Vipepeo Weusi: Mkakati Namba 0034 (Simulizi)

Vipepeo Weusi: Mkakati Namba 0034 (Simulizi)

And..

Upo sahihi sana kusema hakuna The bold bila Nifah na hakuna Nifah bila The bold... Coz unajua wengi hawajui role kubwa anayo play Cheupe wangu mpaka simulizi na makala hizi murua zinakamilika..

She is simply a super woman! Am very lucky..
Awwwwwwwww nashukuru kwa kuutambua mchango wangu ktk kazi zako mpenzi wangu.

Wajua hakuna jambo linaloleta faraja kama kuona mchango wako ukithaminiwa.
Na zaidi kuona yule umpendaye anajivunia kuwa na wewe.

Niseme nini zaidi? Nitake nini tena?
The bold wewe ndio kila kitu changu...
Nakupenda sana [emoji8]
 
Cheupe + Kichwa Niffah Ni Cheupe na Kichwa ni The Bold




Nimeamua nitoboe siri Tu nyie watu ni hatari lakini salama nashindwa niwaelezee vipi ila naona mnaweza endesha hata ndege Boing 717 bila kupata mafunzo yoyote yale bila Niffah hakuna The Bold Bila The Bold Hakuna Niffah Na nimewahi kuwaza kitu flani Ety niko tayari kughalamia hii movie hadi nifilisike kuileta kwenye uhalisia ila nikapata maswali mengi tena kwenye akili yangu........... Nikiendelea sana nitaropoka siri nyingi zaidi haya bhana Ukweli usemwe tu The bold Huna mpinzani kwenye Level za Uandishi hapa Tanzania Tumekaa tukaaminishwa kina E Sh: kumbe wapo Wengi Tu na kwa Humu JF Inabidi Tukutengee tu uishi pekee ako sio kwa kujua huku jamani



Salute


Mkuu,mimi kigezo changu kikuu kwa mwanaume ni akili...tena akili haswaaaa (nimewahi kulisema huku mara nyingi sana,hata kabla ya kuwa na The bold)

Sijui wanawake wenzangu wanawezaje kuwa na akina Bashite,mimi siwezi kabisa.

Kwanini nasema hayo yote? Ni vile nina furaha sasa nimempata mwanaume niliyekuwa namuhitaji na zaidi.

Huyu kijana ana akili hadi huwa nastaajabu.
Ujue ukikaa na mtu mwenye akili kuna mambo ya kawaida tu lakini yeye anayafanya tofauti hadi unashangaa.
Au jambo ambalo kiukawaida lingepaswa kuchua muda mrefu kufikiri ila yeye ni fastaaa na yuko sahihi.

Sijui nisemeje ila ni ana akili kuliko hii mnayoiona huku,he is gifted indeed.

Asante mkuu,ubarikiwe sana.
 
Kuna Kitu Pia nilikwambia Usisahau kusubili Lee Super Suprise The bold na sasa hivi nimeongeza List akiwemo Nifah yani kila siku natamani kuifanya na kuiboresha hiyo kitu iweje iweje ila basi tu itatimia soon


Keep In Touch BOB
Wooooooooow,can't waittttttt [emoji39] [emoji39] [emoji39]
Nisingekuwa na huyu kichwa mambo haya ningeyapatia wapi?
The bold give me life [emoji7]
 
Mkuu,mimi kigezo changu kikuu kwa mwanaume ni akili...tena akili haswaaaa (nimewahi kulisema huku mara nyingi sana,hata kabla ya kuwa na The bold)

Sijui wanawake wenzangu wanawezaje kuwa na akina Bashite,mimi siwezi kabisa.

Kwanini nasema hayo yote? Ni vile nina furaha sasa nimempata mwanaume niliyekuwa namuhitaji na zaidi.

Huyu kijana ana akili hadi huwa nastaajabu.
Ujue ukikaa na mtu mwenye akili kuna mambo ya kawaida tu lakini yeye anayafanya tofauti hadi unashangaa.
Au jambo ambalo kiukawaida lingepaswa kuchua muda mrefu kufikiri ila yeye ni fastaaa na yuko sahihi.

Sijui nisemeje ila ni ana akili kuliko hii mnayoiona huku,he is gifted indeed.

Asante mkuu,ubarikiwe sana.
Hivi tukifanya mapumziko Trinads en tobagos kila mtu na Bae/Boo wake kuna utata?[emoji41]
 
bold tupia kitu mkuu wengine tupunguze kaubaridi na wale fans wa arseten wapunguze stress za 10:02
 
VIPEPEO WEUSI: MKAKATI NAMBA 0034






EPISODE 20





Ilikuwa tayari inakaribia majira ya saa tatu kasoro asubuhi.
Nilikuwa kwenye taxi natoka katikati ya mji wa Dodoma naelekea mitaa ya airport kwenye lodge ya Samali ambayo tumefikia.

Kwenye kimfuko cha nailoni nilichokuwa nimekibeba nilikuwa na vitu kadhaa nilivyonunua.
Kulikuwa na kamera aina ya kodak ya kizamani ya kupiga picha mnato (still poctures), Kulikuwa na mkasi, waya wa kuchomeka kwenye cable, kulikuwa na soldering iron (solda waya kama wanavoita mafundi redio/TV), bisibisi (screw driver) na 'gun' ndogo ya kuchomelea solda waya.
Pamoja na vitu hivi, pia nilikuwa nimenunua situ sita za tekno za elfu ishirini na tao kila moja.

Cheupe yeye nilikuwa nimemuagiza aende bank. Kwanza aende kwenye akaunti yake atoe fedha nyingi iwezekanavyo, pia achukue kadi zangu za ATM pia atoe hela nyingi iwezekanavyo. Nilikuwa nataka tuwe na fedha cash walau milioni tano kutokana na mpango niliokuwa nimeupanga.

Dakika kumi baadae tulikuwa tumefika Samali lodge, nikamlipa dereva na kuingia ndani. Nikashukuru kumkuta cheupe naye amerudi.

"Umefanikiwa?" Nikamuuliza.

"Yeah! Nimefanikiwa" akanijibu.

"Umefanikiwa kutoa jumla shilingi ngapi kwenye akaunti yako na kwangu ATM?"

"Milioni tano na laki nane"

"Na vile vitu umenunua vyote?"

"Yeah vile pale! Nguo zetu za kubadilisha, mabaibui mawili na begi la mgongoni" akanijubu huku ananionyesha begi moja kubwa sakafuni na lingine dogo la mgongoni.

"Well done cheupe! Sasa oga kabisa mimi nipe kama dakika kumi na tano nitengeneza 'kombora' langu" nikamueleza huku nakaa kwenye kiti na meza vilivyomo mle ndani.

"Na unaweza kunidokeza hilo kombora unalolitengeneza ni nini?" Cheupe akauliza huku anaanza kuvua Nguo ili aende kuoga.

"You will love it.!! Umewahi kuona kwenye TV kwenye nchi za wenzetu unakuta askari anamkamata muhalifu na kama muhalifu anakuwa analeta usumbufu na kuwa violent huwa wanatoa kifaa fulani hivi muundo wake kipo kama tochi alafu anampiga shoti muhalifu?" Nikamuuliza.

"Yeah! Nishaona mara kibao.. Na akishampiga shoti muhalifu anaweza kupoteza fahamu kwa muda mchache kama dakika moja au mbili hivi.."

"Exactly… Sasa ile inaitwa Taser au kwa jina lingine mtaani wanaita 'stunt gun'! Inatumia mfumo wa kielektroniki kutoa shoti ya umeme ili kumdhibiti muhalifu kwa kumfanya azimie kwa muda mchache bila kumletea madhara mengine.. Ndicho hicho nataka kutengeneza hapa"
Nikamjibu huku natabasamu nikitoa vitu kutoka kwenye ule mfuko wa nailoni na kuviweka mezani.

"Wow! And can you tell me why we need a 'stunt gun'?" Akaniuliza huku anajifunga taulo.

"Utaona kazi yake leo hii hii" nikamjibu huku natabasamu kwa kujidai.

"Ok! Karibu tuoge" akaaongea huku anatembea kwa madaha kwenda bafuni.

"Hahahaha.! Cheupe please usinifanyie kusudi mama, nitageuka kuwa 'Ngoswe' ujue… inabidi nikamilishe hii haraka tuondoke hapa" nikamjibu kwa kicheko.

"Haya shauri yako hahahah" akaingia bafuni.

Japokuwa nilitamani nijumuike naye bafuni, lakini tulikuwa nyuma ya muda. Napaswa kutengeneza hili 'kombora' haraka na kisha tuondoke.

Nikaichukue ile kamera ya Kodak na kuifungua nati kisha kutoa kasha lake la juu.
Kama nilivyoeleza kuwa hii ilikuwa ni ile Kodak ya kizamani, kwahiyo ukiondoa kasha la juu linalofunika kamera unakutana na 'mkanda wa picha' (film). Huu nao nikauondoa na kuuweka pembeni.

Kisha nikandoa kwa uangalifu betri zake. Kamera za Kodak za kizamani zina uwezo mkubwa sana wa kutunza umeme kwahiyo hata ikiwa imezimwa ukigusa gusa ndani bila tahadhari unaweza kupigwa shoti ghafla.

Baada ya kuondoa betri nikafungua nati kadhaa na kuitenganisha pembeni kadi yake ya umeme (circuit board).

Nikageuza kadi kwa nyuma ili niione Capasitor kubwa ilipo.

Baada ya hapo nikachukua nyaya nilizozinunua na kuzinyongorota mizunguko mingi sana ili kutengeneza 'transformer' ndogo ili iniwezesha kuboost voltage.

Wenye kujua kidogo fizikia wataelewa zaidi namna ambavyo unaweza kutengeneza 'transformer' kwa kutengeza 'coil' ya mizunguko ya nyaya.

Baada ya kutengeneza hiki 'kitransformer' nikakiunga na kukichomelea na solda waya kwenye Capasitor kwa utaratibu na ustadi. Kisha nikafunga kwa 'sole tape' vile nyaya ili zisigisane.

Baada ya hapo nikaiondoa buld kwenye kamera. Hii ni ile bulb inayotoa 'flash' wakati wa kupiga picha, umeme mwingi wa kamera unatumika ili kuifanya bulb iwake kwa mwanga mkali na kutoa 'flash'. Kwahiyo nikaiondoa hii bulb.

.

Baada ya hapo nikachukua waya ule unaotumiaka kuchomeka kwenye 'extension cable' na kuunganisha kwenye kifaa cha umeme.

Nikaukata na kubakisha kipisi kidogo chanye urefu wa kama kidole cha mwisho cha mkono.

Kisha nikatumia 'solda waya' kuuchomelea na kuunganisha kwenye nyaya zinazotoka kwenye Capasitor na kupitia kwenye kile kitransfoma.

Baada ya hapo nikatoboa kasha la Kamera vitundu viwili vidogo kuwezesha ile miguu miwili ya waya kupita.

Kisha nikarudishia betri zake na kasha juu nankuanza kuifunga.

Baada ya kuifunga, Kamera ilikuwa na muonekano wa kawaida kabisa, lakini ukitazama kwa makini pembeni unaona vile vumiguu viwili vimechomoza.

Nikamsikia Cheupe anatoka bafuni.

"Its done! Vaa fasta mama tuondoke" nikaongea huku nakusanya vitu.

"Wow! So how does it work?" Cheupe akaukiza.

"Simple tu! Unabonyeza kwa muda mrefu hapa kwenye button ya kupigia picha kisha unagusisha hivi vimiguu vilivyochomoza kwenye mwili wa mtu"

"Yani simpo tu kiasi hicho?" Akauliza tena.

"Yap! Its that simple.. Hebu nipe hicho kijiko" nikamuambia anipe kijiko kilichokuwa kwenye sahani ya 'breakfast' tuliyoletewa hii asubuhi.

Aliponipa nikabonyeza button ya kamera kwa kama sekunde ishirini hivi bila kuiachia.

"Skia kitu hicho" nikamsikilizisha sikioni jinsi Kamera ilivyokuwa inatoa mlio fulani hivi kwa ndani kama mluzi unaosikika kwa mbali.
Ilikuwa ni Capasitor na transfoma 'vinajichaji' kwa kulimbikiza umeme mwingi ili viweze kuuachia.

Kisha nikagusisha vile vimiguu viwili kwenye kijiko.

"Paaaaaaaaaaaaaa" kijiko kilipiga bonge la shoti lililoambatana na mwanga.

"What the fuuuuccck" Cheupe bado alikuwa anaogopa ogopa utadhani nataka kumoiga shoti na yeye.

"Oooohh yeah! Today am going to blow someone to hell..!!" Nikaongea huku nikitoa tanasamu la kifedhuli.

Tukakusanya vitu vyote na kuondoka mpaka mapokezi. Tukalipa hela nankuwaomba watuitie Taxi.

Dakika kumi baadae tulikuwa stendi kuu ya katikati ya mji. Tukaelekea mpaka upande wanaopaki Noah. Nikamvuta dereva mmoja pembeni.

"Nataka unipeleke Moro! Niko mimi na mkewangu tu.. Itakuwa shi ngapi?"

"Wawili tu peke yenu? Daah kibingwa tutafanya mia hansini bro"

"Acha ujinga sasa, mia hamsini wapi? Nakupa mia kamili"

Tukabishana bei hapo kama dakika tatu hivi, mwishoni tukakubaliana laki na ishirini.

"Nataka yendeshe kama umetoka kulazwa Mirembe jana.. Sasa hivi ni saa tatu na dakika ishirini, kabla ya sita kasoro nataka tuwe tumeingia Morogoro" nikamuelekeza nikiwa nafunga mlango.

"Usiwaze kaka mkubwa"

Siti za mbele tulimuachia dereva peke yake, mimi na Cheupe wangu tukakaa siti ya katikati.
Nikamlaza cheupe wangu mapajani alale usingizi aondoe uchovu wa shughuli ya jana usiku, pia na mimi mwenyewe nipate wasaa wa kutafakari mikakati ya namna tutakavyoweza kutekeleza mipango iliyopo mbele yetu.

.

******************

Tulikuwa tumeshawasili Morogoro na nilimuelekeza dereva atupeleke moja kwa moja Chamwino stendi ya hiace.

"Dakika sifuri tu" nikawaaga nikitoka nje ya gari.

Niakenda moja kwa moja mpaka kwa wajamaa Fulani kama kumi hivi waliokuwa wamekaa kwenye mabenchi.

"Niaje wakuu" nikawasilimia.

"Poa Boss! Niaje" wakaniitikia.

"Poa kabisa! Nahitaji wadhamini.!" Sikutaka kuzunguka mbuyu, nikaenda moja kwa moja kwenye point yangu.

"Umepata Boss.! Unahitaji wadhamini wangapi, kesi inahusu nini na unawahitaji lini.?" Akaniuliza jamaa mmoja ambaye ni mtu mzima kidogo kuliko wenzake. Alikuwa na muonekano fulani hivi wa mfano wa wajamaa 'wajuaji wajuaji' uswahilini.. Mwenye amechomekea shati lake ambalo halijapigwa pasi.. Na chini amevaa viatu vyeusi vya 'foengo' ambavyo sijui vilikuwa na miezi mingapi havijapigwa kiwi.

"Kuhusu jina la ninayetaka mumdhamini, kesi yake, na maelezo mengine yote nimewaandikia humu" nikamkabidhi karatasi.
"Pia kuna namba hapo mwishoni mpigie huyo jamaa anaitwa Issack ndio atawalipa hela na maelezo mengine.. Nataka kesho tu huyu mtu awe uraiani so ni vyema muanze process zenu za barua leo.. Na hii hapa muweke vocha" nikazama mfukoni na kutoa noti mbili za elfu kumi na kumpa.

"Usijali boss! Limeisha hili" akaongea kwa kujiamini yule mzee, akazikunja noti na kuweka mfukoni.
Hakuniliza maswali kwanini nimekuja mimi kuwatafuta wao akafu nawaambia mtu mwingine ndio atakuwa nao kusimamia hilo suala, jamaa alikuwa ni mtoto wa mjini haswa.. Alinielewa kuwa nina sababu za kunifanya nisifuatilie hilo suala mimi mwenyewe.

.

"Twende ukatuache Roby Hotel" nikamuelekeza dereva baada ya kupanda kwenye gari.

"Roby Hotel ya mtaa wa mlapakolo?" Akauliza.

"Yes! Ni hiyo" nikamjibu.

Akatupekeka moja kwa moja mpaka kwenye Hoteli fulani ndogo iliyopo katikati ya mji mtaa wa mlapakolo.

Ilikuwa kama saa saba kamili hivi. Nikaona huj ni muda muafaka kabisa kwa sisi kutekeleza mpango wetu.

Tukiwa humo ndani hotelini, wote mimi na Cheupe tukabadili mavazi na kuvaa yale mabaibui cheupe aliyonunua Dodoma.
Tulivaa haya mabaibui katika mtindo ambao yalificha mwili mzima kasoro uso tu.

"Damn! I really hope Kaburj yuko hospitali" nikamueleza Cheupe huku najifunga vizuri kitambaa cha usoni.

"Kwanini una uhakika kuwa atalazwa?" Cheupe akauliza akiwa ameamua anisaidie kufunga kile kitambaa.

"Unajua kipigo cha askari magereza ni tofauti na kipigo cha mfungwa mwenzako.. Askari magereza anapiga kwa tekniki.. Wamefunzwa namna ya kupiga! Wanapiga kwenye vifundo miguuni, magotini na mikononi..!! Lakini kipigo cha mfungwa mwenzako hakina formula, tena ukizingatia kipigo cha Nyapara na waoambe wake.. Kwahiyo nina hakika kama Kaburi alifuata ushauri wangu wa Kumteteta Godi, basi leo atakuwa amelazwa hospitali kubwa ya Mkoa" nikamfafanulia.

"Aisee I hope Mme wangu haujavaa hili baibui bure.. Umependeza though hahahahah" akanitania.

"Acha ujinga hahah!" Nikamgonga kikonzi cha kimahaba.

Nikatoa simu moja kati ya zile sita na kuiwekea laini. Alafu nikampigia Issack.

"Hellow"

"Damn! Kichwa.. I was so worried.. Are you guys ok?"

"Tuko poa kabisa, sijui wewe Issack?"

"Niko poa kabisa.. Mko wapi?"

"Usijali kihusu hilo.. Vipi mazingira yakoje hapo home?"

"Hawa wasenge wananifuatilia aisee.. Kuna gari imepaki hapa nje iko tangu jana haiondoki"

"Ok! Wanafuatilia nyendo zako wanaamini at some point utakuja kuonana na sisi ili watunyakue.. Sasa skia nataka ufanye kitu kimoja..."

"Nakusikiliza kichwa.!"

"Chukua gari sasa hivi endesha mpaka msamvu.. Ukifika pale paki kwenye kituo cha mafuta cha Puma kisha wewe nenda kapande Hiace kwenda mjini.. Ukifika mjini panda hiace kwenda mzumbe.. Alafu ukifika Mzumbe tafuta sehemu upumzike kusubiri maagizo yangu.. Sawa Issack!"

"Nimekusoma kichwa"

Nikakata simu. Kisha nikavunja vunja simu na laini na kuviweka kwenye dustbin.

"Mzumbe unataka akafanye nini?" Cheupe akaniuliza.

"Haendi kufanya chochote!" Nikamjibu huku natabasamu.

"Whaaat?"

"Hao watu wanaomfuatilia kumbuka wanamfuatilia Issack sio gari... Kwahiyi nina uhakika akishuka kwenye gari na kuliacha pale wataendelea kumfuatilia Isaack mpaka mzumbe.. Na sisi tutapata gepu la kwenda kulichukua na ili tutumie katika hiki tunachoenda kukifanya.. Remember?? Misdirect. Confuse. Dialect.!!"
Nikamkonyeza na kutabasamu.


Tukabeba tena mabegi yetu mpaka reception ya Hoteli. Tukalipa na kuomba watuitie taxi.

Kama dakika saba baadae tulikuwa mbele ya geti la Hospitali kuu ya Mkoa.
Ujinga wa hapa huwa hawaruhusu magari kuingia ndani.. Kwahiyo ikabidi tuhonge elfu mbili kwa mlinzi ili haturuhusu alafu akatueleza tukiulizwa huko ndani kwanini ameturuhusu? Tujibu kwamba tunamchukua mama mzazi hali yake ni tete.

"Sawa! Na majeruhi huwa wanalazwa wodi ngapi?" Cheupe akauliza.

"Namba Tatu" akajibu mlinzi.

"Shukrani"

Tukaingia na gari mpaka ndani.

"Geuza gari kama tunatoka na usizime injini" Cheupe akamueleza dereva huku tunashuka.

Tukaelekea moja kwa moja mpaka wodi namba Tatu.

Japokuwa tulikuja hapa kufanya Jambo la hatari lakini moyo wangu ulilipukwa kwa furaha mara tu tukipokanyaga ndani ya wodi namba tatu.
Mwishoni kabisa mwa wodi, kitanda cha mwisho kabisa alikuwa amelazwa Kaburu na Nguo zake za kifungwa.
Alikuwa amefungwa pingu mkono mmoja na na kungwa kwenye kitanda.
Pembeni yake kulikuwa na kiti ameketi askari magereza mwenye bunduki.

Nikatabasamu na kumnong'oneza Cheupe.

"Its show time.!!"


Itaendelea Ijumaa.. Episode 21
 
EPISODE 20, POST # 3921


Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu @charmie DON SINYORI mij adden
bwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom