DOKEZO Viongozi Tegeta Kwa Ndevu wawajibishwe kwa kushindwa kuzuia uchafuzi wa mazingira unaotokana na machinjio/soko la kuku

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Hawa viongozi ni wala rushwa wakubwa wanasababisha wakazi wa eneo lile tuteseke kwa harufu kali sana wakati wa usiku inayotokana na mabaki ya kuku.

Iko hivi...

Nyuma ya kituo cha daladala cha 'Kwa Ndevu', Tegeta kama unaelekea Bunju kuna mtaro mkubwa unaopeleka maji kwenye mto ulio katikati ya Kituo Kipya na Kwa Ndevu. Nyuma ya Kituo cha kwa Ndevu kuna machinjio ya kuku. Hivyo inapofika usiku kuanzia saa nane, kuna bomba linaelekezwa kwenye huo mtaro halafu yanafunguliwa maji yanayotoka machinjioni.

Yale maji yananuka sana sijapata kusikia harufu ya vile tokea nizaliwe. Nilikuwa nimekaa na bodaboda na bajaji ikabidi tukimbie. Nilipohoji nikaambiwa ile ni kawaida, viongozi wa mtaa huo walishaambiwa ila wakapozwa kidogo. Polisi nao walishakuja ila nao wakapozwa hivyo hakuna ufuatiliaji kabisa, tunabaki kuumia tunaotumia huduma za pale maana kuna soko kubwa tu na wengi mahitaji tunapata pale.

Mamlaka zichukue hadhari kabla ya maafa makubwa hayajatokea.

PICHA: Mabomba ya kimkakati yanayoletwa usiku wa manane kufanya uchafuzi wa mazingira. Mchana ukipita pale huyakuti. Mnaweza kuona aina ya uchafu unaotoka kwenye mabomba hayo.

T2.jpg
T1.jpg
T3.jpg
 
Back
Top Bottom