazo na namba ya akaunti ya benki ambayo Winnie alikuwa amenipa. Mwanzoni nilihisi ingekuwa kazi rahisi tu lakini kwamuda wa siku mbili nilikuwa kama nazunguka mbuyu tu hivi. Waliondaa nyaraka zile walikuwa wamefanya kazi ya umaridadi sana kuficha uhalisia wa wahusika wake. Ni kama ambavyo nilikuwa nimemueleza Jimmy kuhusu ‘shell companies’. Kampuni moja ilifichwa ndani ya kampuni nyingine kivuli na nyingine ndani ya nyingine vivyo hivyo tena na tena.

“where is your bodyguard?”

Nilisikia mtu akinisemesha, nikainua shingo kutazama.Nilitabasamu, alikuwa ni Winnie akinitazama kwa kutabasamu na kisha kukaa pembeni yangu pale kwenye benchi.

“bodyguard?” nilimuuliza huku nikijifanya kana kwamba sikuelewa anaumuongelea nani.

“yes, your bodyguard... that serious guy!”

Nilimuelewa kabisa kwamba alikuwa anamuongelea Jiimy na alikuwa anaongea kwa utani tu.

“he is not my bodyguard… he is a friend!” nilimjibu huku natabasamu.
 
Winnie alionekana kuwa nilivyomuomba tukutane alitegemea kwamba ningekuja na Jimmy kama siku ile ya kwanza. Hata mimi nilitamani kuja na Jimmy. Nilikuwa nafurahia kuongozana nae huku mtaani kwasababu ni kawaida kuwa unapata ujasiri fulani hivi ukizurura mitaani sehemu ya ugenini ukiwa na mwenyeji wa eneo hilo. Lakini Jimmy siku moja iliyopita alinieleza kwamba hawezi kuendelea kuishi na mimi kwenye lile jingo la Hardstrasse. Ati kwamba hajazoea maisha hayo… kwamba anarudi mtaani. Nilielewa wazi kabisa kwamba kuna kitu Jimmy anakificha, kuna sababu ya huu uchokoraa wake, au labda kuna kitu kilimtokea huko nyuma kwenye historia yake… kuna sababu fulani hivi ambayo inamfanya aishi mitaani. Sikutaka kumbana kwa maswali na kumuhoji ni nini hasa kinamsibu, huu haukuwa muda sahihi. Nilihitaji akili yangu kwa sasa kujisumbua kung’amua hiki kilichonileta hapa Zurich.
Tulikubaliana na Jimmy kwamba kila siku jioni nitaweza pizza kwenye boksi na kuiacha nje ya mlango wa nyuma wa jengo lile la hardstrasse. Kama nitakuwa namuhitaji anisaidie chochote kile basi nitaweka karatasi wenye ujumbe ndani ya boksi hilo la pizza.

“what’s up?” Winnie alinisalimia baada ya kukaa kwenye benchi.

Sikumuuliza kama alikuwa ametokea mazoezini ama vipi lakini kwa muonekano wa namna ambavyo alikuwa amevaa alionekana kama vile ametoka ‘gym’. Alikuwa amevalia ‘leggings’ ya rangu ya kijivu ndefu… suruali fulani nyepesi ya mazoezi yenye kushika maungo ya mwili. Juu alikuwa amevaa fulana fupi nyeusi ambayo nayo ilikuwa inabana mwili kiasi.
Macho yangu yalikosa pazia na kushindwa kujizuia kukodolea mwili wake na namna ambavyo ulikuwa umepangika vyema na kuvutia. Hakika alikuwa ni mrembo haswa.

“how have you been?” hatimaye nilimsalimia.

“Great.. how are you?”

Tulisalimiana na kuongea maongezi madogo ya hapa na pale huku nikijibaraguza kujaribu kumuonyesha ni kiasi gani nilikuwa nimekipenda chuo chao na kadhalika. Hatimaye nilianza kumueleza namna ambavyo kwa siku mbili zilizopita nimekuwa nikihangaika kujaribu kutafuta undani wa namba ya akaunti ambayo alikuwa amenipa bila mafanikio yoyote yale.

“how can I help?” aliniuliza.

“I want to know anything that you know about this account number… holders name, the bank and anything else that could be helpful.!” Nikamjibu.

“you couldn’t figure it out yourself? Its very easy.. come here!” Winnie aliongea na kuchukua simu yake na kuanza kubofya.

Nikajivuta na kusogea karibu yake. Akafungua kwenye uwanja wa kuandika ujumbe mfupi na kisha kuiandika ile namba ya akaunti ambayo alinipa juzi.


AECD0210000000693123456
 
Winnie akaanza kunionyesha umahairi wake wa masula ya benki ambayo alikuwa anasomea hapo chuoni.
“You see… this is IBAN.!” Alianza kuongea

“what is that.!” Nikamuuliza

“International Bank Account Number,!” alinijibu huku anatabasamu kwa mimi kushindwa kutambua kitu rahisi hivyo.

“ok ok… continue!”

Akaendelea kunieleza kwamba namba zote za akaunti za benki za kimataifa zinakuwa na ‘digits’ ishirini na tatu ambazo zimegawanywa katika makundi mawili. Namba nne za kwanza zinajulikana kama “Header” na namba kumi na tisa zinazofuata zinajulikana kama “BBAN”.

“what is BBAN” nilimuuliza tena huku nikijihisi mbumbumbu hasa kwa haya maswali yangu.

“that’s a Basic Bank Account Number.” Winnie alinijibu tena huku anatabasamu.

“Ok ok..!”

Winnie akaendelea kunieleza kwamba katika akaunti hizi za kimataifa, tarakimu zile nne za mwanzo kwenye akaunti hizi za kimataifa ambazo ndio zinaitwa ‘Header’, tarakimu mbili za mwanzo zinatumika kutambullisha nchi ambayo akaunti hiyo ipo. Kwa hii namba ya akaunti ambayo alinipa ni herufi ‘AE’ ambayo Winnie alinieleza kwamba ni ‘ISO country code’ ya nchi za United Arabs Emirates (UAE). Kisha akanieleza kwamba herufi nyingine mbili ambazo zinafuata, yaani ‘CD’ zilikuwa ni ‘check digits’.
Winnie akaendelea kunieleza kwamba zile tarakimu kumi na tisa ambazo zinafuata ambazo zinajulikana kama BBAN nazo zinagawanyika kwenye sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ina tarakimu tatu baada ya ‘Header’ ambapo kwa hii namba yetu ya akaunti ni 021. Alinieleza kwamba hii inaitwa ‘Identifier’ na inatumika kutambulisha benki ambayo akaunti hiyo ipo.

“so which bank is it in this case?” nilimuuliza Winnie.

Winnie alianza kubofya bofya simu yake akitafuta kitu Fulani, nikamuona akifungua file ambalo linamfululizo wa namba na kisha akanijibu.

“It’s Citi Bank.”

Baada ya hapo akaendelea kunieleza kuwa zile ‘digits’ kumi na sita ambazo zinafuata ni namba ya akaunti ya mteja kwenye hiyo benki husika. Winnie akamaliza kueleza.

“are we together?” akaniuliuza huku anatabasamu tena akijua kabisa kwamba siwezi kuwa nimeelewa kwa asilimia mia.

“only half of it!” nikamjibu huku nikitabasamu pia na kukuna kichwa.
 
Japo maelezo ya kina na ya kiufundi ambayo alikuwa amenipa nlikuwa sijayaelewa sawa sawa lakini nilikuwa nimepata mwanga juu ya hii akaunti. Kwamba akaunti hii inamilikiwa na mtu ambaye yuko UAE katika tawi la Citi Bank.

“Is there a way we can know the account holder’s name?” nilimuuliza

“yes ofcourse.!” Winnie akaitikia na kasha kuanza tena kubofya simu yake.

Sikujua alikuwa anaangalia nini lakini baada ya kama dakika mbili hivi akanionyesha jina la mwenye hiyo akaunti.

“Here!” akasogea karibu yangu kunionyesha.

“Dr. Athumani R. Chande.”

Moyo ulinilipuka ghafla. Nilijiuliza kama ni majina tu yalikuwa yamefanana au huyu ambaye nilikuwa namfikiria ndiye?

Nilikuwa nafahamu kwamba Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanzania, ndugu Chande Ramadhan Chande ambaye pia ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Jumuiya ya The Board alikuwa na watoto watatu. Mtoto wake wa kwanza wa kiume, Jamal Chande alikuwa ni mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam. Mtoto wake wa pili wa kike, Khadija Chande alikuwa ni mbunge wa jimbo la Dodoma mjini. Na mtoto wake wa mwisho wa kiume, Athuman Chande alikuwa anaishi uarabuni na sikuwahi kufuatilia hasa alikuwa anaishi nchi gani.
Nilijiuliza kama ulikuwa ni mfanano tu wa majina au alikuwa ni yeye haswa.

“are you ok?” Winnie aliniuliza.

“I think I know who this is!” niliongea bila kumuangalia Winnie. Macho yangu bado nilikuwa nimeyakaza juu ya kioo cha simu ambako alikuwa ananionyesha jina la mwenye ile akaunti.

“Who is he.?” Winnie aliniuliza huku nikianza kuhisi taharuki kwenye sauti yake.

“He is the son of our first Prime Minister!” nikamjibu kwa kifupi tu nikimtazama safari hii.

Winnie alitoa macho kweli kweli kwa taharuki. Aliachama mdomo kama vile alitaka kuoongea kitu lakini alishindwa. Alibaki amenikodolea macho kwa mshangao.

“What’s going on Ray?” kwa mara ya kwanza nilihisi mtetemo wa woga kwenye sauti yake.

Nahisi alianza kuelewa ni kwa namna gani labda amejikuta amejitumbukiza kwenye suala zito pasipo yeye mwenyewe kujua. Sikujua nimjibu nini. Kama nimwambie ukweli au ni maelezo gani ya maana nimpe.
Nikiwa nimekodoa macho bado nikitafari nini cha kuongea, mbele yetu pale tulipokaa ng’ambo ya barabara kulikuwa na taxi imesimama. Japo nilikuwa sijatilia maanani sana lakini nilihisi kama ile taxi imesimama pale kwa muda mrefu kuzidi kawaida.

“For how long has this car been here?” nilimuuliza Winnie huku nikumuonyesha ile gari.
 
“a long time… why?” Winnie aliniji bu huku ananitazama kwa udadisi.

Nilianza kupata hisia mbaya juu ya hii taxi. Nikakaza macho kuitazama. Nikatazama dirisha la siti za nyuma ya abiria. Nilihisi kama kuna sura ya mtu ambaye namfahamu. Nikaanza kuinuka taratibu. Nikaanza kupiga hatua taratibu kwenda pale barabarani ambako taxi ilisimama kando.

“Ray! Are you ok?” Winnie aliuliza

Sikujibu kitu, niliendelea kupiga hatua taratibu kuifuata ile taxi huku macho nimeyakaza dirisha la siti ya nyuma ya abiria. Kadiri nilivyokaribia ndivyo ambavyo ilizidi kuwa dhahiri kwamba kwenye ile siti ya nyuma kulikuwa na mtu ambaye namfahamu japo hata kwa sura.
Niliendelea kupiga hatua za taratibu mpaka kufika kama umbali wa mita tano tu kutoka mahala ambako taxi ilikuwa imepaki. Ndipo hapa ambapo niling’amua mtu Yule kwenye siti ya nyuma alikuwa ni nani.

Ni jamaa yule yule ambaye nimemuona mfululizo kwa siku kadhaa zilizopita, mapokezi ya Radison Blu Hotel, kwenye eneo la tukio la Luke alipopigwa risasi, na eneo la tukio ambalo pia Ivanka alipigwa risasi. Jamaa Yule Yule, mwenye kovu upande mmoja wa sura, kofia ya pama rangi ya kijivu kichwani na koti refu jeusi.
Tuliangaliana kwa kukaziana macho kwa karibia nusu dakika. Nilikuwa Napata hisia kwamba nimewahi kumuona huyu mtu… lakini sikuweza kukumbuka ni wapi. Nikapiga hatua nyingine tena mbele kuifuata gari lakini mara moja taxi iliondokakwa mwedo wa kasi. Kichwani nilikkuwa najiuliza ni nani huyu mtu? Anahusika vipi na mfululizo wa haya matukio? Yuko hapa kumfuatilia Winnie au mimi?
Nillibaki pale nikiitazama mpaka ilipopotea kwenye upeo wa macho yangu… niliweza kuishika kichwani namba ya ile taxi, ZH 45789.

“Ray! Are you ok?” Winnie alikuwa amesimama na kuja mpaka hapa nilipo.

“Come with me!” Nilimshika mkono Winnie na kuanza kuondoka pale kwa haraka.


Itaendelea…

Habibu B. Anga ‘The Bold”
To Infinity and Beyond
 
VIPEPO WEUSI

SEASON 2 – FROM ZURICH WITH RULES


EPISODE 28


“where are you taking me?” Winnie alilalamika huku anajaribu kujitoa mkono wake kutoka katika mkono wangu.

“I think you are in great danger!” nilimwambia tena kwa mara nyingine.

“Danger from what? You keep saying that..!”

Nilikuwa nashindwa kupata maneno sahihi ya kumueleza Winnie ili anielewe. Yule jamaa mwenye kofia ya pama ambaye alikuwa kwenye taxi dakika chache zzilizopita alikuwa amenifanya niwe na wasiwasi sana juu ya usalama wa Winnie. Kwa kiasi kikubwa rohoni mwangu nilikuwa naamini kwamba anahusika kwa kiwango fulani na vifo vya Lukena Ivanka. Watu ambao siku chache tu baada ya kuonana na mimi walipoteza maisha. Sikutaka Winnie naye aende na maji.

“I have strong reasons to believe that the man who was in that car is the one who has been following you..!”

“How do you know that?”

Nikajikuta Napata tena kigugumizi cha nini hasa nimwambie. Tulikuwa tumetembea mpaka eneo la ndani ya chuo baada ya kumvuta kutoka pale nje kwenye benchi ambalo tulikuwa tumekaa awali. Sikuwa nataka kumwambia Winnie masuala yote kuhusu mimi au ni nini hasa kilikuwa kinaendelea. Kwanza kwa sababu sikutaka aniogope na pili sikuona busara ya kumueleza siri hizo mtu ambaye bado sijamjua kwa undani. Lakini nilikuwa naona kabisa kuna hatari mbele yake.

“I belive that man was involved it two deaths that happened this week.!”

Winnie alitoa macho na kuachama mdomo huku akijiziba kwa kiganja cha mkono.

“Whaaat??” Winnie alitaharuki huku amenitolea macho.

“Two shootings happened this week and two people were killed and I have strong reasons to believe that guy was involved.!”

“Do the poliece know about this?”

“No! probably not..!”

“Then we should inform the police!”

“No no no! we can’t do that..”
 
“Why not?”

Nilijikuta Napata tena kigugumizi nini hasa nimwambie. Nilijua jibu ambalo nitampa lazima litaleta madhara kwenye huu ukaribu tulio nao.

“aah… you see, aah!” kigugumizi kilikuwa kimenishika roho ikisita kutamka nilichokuwa nataka kumwambia Winnie. Nahisi Winnie alikuwa ameona kusitasita kwangu na alianza kupata wasiwasi.

“what is it Ray? Why you don’t want us to inform the police?” aliniuliza huku ananiangalia kwa macho ya mashaka.

“Winnie… I think the police believe that I did it.!” Nilimjibu kwa uso mkavu huku nikimtazama usoni nione namna ambavyo atakuwa amepokea taarifa hii.

Winnie alitoa macho kama vile mjusi aliyebanwa na mlango. Alinitazama kwa mshituko kama vile ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuniona. Nilimuona akianza kusogea nyuma taratibu kama vile ananiogopa.

”Winnie look… I have nothing to do with it, I swear to God… it’s a long story, I will explain!” niliongea hukunikijaribu kumsogelea ili niweze kumtuliza wasiwasi ambao ulimpata ghafla juu yangu/ ubaya wa kujitetea ni kwamba kadiri unavyojitetea ndivyo ambavyo unaonekana una hatia. Kila hatua ambayo nilikuwa napiga kumsogelea naye alikuwa napiga hatua moja nyuma.

“I am sorry Ray but I think I have to inform the police about this… someone is following me for the past three weeks and now you are telling me that two people died… I am sorry but I have to talk to the police about this!”

“Please Winnie don’t do that!”

“I am sorry Ray!”

Winnie aliongea kwa sauti ya unyonge huku akiniangalia kwa huruma na kisha akugeuka na kuondoka kwa hatua za haraka. Nilimtazama anaondoka mpaka nikijilaumu moyoni. Kwa nini nimemueleza suala hili? Lakini sikuwa na chaguo lingine… nia yangu ilikuwa ni kuokoa maisha yake. Japo ulikuwa ni wendawazimu kumuomba tuondoke wote na mimi lakini sikuwa na njia nyingine ya kumsaidia zaidi ya hiyo. Nilijihisi kuwa atakuwa salama zaidi akiwa pamoja na mimi kule hardstrasse kuliko kuwa peke yake hapa chuoi. Hivyo nilipaswa kumuambia kuhusu vifo vya Luke na Ivanka ili aelewe juu ya ukubwa wa hatari ambayo ilikuwa juu ya maisha yake.
Nilijua fika kabisa nilikuwa nimebakiwa na muda mchache sana, kama kweli Winnie atakwenda kuongea na polisi kuhusu kufuatiliwa na watu wasiojulikana pamoja na taarifa yoyote kunihusu mimi basi muda wowote na sekunde yeyote nitatiwa korokoroni.

Nilitembea mpaka barabarani na kupanda taxi kurejea hardstrasse. Kichwani nilikuwa na mambo mawili ambayo nilikuwa nimeyapa kipaumbele kwa sasa. Kwanza ni taarifa hii ambayo nimetoka kuifahamu kwamba akaunti inayotumika kumlipa Winnie inamilikiwa na mtoto wa Marehemu Waziri Mkuu Chande ambaye anaishi uarabuni, lakini suala la pili nilikuwa nimedhamiria kufahamu japo lolote kuhusu Yule jamaa mwenye kofia ya kijivu ya pama ambaye nahisi amekuwa akifuatilia nyendo zangu.
 
Nilipofika tu kwenye jengo la hardstrasse na kuingia ndani moja kwa moja nikachukua simu yangu na kuanza kuperuzi mtandaoni. Nilikuwa nahitaji kujua taarifa za kutosha kuhusu Dr. Athumani R. Chande mtoto wa marehemu waziri mkuu Chande ambaye pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya The Board. Kitu pekee ambacho nilikuwa nakijua haraka haraka kumuhusu ni kwamba anaishi uarabuni kwa miaka mingi sasa.

Nilifungua simu na kuanza kuperuzi kwa kuandika jina lake kwenye mtandao wa google na kisha kuanza kupitia matokeo ambayo yaliletwa. Habari nyingi ambazo zilikuwa zimeletwa baada ya kubofya kitufe cha kutafuta zilikuwa zinakuhusu marehemu baba yake, nyingine zilimuhusu dada yake Khadija Chande mbunge wa jimbo la Dodoma mjini, habari nyingine zilimuhusu kaka yake Jamal Chande. Niliperuzi karibia nusu saa nzima pasipo kukutana na habari yoyote ile ambayo ilikuwa inamuhusu yeye moja kwa moja.

Nikiwa nakaribia kabisa kukata tamaa ya kuendelea kuperuzi, hatimaye jicho langu lilitua kwenye habari ambayo ilionekana imeandikwa kama siku tatu zilizopita kwenye moja ya blogu maarufu nyumbani Tanzania. Habari hii ilinionyesha pale juu kwamba ndani yake kulikuwa na jina hili ambalo niliandika pale juu kwenye sehemu ya kufatuta, yaani jina “Athumani R. Chande”.
Haraka nikafungua habari hiyo.

Habari ilikuwa inahusu uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa kiwanda cha kuchakata na kusindika gesi (LNG – Liquefied Natural Gas) ujenzi ambao ulikuwa unafanyika huko mkoani Lindi katika kijiji cha Likong’o. habari hiyo ilieleza kwamba uzinduzi huo umefanywa na Mheshimiwa Rais Albert Kafumu kuashiria kuanza kwa ujenzi huo ambao ulikuwa unasuasua kwa miaka kadhaa sasa. Habari iliendelea kueleza kuwa ujenzi huo unafanywa chini ya shirika la mafuta la Tanzania, TPDC kwa kushirikia na kampuni zote za utafutani gesi ambazo zimepewa vitalu nchini Tanzania, yaani kampini ya Statoil, BG Group, Exxon Mobil, Royal Dutch Shell, Ophir Energy na Pavilion Energy.
Jina la Athumani R. Chande katika habri hii liliibuka mahali ambapo habari ilizungumzia kampuni ambayo imepewa zabuni ya kufanya ujenzi huo wa kiwanda. Kampuni hiyo iliitwa PETROFAC Emirates ambayo ilikuwa inatokea huko nchi za Falme za Kiarabu. Kwa mujibu wa habari hiyo, nilisoma namna ambavyo Rais Kafumu aliimwagia sifa kedekede kampuni hiyo ya PETROFAC kwamba wana uzoefu na weledi wa kutosha kuhakikisha kwamba kiwanda hicho kinajengwa kwa umaridi, viwango vya kimataifa na ndani ya muda mfupi.
Kwenye hotuba hiyo pia Rais Kafumu aliongea kwamba alikuwa anajivunia kuona kwamba kuna mtanzania ndani ya bodi ya wakurugenzi ya PETROFAC na hii ilikuwa inampa imani kwamba hatimaye sasa “rasilimali za nchi zinakuwa kwenye mikono sahihi”, rais alinukuliwa na habri hiyo.

Habari hiyo pia ilimnukuu Dr. Athumani Chande mwenyewe akiongea na wanahabari na kuwaeleza kwamba alikuwa anajisikia fahari kampuni yao kumteua yeye kuja kusimamia mradi mkubwa kama huu hapa nyumbani. “Najisikia fahari na kuwa na imani kwamba sasa rasilimali za nchi zinaelekea kuwa katika mikono sahihi.” Dr. Chande alinukuliwa.
Kwa haraka nikagundua namna ambavyo Dr. Chande alikuwa amechagua maneno. Alikuwa ametumia maneno yenye kufanana kabisa na yale ambayo Rais Kafumu alikuwa ameyatumia katika hotuba yake.

Nikahisi labda ni bahati tu kufanana uchaguzi huo wa maneno, lakini pia upande mwingine wa akili ulihisi labda kulikuwa na maana iliyojificha. Nikahifadhi wasiwasi wangu huu akilini.

Nikatoka kwenye blogu hiyo na moja kwa moja kwenda kufungua tovuti ya kampuni ya PETROFAC Emirates. Katika tovuti ya hiyo kampuni moja kwa moja niliingia kwenye sehemu ambayo ilikuwa
 
mahususi kwa ajili ya historia fupi za viongozi wa kampuni hiyo na uzoefu wao. Kulikuwa na orodha ndefu sana lakini nilishuka chini mpaka nilipolikuta jina la Dr. Athumani Chande. Kama ilivyo kwa majina mengine yote kulikuwa na maelezo mafupi tu kwa kila jina, hasa hasa kuhusu elimu yake, uzoefu wake na mawasiliano yake ya barua pepe na simu ya ofisi.
Maelezo yalionyesha kwamba Dr. Athumani Chande alikuwa ni msomi mkemia wa mafuta, yaani Petro-chemist ka umombo akiwa na shahada ya uzamivu ambayo aliipata katika chuo kikuu cha Aberdeen nchini Uingereza. Maelezo hayo pia yalionyesha kwamba Dr. Chande amewahi kufundisha masomo ya kemia ya mafuta katika Khalifa University kilichopo Abu Dhabi lakini pia amewahi kuwa mjumbe wa bodi ya maendeleo ya Elimu nchini Rwanda. Hapa nilishituka kidogo. Rwanda? Kwanini? Huyu si Mtanzania. Tena anaishi uarabuni kwamiaka mingi? Haya mafungamano na Rwanda yameokea wapi?
Sikuweza kupata jawabu la haraka lakini moyoni nilikuwa nimefarijika kiasi kwamba angalau nilikuwa nimemfahamu huyu mtu… mtu ambaye akaunti yake ya benki inatumika kumlipa Winnie, binti ambaye amepewa kazi ya kufanya usafi na kuhifadh barua kwenye anuani ambayo inatumiwa na kikundi cha siri cha HUDINI.

Kuna muda ambao ukikaribia kufanya uvumbuzi fulani unasikia kabisa damu inachemka na mwili wote unakusisimka. Ndivyo ambavyo nilikuwa najiskia muda huu.
Kazi ambayo ilikuwa imebaki mbele yangu ilikuwa ni kuunganisha nukta ili nipate kuelewa Dr. Athumani Chande alikuwa na mfungamano gani na HUDINI mpaka kumtumia kufanya miamala hii ya benki.

Nikiwa natafakari hatua za kuchukua kutokea hapa mara simu yangu ikaita… nikatupa jicho kwenye kioo, alikuwa ni Winnie.

“Haloo.!!” Nilipokea simu harak haraka

“…hallo…”

“Hallooo.!!” Niliita tena kwa mara ya pili. Sauti ya Winnie ilikuwa chini sana na nilikuwa namsikia kwa mbali mno.

“…ray…” aliongea tena taratibu. Safari hii niligundua kwamba alikuwa ananong’ona kwa makusudi. Alikuwa hataki kuongea kwa sauti kubwa.

Moyo ukanilipuka.

“Winnie are you ok?” nilimuuliza huku nahema

“someone is following me!” Winnie alinong’ona tena

“where are you right now?” nilimuuliza huku nasimama haraka haraka mkono mmoja nikishikilia simu na mkono mwingine nikitumia kuvaa viatu.

“I am at Freatch West Street!” alijibu tena kwa kunong’ona.

“What? What are doing at Freatch West? I told you to…. Damn it!” nilijikuta nashindwa hata kumalizia sentensi. Winnie anafanya nini Fretch West? Nilimuacha chuoni na nilimueleza kwamba awe makini mno kwa sababu nilihisi kabisa yuko hatarini. Sasa hivi ananiambia kuwa yuko mitaa ya Freatch West
 
amefuata nini? Kwa makisio hii ilikuwa yapata kama saa moja na nusu au saa mbili usiku. Anafanya nini Freatch West?
“where exactly are at?” nikamuuliza

“there is a chinese restaurant that I told about so…!”

“I know the place, stay put. I am on my way!” sikutaka hata amalize sentensi. Alivyonitajia tu mgahawa wa kichina nilielewa kwa hakika kabisa ni wapi alikuwa.

Nilihisi ni lazima Winnie atakuwa kwenye hatari kubwa mpaka kunipigia simu mimi ukizingatia namna ambavyo tulikuwa tumeachana pale chuoni masaa machache yaliyopita. Sikutegemea kama angewasiliana nami tena au kutaka kuwa karibu nami. Kwa hiyo kama mpaka imemlazimu kunipigia simu mimi tena ni lazima atakuwa kwenye hali ya hatari haswa.
Kitu ambacho kilikuwa kinaniumiza kichwa ni nini hasa kilimpeleka huko Freatch West? Sikutaka kupoteza muda, nikatoka nje na kutafuta taxi tya kunipeleka Freatch West.


Itaendelea…


Habibu B. Anga ‘The Bold’
To Infinity and Beyond
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom