Uchaguzi 2020 Viongozi wetu wa CHADEMA Kanda ya Magharibi, mkoa wa Katavi na Wilaya ya Mlele hujuma mlizomfanyia Tundu Lissu kwa sababu tu ya pesa hazikubaliki

MIMI BABA YENU

Senior Member
Mar 1, 2019
196
500
Jana Tarehe 18/09/2020 Mgombea wetu wa Urais Tundu Lissu alikuwa na ratiba ya kufanya Kampeni katika Mkoa wetu wa Katavi maeneo ya Majimoto katika jimbo la Kavuu Wilaya ya Mlele na Mpanda MJINI katika jimbo la Mpanda.

Hakika viongozi wetu (Musa Masanja Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Magharibi , Roda KUMCHELA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Katavi, SEFU NTIJE, Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Mlele na GELARD PESAMBILI Mwenyekiti wa BAVICHA Wilaya ya Mlele) walichomfanyia Lissu na sisi wanachama na wapenzi wa CHADEMA kwa ujumla hakikubaliki na kamwe hatuna imani tena na viongozi hawa.

Wananchi tuliokusanyika katika viwanja vya Mkuyuni Majimoto kuanzia saa mbili asubuhi tulisikitishwa sana majira ya saa 10:20 jioni kutangaziwa kuwa LISSU hatafika kwa sababu ambazo hazieleweki mara eti Mawasiliano na msafara wake hayapatikani mara msafara umepotea.

Baada ya kufuatilia sababu za LISSU kutofika Majimoto tulibaini kuwa Msafara wa LISSU ulipotea njia panda ya KIZI mpakani mwa Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa na Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi. Kwamba badala ya msafara wa LISSU kufuata Barabara ya Kibaoni Majimoto , ukafuata Barabara ya Sitalike kwenda Mpanda.

Tunajua kuwa LISSU alifanya mikutano CHALA na KIRANDO Wilayani Nkasi kabla hajaja Majimoto. Maswali tunayowauliza viongozi wetu ni:-
1. Walijua Msafara wa LISSU unajua Barabara ya kwenda Majimoto?

2. Kama msafara wa LISSU ulikuwa haujui njia kwanini viongozi wote wanaojua njia kuanzia Kanda, Mkoa na Wilaya Walitangulia Majimoto na kukimbilia kufanya Starehe GWAMBINA LOUNGE? Tunajua pesa zilizokuwa zikichangishwa kwenye mkutano wakipelekewa viongozi GWAMBINA kwa ajili ya kunywa bia.

3. Kama waliona ugumu kuusubiri msafara wa LISSU kwanini hawakuwaweka Vijana njia panda ya KIZI ili wauongoze msafara huo kuelekea majimoto?

Tukumbuke kuwa ni Viongozi hawahawa kupitia Mwenyekiti wa BAVICHA Wilaya ya Mlele walitaka kutuaminisha kuwa kuna kundi lineandaliwa kwa ajili ya kuanzisha vurugu wakati wa Mkutano, kumbe walikuwa na mambo yao ikiwa ni pamoja na kujengea hofu Mhe. LISSU ili asifike kuongea na wana Majimoto ilimradi tu wagawane pesa zilizoandaliwa Kwa ajili ya Mkutano huo zikiwemo zile zilizochangishwa kutoka kwa Wananchi Mkutanoni hapo

Kwa Ujumla tukio hili limewakatisha tamaa Wananchi wa Majimoto na Mkoa wa Katavi kwa ujumla. kwani wanamuona LISSU na CHADEMA kwa ujumla ni wasanii na waongo.
 
Bengal

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
2,196
2,000
Watu wa Sumbawanga alikokuwa na mkutano kabla kuondokq walishafanya yao Hadi Lisu msafara mzina unapotea njia!!!

Chezea Sumbawanga
Hayo Mambo hats sii yakuaminika inategemea Imani ya Ntu na ntu.
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,426
2,000
Hilo La Lisu kupotea njia wachawi wa Sumbawanga alipokuwa na mkutano walimpima Kama kweli Uraisi anauweza sababu kuwa Raisi ni pamoja na kutawala wachawi

Hivyo wakam test yeye na msafara wake wamewaona hamna kitu ndio maana walipotea barabara

Taarifa zilizoko Sumbawanga ni kuwa Lisu Hana uwezo wa kuwa Raisi kwa Test hiyo ya wana Sumbawanga ambayo kafeli
 
Bengal

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
2,196
2,000
Hilo La Lisu kupotea njia wachawi wa Sumbawanga alipokuwa na mkutano walimpima Kama kweli Uraisi anauweza sababu kuwa Raisi ni pamoja na kutawala wachawi...
Imani potofu hazina nafasi katika taifa letu. Sema Ameen
 
Siwamilele

JF-Expert Member
Oct 22, 2019
253
1,000
Hilo La Lisu kupotea njia wachawi wa Sumbawanga alipokuwa na mkutano walimpima Kama kweli Uraisi anauweza sababu kuwa Raisi ni pamoja na kutawala wachawi

Hivyo wakam test yeye na msafara wake wamewaona hamna kitu ndio maana walipotea barabara

Taarifa zilizoko Sumbawanga ni kuwa Lisu Hana uwezo wa kuwa Raisi kwa Test hiyo ya wana Sumbawanga ambayo kafeli
Ndio hoja za chama cha wachawi (ccm) mlizobakiza now days

Sent from my Infinix X606B using JamiiForums mobile app
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,866
2,000
Jana niliona picha Lissu kapiga na mgombea ubunge wa Mpanda Mjini Rhoda, sasa kama kituo kilikuwa na kufika hapo jimboni Kavuu ila tatizo alibadilisha tu njia sioni ubaya wowote kwenye hilo, unless uwe na sababu zako nyingine; na hizo bia walizokunywa kama ni baada ya mkutano aliofanya Lissu pia sioni ubaya kwenye hilo, nakuona umepanic bila sababu yoyote ya maana.

Unless kama ulitaka Lissu apite njia mbili kwa wakati mmoja, which is insane to think about that, provided lengo kuu la hiyo ziara lilitimia kujinadi yeye binafsi na mgombea ubunge wa Kavuu, I see no problem.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,866
2,000
Hilo La Lisu kupotea njia wachawi wa Sumbawanga alipokuwa na mkutano walimpima Kama kweli Uraisi anauweza sababu kuwa Raisi ni pamoja na kutawala wachawi

Hivyo wakam test yeye na msafara wake wamewaona hamna kitu ndio maana walipotea barabara

Taarifa zilizoko Sumbawanga ni kuwa Lisu Hana uwezo wa kuwa Raisi kwa Test hiyo ya wana Sumbawanga ambayo kafeli
Nyie wachovu tu, hamna madhara yoyote kwa chama kubwa, endeleeni kubweka tu, ila meno yenu yako tume, nyie ni sawa na mbwa vibogoyo.
 
Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
6,588
2,000
Hilo La Lisu kupotea njia wachawi wa Sumbawanga alipokuwa na mkutano walimpima Kama kweli Uraisi anauweza sababu kuwa Raisi ni pamoja na kutawala wachawi

Hivyo wakam test yeye na msafara wake wamewaona hamna kitu ndio maana walipotea barabara

Taarifa zilizoko Sumbawanga ni kuwa Lisu Hana uwezo wa kuwa Raisi kwa Test hiyo ya wana Sumbawanga ambayo kafeli
Nimekuelewa! Hapa unathibitisha pasi na shaka kuwa Yale ya kuwarundika waganga na wachawi wa Kanda ya ziwa kwa akili ya kumzindika mwenyekiti wenu yakisimamiwa na bashite ni kweli!

Kwa taarifa yako na wachawi wenzako, uchawi wenu ulishashindwa siku nyingi kwani Lissu analindwa kwa damu ya Yesu aliye hai Leo na daima!

Kawaleteni wale wachawi wa Senegal Tena!
 
Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
7,148
2,000
Hilo La Lisu kupotea njia wachawi wa Sumbawanga alipokuwa na mkutano walimpima Kama kweli Uraisi anauweza sababu kuwa Raisi ni pamoja na kutawala wachawi...
Bado mpo tu kwenye mambo ya"Meta-Physics". Halafu eti na nyie mnawaza maendeleo, eti kuwa kiongozi lazima uwe mshirikina. :p :p Bado tuna safari ndefu sana, bado mno.
 
Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
47,939
2,000
Jana Tarehe 18/09/2020 Mgombea wetu wa Urais TUNDU LISSU alikuwa na ratiba ya kufanya Kampeni katika Mkoa wetu wa Katavi maeneo ya Majimoto katika jimbo la Kavuu Wilaya ya Mlele na Mpanda MJINI katika jimbo la Mpanda...

Sasa mnatakaje kumpa mtu Urais wakati wako zaidi ya 100 lakini wanapotea tena hapa hapa tanzania? Sasa huyu Urais wa nini ikiwa yeye na wenzie 100 wanapotea?
 
Fast Forward

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
442
500
Hilo La Lisu kupotea njia wachawi wa Sumbawanga alipokuwa na mkutano walimpima Kama kweli Uraisi anauweza sababu kuwa Raisi ni pamoja na kutawala wachawi

Hivyo wakam test yeye na msafara wake wamewaona hamna kitu ndio maana walipotea barabara

Taarifa zilizoko Sumbawanga ni kuwa Lisu Hana uwezo wa kuwa Raisi kwa Test hiyo ya wana Sumbawanga ambayo kafeli
Daah kwa hiyo hii post umeifikiria vizuri au wamedukua ID yako ?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom