Vipepeo weusi season 2: From Zurich with rules

Vipepeo weusi season 2: From Zurich with rules

tapatalk_1519472923336.jpeg



VIPEPEO WEUSI


SEASON 2 - FROM ZURICH WITH RULES



EPISODE 23




Nilikuwa tena kwenye taxi kutokea mtaa wa Affolterntrasse ambako nilienda kutazama nyumba yenye anuani ambayo ilikuwa kwenye zile nyaraka nilizonazo. Kitu pekee ambacho niliondoka nacho kwenye ile nyumba ilikuwa ni ile picha ukutani. Picha ambayo inawaonyesha yule binti Erica muhudumu wa pape hotelini lakini kwenye nyaraka zangu picha yake imeandikwa jina la Ivanka, pamoja na Luke utotoni mwao wakiwa na mtu ambaye kwenye picha yuko kwenye picha nyingine nilizonazo.

Kuna wazo lilikuwa linanijia kichwani. Kuna taa ilianza kuwaka na kuanza


Niliitazama tena ile picha. Nikaitazama kwa makini kweli kweli. Yes! Huyu ni Erica akiwa mtoto, na huyu ni Luke akiwa mtoto. Na huyu mwanaume ndiye huyu ambaye yuko kwenye picha nyingine tatu nilizonazo. Moja akiwa na Rais Kafumu, ya pili akiwa mahala fulani mtaani na ya tatu akiwa na cheupe na baba yake. Mtu pekee ambaye sikumtambua kwenye ile picha alikuwa ni yule mwanamke. Kwa muktadha wa mantiki na mtindo wa upigaji huu picha ilionekana kabisa ilikuwa ni picha ya familia. Ikimaanisha kwamba Erica na Luke ni mtu na dada yake. Na yule jamaa ni baba yao. Na yule mwanamke ni mama yao.

Lakini kuna kitu ambacho kilikuwa kimenishangaza zaidi. Huyu mtu alikuwa anaonekana kana kwamba ni kijana mno kutosha kuwa mzazi wa kina Erica na Luke. Kwa sababu picha ambayo amepiga na Rais Kafumu inaonekana wazi kabisa kwamba imepigwa miaka ya hivi karibuni.

Nikaitazama tena picha kwa makini. Naam! Taa ilikuwa inawaka zaidi… nilianza kung'amua ile anuani ilikuwa na maana gani. Nilikuwa nahitaji tu kuhakikisha kama ninachokifikiria kilikuwa sahihi.

Nikiwa nimezama sana kwenye kutafakari ile picha mpaka sikujua kama tulikuwa tumefika tayari Haedstrasse mpaka pale dereva taxi aliponishtua na kunirejesha tena kwenye mawazo ya kawaida. Nikalipa na kushuka.

Nilikuwa natembea taratibu kuelekea kwenye uchochoro wa jengo ambao unaenda kwenye mlango wa nyuma ya jengo ambao nimekuwa nautumia mara zote. Nilikuwa natembea taratibu ili nisitoneshe kidonda pale tumboni. Nikakumbuka tena kwamba nahitaji daktari wa kukitazama hiki kidonda kabla hakijanipa madhara zaidi.
Nikakukumbuka tena kwamba napaswa pia kulitazama hili jengo zaidi, floor za juu kuna nini? Na pia The Board walilinunua kutoka kwa nani? Na walinunua kwa lengo lipi haswa?
Hili napaswa kulifanya asubuhi… kwa usiku huu napaswa kupumzika na kuchekecha akili kuhusu Erica, Luke na yule jamaa wa kwenye picha.

Nilipoufikia mlango niliukuta ukiwa umefunguliwa na kuegeshwa tu. Yaani kwamba ulionekana kuwa ulifunguliwa na kisha kurudishwa bila kufungwa tena tofauti na ambavyo niliuacha ukiwa umefungwa. Eidha kulikuwa na mtu ndani au mtu huyo aliingia na kutoka kwa haraka bila kufunga mlango.

Kama ambavyo nilijiapiza kwamba, safari hii sikimbii… nitapambana. Ndivyo ambacho nililifanya. Nilishinda woga wote ambao nilikuwa nausikia muda huu. Nikavuta pumzi ndefu ndani na kuishusha. Kisha nikafungua mlango na kuingia kwa tahadhali.
Pale koridoni kulikuwa na giza kama siku zote kwa hiyo nilitembea kwa kunyata taratibu mno ili nisimgutushe yeyote kama yuko humu ndani. Moyoni nilikuwa najilaumu sana kwa kutofanyia kazi mapema wazo la kuwa na silaha ambalo nilikuwa nalo tangu asubuhi.

"Damn! I really need a gun!"

Nilijilaumu moyoni huku nikinyata taratibu.

Nikiwa nanyata hivi taratibu pale pale koridoni nikaanza kusikia sauti. Sauti ya mtu akigugumia.

Mwanzoni nilihisi labda ni mtu yuko kwenye maumivu lakini niliposikiliza kwa makini niligundua kwamba alikuwa ni mtu analia, alikuwa analia kwa uchungu sana kiasi kwamba alikuwa inaifunda sauti ndani ili isitoke. Sauti iliashiria kwamba mtu huyo alikuwa analia kwa mida mrefu kiasi kwamba sauti ilianza kumkauka.

Nikatoa simu yangu mfukoni taratibu na kuwasha tochi. Hamad.!! Mbele yangu alikuwa Jimmy. Yule chokoraa ambaye juzi waliniokota yeye na Luke. Alikuwa amekaa chini amejikunyata kwa kuinamisha kichwa chake kwenye magoti ambayo alikuwa ameyakunja mpaka usawa wankifua.

Alipoona mwanga akainua kichwa chake kutazama. Usoni alikuwa amelowa machozi chapa chapa. Ule waupe wake wa kizungu ulikuwa umebadilika na kuwa mwekundu usoni kuashiria kwamba amekuwa akilia kwa muda mrefu sana.

"Jimmy!! What's wrong?" Nilitahamaki huku naenda haraka ukutani kuwasha taa.

"Get away from me.!!! Go away.!!" Jimmy alifoka huku analia.

Nilibaki nimepigwa butwaa tu. Jimmy alikuwa na nini? Au amepata habari juu ya kifo cha swahiba wake Luke?

"Look Jimmy, I am really so…"

"You are a jinxy! You are a jinxyyy.!! Jimmy alinikatisha na kufoka kwa hasira huku bado akiwa analia.

"Jimmy! I am sorry, I know Luke was your friend… I am really really sorry mate.!" Nilijitahidi kuongea kwa huzuni na kufariji kwa kadiri ambavyo niliweza.

Lakini nilishangaa Jimmy anainua uso na kunitolea macho kwa mshangao. Alitoa macho kana kwamba amesikia jambo kubwa asilolijua. Aliacha kulia ghafla. Aliinua uso na kunitazama kwa mshangao mkubwa. Mpaka nilianza kuogopa kutokana na mshangao wale usoni.

"What is it.!" Nilijitahidi kumuuliza.

"What did you just said?" Aliniuliza huku anaanza kuninuka.

Nilitafakari kama kwenye sentensi yangu nimeongea kitu chochote cha kukera au dhihaka? Lakini sikukiona… Jimmy alikuwa anainuka taratibu kana kwamba ni chui anajiandaa kurukia windo lake la siku.

"Chill out mate!" Nilijitahidi kumtuliza huku nimenyoosha mkono kuashiria awe mtulivu.

"No no no! What did you just say?"

"I said…I am sorry for Luke's death.!"

Mshangao usoni mwake ulikuwa mkubwa zaidi.

"Whaaaatt! When did this happen?"

"You dont know.?" Nilishangazwa. Ina maana hajui kwamba swahiba wake amefariki leo asubuhi? Kama hajui ni kitu gani kilikuwa kinamfanya alie kiasi hiki kama mtoto mdogo?

"When did this happen?" Aliniuliza tena kwa taharuki.

"Today morning… he was shot! Wait a minute… you dont know anything about this? Then why are you craying?"

Nikamuona anainamisha tena kichwa chini kwa uchungu. Nikaanza kusikia kwikwi. Mara moja akaanza tena kulia na kukaa tena chini sakafuni.

"You are jinxy mate! You are a jinxy!!" Jimmy alilalama huku analia pale sakafuni.

"Jimmy! Whats going on?"

Jimmy anasema kwamba alikuwa hajui kuhusu kifo cha Luke? Kwa nini analia? Na kwa nini kilio kimeongezeka zaidi baada ya kumuambia kuhusu kifo cha Luke?

"Jimmy! What's going on here?" Safari hii nilifoka.

Akainua kichwa na kunitazama cha uchungu.

"My sister died today! She shot.!!" Alinijibu kwa kifupi huku amenikazia macho.

Nikihisi kama jiwe zito limedondoshwa ndani ya nafsi yangu? Dada yake? Ina maana Jimmy huyu chokoraa naye ana dada? Na huyo dada naye ameuwawa leo? Tena naye kwa kupigwa risasi kama Luke?
Lazima kutakuwa na uhusiano.

"Your sister? Who is she… I mean am so sorry! When didi this happen?" Niljikuta napata kigugumizi nisijue ni kitu gani hasa niongee.

"I would rather show you!" Jimmy aliongea kwa hasira huku anainuka. "Lets go!"

"Where? To do what exactly?" Nilihamaki kwa mshangao.

Nini kimempata Jimmy? Nimemuuliza kuhusu dada yake aliyeuwawa badala yake ananieleza kwamba ni bora alinionyesha. Anataka kunionyesha nini?

"Do you want to know or what?" Aliniuliza bila kuniangalia akiwa amesimama kuelekea mlangoni.

"Ofcourse I want to know but…"

"Then lets go!"

Hakunisubiri nimjibu au chochote… tayari alishafika mlangoni na kuufungua kutoka nje.
Sikuwa na chaguo lingine zaidi ya kumfuata japo sikujua tunaenda wapi au anataka kunionyesha nini?

Tulifika barabarabi na kusimamisha taxi kwa mara nyingine tena.

"Freacht West!" Jimmy alimueleza dereva taxi baada ya sote kukwea ndani.

Moyo ulinipasuka. Huo ndio mtaa ambao iko hoteli ya Radisson Blu Hotel ambayo nilifikia siku nilipoingia hapa Zurich. Sikutaka kuonyesha mshangao wangu au kumuuliza Jimmy kitu chochote. Nikasubiri nione mwisho wa hii safari.

Kwenye taxi wote tulikuwa kimya. Kila mmoja akiwaza na kuwazua lakwake kichwani.

Nilikuwa najihisi kama vile niko kwenye "maze". Kana kwamba ni uwanda mpaka wenye mamia ya kuta na mamia ya kona kona na kukiwa na mlango mmoja tu wa kuingilia na kutokea. Ukiwa kwenye maze ukikata kona moja tu isiyo sahihi umekwisha. Utazunguka na kuzunguka ndani yake na kamwe hutouona mlango wa kutokea. Unapaswa kila kona ambayo unaipinda iwe sahihi.

Ndivyo ambavyo nilikuwa najihisi muda huu. Kulikuwa na kona kona nyingi mno za mafumbo na kama nitakosea hata suala moja tu nitajitumbukiza gizani zaidi kuzidi hata giza nililokuwepo kabla ya kufika hapa Zurich.

Tulienda kama mwendo wa dakika kumi na tano hivi tukiwa wote kimya kama mabubu. Taxi ilifika mpaka Freacht West. Tulikuwa kwenye 'blocks' zile zile ambazo ilipo Radisson Blu Hotel.

"Stop here!" Jimmy alimuamuru dereva taxi.

Gari ilipaki mkabala kabisa na Radisaon Blu Hote. Mahala pale pale ambako asubuhi ya leo nilikuja niliposikia kifo cha Luke.

Sasa nilielewa dada yake Jimmy ni nani. Sikuwa na hata haja ya kuuliza.

Safari hii Hoteli ilikuwa imefungwa kabisa. Pale mlangoni kulizungushiwa utepe wa njano wa polisi. Hii iliashiria kwamba mauaji hayo yalifanyika ndani ya Hoteli.

Niligeuka na kumtazama Jimmy kwa kumkazia macho. Kichwani mawazo kadhaa yalipita. Hivi huyu Jimmy ni chokoraa kweli au ni mtu tu amepandikizwa kwa kazi maalumu hapa Zurich?

"So Erica was your sister?" Nilimuuliza kwa hasira huku nahema.

Hasira nilizokuwa nazo ni kwa jinsi ambavyo Jimmy muda wote tangu siku ile wameniokota pale kwenye jengo Hardstrasse alikuwa anajifanya hajui chochote kuhusu mimi au kinachoendelea.

"Her name was Ivanka!" Jimmy alinijibu bila kuniangalia macho ameyalaza kuelekea mbele.

Jimmy alitaja jina la yule binti ambalo pia nililiona kwenye nyaraka zikiwa na picha yake.

Nikijikuta na hasira zaidi, kuchanganyikiwa zaidi lakini pia nikisikia hatia ndani yangu. Watu hawa wawili wameuwawa mara tu baada ya kukutana na mimi. Kwa namna fulani nilihisi kuna uhusiano wa vifo vyao na kukutana na mimi. Nilihisi ndio sababu ya Jimmy kung'aka akisema "you are a jinxy!"

"Jimmy!" Nilimuita kwa utulivu.

Hakugeuka. Aliendelea kukaza macho yake mbele.

"Jimmy! Do you know who I am? I mean before we met… did you know who I was?" Nilimuuliza tena kwa sauti ya utulivu.

"For two years she was obsessed with finding you… I knew this would bring bad luck. But she dint listen… she was too determined to find you!"

Jimmy alinijibu kwa uchungu huku bado akiwa amekaza macho mbele.
Kwa maneno mepesi alikuwa amekubali kuwa alikuwa ananijua kabla hata ya kuonana ile juzi pale kwenye jengo nilipopigwa risasi. Kwamba dada yake Erica, au Ivanka kwa usahihi zaidi… alikuwa na mshawasha na nadhiri ya kunipata. Kwa nini?

Mara ya kwanza baada ya kukuta ile picha kwenye nyumba ya Affolterntrasse nilidhani kwamba Luke na Erica ndio ndugu. Lakini Jimmy anasema Erica ni dada yake? Ina maana wote watatu ni ndugu? Haiwezekani, Jimmy ameguswa zaidi na kifo cha Erica kuzidi Luke.
Uzuri safari hii siko gizani tu peke yangu, bali niko hapa na mtu wa kunipa majibu yote haya ya maswali yangu, Jimmy.

"Jimmy! We need to talk. I need answers.. you hear me? we need to talk… hey take us back to Hardstrasse!"

Nilimuamuru dereva. Kuturudisha tena Hardstrasse. Jimmy hakukaidi. Nilihisi nae alikuwa amechoka kukaa na siri moyoni mwake. Alikuwa anataka hatimae atue mzigo huo alionao moyoni.

Dereva aligeuza gari na kuanza kurejea tulikotoka.

Tukiwa tunaondoka eneo hili. Nilitupa tena jicho pale nje ya hoteli palipozungushiwa utepe wa njano wa polisi. Inaonekana tukio lilikuwa limetokea si masaa mengi yaliyopita. Bado polisi walikuwa wanahoji watu hapa na pale. Na kulikuwa na wapita njia kadhaa kama kawaida wamesimama kushangaa na kupata 'umbea' wa kilichotokea.
Katika mkusanyiko huu wa wapita njia wachache waliosimama kutazama, nilimuona tena yule jamaa… yule jamaa wa asubuhi, mwenye kofia ya pama ya kijivu, koti refu lenye kufika usawa wa magoti, mkononi akiwa na gazeti, Jamaa yule yule ambaye juzi usiku alikuwa ameketi kwenye sofa za mapokezi ya hoteli akisoma gazeti nilipokuwa nabishana na Erica.

Inaonekana alikuwa anaangalia taxi yetu muda wote. Tulipoondoka nilimuona akitusindikiza kwa macho mpaka tulipopotea upeo wa macho yake.

Nikamgeukia Jimmy.

"Wewe mpumbavu leo una maswali mengi sana ya kunijibu!" Nilijikuta na hasira mpaka nimemsemesha kwa kiswahili nikijua kabisa hakuelewa chochote.

Nilitamani taxi ipae na kufika haraka nianze kupata majibu kutokakwa Jimmy.



Itaendelea…


Habibu B. Anga 'The Bold'
To Infinity and Beyond
 
tapatalk_1519472923336.jpeg


*VIPEPEO WEUSI*


SEASON 2 - FROM ZURICH WITH RULES




EPISODE 24


Cheupe,

Haijalishi ni sauti ya kinanda ama kinubi. Haijalishi kama ni sauti ya zumari ama gitaa. Ala murua inaweza kuinua roho ya binadamu, inaweza kuinua na kuitweza katika mawanda ya juu ya nguvu iliyonayo na kumpa ushujaa.
Si lazima muda wote kusikia ala murua kwa masikio ya kawaida. Roho inapohitaji kutwezwa, inapohitaji kuinuliwa, inapohitaji kupata ushujaa… nafsi ndiyo mahala sahihi zaidi pa kusikilizia ala murua.

Roho ikiwa imepondeka unaweza kufumba macho na kuzama nafsini kusikiliza ala murua ya kinubi. Roho yako ikowaimepondeka unaweza kukaa sakafuni ukaegemea ukuta na kufumba macho na nafsi kusikia ala murua ya zumari.

Macho si lazima yaone mpiga gitaa. Na wala masikio si lazima yawambwe kwa mawimbi ya sauti ya kinanda. Ni nafsi ndiyo yenye kuhitaji kusikia ala hii murua.
Fumba macho, kaa sakafuni, egemea ukuta. Acha nafsi iambae kwenye ngazi ifuatayo ya ufahamu. Iachie roho ipate ushujaa. Ushujaa unaohitaji kwa ajili ya kuikoa roho iliyopondeka. Ushujaa unahohitajika kwa ajili ya uendelevu wa mbari ya mwanadamu.

Kila mapenzi yanahitaji ushujaa. Kila familia inahitaji shujaa. Na kila taifa linahitaji shujaa. Lakini ushujaa wahitaji utayari wa kuitoa nafsi kuwa dhabihu. Ushujaa wahitaji utayari wa kuwa kafara.
Na pasipo kafara hakuna ushindi. Na pasipo ushindi hakuna survival.

Uwe na moyo mkuu.

Kwa ushujaa, unyenyekevu na upendo wa hali ya juu,

Ndimi,

Mumeo R.C. Kajuna


Nilivuta pumzi ndefu ndani na kuishusha. Nikakunja kikaratasi chenye ujumbe huu niliouandika na kukiweka kwenye mfuko wa pembeni wa begi langu la nguo.

"What are you writting mate?" Jimmy aliniuliza kwa udadisi.

"Nothing!"

Nilifunga zipu ya begi na kisha kukaa vyema kwenye kiti kilicho karibu na meza.

Tulikuwa tumerudi kwenye jengo la mtaa wa Hardstrasse kama nusu saa hivi iliyopita.
Safari hii hatukuwa tumekaa koridoni pale bali tuliingia kwenye lile lichumba likubwa ambalo mara ya kwanza kufika hapa nilijikutaga nikiwa nimeamka ndani yake. Chumba kile chenye mlango wa kuhitaji kuufungia kwa alama za vidole.

Jimmy alikuwa amemaliza kunijibu maswali kadhaa ambayo nilikuwa najitaji kufahamu. Baada ya kumaliza kunieleza kile ambacho anakifahamu nilihisi kwamba watu ninaokabiliana nao hawakuwa wa kawaida. Naweza kupoteza maisha muda wowote. Ilinibidi niandke ujumbe huo kwa ajili ya Cheupe kama ikitokea chochote kibaya kikinipata na nisipate fursa ya kumueleza kile ambacho kiko moyoji mwangu.

Jimmy alikuwa amenieleza kwamba, yeye na Erica au Ivanka kama ambavyo mwenyewe anapendelea kumuita, ni ndugu wa damu kabisa. Wazazi wao wote wawili walifariki kwa ajali ya gari kipindi wao wakiwa na umri wa miaka sita tu. Baada ya hapo yeye na dada yake walikuwa wakihama hama kuishi kwenye "foster homes" kwa karibia kipindi cha miaka minne mpaka pale ambapo dada yake alipata bahati ya kuasiliwa na familia.

Jimmy alinieleza kwamba Ivanka aliasiliwa na familia ya Mr. Kimberly Delani ambaye ndiye yule jamaa aliyeko kwenye picha zile nyingine nilizonazo moja ikimuonyesha akiwa na Rais Albert Kafumu na nyingine akiwa na Cheupe na mzee wake. Jimmy akanieleza kwamba huyo ndiye Kimberly Delani ambaye yeye pamoja na mkewe Zarah mwenye asili ya mashariki ya kati walimuasili Ivanka.

Jimmy alinieleza zaidi kwamba inaonekana kuwa Mr. Delani na mkewe Zarah walikuwa ni wagumba au hawakutaka kuzaa mtoto wao wenyewe maana Ivanka alipofika huko kwenye familia yao alikuta wakiwa na mtoto mwingine mkubwa zaidi ambaye walimuasili miaka mitatu nyuma. Mtoto huyu ni Luke, yule jamaa ambaye walinikota hapa pamoja siku mbili zilizopita na ambaye ameuwawa leo hii asubuhi nje ya Radisson Blu Hotel.
 
Jimmy alinieleza kwamba kama miaka miwili baada ya Ivanka kuasiliwa aliona mabadiliko makubwa sana kwa dada yake. Mawasiliano yao yalipungua kabisa. Hata utamaduni wao wa kuonana walau kila mwisho wa wiki ulikoma.

Baadae Ivank alichaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Zurich. Chuo hicho hicho ambacho pia Jimmy alikuwa anasoma. Nilishituka kidogo aliponieleza hili kuhusu yeye kusoma chuo

"You went to University??" Nilimuuliza kwa mshangao.

"Yes mate! Why… I look dumb?" Jimmy alitia utani kidogo.

"No no! Not at all… what did you study?"

"Medicine!" Alijibu huku anatabasamu.

"Wooo!! No offince mate but how did you end up homeless?"

"Long story mate! Dont wann' talk about it!"

Fair enough! Sikutaka kumlazimisha anipe historia ya maisha yake kwa sasa. Sikutaka mwishowe aghairi hata kunipa taarifa kuhusu Ivanka na Luke. Japokuwa sasa nilielewa kwamba yeye ndiye lazima ambaye akinitibia lile jeraha la risasi juzi aliponiokota na baadae kupoteza fahamu.

Jimmy aliendelea kunieleza kuwa hata walipokuwa hapo chuo kikuu cha Zurich, Ivanka hakutaka kabisa ukaribu nae. Ilionekana dhahiri kabisa kwamba hakutaka watu wafahamu kuwa wana undugu.

Jimmy akanieleza kwamba kipindi hicho Ivanka yuko chuo, Luke alikuwa amejiunga na jeshi la Uswisi kitengo cha "Kommando Spezialkräfte" (Special Forces Command) akipangiwa kikosi cha Grenadier Command 1 chenye wanajeshi wasiozidi elfu tatu tu nchi nzima ya Uswisi.

Jimmy alinieleza kwamba Delani mwenyewe hakuwa mtu wa kukaa sana pale nyumbani, mara nyingi alikuwa akisafiri nje ya nchi kibiashara.

"What business was he into?" Nilimuuliza.

"I dont know for sure, but I think he was some type of a banker or something.!"

"A banker? Ok.." kichwani nukta ziliendelea kujiunga. Kwanza ile anuani. Zile picha na sasa kujua kwamba yule jamaa wa kwenye picha zote nilizonazo kwamba ni 'banker'.

Jimmy aliendelea kunieleza.

Aliniambia kwamba baadae yakaanza kufululiza matukio ya ajabu zaidi. Kwa mfano Ivanka aliacha chuo na kusafiri kwenda Marekani na kutokomea huko. Luke aliacha utumishi jeshini naye pia kutokomea kusikojukikana.
Pale nyumbani kwao alibaki Zarah na Delani pekee na huku Delani mwenyewe ambaye nae pia muda mwingi analuwa yuko safarini je ya nchi kwa hiyo muda mwingi ni Zarah pekee ndiye alikuwa nyumbani.

Jimmy alinieleza kwamba kama miaka mitatu iliyopita, Delani na mkewe zarah walisafiri na hawajahi kurejea tena mpaka leo hii.

Ili nipate uhakika zaidi nakumbuka nilimuuliza swali,

"Where were they living exactly?"

"Affolterntrasse!" Jimmy alinijibu.

Nikatingisha kichwa kwa kuitikia. Sikuhitaji kumuuliza anuani. Nilikuwa na hakika ni nyumba ile ile ambyo nilienda kuipekua masaa machache yaliyopita. Nyumba ambayo anuani yake iko kwenye nyaraka nilizonazo kutoka kwa mzew wangu.

"So what happened next?" Nikamuuliza.

"Two years ago… out of no where they both came back!"

"Who?"

"Ivanka and Luke!"

Jimmy alijijibu. Alinieleza kwamba miaka miwili iliyopita ghafla tu Ivanka na Luke walirejea.

Kichwani niliikumbuka kwamba miaka miwili iliyopita ndio muda ambao niliidondosha jumuiya ya The Board na mzee wangu kujipiga risasi. Nilihisi kwa hakika kabisa kulikuwa na uhusiano wa matukio haya na kile ambacho kilitokea kule nyumbani Tanzania.

Jimmy alinieleza waliporejea walikuwa na jambo moja tu kichwani.

Jimmy alinieleza kwamba inaonekana walikuwa wanafahamu kwamba siku hizi yeye ni chokoraa anayelala mitaani na walikuwa wanajua namna ya kumpata. Aliniambia kuwa waliporejea walimpa kazi moja kubwa. Walimuonyesha picha yangu na kumueleza kwamba kila siku anatakiwa afuatilie mahali hapa kwenye hili jengo la Hardstrasse mpaka siku atakaponiona nikiingia humu na kisha awape taarifa haraka.
 
Jimmy alinieleza kwamba kazi hiyo ilikuwa ngumu na yenye kuchosha. Kila mara aliwalalamikia Ivanka na Luke kwamba amechoka na hawezi kuendelea tena. Ivanka na Luke walimtishia kwamba wataacha kumpa hela ya chakula na matunzo mengine ambayo alikuwa anayapata. Hakuwa na jinsi ilibidi aendelee tu japo kwa shingo upande.

Ndipo hatimaye juzi, baada ya kusubiria kwa muda wa miaka miwili… alinishuhudia nikiingia ndani ya jengo hili.

"So tell me mate… why were they obsessed with finding you?" Jimmy aliniuliza huku amenikazia macho usoni.

Kwa muda wa dakika nzima nilikuwa natafakari nimueleze nini haswa? Nimdanganye? Au nimwambie ukweli?
Nikimdanganya na akigundua anaweza kupoteza imani na mimi… nahitaji aendelee kuwa upande wangu. Wacha nimueleze ukweli, japo sio ukweli kamili. Ukweli hata nusu tu.

Nilimueleza Jimmy kwamba, mzee wangu alifariki miaka miwili nyumbani Tanzania. Katika karatasi zake za wosia aliacha maagizo yenye anuani ya nyumba ya kina Ivanka na kwamba natakiwa nije kufuatilia.

Nakumbuka aliniuliza kufuatilia nini? Nikamjibu kuwa sijui…

"You are dumb mate. You travelled all the way up here for something you dont know..?"

"I know it sounds stupid but that's it.!"

Jimmy hakunijibu chochote. Alibakia tu kunikodolea machokwa mshangao.

Kichwani niliendelea kuunganisha nukta kuhusu ile nyumba nilienda kuipekekua masaa machache yaliyopita na hizi taarifa ambazo Jimny amenipa. Hisia zangu kwamba nyumba ile ilikuwa haikaliwi na mtu zilikuwa sahihi kama alichonieleza Jimmy ni cha kweli. Kwamba Delani na Zarah wameitelekeza nyumba hiyo kwa miaka mitatu sasa. Lakini kuna kitu kilikuwa hakiniingii akilini. Nyumba ile ilikuwa safi mno na vitu vimepangiliwa sawia. Lazima kuna matunzo yanafanyika.


"So who is taking care of the house… the one Delani and his wife left?"

"Why do you ask that?"

Nikamueleza kuhusu safari yangu kwenye hiyo nyumba siku ya leo masaa machache yaliyopita na nilichokiona na kusababisha wasiwasi wangu kuwa kuna mtu anaitunza.
Nikamueleza pia kwamba niliwahi kuandika barua nikiwa Tanzania kuja kwenye anuani ya nyumba hiyo na ikajibiwa.
Jimmy alibaki kunikodolea macho tu kwa mshangao.

"There must be someone taking care of the house and picking up mails… and that is our lead.!" Nilimueleza.

Jimmy alibaki ananitazama tu. Sikujua anawaza nini lakini nilihisi kabisa alikuwa anajiuliza kichwani "who is this guy". Alinitazama tu kwa karibia dakika nzima kisha hatimaye akaongea.

"Let me take a look at that wound!"

Nikafunua shati tumboni. Nikamuacha akifanya shughuli yake ya kidaktari. Nikaegemeza kicha ukutani. Nikafumba macho.
Kana kwamba nilikuwa nasikia ala ya muziki kwa mbali nafsini mwangu. Ala ambayo ilikuwa inanifanya nizidi kujipa moyo kufumbua fumbo lililo mbele yangu. Kukabiliana na udhalimu mkubwa ambao nilikuwa nahisi umejificha. Japo nilihisi unaweza kugharimu uhai wangu… lakini nilijipa moyo… Kila mapenzi yanahitaji ushujaa. Kila familia inahitaji shujaa. Na kila taifa linahitaji shujaa. Lakini ushujaa wahitaji utayari wa kuitoa nafsi kuwa dhabihu. Ushujaa wahitaji utayari wa kuwa kafara.
Na pasipo kafara hakuna ushindi. Na pasipo ushindi hakuna survival.

Nilitamani usiku ukuche haraka nianze kufuatilia ni nani hasa anayeitunza ile nyumba na kuchukua 'mails' zinazotumwa pale.



Itaendelea...


Habibu B. Anga 'The Bold'
To Infinity and Beyond
 
EPISODE 25



Yalikuwa yamepita karibia masaa mawili tangu tufike hapa mimi na Jimmy. Ilikuwa ni asubuhi ya kama saa nne hivi. Siku ya leo ilikuwa na baridi haswa, kwa hiyo tulikuwa tumevalia masweta mazito na kofia ya mzula kwa ajili ya kujikinga na baridi.

Nilikuwa nasikia auheni kubwa sana pale tumboni kwenye kidonda. Jimmy hakuwa anatania, kitendo chake cha kunikagua kidonda jana usiku na kusafisha alinidhihirishia kuwa yeye ni daktari haswa licha ya huu uchokoraa alionao sasa. Japo kila baada ya dakika kadhaa kichwani swali lile lile lilikuwa linanijia tena na tena, "huyu mtu ilikuwaje mpaka akawa chokoraa?"
Lakini sikutaka kuwahisha mambo, nilidhamiria kusubiri mpaka wakati sahihi ukiwadia nimbabe kwa maswali mpaka anieleze ukweli wa nini hasa kilimtokea mpaka kimfanya awe na maisha haya aliyonayo sasa.

Gari ambayo tulikuwa tunaitumia tulikuwa tumeikodi kutoka kwa kampurufu ya ukodishaji magari hapa Zurich inayoitwa ILOM. Nililipia dola za kimarekani 388 gharama kukodi gari pamoja na kodi kwa ajili ya kuwa nayo hii gari kwa muda wa wiki nzima. Ilikuwa ni gari aina ya Nissan Juke AWD.

Nilikuwa nahisi kwamba katika siku hizi zijazo tutakuwa na mizunguko mingi sana hapa Zurich na sikutaka kutumia usafiri wa umma kwa kuhofia labda kuna uwezekano polisi wakawa wananitafuta kutokana na kifo cha Luke na kunikuta nyumbani kwake juzi na kuwapa taarifa zangu za uongo.

Tulikuwa tumepaki gari ng'ambo ya barabara mkabala na nyumba ambayo juzi usiku nilikuwa hapa kuipekua, nyumba ile mtaa wa Affolterntrasse. Nyumba hii hii ambayo pia Jimmy amekieleza kuwa ndipo ambapo Luke na Ivanka waliishi na wazazi wao waliowaasili, Bwana Delani na mkewe Zarah.

Leo ilikuwa ni siku ya pili tumekuja tena hapa. Siku ya jana tulishinda hapa siku nzima pasipo kuona mtu yeyote akiingia ndani ya nyumba hii.

"Nobody is gonn' come mate!" Jimmy aliniambia tena wasiwasi wake kwa mara nyingine tena karibia ya ishirini.

Hakuwa anaamini kwamba kuna mtu ambaye alikuwa anakuja kwenye nyumba hiyo. Aliamini moyoni mwake kwamba tangu nyumba hiyo itelekezwe na Delani na mkewe hakukuwa na mtu ambaye anaishi humo.

Nilikubaliana naye kwamba pia nilikuwa naamini hakukuwa na mtu anayeishi humo. Lakini nilikuwa na hakika kabisa kuna mtu lazima awe anaitunza. Kwa sababu ndani mwake imepangiliwa maridhawa mno na ni kusafi kana kwamba ni kila siku nyumba hii kuna mtu ambaye alikuwa anaifanyia usafi.

Lakini kuna upande fulani moyoni nilikuwa natamani nikubaliane na Jimmy kwamba hakukuwa na mtu ambaye anaitunza nyumba hii. Nilihisi kama hisia zanhu hazikiwa sahihi tulikuwa tunapoteza muda mwingi sana hapa badala ya kufuatilia taarifa nyingine. Lakini kuna upande mwingine moyoni mwangu ulizidi kunitia moyo kwamba lazima kuna mtu anayefanya matunzo ya hii nyumba. Kwa nini barua ambayo niliandika nikiwa Tanzania kuja anuani hii ipokelewe? Kwa nini ndani kuwe kusafi namna ile? Hapana… nilijipa moyo kwamba hisia zangu ni sahihi?

"If someone comes, then what?" Jimmy aliniukiza.

Nilikuwa sina uhakika sana ni nini hasa nitakifanya kama mtu akitokea kweli na kuingia kwenye nyumba hiyo… ni kipi ambacho nitakifanya.

"Not so sure of what I will do… lets wait and see!"

"You are insane mate… we spend two days out here and you……"

"…quite… look… look.!"

Nilimkatisha Jimmy alichokuwa anaongea na kumuonyesha ng'ambo ya barabara. Kulikuwa na gari imefika na kupaki barabarani nje ya ile nyumba.
 
Ilikuwa ni gari ndogo aina ya Volkswagen Polo nyekundu. Ilisimama barabarani karibu na ile nyumba. Akashuka binti mmoja mweusi, mrefu kiasi… alikuwa amevalia suruali ya jinzi ya buluu yenye kubana na juu alivaa blauzi kama ya rangi ya kahawia. Mkononi alikuwa amebeba mifuko kadhaa… kama mifuko mitatu hivi ya plastiki ya rangi ya maziwa ikiwa na vitu ndani yake kana kwamba ni mtu ametoka supermarket na sasa alikuwa anarejea.

"Is it her?" Jimmy aliniuliza.

"I don't know… let's see!"

Alikuwa ni binti ambaye nilikadiria kwamba hawezi kuzidi umri wa miaka ishirini na tatu au ishirini na nne.
Alifunga mlango wa gari na kisha kuanza kutembea mpaka kwenye ile nyumba. Alipofika mlangoni alisimama na kugeuka nyuma. Aligeuka na kisha kukaza macho kutazama gari yetu. Ilikuwa kana kwamba alikuwa ana mashaka hivi na gari yetu hapa ilipopaki. Aliitazama kwa muda wa karibia dakika nzima. Kisha akageuka na kuingia ndani ya nyumba.

"Shiiiit.! She saw us!!" Jimmy aling'aka

"It dosn't matter… we got her!" Niliongea huku natabasamu.

Nilitabasamu kwanza kwa kusikia raha moyoni kwamba kwa mara nyingine tena hisia zangu zilikuwa sahihi. Lakini pia nilitabasamu kwa kuwa sasa nilikuwa nahisi kabisa nakaribia kutatua kitendawili ambacho kiko mbele yangu na kilichosababishe nije hapa Zurich.

"Let's go!" Nilimuamuru Jimmy

"Wait… wait! Go where?"

"Let's go talk to her..!"

"And tell her what exactly? Nah mate… i will wait here.! You go ahead."

Jimmy alikuwa anagoma kuongozana nami kwenda kwenye ile nyumba. Uzuri sikuhitaji sana uwepo wake japo nilipendelea zaidi kama tungeongozana wote.
Nikawa najiandaa kufungua mlango wa gari ili nielekee kwenye ile nyumba. Lakini kabla sijafungua mlango wa gari nilitupa jicho kwenye ile nyumba na kuona mlango ukifunguliwa. Mlango ulifunguliwa na kisha yule binti kutoka. Alitoka pamoja na ile mifuko yake ya plastiki yenye vitu ambayo alikuwa ameingia nayo. Alipotoka safari hii hakuangalia gari yetu kama mara ya kwanza. Alikuwa anatembea kana kwamba haoni gari yetu hapa ilipo, alitembea huku anatazama chini kwa hatua za haraka mpaka kwenye gari yake.

"Is she leaving? She has been inside for only like two minutes!!" Jimmy aliongea kwa kunong'ona huku wote wawili macho yetu tunaangalia nje kutazama yule binti.

Alifungua mlango wa gari yake, akakwea ndani na kisha kung'oa gari.

Sikupoteza muda. Niliacha gari yake iondoke na kututangulia mbele kama sekunde ishirini tu hivi kisha na mimi nikang'oa gari na kuanza kumfuata kwa nyuma.

Kichwani nilikuwa najiuliza, kwa nini huyu binti ameondoka haraka haraka kwenye ile nyumba? Au ametushitukia? Na kwa nini aogope watu kupaki gari karibu na ile nyumba?
Nilikuwa na hakika kabisa kwamba huyu binti ndiye ambaye anaitunza ile nyumba kama ambavyo kilikuwa na hisia tangu juzi kwamba kuna mtu lazima anatunza ile nyumba.

Kutoka mtaa huu wa Affolterntrasse kuna barabara inanyooka moja kwa moja kama umbali wa kilomita tatu hivi na kisha kukutana na barabra kuu. Ukiifikia barabara kuu ukipinda kulia unakutana na barabara inayoelekea katikati ya mji wa Zurich na kama utapinda kushoto unarudi kwenye maeneo yenye mitaa kama Hardstrasse.

Huyu binti alipofika hapa kwenye makutano ya barabara akapunguza mwendo kidogo na kisha kusimama kabisa. Na mimi nikasimamisha gari nikimuacha umbali wa kama mita mia moja hivi mbele yetu.

Alisimama pale kwa muda wa kama dakika moja hivi kisha akang'oa tena gari.
 
Alipong'oa gari alipinda kona kwenda kulia barabara ambayo inaelekea katikati ya mji wa Zurich. Nami nikapinga kona kulia.
Aliendesha mwendo wa kama dakika mbili hivi kisha akasimama tena. Nami nikasimamisha gari nyuma yake umbali wa kama mita mia moja.

"What the *** is she doing!" Jimmy Aliuliza huku amekodoa macho kwa mshangao.

"She trying to see if she is being followed!" Nikamjibu

Nilishaelewa ni nini hasa huyu binti alikuwa anakifanya. Inaonekana pale kwenye ile nyumba alipotoka kwenye gari yake na kisha kutembea mpaka mlangoni na kugeuka kututazama tayari alikuwa na mashaka na gari yetu. Ndio maana hakukaa sana ndani alitoka na kuondoka. Aliposimamisha gari mara ya kwanza alitaka kuona kama sisi tutampita na hii ingemfanya ajue kwamba atumfuatilii. Lakini kitendo cha sisi kusimama nyuma yake yeye aliposimama kilimuhakikishia kwamba tunamfuatilia. Sikuelewa kwa nini aliamua kusimamisha gari tena kwa mara ya pili.

Ghafla tuliona mlango wa ile gari ukifunguliwa na yule binti kushuka. Aliposhuka alianza kutembea kwa haraka kuja lilipo gari letu.


"Mate… mate! Mate.!! She is coming for us.!" Jimmy alihamaki huku anataka kufungua mlango atimue mbio.

"Hey! Relax.!" Nilimtuliza

Siku zote nimekuwa naamini katika dhamira. Ukiwa na dhamira safi huwezi kudhulika. Unaweza kukutana na simba mwituni na kuangaliana naye macho kwa macho… ukiwa na dhamira safi na huna nia ovu juu yake anaweza kabisa kuona usoni mwako kwamba dhamira yako ni safi. Atageuka na kuelekea njia nyingine na safari yake.
Ndivyo vivyo hivyo pia ilivyo kwa binadamu.

Nilikuwa na uwezo wa kung'oa gari kuondoka kumkimbia huyu binti. Lakini sikutaka kufanya hivyo japo alikuwa anatembea kwa hasira kuja hapa tulipo akionekana dhahiri kabisa anakuja kwa shari.
Siwezi kumkimbia, kwanza nataka kuzungumza naye na pia sina nio ovu dhidi yake.
Nikatulia na kumwambia pia Jimmy atulie.

Yule binti alifika kwenye gari yetu na kugonga kioo cha pembeni kwa nguvu kwa hasira. Nikashusha kioo.

"Pourquoi me suivez-vous.!?" Binti alifoka kwa kifaransa mara tu baada ya kushusha kioo.

"Sorry mam i don't speak french!" Nilimjibu kwa kutabasamu japo kwa kifaransa changu cha kuungaunga nilikuwa nimeelewa kabisa nini ambacho alikuwa anafoka.

"Why are you following me?" Alifoka kwa kingereza safari hii.

Niliweza kusikia lafudhi ya bara la Afrika safari hii alipoongea kingereza. Hii ilinifanya niwe 'curious' zaidi. Africa??

"Sorry mam, we just want to talk!"

Sikutaka kukataa kwamba tulikuwa tunamfuatilia. Niliona ni vyema tu niongee ukweli.

"Then why don't you just come and talk to me! This is a third time you just park your car there and watch me.! Listen, If you don't stop following me I am to report you to the police… Bastard.!!"

Yule binti alifoka na kisha kugeuka kwa hasira kurudi kwenye gari yake.

"Third time?" Nilijikuta akili yangu imenasa neno hilo tu. Hii si mara ya tatu tunamfuatilia. Hii ni mara ya kwanza. Huyu binti anaongea kitu gani?
Nikashuka haraka kwenye gari na kumkimbilia.

"Hey miss! Sorry… Hey miss!" Nilimsimamisha kwa kumshika bega.

"Don't touch me you bastard!" Aling'aka kwa hasira na kuendelea kutembea haraka kuelekea kwenye gari yake.

"Miss I am trying to help you here… listen, your life could be in danger!"

Nilipoongea kauli hii alishtuka kidogo. Alisimama na kugeuka kuniangalia. Alikuwa amefika kwenye gari yake tayari na alikuwa anajiandaa kufungua mlango. Lakini nilipomwambia kuwa maisha yake yako hatarini hakufungua mlango, aligeuka kuniangalia.

"What are talking about?" Aliniuliza akiwa na taharuki usoni.

"You said this is a third we have been following you… No, actually this is our first time… someone else is following you and you could be in great danger!"

"What? Who are you then and why are following me… are you the police?"

"No we are not… we just want to talk to the owner of that house!"

"I am not the owner!" Alinijibu kifupi

Moyoni nilijipa 'tano'. Nilikuwa sahihi. Kuna mtu kazi yake ni kuitunza tu ile nyumba.
 
"I know! I just want to talk.!"

"I don't understand… who are you people?" Akauliza kwa kingereza chake kilichojaa lafudhi ya bara la Africa huku uso wake ukionyesha mashaka aliyonayo juu yetu.

"My name is Ray and that is my friend Jimmy… if you could give us just a few minutes of your time we will really appreciate it… please!"

Nilijitahidi kuongea kistaarabu na unyenyekevu wote uliomo ndani yangu. Nilitaka ajue ni kiasi gani ilikuwa muhimu sisi kuongea naye.

Alinikazia macho kwa muda mrefu kana kwamba alikuwa ananisoma dhamira yangu. Kwa muda wa karibia dakika nzima hakuingea chochote, alikuwa ananitazama tu usoni.

"Ok.!" Hatimaye akakubalikubali.

"Thank you mam! Let's go over there.!" Nilimuonyesha mgahawa mmoja ambao ulikuwa karibu na barabara.

Jimmy hakutoka ndani ya gari na sikutaka kumlazimisha afuatane nasi. Nilihisi kama vile alikuwa hapendi kuonekana hadharani.
Mimi na yule binti tuliingia kwenye mgahawa ulio karibu yetu na kuagiza kahawa.

"Make it quick, am running late!" Yule binti aliongea huku akipiga funda la kwanza la kahawa baada ya kuletwa.

Nilijiandaa kuanza kuongea huku nikipiga hesabu haraka haraka vitu gani vya kumuambia na kumuuliza huyu binti.


Itaendelea…



Habibu B. Anga 'The Bold'
To Infinity and Beyond
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom