Vipepeo Weusi: Mkakati Namba 0034 (Simulizi)

Vipepeo Weusi: Mkakati Namba 0034 (Simulizi)

VIPEPEO WEUSI: MKAKATI NAMBA 0034









EPISODE 21





Baada ya kuingia tu wodi namba tatu, nikaishika vizuri Kamera yangu ya Kodak kujiandaa na ninachotaka kukifanya.! Nikaibonyeza pale kwenye button ya kupigia picha, nikaanza kusikia ikipiga mluzi hafifu kwa mvali "siiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii".. Ilikuwa inakusanya 'chaji' ili iweze kuachia umeme..

Nikaanza kutembea kwa haraka kuelekea mwisho wa wodi kwenye kitanda cha mwisho kabisa ambacho alikuwa amelazwa Kaburu na pingu mkononi.
Cheupe alikuwa ananifuata nyuma yangu.

Yule askari alikuwa bado amekaa kwenye kiti akituangalia tunavyokuja.
Kadiri tulivyokuwa tunamkaribia alizidi kutukazia macho, mpaka tukawa tumemkaribia karibu kabisa.
Kadiri tulivyokuwa tunamkaribia huyu askari sura yake nikaanza kuikumbuka. Huyu ndiye yule askari magereza mtemi aliyekuwa anatupekua siku yangu ya kwanza nilipopelekwa gerezani. Ni huyu askari ambaye aliniambia nibong'oke ili anipekue matakoni. Ni askari huyu ambaye nilipokataa alinishamhulia kwa makofi, ngumi na vifuti vya tumbo.
Hatimaye leo ameingia kwenye 'anga zangu'.! Nikatabasamu na kujisemea kimoyo moyo, "karma is a bitch"

"Hey amruhusiwi huku" akaongea yule askari huku anainuka kwenye kiti.

"Tunaomba picha" Cheupe akamueleza huku mimi nimeinua mkono kumuonyesha kamera bila kusema neno lolote. Sikutaka sauti yangu ya kiume kusikika kuepuka kushtukiwa.

"Hamruhusiwi kupiga picha hapa" yule askari akaongea huku anaanza kunisogelea.

Kidole changu bado kilikuwa kimebonyeza button ya kamera na kwa mbali bado nilikuwa nasikia mlio ikijichaji.

"Picha moja tu!" Cheupe akaongea tena.

"Nimewaambia hakuna kupiga picha" akaongea kitemi yule askari magereza huku anazidi kunisogelea.

Akafanya kosa.

Akanininyokshea mkono ili anisukume kifuani. Kabla mkono haujanifikia nikainua kamera na kumgusisha vile vimoguu viwiki vya nyaya.

"Paaaaaaaaaaaaaaaaaa" mlio mkali wa shoti ya umeme ukalia.

"Mamaaaaaaaaaaaaaaaaaa" yule askari alitoa mlio mmoja tu wa kilio na kudondoka chini na kuanza kupapalika kama mtu mwenye kifafa au mwanamke aliyefika kileleni.

"Ole wake mtu yeyote hata atingishike" Nilimsikia Cheupe anaongea kishujaa kwa sauti ya juu.

Nikageuka kumuangalia. Sijui alikuwa amepaa au ametembea kwa kasi gani, lakini alikuwa amesimama ule tukioingilia.
Uzuri wa hii wodiilikuwa na mlango mmoja tu.

Cheupe hakuwa ameshika kitu chochote, lakini ule mkwara aliowapiga na jinsi tulivyomzimisha huyu askari hakuna mtu ndani ya wodi aliyesogea hata hatua moja. Walibaki wamegansa kama sinema imewekwa "Pause"!

Nikamgeukia tena yule askari anaye gara gara pale chini.

"Hii kwa ajili ya kutaka kunipekua na mingumi uliyonipiga siku ile" nikamgusisha tena vimiguu miwili shingoni. Akapaparika kama kuku bila kutoa sauti. Alikuwa amezirau tayari.

Nikainuka na kumrushia kamera cheupe kama tunacheza marede. Cheupe akaidaka alafu akawanyooshea watu mle wodini kama vile ni bastola.
Tungekuwa tupo kwenye mazingira mengine, lazima ningeangua kicheko kwa huku kujitutumua kwa Cheupe.

Nikamgeukia tena yule askari magereza na kuanza kumshachi mifukoni. Nikazipata funguo.

"Wow wow wow! You full of suprises dogo!" Kaburu akaongea nikiwa namfungua pingu mkononi.

"Shut the *** up!" Nikamfungua pingu.

Nikamnyanyua kutoka kitandani.
Alikuwa anatembea kwa kuchechemea kidogo, hivyo ikanibidi nimuweke mkono wake mmoja kuzunguka mabega yangu ili nimepe 'sapoti' kutembea.

"Taratibu dogo" Kaburu akaongea huku anagugumia maumivu.

Nikamtembeza haraka haraka mpaka kutoka nje ya wodi. Cheupe naye akatufuata na kwenda kufungua mlango wa nyuma ya gari kwa haraka.

Nikaingia na Kaburu siti ya nyuma na Cheupe akazunguma akapanda siti ya mbele.

"Eeeeeeeeehh vipi tena" dereva akang'aka huku anamshangaa Kaburu. Naamini alikuwa anamshangaa zile Nguo zake za kifungwa.

"Endesha gari kum* weweeee" nikamfokea na kumtukana kitemi.

Dereva akashtuka kusikia sauti ya kiume ikitoka kwenye baibui. Tangu atuchukue hotelini ni cheupe ndiye ambaye alikuwa anaongea naye. Mimi nilikuwa kimya muda wote.
Naamini aliposikia sauti ya kiume inaongea kutoka kwenye baibui akaelewa hii ni "ishu siriazi".!

Akang'oa gari kwa haraka tukatoka hospitalini.

"Tunaelekea wapi?" Dereva akauliza kwa woga.

"Msamvu, na nataka uendeshe kwa spidi zote" nikamuamuru.

"Wow! Sikutegemea kama utafanikiwa dogo" Kaburu akaanzisha maongezi.

"Nimekwambia funga mdomi wako" nikamfokea na yeye. Sikutaka aongee chochote mbele ya huyu dereva.

Nikavua tisheti yangu avae juu na avue ile shati ya magereza ya rangi ya chungwa.

Dakika tano baadae tulikuwa Msamvu. Tukashuka kwenye gari. Cheupe akatoa kwenye gari mabegi yetu yale mawili, begi la mgongoni na begi begi kubwa, kisha akampa dereva noti mbili za elfu kumi kumi.
Yuke dereva akapokea huku ametoa macho hakudhani kama "majambazi" sisi tungemlipa.

Tukamsubiri dereva Taxi alipoondoka na kutokomea ndipo tukavuka bara bara kuelekea kituo cha mafuta cha PUMA.

"Unajua hata usingemlipa hela wala asingetudai nauli kwa jinsi akivyoshikwa na hofu" nikamwambia cheupe huku natabasamu tukiwa tunavuka bara bara.

"We are not thieves Ray!!" Cheupe akanishushua.

.

Nikaliona mahala ambapo Issack alikuwa amepaki gari.. Tukatembea kulifuta.

Tulipolifikia, tukaweka mabegi yetu, tukapanda ndani. Nikakaa kwenye usukani, Kaburu akaa siti ya mbele pia na Cheupe akakaa siti ya nyuma.. Nikang'oa gari kwa mwendo wa kasi tukaondoka.

Nikaendesha kwa kasi kama tunaelekea Dar es salaam mpaka kmtukafika maeneo ya Nane Nane kwa mbele kidogo kwenye Chuo kikuu cha Jordan kuna barabara inachepuka kutoka barabara kuu kwenda chuoni, nikaifuata barabara hiyo.

Mbele kidogo nikapaki gari pembeni.

"Ok! Nadhani nimeshatimiza wajibu wangu, now its your turn!!" Nikaongea nikimuangalia Kaburu.

"What unamaana gani?" Kaburu akaongea kwa mshangao.

"Tulikubaliana nikutoroshe gerezani, na nimekutorosha gerezani!! Now its you turn kunipa taarifa kuhusu The Board" nikafoka huku nimemkazia macho.

"Tulikubaliana pia unisaidie kuzipata documents zangu ambazo zimechukuliwa na Obama" Kaburu akoangea kwa hofu na hasira.

"Yeah nitakusaidia ila kabla ya hapo nahitaji taarifa kuhusu The Board"

"Ray documents Obama ameziiba toka jana na tukichelewa zinzweza kufika mikononi mwa The Board na wakiziona hakuta kuwa hata na maana ya mimi kuwa uraiani.. Sacrifice yangu yote ya kukubali kukaa jela miaka miwili yote hii itakuwa haina maana.. Kwa ufupi hizo documents zina mambo Mengi na zina taarifa kuhusu alipo Veronica" Kaburu akaongea wa hofu iliyochabganyika na hasira.

Nikaona huyu anataka kuniletea ujinga..

"Sikiliza Kaburu, nimevunja Sheria za nchi, nimehatarisha maisha yangu, nimehatarisha maisha ya mpenzi wangu na nimehatarisha uhai wa mwanangu... Usianze kuniletea ngonjera!! Unanijua nikiamua kuwa Mafia ni nini naweza kukifanya.. Hizo documents tutazitafuta!! Nipe taarifa za The Board!!" Nikafoka kwa hasira mpaka natetemeka.

"Ray pleeeaase! Naomba uelewe.. Maisha ya veronica yako hatarini mpaka muda huu!! Najua nikikupa taarifa unazotaka huwezi kujisumbua tena kusisaidi.! Please Ray.. Tusaidiane tupate hizi documents.!"
Kaburu akaongea kwa sura ya huruma kabisa mpaka imani inaanza kunijaa.

"Ok! Ok... Ok! Unamfahamu vipi Obama?? Jina lake na mengineyo.?" Nikamuuliza huku nachukua begi dogo la mgongoni kutoka siti ya nyuma na muanza kupekea pekua nikitafuta moja ya zile simu nilizonunua Dodoma.

"Aaaah jina lake hakisi anaitwa... aaah... anaitwa Rashidi... Rashidi aaah Rashidi Namahal! Yes Rashidi Namahala... Pale gerezani alihamishiwa kama mwaka na nusu uliopita! Sijajua alitokea gereza gani ila kama mwaka na nusu uliopita alihamishiwa pale... Kwa hiko kilichotokea na amini alipandikizwa pale na The Board ili afuatilie nyendo zangu.

"Ok.!" Nikamjibu kwa kifupi huku naweka line kwenye simu mojawapo ya zile nilizonunua.

"Unataka kumpigia nani?" Kaburu akauliza kwa wasiwasi.

"Nataka nimpigie mtu wa Usalama wa Taifa naamini wao wanarasilimali watu wa kutosha na ujuzi wa kudili na hili suala" nikaongea huku nawasha simu.

"No no no no! You can't do that.. Ukiwapigia simy na wakizitia mkononi hizo documents wakaona mambo yaliyo ndani ikiwemo location ya Veronica lazima watawasiliana na Idara ya Ujasusi ya Rwanda na wakifanikiwa kumpata Veronica lazima watamfunga gerezani kwa kuasi Idara na ncho yake!"

"Skia Kaburu! Nadhani ni bora walau kama ikitokea bahati mbaya Veronica akatupwa gerezani ina afadhali kuliko The Board wakikuwahi na kumtia mikononi, lazima watamuua!! So namba ukubaliane na hili, Usalama wa Taifa ndio watu sahihi wa kudili na hii ishu.. Wana uwezo wa kumtrace Obama kwa haraka zaidi na kuzipata hizo documents!! Ok??"

Kaburu akavuta pumzi ndefu na kuishusha. "Ok! Do it.

Nikabofya bofya simu na kisha nikabonyeza kitufe cha kupiga. Kama sekunde ishirini hivi simu ikapokelewa.

"Hallo"

"Halo"

"Ray hapa"

"***! Kwanini unanipigia simu si tulikuambia ukitaka tuonane unatakiwa ufanyaje?" Baba bite aliongea upande wa pili wa simu.

"Yeah nakumbuka ila ni suala urgent ndio maana nimepiga simu"

"Kitu gani?? Na nimepewa taarifa na watu wetu wa Morogoro kuwa Kaburu ametorshwa gerezani leo!! Vipi unahusika na hilo??"

"Thats not importnat na naomba mjitahidi hizo habari mzidhibiti zisitokee kwenye media!!"

"Na kwanini tukusaidie kiasi hicho??"

"Kwa sababu ndani ya masaa machache yajayo naweza kuwa na mafaili yenye siri zaa The Board mkononi mwangu"

Baba bite akakaa kimya kwa sekunde kadhaa. Nilihisi hii habari ya mimi kuwa karibia kuoata files za The Board jinsi ilivyomkuna.

"Ok! Unakata nini?" Hatimaye akauliza.

"Kuna askari magereza pale gereza kuu la Morogoro anaitwa Rashidi Namahala au maarufu kama Obama! Jana kuna documents alitakiwa azifiishe mahali lakini kwa makusudi akabadili hizo documents na kuweka nyingine na zile documents halisi bado yuko nazo.. Sasa imani yangu ni kwamba huyu ni kibaraka wa The Board na hizi documents zitaleta kizaazaa kikubwa kikubwa sana.. Kwahiyo naomba mtumie kila mbinu mliyo nayo kumnyakua huyu bwana na kumbana awape hizo documents kabla hazijafika sehemu zisipotakiwa na naomba ukizipata unikabidhi mimi kwasababu zinahusu masuaka binafsi na sidhani kama zitakuwa na faida kwenu huko kwenye Idara." Nikamfafanulia kwa mapana.

"Ok! Ngoja niwasiliane na watu wa Morogoro" akanijibu.

"Na naomba mkizipata hizo documents unisaidie kitu kimoja.. Ndani yake zinaweza kuwa na taarifa nyeti kuhusu mtu Fulani ambaye anatafutwa na marafiki zenu wa Rwanda.. Naomba ufahamu kuwa mtu anayetusaidia kupta mafaili ya The Board anafanya hivi ili kulinda usalama wa mtu huyo anayetamaniwa na wenzenu wa Rwanda.. Lakini sidhani kama ni interest ya Taifa la Tanzania kusaidia taifa la kigeni kudili na 'mizimu' yao.. Kwahiyo naomba utumie busara zako zote na huruma zako zote kulinda usiri wa hiyo taarifa mtayoipata.. Najua interest yenu kwenye hii ishu ni kupata mafaili ya The Board.. Naomba hilo ndilo libaki kuwa lengo kuu moyoni mwako."
Nikaongea kwa mafumbo na busara zangu zote ili kubembeleza huruma ya Baba bite akinde taarifa kuhusu Veronica zisiwafikie Idara ya Ujasusi ya Rwanda.

Nikakata simu. Kisha nikaivunja vunja na kuitupa.

"Ok! Naamini ndani ya masaa kadhaa watakuwa wamemnyakua! Now its you turn Kaburu!! Napataje hizo files za The Board?"

Kaburu akashusha pumzi kwa nguvu.

"Ok! Unakumbuka nilikwambia kuwa kumbukumbu zote za The Board haziwekwi kwenye mifumo wa kompyuta, kwamba taarifa zote zinatunzwa kwenye hardcopy ili kuepuka udukuzi??" Akaniuliza.

"Yes, nakumbuka!" Nikamjibu nikiwa na shauku kubwa.

"Now, kama nilivyokwambia kuwa mtunza kumbu kumbu huyu ambaye The Board wanamuita Book Keeper, ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRBB Bw. Vincent Mallya.. Na kumbu kumbu hizi anahakikisha ziko naye muda wote haziondoki kwenye uwepo wake" akaongea huku anafumba macho na kuangalia juu.

"Sijaelewa una maana gani??" Nikauliza tena kwa shuaku kubwa zaidi.

"Namaanisha documents ziko na Vincent Mallya muda wote"

"Sikuelewi Kaburu"

Akavuta tena pumzi ndefu ndani na kuishusha kwa nguvu.

"I cant believe that am telling you this" Kaburu akafumba macho kwa nguvu kwa woga.

"Stop playing around! Where are those damn files??" Nikafoka kwa shauku.


"Ziko katikati ya jiji la Dar es salaa, maeneo ya Posta kwenye Strong Room ya CRBB makao makuu, Golden Jubilee Tower"

"Whaaaaaatt" nikapatwa na mshituko.

"Yeah! Siri zote kuhusu The Board, wanachama wao, mikakati yao, vibaraka wao na akaunti zao za siri nakadhalika na kadhalika... Files zake zote zipo kwenye Strong Room ya CRBB makao makuu, Golden Jubilee Tower"

Kaburu akajibu huku amefumba macho na kulalia kiti.

"Nakumbuka ulinambia kuwa 'nitazichukua kama naokota dodo kwenye mwembe'??"

"Hiyo ni misemo tu Ray! Ila sasa unafahamu moja ya siri kubwa sana katika hii nchi"

Nikajiinamia kwenye usukani wa gari. "Fuuuucckk!!" Nikatukana kimoyo moyo kwa sauti ya chini.
Strong Room??? Nimefeli akyamungu!! Inyeshe mvua au liwake jua, na hata niwe na miakili kiasi gani... Never never ever, hakuna namna ambayo nitaweza kufanikisha kukanyaga mguu wangu ndani ya strong room ya Benki kubwa kama CRBB.

"This is impossible!! But we need to think of something" nikaongea huku bado nimejiinamia kwenye usukani.

"The only way unaweza kufika kwenye strong room ni kwa kufanya tukio la ujambazi" akaongea kaburu.

"Hey hey boys! Mnafika mbali sasa, huko sasa mnatafutwa mpigwe risasi... Ray please usianze hij mipango ya kiwendawazimu sitaki kuwa mjane kabla hata hujanioa na wala sitaki kumlea huyu mtoto peke yangu.." Cheupe akafoka kwa msisitizo.

Nikainua kichwa kutoka kwenye usukani. Nikajifanya kama sijamsikia Cheupe.

"What are suggesting?" Nikamuuliza Kaburu.

"Kuna Mzee namfahamu.. Ni Mzee wa kipemba anaitwa Abdul Zakir lakini tumezoea kumuita 'Chifu'... Matukio Mengi makubwa yanayotokea Dar na kufanikiwa yeye ndio mchora ramani, yeye mwenyewe huwa hajihusishi kuyatekeleza, yeye ni mtu wa mikakati tu.. So tukiongea naye anaweza kutoa mawazo mawili matatu ya kujenga" anakongea kaburu.

"Anaishi wapi?"

"Anishi Dar, mbagala Kizuiani"

"Let's go see him" nikaanza kuwasha gari.

"Honey?? What the *** are doing?? Siamini kama unafikiria kitu cha hatari kiasi hicho!" Cheupe akafoka.

"Babes! Skia, umesikia kuwa mafaili yako strong room.. Hebu twende tukaongee na huyo Mzee tusikie idea zake.. Kama idea za mbaya naachana nazo"

"Na kama ni idea nzuri?? Utafanya tukio la ujambazi??"

"I don't know what am going to do honey.. I'm still thinking" nikaongea huku naanza kuendesha gari. Sikutaka kusubiria jibu lake, niliona jinsi alivyokuwa amenuna.


******************

Ilikuwa inapata saa tatu na nusu usiku, na ndio tulikuwa tumewasili mbagala kizuiani.

Tulipofika barabara kuu pale kizuiani, tulikata kushoto kama tunaekekea kwenye kambi ya Jeshi la JWTZ.
Katikati hapo kukikuwa na mtaa mkubwa tu.. Kaburu akanielekeza nisimamishe gari kwenye nyumba Fulani hivi nzuri tu na kwa haraka haraka nikagundua ndio ilikuwa nyumba pekee yenye uzio wa ukuta hapo mtaani.

Tukapaki gari na kushuka. Tukaenda mpaka kwenye geti la nyumba na kugonga.

"Naniiiiiii??" Sauti nyororo ya like iliitikia kutokea ndani.

"Wageni wa Mzee" aliitikia Kaburu.

Mara geti dogo likafunguliwa na msichana fulani akachungulia. Akikuwa amejitanda kanga na nyingine ameifunga kama hijabu.

"Salaam aleykum.!" Yule bint akatusalimia.

"Aleykum salaam" Kaburu akaitikia kwa ufasaha mpaka nikshtuka.

"Niwasaidie nini?"

"Tuna shida na Mzee"

"Baba Fahimu amepika" yule binti akatujibu kwa lafudhi ya pwani.

"Nenda kamuamshe mwambie Eric yuko hapa"

"Baba Fahimu akipumzika hataki mtu kumsumbua kumuamsha!"

"Sikia binti kama nikondoka hapa, na kesho Chifu akijua kuwa Eric alikuja na haukumuamsha, nakuapia walahi kesho hiyo hiyo anakutwanga twalaka urudi kwenu" Kaburu akamchimba mkwara.

"Karibuni ndani" yule binti akatupisha getini tuingie.
Nikahisi kuwa Kaburu aliongea kwa mafumbo na walielewana na yule binti kuwa tuko hapa "kikazi".

Tukakaribishwa kwenye sebule kubwa iliyokuwa ina kila aina ya mikogo ya kiarabu.
Yule binti akatuacha na kwenda vyumbani.

Kama dakika Tatu baadae, kutoka vyumbani mwenyeji wetu akawasili sebuleni.

Alikuwa ni Mzee wa makamo tu wa kama miaka 62 tu hivi. Alikuwa na ndevu ndefu za wastani zenye mvi chache.
Alikuwa amevalia msuli na singlendi, na ingawa ilikuwa usiku kichwani alikuwa amevaa baraghashia.

"Ericccccccc" yule mzee akahamaki kwa mshangao na furaha.

Kaburu akainuka wakakumbatiana kwa furaha.

"Siamini macho yangu ati" yule Mzee akaongea kwa furaha zaidi. "Na hawa kina nani?" Akaukiza.

"Chifu hawa wanajambo Fulani wanahitaji hekima yako"

Chifu akaelewa Kaburu akichomaanisha.

"Karibu ofisini, karibuni"

Akaanza kutuongoza kutoka pale sebuleni kuelekea kwenye korido.
Tukaifuata korido mpaka mwishoni kulikuwa na chumba. Akakifungua tukaingia "ofisini".

"Karibuni sana.. Karibuni"

Chifu akatukaribisha "ofisini" kwake. Hiki chumba ambacho mwenyewe alikiita ofisi ndio labda ilikuwa ofisi pekee duniani ambago haina viti wala meza.

Kulikuwa na zuria zuri la manyoya manyoya kimetandika kuenea kwenye chumba kizima.
Alafu kukikuwa na mito mito ya kuegemea kila pahala.

"Aiseee! Eric tuna Mengi sana ya kuongea ila kwanza niwasikilize vijana" akaongea Chifu baada ya wote kuwa tumekaa chini.

"Mzee kwanza pole sana kwa kukusumbua usiku wote huu" nikafungua maongezi 'kisiasa'.

"Usijali kijana, shida hazina majira! Kuwa huru tu, nieleze kinachowasibu" Chifu akanijibu.

Nikaona hakuna haja ya kuzunguka mbuyu. Huyu ni 'profesheno'.

"Chifu, hapa unapotuona tuna changamoto kubwa sana inatukabili, na ili tupate suluhu inatupasa tufanye jambo moja gumu sana"

"Jambo gani kijana?" Akauliza.

"Tunahitaji utusaidie tuingie strong room ya CRBB mako makuu" nikaongea bila kupepesa macho.

Chifu aliganda ananiangalia bila kusema chochote kwa takribani dakika nzima. Sijui alihisi nimekosea kuongea kwahiyo ananosubiri nosahihishe. Au labda alikuwa anatafsiri nilichoongea. Vyovyote vile lakini naamini hakudhani kama nitamueleza suala la "kiwendawazimu" kama hili.

"Mnahitaji kuingia Strong Room ya Makao makuu ya CRBB??" Akinuliza kwa kafudhi yake ya kipemba.

"Yes! Tunahitaji kuingia Strong Room ya makao makuu CRBB na tunahitaji kufanya hivyo haraka iwezekanavyo" nikamjibu kwa kujiamini nikiamkazia macho bila kuyapepesa hata kidogo.





Iteandelea JUMANNE..
 
EPISODE 21, POST # 3965


Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu @charmie DON SINYORI mij adden
bwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi
 
Pamoja sana Mkuu..

Utamu umekolea ndio maana inaonekana kafupi
Naona sana kaka..ila ungejitaid uwe unaelezea na side zingine

Kwa mfano nyapala alipo mtwata godi na kaburu alipo anzisha mapambano nataman kuona alipambana vipi??

Na pia ile siku sinyorita alipo enda kuadhibiwa sijui aliaje,eiza kilio cha kike au chakiu??

Na pale isack alipo acha gar sheli ,napenda kutazama kam movie walio kuwa wanamfwatilia na kujiuliza uliza


Hii ngoma lazima tutengeneze movie hata kwa kujichanga aisee

Itafunika mbayaaa hii series aisee
 
Tam sana hiii The bold,..ila nina maswali kibao kichwani....ngoja nivumilie yawezekana yakajibiwa mbele kwa mbeleee!
Hongera uko vzuri sana...ndo maana NAKUPENDA Aseeeee...si bure ![emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji39] [emoji39]
 
Vipi mkuu maandalizi ya kumpokea mrembo kutoka Koromije yanaendeleaje?[emoji4]
Taratibu zote zimekamilika japo kuna changamoto za hapa na pale ila hope kila kitu kitakua sawa,japo shemeji yangu bashite hajarudi mjini naamini hakutakua na shida,mkuu niombeee nisije nikamuuliza swali linalo husiana na vyeti vya kakake.😵😵😵😵😵😵
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom