Habari wakuu,
Kuna wazo nalileta kwenu ili tulijadili..
Nimepata maoni ya watu wengi kuhusu namna bora ya kuendelea na hii simulizi ya Vipepeo Weusi: Mkakati namba 0034, pamoja na aina za thread ninazoandikaga Jamii Intelligence na nimekuwa natafakari na kufanyia kazi maoni hayo kwa muda sasa na baada ya kutafakari kwa kina nimekuja na wazo hili;
Nimeonelea tuwe na "premium convo" huko PM hapa hapa JF kwa wale ambao wako tayari au tuwe na group ya whatsapp exclusively kwa ajili simulizi hii pamoja na simulizi nyingine ambazo nina mpango wa kuziweka.
Now, how is this going to work??
Katika hiyo convo/whats group nimelenga niwe naweka 4 episodes kila wiki za simulizi hii ya vipepeo weusi na kila weekend nitakuwa naweka Makala maalumu kama zile za kina D.B Cooper au Geranimo ambazo huwa naziweka Jamii Inteligence..
But.. Katika hii convo/whatsapp group kutakuwa na "subscription fee" kwa kila mwezi, na napendekeza iwe Tsh. 5,000/- kwa mwezi.
Lengo ni nini?
Lengo langu kuu kutaka kuweka utaratibu huu ni kama ifuatavyo;
1. Nadhani si dhambi The Bold walau akiwa na kijihela cha kununua juice atulize koo wakati anaandika hizi simulizi na makala. LOL
2. Kwa utaratibu huu ninaopendekeza nadhani walau simulizi itakuwa inaenda haraka so naamini itaisha haraka, maana kwa utaratibu huu wa sasa ambao tumekuwa tunaenda nao hii simulizi inaweza kuisha May/June.. Ila kwa utaratibu huu mpya nadhani ndani ya miezi miwili itakuwa imeisha.. Ziko simulizi nyingine mbili tamu sana natamani kushea nanyi ila nashindwa kwa kuwa hii bado inaendelea. Simulizi hizo moja inaitwa "La Ultima Letra (Herufi ya mwisho)" na nyingine inaitwa ZEO. Ni hadithi mbili matata sana..
3. Sababu yangu ya mwisho, ni kuweka muelekeo mzuri ili kuweza kujua kama kuna 'base' ya kutosha ili kuanza kutoa vitabu hapo miezi ya baadae mwaka huu.
Sasa, najua kuna maswli nitaulizwa! Na moja wapo ni hili; Je, simulizi hii ya Vipepeo Weusi itaendelea humu na je vipi kuhusu makala za Jamii Intelligence?
Jibu: Thread itaendelea humu ila itasimama kwa wiki moja ya kwanza (kuanzia Jumamosi) na ikirejea baada ya wiki hiyo moja, nitakuwa naweka episode moja kwa wiki.
Kwa lugha nyingine, kule kwenye group tunaweza tukawa tumefika episode 21 but huku kwenye huu uzi ikawa episode 9. Na tutaendelea na utaeatibu huo. Hapa itatolewa episode moja per week!!
Na kuhusu makala za Jamii Intelligence, zitaendelea but nitakuwa naweka makala moja kwa mwezi tofauti na kule kwenye group nitakuwa naweka makala kila weekend (makala za uchambuzi) na simulizi nitakuwa naweka episode 4 kwa wiki.
Mwisho,
Kama kuna mwenye maoni, naomba tujadili but naomba tutumie lugha ya staha.
Na kwa walio tayari, naomba uniPM namba yako au nitumie meseji whatsapp kupitia namba 0718 096 811
Asanteni!
The Bold.