Viongozi wakuu Tanzania wanafanya kazi nzuri sana wapongezwe, waombewe kwa Mungu

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
8,166
11,569
Ni dhahiri na ukweli usiopingika, Dr.Samia Suluhu Hassan, Rais na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalamaTZ, na safu yake nzima ya viongozi serikalini.

Wanaiongoza nchi kwa umahiri mkubwa, uwazi sana, weledi wa viwango, upendo, bidii na mapenzi ya dhati sana.

Mipango yao inachochea sana maendeleo ya watu na vitu. Tena ni kwa waTanzania wote bila kujali rangi, vyama, dini au kabila zao.

Bali wote wananufaika kwa haki, usawa na matunda ya kazi za viongozi hawa waliobarikiwa na Mungu, kiuchumi, kijamii, kisiasa, kiutamaduni Sayansi na Tecknologia yanaonekana kwa wananchi wenyewe.

Tuwapongeze na kuwatia moyo sana. Wasonge mbele bila kuchoka wala kukata tamaa. Nchi imefunguka, maendeleo yanaonekana, tuchape kazi na tusonge mbele sasa.

Tuwaombea kwa Mungu, afya njema, utimamu wa mwili na Roho katika kuwatumikia waTanzania wote. Aimen.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Upumbavu mtupu!

Hayo majizi labda uyaombee wewe, si ajabu Tanzania kuna matapeli wanapose kama manabii kumbe wanatapeli watu.

Labda mjinga ndio apoteze muda kuombea majizi na matapeli ya kisiasa.

Hawa viongozi halali yao wengi ilikua ni nyuma ya nondo tu kwa sasa tupate sura mpya zenye uchungu na kodi za wananchi.

images (20).jpeg
 
Kwani chawa hiyo kazi imewashinda hadi mtake Kila mtanzania afanye kazi ya kujipendekeza kama nyinyi?
Mwenyezi Mungu akujalie utulivu, ustahimilivu na subra.

Usikate tamaa, anaweza kwako na anaweza kwa wengine pia.

Mungu ni wakwtu sote, tuombeane mema kwa upole na upendo.

Ni hiari...
 
Ikiwezekana tuchangishe hela mwisho wa mwaka tuwakabidhi kama shukrani ya kujitolea kufanya kazi ngumu sana ya kupambania maendeleo ya taifa letu au nasema uongo ndugu zangu ?
Tuwaombee tu, afya njema, hekima na Busara ya kuongoza vema nchi yetu, na hayo mengine Mwenyezi Mungu atawoongeza kwa ziada kwa wakati wake...
 
Upumbavu mtupu!

Hayo majizi labda uyaombee wewe , si ajabu Tanzania kuna matapeli wanapose kama manabii kumbe wanatapeli watu .

Labda mjinga ndio apoteze muda kuombea majizi na matapeli ya kisiasa.

Hawa viongozi halali yao wengi ilikua ni nyuma ya nondo tu kwa sasa tupate sura mpya zenye uchungu na kodi za wananchi.
View attachment 2819940
huruma ya Mungu iambatane nawe daima, pole ndugu mwenzangu...

ni katika Roho na Kweli, tunamshiriksha Mungu katika maumivu, hasira, na ghadhabu zetu dhidi ya uharibifu. Na Mungu mwenyezi atupendae, hawaachi waja wake wakilia tuuu.. na kunung'unika bali huwaonyesha njia ya kupita kwa salama na Amani,

Usiogope, usikate tamaa..
Muombee tuu... hata kama ni adui yako, ili aishi siku nyingi, ili unapobarikiwa wewe ajionee kwa macho baraka na neema alizokujalia Mungu wew uliekua ukiteseka...
 
Back
Top Bottom