Vipepeo Weusi: Mkakati Namba 0034 (Simulizi)

Vipepeo Weusi: Mkakati Namba 0034 (Simulizi)

Habari wakuu,


Nilikuwa na dharura binafsi tangu siku ya Ijumaa.. Miniswamehe bure kwa usumbufu uliojitokeza..


Nitaweka muendelezo leo hii baada ya kama lisaa limoja kutoka sasa!


Kumradhi sana kwenu nyote!



The Bold

Mkuu Pamoja sana japo Sitaki kuihusisha Dharura hio na kipigo cha J mos

Kikubwa Uzima wako na wetu pia Basi wacha Tujongee Jamvini tayari kwa Mkao wa Kula
 
Habari wakuu,


Nilikuwa na dharura binafsi tangu siku ya Ijumaa.. Miniswamehe bure kwa usumbufu uliojitokeza..


Nitaweka muendelezo leo hii baada ya kama lisaa limoja kutoka sasa!


Kumradhi sana kwenu nyote!



The Bold
Umerudi hahaaahaaa mkuu bora umerudi aisee mi nilijua wakiba the board wameshakuteka
 
Asante mtani, basi mpe pole na yeye.

Nasikia eti mechi zinazokuja itakuwa Simba akipewa kadi nyekundu mnamwomba refa aisamehe tu, ili Simba wasibaki pungufu.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Rai bhanaaaa
 
VIPEPEO WEUSI: MKAKATI NAMBA 0034


SEHEMU YA 15




GEREZA KUU LA MKOA MOROGORO

SIKU YA NNE.

Moja kati ya vitu ambavyo vinanikera kuhusu kukaa ndani ya gereza ni kutokujua muda.
Kwa namna nilivyojizoesha katika maisha ya uraiani kutokana na ratiba zangu nyingi ni kuangalia saa kila baada ya muda mchache.

Gerezani mfungwa hauna hata 'access' ya kujua muda. Kwahiyo ili kujua muda inatakiwa utumie uzoefu wako wa kulisoma jua na kuhisi muda.

Na katika hisia zangu, hii ilikuwa yapata saa tatu asubuhi.
Tulikuwa tumemaliza kunywa uji takribani masaa mawili yaliyopita. Sikujua ni kwanini lakini siku za jumamosi na jumapili hakuna mazoezi gerezani.

Siku za 'weekend' ni siku zinazopendwa zaidi humu gerezni, kwasababu ni siku ya kutembelewa na ndugu, jamaa na marafiki.

Wafungwa wenyewe wanaitwa siku za 'Vistazi'.

Mimi na Godi pia tulikuwa tumekaa tukiwa na shauku kubwa na siku hii. Nilikuwa na tumaini leo kuna uwezekano Cheupe na Issack wanaweza kuja kuniona na labda wanaweza kuwa na taarifa muhimu kuniwezesha kumshawishi Kaburu kunipa taarifa ninazohitaji.

Siku ya Jana Ijumaa ilikuwa imepita bure pasipo kufanikisha jambo lolote la maana kuhusu kilichonileta humu.

Siku ya jana Kaburu alitumia karibia muda wote katika zahanati ya magereza. Hii ilikuwa ni moja ya visanga vilivyokuwa vinanichekesha na kunishangaza kuhusu magereza. Ni juzi tu ambapo maaskari magereza walifuata amri ya Mkuu wa gereza na kuwashushia kipigo cha virungu Kaburu, Blaki, Bokela na wapambe wao, alafu kesho yake wafungwa hao wakashinda zahanati ya magereza kutibiwa majeraha na maumivu.

Siku ya jana kitu pekee labda cha maana nilochokifanya ni kuendeleza mazungumzo yangu ya makubaliano na Sinyorita na Msauzi japokuwa sikufanikiwa kuonana na Obama.

Kwa kawaida muda wa watu kuja kutembelea ndugu zao hapa magereza ni saa nne asubuhi na ilikuwa imekaribia tayari, zilikuwa zimesalia dakika kadhaa tu.

"Naomba Mungu wasisahau mapocho pocho ya kula, kudadeki maana hili dona la jela lishanikinai aisee" Godi akaongea kwa msisitizo na kukereka. Tulikuwa tumekaa chini ya mwembe kule yard ya pili ambayo tunaipenda.

"Daah!! Ndio unachowaza tu fala wewe.. Badala ufikirie unatokaje jela, unawaza kula tu" nikamjibu kwa 'dongo'. Jela ilokuwa imenza kuniingia kwenye damu. Maana kuongea lugha ya maudhi nilikuwa naiongea bila hata kushtuka.

"Kutoka jela nataka na ni lazima, lakini kipindi nasubiria muujiza wa kutoka humu ndani sio dhambi roho yangu ikifurahi walau hata kidogo." Akaongea huku anajinyoosha. "Na sio misosi tu! Usisahau tunadaiwa buku kumi na nyapala".

"Oooopps! Tuombe Mungu" nikamjibu huku nainuka.

Tukainuka na kuanza kunyoosha miguu pale yard.

Kuna muda kwa kiasi fulani nilitamani kama siku zote humu gerezani ziwe za utulivu kama siku ya leo.
Siku amabayo hakuna mipango ya siri, hakuna pilika pilika za kuchoma moto vitu vya watu, hakuna mipango ya kuhatarisha maisha.
Lakini si sahihi kuruhusu hisia hii ya kutamani utulivu initawale. Sikuja humu ndani gerezani ili niwe na utulivu.
Lakini bado nikiri kuwa kuna muda nilitamani utulivu kama wa siku hii ya leo uendelee.

"Faridi Mkudeeeeeeeee! Eeeee faridi mkudeeeeeeee"

Mfungwa maalumu ambaye 'kitengo' chake kilikuwa ni kuchukua majina ya wageni na kuja kutangaza wafungwa wanaohitajika kwenda kuonana na ndugu zao, alipita yard anaita majina ya wafungwa.

Roho ikapata tumaini. Saa nne ilikuwa imewadia na Mungu akipenda muda wowote kuanzia sasa naweza kupokea ugeni wa Cheupe na Issack.

"Kaburu umemuona asubuhi hii" nikamuuliza Godi bado tukiwa tunaendelea kunyoosha miguu pale yard.

"Yuko sehemu ya kupumzika wagonjwa"
Godi akanijibu huku akinifahamisha kuhusu sehemu alilopo Kaburu sehemu ya kupumzika wagonjwa ambayo ipo sehumu ya upande wa gereza kule mbele liliko jiko.

"Yule mjinga leo lazima inabidi afunguke" nikaongea kwa sauti serious.

"Hao ndugu zako ndio waje na info za maana sasa! La sivyo tutakufa jela humu maana ni suala la muda tu kabla watu hawajafahamu tulichokifanya juzi"

"Yeah ofcorse unajua……." Kabla sijamaliza kuongea nikasikia jina langu linaitwa kwa nguvu na yule mfungwa mtangaza majina ya kwenda kuwaona wageni.

"Eeeeeeehh Rweyemamu Charles! Eeeeeehh Rweyemamu Charles…" Yule mfungwa alikuwa anapayuka.

"Nipooooooooo" nikaitika kwa sauti ya juu.

"Kilala kheri boss" Godi akaongea huku ananipigia saluti kwa utani..

"Yeah!" Nikamjibu kwa kifupi huku naondoka kwa mwendo wa kasi kuelekea upande wa gereza kule mbele kwenye vyumba vya maofisi ambapo pia kuna upande maalumu wenye chumba cha kuongea mfungwa na mgeni wake.

Utaratibu ni kwamba jina lako likiitwa unakuja hapa unaingia moja kwa moja kwenye chumba cha kuonana na wageni na kusubiri. Wageni wako waliokuja kukuona wakikamilisha taratibu huko nje nao wanaletwa katika chumba hiki wanakukuta hapa kisha askari anaondoka , mnaendelea na mazungumzo yenu.

Katika muda ambao wageni waliokuja kuwaona wafungwa wakiwa wengi mnaweza kujikuta hata wafungwa watatu au watano mmeingia humu kwa pamoja ili kuzungumza na wageni wenu.
Nilishukuru kwa wageni wangu kuja mapema kwani hii ilihakikisha kuwa titakuwa na faragha ya kutosha mimi na wao kuzungumza.

Nilisubiri kama dakika mbili hivi nikiwa nimekaa kwenye kiti, ndipo mlango ukafunguliwa na askaria kisha wakaingia Hasnat, Cheupe akiwa ameongozana na Issack.

Sikujua ni nini ila nilijikuata nasimama wima kutoka kwenye kiti baada ya kumuona cheupe.
Ubaya wa chumba hiki kama nilivyoeleza huko nyuma ni kwamba katikati kimetenganishwa na wavu mkubwa. Yani mnakuwa mnaonana lakini hamuwezi kuwa na "physical contact".

Zilikuwa karibia siku sita pekee toka nionane ma Cheupe, lakini nilijihisi ninakaribia mwaka mzima sijamuona Cheupe wangu. Nilitamani ning'oe ule wavu kisha kimkumbatie so tightly Cheupe wangu.

Nikajikuta tu naweka kiganja cha mkono kwenye ule wavu. Cheupe naye akaweka kiganja upande wa pili wa nyavu. Tukawa kama tumegusana viganja vya mkono lakini hatuja gusana kutokana na ule wavu kati kati.

Nikamtazama Cheupe kwenye macho. Nikaona ni jinsi gani amenimiss, ni jinsi gani anatamani nimkumbatie sekunde hii. Lakini pia nikagundua ni kiasi gani alikuwa anajitahidi kujikaza asilie mbele yangu na kunitia huzuni zaidi. Lakini pia Nikaona hofu iliyopo ndani yake.

"Hujambo Cheupe" nikamsalimia roho yangu kwa hisia kubwa.

"Sijambo baba! How are you?" Akanisalimia pia Cheupe akiongea kwa hisia karibu machozi yamdondoke.

"Niko poa mama! Am doing great"

"Na mimi sijambo pia jamani!!" Issack akatukatiza salamu zetu za hisia.

Wote tukageuka kumuangalia na kutabasamu.

"Niaje Issack?" Nikamsalimia.

"Poa Kichwa! Ishu vipi"

"I'm great!" Nikajibu kwa kutabasamu.

"You are not great!! You are in a prison.. Hebu tumalize huu mpango wako haraka utoke humu.. I tottaly don't like this" Issack akaongea kwa kukereka.

"Ok! Si mnajua kuna muda maalumu wa mazungumzo hebu tuongee fasta kabla hamjatolewa nje!! What do you got??" Nikaongea kwa shauku huku nakaa kwenye kiti na wao wakakaa.

"Well kama ulivyonieleza kuwa nianze kumchunguza Kaburu kwa kuanzia kwenye kesi yake na huko ndiko nilikoanzia" Issack akaongea kwa kunong'ona japokuwa tulikuwa peke yetu watatu tu ndani ya hiki chumba.

"Ok! Kuna chochote interesting mmekipata kwenye kesi yake?" Nikamuuliza.

"Actually tumepata a lot" Issack akaongea kwa tabasamu la ushindi.

Shauku yangu ikazidi.

"Ok! I'm listening" nikakaa sawa sawa kwenye kiti nimsikilieze.

"Hii kesi ya Kaburu alituhumiwa kumuua mpenzi wake Veronica Nyaulingo nadhani unakumbuka hilo" akaniuliza.

"Yes! Nakumbuka vizuri tu" nikamjibu.

"Ok! Sasa kabla ya kuanza kufukunyua kesi yenyewe na vitu vingine, tukajiuliza huyu Veronica Nyaulingo ni nani hasa? Na alikutanaje na Kaburu mpaka kuwa wapenzi" akaongea kisha akanyamaza kidogo kuniangalia na kuendelea "Tukafahamu kuwa alimaliza kidato cha nne sekondari ya Songea girls mwaka 2005, kisha akajiunga na Sekondari ya Kilakala na Kumaliza kidato cha sita mwaka 2008 na baada ya hapo akajiunga na chuo kikuu cha Dar es Salaam na kuchukua shahada ya Mass Communication na alihitimu mwaka 2011.! Kisha mwaka uliofuata akaanzisha kampuni yake ya consultation kuhusu masuala Public Relations na moja ya clients wake akawa ni kampuni ya Ndeshema Safaris ambayo inamilikiwa na Eric Kaburu na tunaamini hivyo ndivyo walivyo kutana" akanyamaza tena kidogo na kuniangalia.

"Ok!" Nikamjibu nikihisi kama bado kuna taarifa anataka kunipa.

"Ni taarifa nzuri, right??" Issack akaniuliza huku anatabasamu.

"I guess!" Nikamjibu kwa kifupi.

"Well ni taarifa mzuri except for the fact kwamba hakuna mtu anayeitwa Veronica Nyaulingo" Issack akaongea kwa kunishtuliza.

"Whaaaaat?? Sikuelewi!!" Nikauliza kwa mshangao.

"Ni hivi Ray! Binafsi nilikuwa curious kidogo kwa record zake jinsi zilivyo.. Ameenda Songea girls akapasua akapelekwa Kilakala nako akapasua akaensa UD nako anahitimu na ghafla tu mwaka ukiofuata anamiliki kampuni yake!! Its inspiring but binafsi nikawa curious" akaongea Issack kwa tabasamu la kujidai.

"Nakusikiliza" nikaongea tena kwa shauku.

"Nikaingia kwenye mtandao wa baraza la mitihani kuangalia usahihi wa hizo taarifa, na nikazikuta zipo tena kwa usahihi kabisa bila kukosewa hata spelling!! Lakini sikuridhika, Kuna mtu yuko Songea nikamtumia picha ya huyu mpenzi wa Kaburu nikamwambia aende Songea girls pale kuuliza kama wana kumbukumbu zozote za huyo mwanafunzi!! Kilichoonena kwenye mavitabu yao ya shule ni kwamba ni kweli kulikuwa na jina la mwanafunzi anayeitwa Veronica Nyaulingo mwaka huo lakini walivyoonyeshwa picha ya mpenzi wa Kaburu wote walidai kuwa hawakumbuki mwanafunzi mwenye mwenekano huo katika darasa la 2005!! Kisha mimi na Hasnat tukaenda hapa shule ya Kilakala na tukakumbana na kitu hicho hicho.. Kwenye kumbukumbu za shule yupo mwanafunzi mwenye jina la Veronica Nyaulingo lakini tulipowaonesha picha wote wakadai hawakumbuki mwanafunzi mwenye muonekano huo hapo shuleni..!! Hatukutaka kufukunyua sana ili tusije kuwatia mashaka, tukaona kama tukihitaji taarifa nyingine basi tutarudi siku nyingine.. Sasa nina rafiki yangu amesoma UD na alikuwa pale mwaka huo aliohitimu Veronica 2011..,akanitafutia mawasiliano na mtu aliyekuwa anasoma Mass Communication mwaka huo na nilipompata huyo mtu na kumuonyesha picha ya Veronica guess what he said?? Akasema yes anamkumbuka huyo binti walisoma naye mwaka huo!! Unajua hii maana yake nini??" Issack akaniuliza huku anatabasamu.

"Ameiba 'identity' ya mtu.." Nikamjibu huku natizama chini najaribu kufikiri.

"You got that right!! My theory ni kwamba kulikuwa na Veronica Nyaulingo mwenyewe ambaye alisoma Songea girls na Kilakala.. Lakini hapo kati kati akapotea na 'identity' yake ikachukuliwa na huyu binti ambaye alikuja kuwa mpenzi wa kaburu!! Swali ni je, Veronica Nyaulingo halisi alienda wapi?? Na kwanini huyu mpenzi wa Kaburu aibe Utambulisho wa mtu?? Na je hii ni coincidence mwizi wa utambulisho wa mtu kwenda kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanachama wa The Board.??" Issack akaongea na kuuliza safari hii akiwa serious kweli kweli.

Nilihisi kichwa kinazunguaka bila hiari yangu. Kulikuwa na karibia mawazo mia moja yanapita kichwani mwangu. Sikujua niwaze lipi au nishike lipi. Sikutegemea taarifa ya utata kiasi hiki.

"Ok ok ok! Najua hapa hamjaruhusiwa kuingia na makaratasi.. Binafsi licha ya kuisoma sana kesi ya kaburu kwenye vyombo vya habari lakini nimesahau vitu vingi hata Veronica mwenyewe sikumbuki anafananje! Nadhani kwamba ………." Sikumalizia sentesi yangu nikamsikia Issack ameanza kuongea na kunikatisha..

"Ni kwa vile cheupe amekudatisha sana ndio maana humkubuki Veronica.. Ila hakuna mwanaume anayeweza kumuona Veronica na kumsahau.. Mtoto mkare utadhani toto la kitusi hahah" akaongea kwa utani na kucheka.

Lakini kwangu sentesi yake hii ya utani iliwasha taa kichwani mwangu. Nikabaki nimeduwaa.

"Umesemaje" nikauliza kwa mshangao.

"Nimesemaje kuhush nini" Issack akanijubu kwa kunishangaa.

"Umesemaje kuhusu mwonekano wa Veronica" nikamuuliza tena kwa mshangao.

"Ni mtoto mkali unaweza kudhani mi mnyarwanda" akanijibu huku ananishangaa.

Sikuamini kile nilichokibaini kwa taarifa hii iliyowash taa kichwani mwangu na kung'amua kilichojificha. "Unaweza kudhani ni mnyarwanda", nikajikuta hii sentesi inajirudia tena na tena kichwani.
Sikutaka kuamini kile nilichong'amua.

"Nadhani naweza kuwa nimebaini siri iliyo nyuma ya huyu 'Veronica' feki" nikawaeleza huku nashusha pumzi.

Ni nini ameking'amua na kinawasaidiaje katika kutekeleza azma yao??





INAENDELEA POST NAYOFUATA..
 
VIPEPEO WEUSI: MKAKATI NAMBA 0034





EPISODE 16



Wote wawili, Issack na Cheupe wakabaki wamenikodolea macho kwa mshangao.

"Una maana gani kuwa umeshajua Veronica feki ni nani!" Issack akaniuliza kwa mshangao.

"Mnakumbuka nilivyo waambia nilipochukuliwa na Maafisa wa Usalama wa Taifa na kunipeleka maeneo ya Mbezi walikuwa maafisa wanne na mmoja ni mwanamke??" Nikawauliza.

"Yeah nakumbuka" wote wakaitikia kwa pamoja.

"Sasa yule mwanamke alikuwa ni Mnyaruanda. Hata kiswahili hajui kukiongea ingawa anakielewa, na nikawa najiuliza sana kwanini Maafisa Usalama wa Tanzania washirikiane na Mnyaruanda na Rwanda wana maslahi gani mpaka watume mtu huku?? Sasa kidogo nimeanza kuelewa!"

"Well, na umeelewa nini" Issack akauliza.

Nikasogea karibu na nyavu na kuongea kama nawanong'oneza.
"Nina hakika kuwa kuna kitu nchi ya Rwanda inachunguza kwenye mtandao wa The Board. Kwahiyo ninachokihisi ni kwamba Veronica ni mwanausalama wa nchi ya Rwanda na akatatumia mbinu kuanzisha uhusiano na Eric Kaburu ili aweze kupepeleza na kupata hiyo taarifa wanayohitaji. Ndio maana Rwanda mpaka leo hii wako interested na hii ishu ya The Board"

"Wow! Ina make sense kabisa. Nadhani ndio sababu kwanini Kaburu akamuua, itakuwa alikuja kubaini Veronica ni Afisa Usalama" Issack aongezea.

"No sidhani kama alimuua." Nikamjibu.

"Kwanini unasema hivyo" akauliza kwa mshangao.

"Nimekaa hii karibia siku ya sita gereza moja na Kaburu, nimeongea nae ana kwa ana na kumsoma ni mtu wa aina gani. Trust me, Kaburu sio dizaini ya mtu mwenye uwezo wa kuua! So nina uhakika kabisa hakumuua Veronica." Nikamfafanulia.

"But Kaburu mwenyewe alikiri kuwa amemuua!"

"Whaaaat??" Nikajikuta nauliza kwa mshangao.

"Yes kipindi kesi inasikilizwa mwanzoni kabisa mwa kesi, Kaburu akakiri kutenda hilo tukio! Ndio sababu kwanini kesi iliisha haraka haraka"

Nikashikwa na butwaa. Nikahisi hapa kuna jambo zito limejificha. Inawezekanaje mtu akiri kuua alafu ahukumiwe adhabu ya kuua bila kukusudia na apewe miaka saba pekee jela. Nikawa na uhakika kabisa kuna jambo limejificha hapa.

"Veronica alikuafaje?" Nikamuuliza Issack, licha ya kesi hii kuandikwa sana lakini nilikuwa nimesahau matukio mengi kuhusu kesi hii.

"Walikuwa Nyumbani kwa Kaburu, wakaanza kugombana na baadae Kaburu akaanza kumpiga! Inaelezwa kuwa akampiga mpaka akapoteza fahamu kisha akamchoma moto.. Na kwa mujibu ya magazeti yalivyoandika kipindi kile... Wanaeleza kuwa kisa ni wivu wa mapenzi" Issack akanifafanulia.

Taa ikazidi kuwaka kichwani mwangu. Nikahisi naanza sasa kuungajisha dots na kupata picha kamili.

"Wow! Ok ok, wow" nikajikuta naongea huku natikisa kichwa baada ya dots kuanza kuungana.

"What is it!" Cheupe akauliza kwa shauku.

"They fell in love" nikamjibu huku nawaangalia kwa tabasamu kwa furaha.

"Who fell in love?" Cheupe akauliza tena.

"Kaburu na Veronica! They fell in love!" Nikawajibu huku bado natabasamu.

"How? Kaburu amekiri kuwa alimuua?" Issack akauliza kwa mshangao.

"No hakumuua! Hicho ndicho Kaburu anachotaka watu wa amini.. Na amefanikiwa kuwaaminisha watu.. But the truth is hakumuua.. They fell in love"

Nikaongea huku natabasamu lakini niko serious.

"Oyaaaaa! Muda wenu ushaisha.. Tokeni huko" nikasikia sauti ya askari inaitilia nje ya chumba.

"Leo nitaongea na Kaburu na najua nimbane vipi ili aongee na mimi kwa hizi taarifa mlizonipa.. Nahitaji kesho mje tena hapa kuna maagizo tupene tena nina hakika nikiongea naye lazima nitapata kitu amabcho nitahitaji mkakifanyoe kazi huko nje"
Nikaongea huku tunainuka kwenye viti kwenye kile chumba cha kuongea na wageni.


* * * * * *

Nilikuwa nimeketi mbele ya Kaburu kwenye upande wa gereza ambao kuna kisehemu cha wagonjwa kupumzika.

Kaburu alikuwa amekaa hapa ametandikiwa godoro amepumzika baada ya kutoka zahanati ya magereza kutokana na kipigo kizito cha virungu juzi.

"I'm impressed! Sikudhani kama unaweza kufanya kama kitu ulichokifanya juzi" aliongea akikumbushia tukio la juzi. Ni dhahiri alikuwa amegundua kuwa mimi ndiye niliyeufanya ule mchezo wote.

"Na hapo haujaona hata nusu ya kile ninachoweza kukifanya my friend" nikamjibu seriously nikimkazia macho.

"Ni nini unachoweza kukifanya?" Akaniuliza kwa dharau.

"Nina uwezo wa kukufanya uongee na mimi na unambie ninachokitaka kwa hiari yako au kwa kukulazimisha ufanye hivyo" nikajibu kwa kiburi.

"Hahahahaha!! Wooow, i'm really scared!" Akaongea huku anacheka kwa dhihaka.

"Unajua kipindi nasoma advance Sekondari ya Tambaza!! Kulikuwa na jamaa mmoja hivi ambaye alikuwa na tabia za kishenzi sana.. Kutukana watu, kupigana, uonevu wa kijinga jinga.. Sasa kuna siku akajichanganya akanitukana mbele ya darasa zima!! Unajua nilianyaje" nikamuuliza huku nimemkazia macho.

"Ulifanyaje" akaniuliza.

"Nikamfuata faragha akiwa peke yake, nikamwambia nampa siku tatu aniombe msamaha mbele ya darasa zima na asipofanya hivyo atajuta kwa kitakachomkuta"

"Alikuomba msamaha?"

"Hapana! Alinitukana tena hapo hapo.. Lakini unajua nini kilifuata?" Nikamuuliza.

"Ukampiga ngumi?"

"No! Wiki moja baadae akafukuzwa shule kwa kosa la kusambaza picha za uchi za demu wake" nikamueleza huku nimemkazia macho na kumsogelea.

"Wow! Kumbe hii michezo ya kuwafanya watu waonekane wamefanya vitu ambavyo hawajavifanya umeianza zamani sana kijana" akaongea huku anang'ata midomo kwa hasira.

"Ninachojaribu kukwambia ni kwamba, I always get what i want.. Nikitaka kitu kitokee akili yangu itapata namna ya kufanya ili nipate hicho kitu"

"And unahitaji nini kutoka kwangu?" Akaniuliza huku amenikazia macho.

"Nahitaji unieleze kila unachokijua kuhusi The Board" nikamjibu huku pia nimemkazia macho.

"Hahahahaha! Unaota kijana.. Kirahisi tu hivyo?? Hahahaha, endelea kuota" akajibu huku anacheka kwa dharau.

"Well, sio kirahisi rahisi tu... Itabidi unieleze ninachohitaji ili nikae kimya nisiwaeleze watu wa Usalama kwamba Veronica bado yuko hai" nikaongea kwa kusogelea karibu kabisa nikitoa sauti kama nanong'ona.

Nikauona mshtuko wake kwenye macho yake. Nilikuwa nimegusa 'ikulu'.

"Umeanza kuchanganyikiwa Dogo" akanijibu kwa sauti ya woga huku anajigeuza kwenye gorodo na kuangalia pembeni.

"Really?? Nimechanganyikiwa? Una hakika?" Nikaongea huku nazunguka godoro kwenda upande ule aliogeukia. Nilikuwa nataka niongee naye huku namuangalia usoni ili maneno yangu yawe na effect niliyoitaka.

"Sikiliza Kaburu" nikaanza kuongea mara bada ya kuwa upande ule mwingine tunaangaliana. "Nafahamu kuwa Veronica Nyaulingo sio jina la mpenzi wako ambaye watu wanaamini amekufa. Amechukua jina la mtu ambaye mpaka sasa najiuliza amepoteaje huyo mtu. Ninachokiwaza ni kwamba wewe na wenzako The Board, kuna kitu mlikuwa mnakifanya nchini Rwanda na serikali ya Rwanda ikaja kugundua. Baada ya kugundua ndipo wakampandikiza afisa usalama wao ambaye alichukua 'identity' ya Veronica Nyaulingo ma kujiweka karibu na wewe na matokeo yake mkawa wapenzi. Naamini kuwa baada ya muda ingawa hii kwake kuwa na wewe kimapenzi ilikuwa ni assignment lakini akajikuta amekupenda kikweli kweli na wewe ukampenda. Na kama watoto wa sekondari vile mkajikuta mpo kwenye mapenzi mazito. Sasa lazima ikafika kipindi The Board wakagundua kuwa Veronica ni 'spy' na amepandikizwa kwenye maisha yako ili akupeleleze. Nina hakika kuwa kuna siri nyingi tayari alikuwa amezijua kuhusu wewe na The Board, kwahiyo The Board lazima wakafikia uamuzi kuwa inabidi auwawe. My guess is, wewe Kaburu ukawaambia wenzako kuwa wakuachie wewe hiyo kazi ya kumuua Veronica." Nikanyamaza kidogo na kumuangalia usoni. Nikaona jinsi haya maneno yanavyomgusa moyoni. Niakaendelea.



"Najiuliza sana mwili ulioichoma moto uliutoa wapi. Na ni mwili wa nani, lakini nafahamu na nina uhakika kabisa sio Veronica Nyaulingo. Mpenzi wako Veronica kwa kutumia uzoefu wake wa ushushushu ukaenda kumficha mahali salama kabisa ambako anaishi mpaka leo hii, lakini huku nyuma ulimwengu mzima ukaamini kuwa wivu wa mapenzi umekufanya umempiga mpenzi wako na kumchoma moto!! Sasa wanasema kuwa 'you can fool some people for some time but can't fool all the people all the time'! Nina hakika kuwa watu wa usalama kutoka Rwanda wakaja kugundua mchezo ulioufanya wewe na mpenzi wako, na si wao tu peke yao bali pia The Board nao wakagundua kitu ulichokifanya. Ndio hapo sekeseke lilipoanzia. Watu wa usalama wa Rwanda wanahitaji afisa wao wampate lakini pia nina hakika kuna taarifa muhimu wanaamini anayo ambayo wanahitaji waipate. Lakini pia The Board wamegundua kuna taarifa muhimu mno wanaamini utakuwa nayo na ni taarifa 'vital' mno kwao na hii ndio sababu mpaka leo hii upo hai hawajakuua.!"

Nikanyamaza tena kumuangalia. Alikuwa amenikodolea macho haamini ni namna gani nimeweza kuchekecha akili na kung'amua haya ninayomueleza. Sikutaka kumchelewesha, nikaendekea.

"Sasa basi, kama wanavyosema watu.. Mapenzi ni upofu, mapenzi yanatia ukichaa ndicho hicho ninachokiona kati yenu wewe na Veronica! Veronica akaamua kuwasaliti wanausalama wenzake ili awe na wewe, na wewe ukawasaliti wenzako The Board ili uishi maisha ya furaha na Veronica. Ndio sababu kwanini ulikiri mahakamani kuwa umemuua. Ulikuwa unaogopa kuwa mtaani baada ya tukio lile kutokea. Nina hakika The Board walimuhonga Jaji ili asikutie hatiani uachiliwe urudi uraiani ambapo wenyewe wanajua ni namna gani wataipata hiyo taatifa uliyo nayo. Kwahiyo kabla kesi haijaenda mbali sana ukaamua ukiri kuwa ulimuua ili kumnyima nafasi Jaji asikuachie huru mwisho wa kesi. Kwa hiyo Jaji ambaye nina hakika labda alikuwa anatumiwa na The Board licha ya kutamani kukuachia huru urudi uraiani ambapo The Board wanakusubiri wakudhibiti, ikabidi akupe kifungo chepesi cha miaka saba tu kwa hukumu ya kuua bila kukusudia"

Nikanyamaza tena na kumkazia macho.

"Umeongea maneno mengi bado haujaniambia point ni nini dogo?" Akaniuliza kwa hasira.

"My point is. Kwa hii hukumu yako ya miaka saba gerezani, tukiondoa 'remission' ya magereza maana yake unatumikia kama miaka minne na nusu pekee, na ukizingatia umeshakaa karibia miaka miwili na nusu that means umebakisha miaka miwili pekee urudi uraiani. Najua wewe ni mtu makini lazima umeshaweka mipango ni namna gani utawaepuka The Board ukiachiwa baada ya miaka miwili. Sasa unaonaje nikifanya figisu ushtakiwe upya kwa kosa la ule mwili uliouchoma moto safari hii iwe kesi halisi kabisa ya kuua na ulimwengu mzima ujue udanganyifu mlioufanya wewe na Veronica wako? Na amini mahakama safari hii itakusweka humu miaka mingi uozee humu humu maisha yako yote huyo veronica uwe unamuona kwenye ndoto pekee badala ya miaka miwili kutoka sasa?"

Kama kawaida nikanyamaza ili nione reaction yake. Alikuwa ameng'ata midomo kwa hasira. Maneno yangu yalikuwa yanamgusa penyewe kabisa. Sikumchelewesha tena, nikaendelea.

"Kama hiyo haitoshi, unaonaje nikiwamegea siri Usala wa Taifa au The Board kuhusu mahali Veronica alipojificha? Naomba nikuhakikishie kuwa kama unavyoona nywele zako zilivvyo karibu karibu ndivyo nilivyo close kufahamu Veronica alipo" nikampiga mkwara.

"Wenzako watu wa Usalama na The Board, mwaka wa pili wanakimbiza kivuli tu hawajui Veronica yuko wapi" akaongea kwa hasira.

"Well, mimi sio Usalama au The Board, mimi ni Rweyemamu Charles Kajuna!! Na kama nilovyomuonya yule jamaa niliyekwambia shuleni Tambaza, nakuambia na wewe na wala sikupi wiki au siku tatu, nakupa chance sasa hivi! Nieleze ninachokubembeleza siku zote hizi.. La sivyo help me God, usinilaumu kwa nitakacho kifanya" nikaongea kwa hasira nimemkazia macho huku nimemsogelea karibi pua zigusane.

Kaburu akashusha pumzi na kisha kuanza kuongea.

"He was right you know!"

"Who was right?" Nikamuuliza kwa kukereka.

"Dr. Shirima! He was right!" Akaongea.

"Right about what??" Nikamuuliza kwa hasira nikiona kama anataka kuhamisha magoli.

"Miaka mitatu kama na nusu hivi iliyopita nilikuwepo kwenye kikao ambacho alipendekeza kuwa tumuingize kwenye michakato yetu mwanafunzi wake anayeitwa Rweyemamu Charles Kajuna. Nakumbuka namna ambavyo alikuwa anasifia. Kuwa ni kijana genius na persistent! Kwamba unapontential hata tunaweza kukutengeneza ukawa kiongozi mzito huko mbeleni. Nilipokuja kupewa file lako na kulisoma nilikuwa impressed sana na ni moja ya watu ambao waliunga mkono pendekezo la Dr. Shirima kuwa tukuingize kwenye michakato yetu! Kijana genius ma persistent!"

Kaburu akaongea huku kwa kiasi fulani akiwa ana maanisha anachokisema na kuna kiasi Fulani alikuwa ananiinjoi.

"Thank you for your vote of confidence" nikamjibu kwa kumuinjoi pia.

"Except for one thing kijana! Kuwa king'ang'anizi kwenye maisha ni asset na pia ni liability.! Ni asset pale tu unapokuwa king'ang'anizi kwenye jambo sahihi na ni liability pale unapokuwa king'ang'anizi kwenye jambo lisilo sahihi. Na kwenye hili hauko sahihi kijana.. No one can take down The Board! No one"

Akaongea huku amenikazia macho.

"Don't worry about that! I will take my chances.. Hilo halikuhusu kabisa! Just tell what I want to know" nikamjibu kwa hasira nimiona kama anazunguka mbuyu tu.

"Ok! Nahitaji unisaidie kutoroka humu gerezani!" Akaongea akinikazia macho.

"What?" Nikamuuliza kwa mshangao.

"Nahitaji unisaidie kutoroka gerezani! Nataka uchekeche hizo akili zako kama unavyojigamba."

"Ok! Na unaweza kuniambia kwanini unataka kutoroka" nikamuukiza tena kwa mshangao.

"Humu sio mahali Salama tena kwangu, umeshaharibu kila kitu. Huo utaratibu tu aliouweka Mkuu wa gereza kuwa kuanzia jumatatu nianze kwenda shamba mi hatari kwa usalama wangu.. Na si hivyo tu! The Board wanajua uwezo wako wa kupanga mipango na ulivyo king'ang'anizi, wakihisi tu kuwa naweza kukupa taarifa muhimu nakuapia kwa Mungu watatumaliza wote wawili ili waondoe udhia once and for all"

Kaburu akaongea huku nikihisi hofu iliyokuwa kwenye sauti yake.

"Ok! Nitafikiria hilo but first things first.. Naomba info ninazozitaka kwanza" nikamkazia macho.

"Ok! Unapaswa kufahamu kuwa ndani ya The Board ni watu wawili pekee wanaojua kila kitu kinagaubaga. Hao wawili ndio wanaojua akaunti zote za siri, majina yote ya vibaraka wao serialini, kwenye vyombo vya usalama, majina ya wanachama wote walio hai na waliokufa, na mikakati yote kuanzia wa kwanza mpaka mkakati wa sasa wa 34!!"

Akaongea huku anafumba macho. Nilihisi kuwa alikuwa anajijutia kwa haya mambo anayonieleza.

"Ok! Ni nani hao wawili" nikauliza kwa shauku kubwa.

"Ni chairman na kuna mtu tunamuita The Book Keeper! Chairman huwezi kumpata na wala siwezi kukuambia lakini The Book Keeper una mfahamu vizuri sana" akaongea huku anafumbua macho baada ya kuyafunga alipokuwa anaongea.

Moyo ukaanza kunienda mbio.

"Ni nani?" Nikaukiza kwa shuku kubwa.

"Vincent Mallya" akaongea kwa kifupi huku akifumba tena macho.

"Whaaaaatt!" Nikapigwa na mshangao.

"Yes, Vincent Mallya" akaongea kwa kifupi tu huku bado amefunga macho.

"Vincent Mallya Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRBB??" Nikamuuliza kwa mshangao.

"Yeah! That's him, ndiye The Book Keeper wa The Board.! Yeye ndiye anatunza kumbukumbu zote za The Board ambazo nimekueleza. Na kumbukumbu hizi haziwekwi kwenye vifaa vya digitali kama computer kuogopa watu kudukua.. Taarifa zote zinahifadhiwa kwenye karatasi na mafaili na yapo mahali yamehifadhiwa ambapo naweza kukuelekeza ukaenda kuyachukua kama unaokota dodo kwenye mwembe, but first inabidi unitoroshe humu gerezani." akaongea akiwa amenikazia macho kweli kweli.

Moyo ulienda kasi kweli kweli. Nikatafakari karibu vitu mia kwa wakati mmoja. Mbele yangu nimebakiza hatua moja tu nitimize lengo langu la kunileta humu. Lakini hatua yenyewe ni dhahiri ilikuwa ni impossible.


Nini kitafuata??

ITAENDELEA JUMATANO…
 
EPISODE 15, POST # 3431

EPISODE 16, POST # 3432



Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu @charmie DON SINYORI mij adden
bwii ONTARIO
 
Mkuu.. Welcome Back...na nikishukuru kwa dhati kabisa kwa hizi release za jioni.. what a beautiful ending to a very long Day.. GodBless
 
Habari wakuu,


Nilikuwa na dharura binafsi tangu siku ya Ijumaa.. Miniswamehe bure kwa usumbufu uliojitokeza..


Nitaweka muendelezo leo hii baada ya kama lisaa limoja kutoka sasa!


Kumradhi sana kwenu nyote!



The Bold
Mkuuu,nakuelewa sana na asante kwa kaz yako

Nadhan baada ya kupepeluka lasmi umetua

Nilikuwa kule behind the..

Sasa ngoja nisome hz
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom