Vipepeo Weusi: Mkakati Namba 0034 (Simulizi)

Vipepeo Weusi: Mkakati Namba 0034 (Simulizi)

Nilipotea kwa muda online, kakimeo kakngu kalianguka kakavunjika kioo na kwa jinsi nilivopata shida kuzisaka hizi episodes humu ndani nikaona niwasaidie na wana ndugu wengne najua itasaidia wachache..


EPISODE 15 IPO KWENYE POST YA 3431

EPISODE 16 IPO KWENYE POST YA 3432

EPISODE 17 IPO KWENYE POST YA 3488

EPISODE 18 IPO KWENYE POST YA 3556

EPISODE 19 IPO KWENYE POST YA 3603

EPISODE 20A IPO KWENYE POST YA 3791 (YENYE MAMBO YA KIKUBWA)

EPISODE 20B IPO KWENYE POST YA 3921

EPISODE 21 IPO KWENYE POST YA 3965

EPISODE 22 IPO KWENYE POST YA 4013
 
1daf863dc8089ef33d0b7292c04210f0.jpg
 
VIPEPEO WEUSI: MKAKATI NAMBA 0034





EPISODE 22





Zilikuwa zimepita takribani siku mbili tangu tulipoenda Nyumbani kwa Chief siku ile usiku.

Licha ya kutushangaa kuhusu azma yetu ya kutaka kuingia strong room ya makao makuu ya banki ya CRBB lakini mwisho wa siku alikubali kulifanyia kazi suala letu na alituomba turudi baada ya siku mbili.

Kwa siku mbili zote hizi tulikuwa tumefikia katika lodge Fulani hivi ndogo maeneo ya sinza na hatuku toka nje kwa siku zote hizi. Kila kitu tulifanyia ndani. Chakula tuliagiza ndani na kila kitu.

Nilikuwa nimefanya mawasiliano na Issack na alinieleza kuwa wameshafanikiwa kumtoa Godi gerezani kwa dhamana. Nilochokuwa nasubiri sasa ni kujua mpango ambao Chifu ataupendekeza ili niweze kujua tunawezaje kumtumia Godi katika timu yetu.

Kaburu naye alikuwa nasi. Bado tulikuwa tunasubiri mrejesho kutoka kwa Baba Bite ili kufahamu kama amaefanikiwa kuzipata documents zake ama la. Na namna pekee ambayo ningeweza kufahamu hili ni kwa kuonana na watu wa usalama kwa kutumia njia waliyonielekeza siku ya kwanza kwa kwenda duka la vitabu la Stolastika maeneo ya Mlimani City.
Nilichokuwa nasubiri, nilitaka kwanza nijiue mpango utakaopendekezwa na Chief ili nikienda kuwaona watu wa Usalama Wa Taifa kama kuna jambo lingine ambalo tunahisi kuwa watu wa usalama wanaweza kutusaidia katika huu mpango wetu basi niunganishe humo humo.

Ilikuwa inakaribia kabisa mida ya saa sita mchana na nilikuwa namalizia kujiandaa ili niende Nyumbani kwa Chief pamoja na Kaburu. Cheupe atabaki hapa lodge.

"So itakuwaje kama chief akipendekeza njia pekee ya kufika Strong room ni kuivamia bank?" Cheupe akaniuliza nikiwa namakizia kuvaa.

"Obviously siwezi kufanya tukio la ujambazi lakini nadhani itabidi tuangalie nini mbadala wake tunaoweza kufanya badala ya tukio la ujambazi" nikamjibu huku nachukua begi la mgongoni.

"Be careful Ray, please! Usifanye kitu au maamuzi ya ajabu huko tafadhalu"

"Siwezi kufanya jambo la ajabu mama, uamuzi wowote nitakao ufanya nitazingatia maslahi yako na mtoto! Kwahiyo relax mama" nikambusu cheupe na kuanza kuondoka.

"Kilala heri baba!"

"Thank you!"

Nikatoka nje ya chumba na kwenda kumgongea Kaburu. Baada ya hapo tukakwea kwenye gari na kuondoka.

Kama nusu saa hivi baadae tulikuwa tumewasili nyumbani kwa chief na tulikuwa katika kile chumba chake ambacho mwenyewe anakiita 'ofisi'

Baada ya salama na mazungumzo ga hapa na pale hatimaye tukaanza kujadili kilichotuleta hapa.

"Kijana! Lile suala lako nimelishughulikia kwa kiasi fulani hivi na nimefika mahala pazuri kidogo" chief akaongea huku anasogeza karibu makaratasi fulani hivi aliyokuwa ameyaweka pembeni.

"Hii ni ramani ya jengo zima la Golden Jubilee Tower" akatandaza kwenye zuria katatasi fulani ndefu ya mchoro wa jengo.

Akaanza kutuonyesha namna mpangilio wa vyumba na maofisi katika jengo hilo.

CRBB wenyewe walikuwa wamechukua 'floor' nne za kwanza za jengo. Jengo zima kwa ujumla wake lilikuwa na jumla ya ghorofa 12.

Akatueleza kuwa strong room yenyewe kwenye jengo hili iko chini kabisa kwenye 'basement' ya jengo.
Watu kadhaa kwenye makao makuu walikuwa na 'access' na strong room na watu ambao walikuwa na access hiyo ya moja kwa moja walikuwa ni meneja wa hapo makao makuu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji mwenyewe Bw. Vincent Mallya.

Wafanyakazi wengine wachache walikuwa na access lakini walikuwa mpaka wapate kibali cha Meneja au Mkurugenzi Mtendaji.

.

Chief akatuelekeza pia namna ambavyo kuna 'procedure' ambayo ni standard kama kwenye majengo mengine yote ya ghorofa kuwa lifti alikuwa haishuki mpaka chini kwenye basement.
Ili ufike chini kwenye basement, inabidi ushuke kwa kutembea kutoka 'ground floor'.

Chief pia akatoa makaratasi mengine ambayo sikujua aliyapataje lakini naamini aliyapata kutoka kwenye kampuni iliyofanya 'installation' ya strong room.
Hapo akatuonyesha namna mfumo wa ile strong room ulivyo, sensors zake, milango, na kadhalika.

Baada ya hapo akaanza kutueleza kuhusu mfumo wa ulinzi wa benki, washika funguo za strong room na mambo mengine Mengi sana ya ulinzi 'uliotukuka' hapo makao makuu.

"Kwahiyo kijana kwa ufupi hicho nilichokueleza ndicho unachotakiwa kukijua kabla ya kutakabkuvamia strong room ha pale makao makuu" chief akaongea huku anakusanya makaratasi yake na kuyakunja kunja kurudisha pale pembeni.

"Kwa hiyo pendekezo lako ni nini Chief" nikamuuliza.

"Unahitaji timu! Tena timu ya watu wazoefu ili kufanikisha huu mpango"

"Kwa maneno mengine unapendekeza tuvamie benki" nikamuuliza.

Chief akatoa macho na kunishangaa. Alikuwa kama haamini nimetamka hayo maneno.

"Kijana! Utawezaje kuiba fedha za benki tena kwenye strong room bila kufanya uvamizi??" Akaniuliza kwa mshangao.

"Well, ishu ni kwamba hatutaki kuiba fedha za banki" nikamjibu huku natabasamu kwa kujishtukia. Nilijishtukia kiasi maana mpaka sasa tulikuwa hatujamueleza ukweli wa tunachotaka kukifanya kwenye strong room.

"Atiiiii??" Chief akashangaa na kumkodolea macho Kaburu.

"Chief... aaaah ni kweli.! aaah hatutaki kwenda kuiba fedha kwenye strong room!! Kuna makabrasha fulani muhimu sana yapo humo na ndiyo hayo tunataka kuyachukua" Kaburu akamfafanulia.

"Sasa mimi percent yangu ya mgao naipataje kama kumbe mnaenda kuiba mikaratasi!! Maana nilijua nitaongeza nyumba nyingine ati??" Chief akaukiza huku bado akiwa na mshangao mkubwa.

"Well, utatueleza tukulipe kiasi gani kwa huu msaada wako na sisi tutajitahidi upate hiyo hela" Kaburu akajaribu kumpoza Chief kuwa hafanyi kazi hii bure.

"Kwani hayo makaratasi yanahusu nini?" Akauliza chief.

"Ubaya ni kwamba hatuwezi kukueleza yanahusu nini.! Lakini yana thamani kubwa na tukiwa nayo mkononi, huyo tunataka kumpelekea hakutakuwa na shida yoyote kuhusu kutoa kiasi chochote cha fedha"

"Eric wewe unajua utaratibu wangu! Kwenye kazi yoyote nikichora 'racket' nachukua asilimia kumi ya mzigo unaopatikana... Sasa hapa mananipa mtihani ati.! Maana nashindwa kujua asilimia kumi ya makaratasi!! Mimi hilo niwaachie nyinyi sasa, tutasaidiana hili lifanikiwe na naamini hata niangusha kunipa kile ninachostahili kukipata inshallah"

.

"Haina shaka kabisa mkuu! Ondoa wasi wasi kuhusu hilo" Kaburu akaendelea kumtoa hofu Chief.

Uzuri kwa namna ambavyo niliwasoma, nilihisi kabisa Kaburu na Chief wamefanya kazi nyingo pamoja huko siku za nyuma, kwahiyo hii walau ili rahisisha kupata kuaminiwa na Chief.

"Naweza kuazima hii michoro niende nayo?" Nikamuomba zile ramani na jengo la Golden Jubilee Tower na ile karatasi inayoonyesha mfumo wa strong room jinsi ulivyo.

"Hainq shida kijana" Chief akakunja yale makaratasi na kunikabidhi.

Baada ya hapo tukaagana naye na kuanza Safari ya kurejea lodge Sinza.

"So what are you thinking??" Kaburu akaniukiza tukiwa kwenye gari.

"Hatuwezi kuingia strong room.!" Nikamjibu kwa mkato tu.

"Huwa nadhani hakuna jambo linalokushinda Ray! Kwanini hili ulikatie tamaa mapema hivi?"

"Well, moja ya vitu ambavyo mtu yoyote makini anapaswa kuvifahamu ni kujua mahali gani unapaswa kuchora mstari.. Haijalishi una akili au ujuzi kiasi gani, lakini hutakiwi kujifanya wewe ni 'almighty'.! Lazima kuna vitu vitakuwa nje ya uwezo wako na mfano mzuri ni hili.. Tukijifanya tukavamie benki, kumbuka benki ina ulinzi mkali, tunaweza kujikuta tunapigwa risasi na kukosa vyote!! Na tusitake kujifanya kuwa tunaweza kutumia mbinu za kiakili akili kuingia kwenye vault.. Hayo mambo yako kwenye sinema tu!! Haya ni maisha halisi na uhalisia uliopo mbele yetu ni kwamba hatuwezi kuingia ndani ya vault"

"Kwa hiyo unapendekeza nini?? Au tuwapa tu taarifa Usalama wa Taifa Wamalize hili suala wao wenyewe??" Kaburu akaniuliza.

"Tatizo hao Usalama wenyewe siwaamini.. Wakizipata hizo documents mkononi mwao sidhani kama watatimiza ahadi yoyote ile tukiyokubaliana.. We need to get those by ourselves.. Na pia kuna vitu nataka kuviona kwenye hizo files" nikamjibu huku najaribu kufikiria vitu kadhaa kichwani.

.

**************

Tulikuwa tumewasili tayari lodge Sinza na wote watatu tulikiwa chumbani kwetu tunajadili nini cha kufanya.


"Sijaelewa bado, kwahiyo tunagive up au tunawaachia watu wa Usalama Wa Taifa??" Cheupe akauliza.

"Well nadhani Ray atueleze anachofikiria" Kaburu akaongea huku ananiangalia kwa kuniinjoi.

Nahisi alikuwa anajua ni kiasi gani kichwa kilikuwa kinaniwaka moto kufikiria nini cha kufanya.
Tangu tumetoka kuonana na Chief kuna idea kadhaa nilikuwa nazifikiria lakini nikikuwa bado sijaamua ni ipi inafaa zaidi kuitekeleza.

"Wow! Wow, wow hahaha" nikajikuta nafurahi peke yangu baada ya wazo moja kukaa sawia kichwani mwangu.

"What is it" wote wakaniuliza.

"I got it.! Hahahah.. I got this" nikaongea huku nachukua funguo za gari na kuanza kuinuka.

"Hey ndio utuambie sasa What is it" Cheupe akauliza tena huku wananishangaa kama wamemuona mtu aliyechanganyikiwa.

"Tutaongea nikirudi.!" Nikainuka na kuanza kutoka nje.

"Unaenda wapi?" Cheupe akauliza.

"Naenda kutafuta dalali!" Nikawajibu huku natabasamu.

"Dalali?? What the ***" Kaburu akajibu kwa mshangao mpaka akainuka.

"Tutaongea nikirudi" nikatoka nje na kuingia kwenye gari.

Nikaendesha gari mpaka maeneo ya Shekilango. Kuna wajamaa nikawaona wamekaa kijiweni pembeni ya barabara. Nikapaki gari pembeni na kwenda kuongea nao.
Nikawaeleza shida yangu kuwa natafuta dalali.

Tatizo la Dar.. Kila mtu anajifanya "mtoto wa mjini", kila mtu 'dalali', kila mtu "mdananda", kila mtu mjuaji..
Hawa wajamaa nilipowaambia nahitaji dalali, badala ya kunielekeza nampataje dalali, wanaanza kuniuliza nataka nyumba au chumba cha aina gani... Kabla hata sijawaeleza nahitaji nini wanaanza mbwembwe kibao... Sijui kuna nyumba ya mzee nani sijui... Porojo kibao, sijui nyumba 'Kali', ina 'tiles', ina 'jipsamu, choo ndani kwa ndani.. Maneno meeengiii..

Nilikuaa nikigundua tu kuwa huyu 'kanjanja', namwambia tu anipe namba yake, namuahidi 'nitamtafuta', kisha 'nasepa'..

Nikahangaika takribani lisaa lizima.. Mpaka mama mmoja dukani akanipa namba ya dalali anaitwa 'Tunda'... Nilipo mpigia, kwanza nikashangaa kumbe ni 'demu'.. Nikaongea nao kwa uchache tu na kumueleza shida yangu.. Akanijibu kwamba niende ofisini kwake kinondoni.!

Nikajisemea kimoyo moyo, haya ndio mambo mubashara! Hata kama unakuwa 'mpigaji' mjini, basi kuwa mpigaji 'profesheno'.! Walau unaweka na mbwembwe za kuwa na kiofisi kama huyu dada... Sio blah blah za kuharakisha kumwambia mtu "nyumba ina jipsamu".

Nikaendesha gari mpaka Kinondoni Mkwajuni ambapo ndiko ilipo ofisi ya huyu dada.
Dada alikuwa na mbwe mbwe kweli kweli, ukifika tu kwanza unaukizwa kama unakunywa maji, soda au juice, mara uulizwe kama uletewe matunda.. Mezani kuna 'vijarida' vya majengo mbali mbali hapa Dar!

Baada ya mbwembwe kuisha tukaanza kuongea kilichonileta.. Nikamueleza kuwa nahitaji kupanga ofisi. Ila nataka ofisi ndogo tu.. Isizidi vyumba vitatu na sitaki katikati ya mji ndio maana nimekuja kwake.

Tukaanza kujadili hapo nataka ofisi iwe maenao gani ambayo napendelea, ofisi iweje, bajeti yangu ikoje na kadhalika.

Baada ya hapo tukatoka na kuanza kunionyesha ofisi mbali mbali ambazo zinapangishwa.
Tukaenda ghorofa fulani hivi mwembe chai lakini sikupapenda. Sikutaka kuwa na ofisi hapa, huu ndio mtaa niliokulia. Kwahiyo sikutaka kutambulika kirahisi.

Tukatoka hapo tukaenda Mapipa, nako sikupataka! Karibu mno na Mwembe Chai. Akanipekeka Morocco, nako sikuipenda Ofisi kwa kulingana na nikichotaka kukifanya.

Baada ya hapo tukaelekea maeneo ya Makumbusho. Nyuma ya stendi ya daladala, kuna kighorofa Fulani hivi. Akanionyesha hiyo ofisi inayopangishwa.
Hii niliipenda, ilikuwa inakidhi kabisa kile nilichotaka kukifanya.

Akampigia simu mwenye nyumba na kisha tukaenda kuonana naye.
Alikuwa anaishi maeneo ya Sayansi karibu kabisa na mgahawa wa "Pweza Café".

Tukazungumza hapo na mwishoni tukakubaliana nije nilipe kesho kodi ya miezi sita. Mwenyewe alikuwa anataka mwaka mzima, lakini ukizingatia mimi nitaitumia ofisi kwa wiki kadhaa pekee, kwahiyo nikakomaa naye mpaka akakubaki miezi sita.

Tukarudi mpaka Kinondoni ofisini kwa Tunda, nikamuacha hapo na kuondoka kurejea Sinza.

***************

Nilipofika lodge ilikuwa inakaribia saa moja jioni. Ilikuwa kana kwamba walikuwa wananisubiri, maana nililoingia tu, Kaburu akaja chumbani kwetu.

"Naona umerudi.!" Kaburu akaongea akiwa anaingia chumbani.

"Yes! Am back, nimepata ofisi..!!" Nikamjibu huku natabasamu meno yote nje.

"Ofisi??? Unaweza kutueleza what you are up to??" Kaburj akauliza kwa mshangao.

"Ok! Mnajua maana ya neno 'con'.??" Nikawauliza.

"corn?? Si ni nafaka sijui mahindi?? What the f*ck does corn has to do with this" Kaburu akanijibu akiwa amekereka.

"Dumbass!! Sio 'corn' nimesema 'con'... C-O-N, hakuna 'r' katikati" nikamfafanulia.

"Oooohh con!! Yeah.. Si ni utapeli sijui nadhani" Cheupe akadakia.

"Yes! 'con' ni utapeli.. Sasa kuna 'long con', sijui hata kiswahili inasemwaje.. But ndio tunaenda kufanya hiyo, a long con!!" Nikatabasamu huku nawatazama.

"Fafanunua kidogo please!" Cheupe akaongea huku ameweka kisura cha huruma.

"Look! Obviously hatuwezi kuingia strong room makao makuj CRBB.. So that means hatuwezi kufika files zilipo.. Sasa kama hatuwezi kuzifuata files zilipo.. Inabidi tufanye files zitufuate sisi tulipo"

"Whaaaat?? How are you going to do that??" Kaburj akaliza kwa mshangao kama ameona jini.

"Wait and see!! You guys are going to fucking love this one" nikaongea na kutoa tabasamu kwa raha kabisa.








ITAENDELEA JUMATANO..
 
EPISODE 22, POST # 4013


Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu @charmie DON SINYORI mij adden
bwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom