kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,307
- 12,602
Kuona ni kuamini, think globally and act locally. Tunaomba viongozi wetu wa bara la Afrika tuliowasafirisha kwenda New York kwa kodi zetu kuhudhuria mkutano mkuu wa Baraza la Dunia, UN mrudi nyumbani na mipango mkakati ya kuboresha maisha ya watu wenu.
Sina shaka kila kiongozi aliyekwenda New York aliona na kusikia mambo mengi huko yakiwemo maduka makubwa (Malls) yaliyosheheni bidhaa zenye ubora, lakini sisi wananchi wenu tungependa mrudi na yafuatayo:
1. Usafi wa mitaa na majengo ya New York unafanyukaje. Je wana takataka zilizozagaa barabarani wala vibanda vya wasiokuwa na ajira kwenye njia za waenda kwa miguu?.
2. Mkutane na marais waliopatikana kwa njia za kidemokrasia, muwaulize wao wanafanye?
3. Mkutane na wenyeviti wa vyama vya siasa mjue vinavyoendeshwa
4. Uchumi wao unavyoendeshwa na kusimamiwa.
5. Namna ya mikataba ya kimataifa inavyofungwa na mambo ya kuzingatia wakati wa kuingia mikataba
6. Namna bidhaa zetu zinavyoweza kupenya kwenye masoko yao kwa wepesi
7. Mpate na mrudi na elimu ya namna mifuko ya jamii inavyojiendesha na kusimamiwa
8. Ulizeni uhusiano uliopo kati ya kulipa mishahara mikubwa watumishi na ukuaji wa sekta nyingine kama viwanda, kilimo, biashara, afya na elimu.
9. Ulizeni kuhusu adhabu wanazopewa wakwepa kodi na wanaoiba mali za umma.
10. Waulizeni namna wanavyodhibiti ubora wa bidhaa na huduma zinazozalishwa, kutolewa na kuingia kwenye masoko yao.
11. Kilimo chao wanalima vipi na wakulima wanawezeshwa vipi ili kulima kwa tija.
Ni matumaini yetu kuwa muda wa kujifunza haya mambo 11 mnao huko, tafadhalini sana msirudi nyumbani na mabegi mapya makubwa ya nguo kutoka huko na kuja kuendelea na business as usual.
Ni aibu kubwa kuyaacha mazuri yote hukohuko na kubeba suti zake na za uwapendao.