Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 877
- 4,105
Watu wengi wasiotenda haki ni wepesi sana kuamini katika kulogwa na kudhurika. Upenda sana kuifanya jamii ionekane kama ina kizazi cha watu wakatili na ambao wasingependa wenzao wafanikiwe.
Kwa upande wa pili viongozi hawa upenda sana simpathy na perfection huku walio chini yao wakitakiwa kuwa wajinga na wasio fikiri sawa sawa.
Ni kundi la watu lisilopenda kujiridhisha kwa chochote badala yake kila kinachoingia ndani ya masikio yao ukurupuka na kukifanyia kazi bila kujali kinadhuru wangapi.
Kwao wao familia ni yeye na familia yake na siyo jamii au Taifa. Upenda kuambatana na binadamu ambao uwafanya kama watumwa. Upendelea sana kujikweza na kuambatana na binadamu wakumlinda bila kumtegemea Mungu.
Viongozi hawa ni wepesi sana kuondoa uhai wa mtu kwa kigezo cha maendeleo. Kwao wao maendeleo ni elimination; kwao wao hakuna checks and balance na anayeheshimika japo kinafiki ni yule aliyewazidi cheo.
Kundi la watu wa aina hii limeanza kuongezeka nchini na watawala wamekuwa wakiwatumia kutimiza malengo yao. Mwanasiasa anaamini kuwa na kiongozi asiyeheshimu sheria na katiba ya nchi ni sahihi as long as familia yake na yeye mwenyewe awahesabiki kuwawakosefu katika macho ya binadamu.
Tanzania inaanza kuacha misingi ya utu na kwenda kwenye misingi ya vitu. Viongozi wa sasa kwao watu ni silaha ya kuangamiza wenzao na siyo silaha yakuunganisha watu.
Kinachofanywa kwa ubaya kwa viongozi wa sasa hakitachukuliwa hatua endapo aliyetenda anaweza kuwafikia na wanakunywa nakula naye. Mafisadi Tanzania ndio watoa maamuzi kuhusu siasa na wananchi wanyonge. Magereza yanajazwa maskini huku matajiri wakiishi kwa kuamua wafanye uhalifu gani kwa wakati gani.
Lini utatambua kwamba tunakosa?