kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,319
- 12,622
Viongozi wa nchi zote za dunia wanakutana Marekani kwenye mkutano mkuu wa Baraza la usalama la umoja wa mataifa (General Assembly of United Nations). Hotuba nyingi za viongozi kutoka Afrika ni za malalamiko kuhusu nchi za Magharibi na Marekani kama chanzo Chao kikuu Cha matatizo kwenye nchi zao. Hotuba nyingi za viongozi wetu ni kuhusu wazungu kutotimiza ahadi zao za kutoa mapesa kwa nchi za Afrika kugharimia miradi Yao, madeni makubwa wanayodaiwa na ukosefu wa masoko na technology.
Bahati mbaya sijamsikia kiongozi wetu hata mmoja akizungumzia shida wanazozisababisha wao wenyewe kama vile:
1. Kuiba kura kwenye chaguzi
2. Kung'ang'ania madarakani
3. Wizi wa mali za wananchi wao na ubadhilifu.
4. Matumizi mabaya ya mikopo wanayopewa.
5. Kushindwa kukusanya kodi
6. Rushwa kwenye nchi zao.
7. Viongozi kujiwekea kinga za kutokushitakiwa.
Bahati mbaya nchi za Magharibi wanayajua madhaifu yote ya viongozi wa Afrika, ndio maana wakati wa hotuba za viongozi kutoka Afrika Wazungu wengi wanapuuza na wanatoka nje.
Afrika hawana mshipa hata mmoja wa aibu, kazi Yao ni kuwanyooshea vidole nchi za Western na kusahau udhaifu wao kwanza.
Mfano, nani anawazuia nchi za Afrika kuuziana bidhaa wao kwa wao kwa kutumia fedha zao. Nani kawazuia waafrika kuondoa VISA kati ya nchi na nchi ili watu Waafrika wawe huru kwenda na kutoka nchi nyingine ya ya Africa kufanya kazi au biashara? Nani kawazuia waafrika wasilime chakula Chao? Nani kawazuia kukusanya kodi?