Viongozi Kama Rais Samia Wenye Mioyo ya uvumilivu Hawazaliwi kila Siku Na hawapatikani kila nchi, Watanzania Tuna kila Sababu ya kushukuru kumpata

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,305
9,734
Ndugu zangu huo ndio ukweli ulio wazi, Mtu kuwa kiongozi hakubadilishi Tabia yake ya Asili, Kama mtu alizaliwa Ni katili Basi fahamu ya kuwa akipata madaraka atakuwa katili zaidi ya awali kwa kuwa tu Anayo Amri ya kuamrisha lolote kufanyika, lakini pia Kama mtu alizaliwa na moyo wa upendo na uvumilivu hata akipata madaraka Ataendeleza Tabia hiyo na atataka kupanda mbegu hiyo kwa wateule wake na wale anao waongoza ili waishi kwa kuvumiliana hasa kwa kutambua ukweli kuwa Ni kawaida ya binadamu kutofautiana kimtizamo

Tabia ya mtu hata Kama alikuwa anaificha lakini akishapata madaraka au mamlaka fulani yanayomuweka katika nafasi ya kufanya maamuzi ya mwisho au kutoa Amri Ni lazima mnaoongozwa au mliochini yake mtaitambua tu Tabia yake Ni ipi, kwa kuwa mamlaka na madaraka hufunua Tabia ya mtu ya Asili, kwa kuwa madaraka humfanya mtu asiye makini kujiona yeye Ni Alfa na Omega na hivyo kuona hakuna kama yeye hapa Duniani, wakati mwingine anaweza kuhisi yeye anafaa kuwa biblia au kurani Takatifu , kanisa au msikiti wa kuabudiwa na kuswalia,

Ndugu zangu lakini ukimfuatilia na kumtizama mh Rais Samia Ni mtu na kiongozi mwenye moyo wa uvumilivu Sanaa, Ni kiongozi anayemheshimu kila mtu, Ni kiongozi ambaye Hataki amuumize mtu kwa kutumia madaraka yake ya Urais, Ni kiongozi ambaye anataka hata wateule wake watambue ya kuwa kiongozi unapaswa kuwa na ngozi ngumu na moyo unaopaswa kuwa na uvumilivu na Subira, Ni kiongozi ambaye hata asemwe na kutukanwa vipi huoni akihemuka au kuamrisha vyombo vyake vya ulinzi alivyokabidhiwa kisheria kuchukua hatua

Nikiongozi anayesikiliza kila sauti hata zinazomkosoa kwa kumkosea heshima, Anasoma kila andishi bila kujari limeandikwaje, Nikiongozi anayefanya maamuzi kwa kufuata misingi ya Sheria na utawala Bora, Ni kiongozi anayemhurumia kila mtu hata aliyemtusi Jana, Ni kiongozi ambaye anamchukulia kila mtu kuwa anapaswa kupewa nafasi ya kusikilizwa hata Kama anamaneno ya kuuzi na yasiyo na adabu, kwa uvumilivu wake ndio maana anaweza kukaa na kujadiliana na yeyote

Rais mama Samia Ni kiongozi aliyejiweka katika Ubinadamu na siyo Umungu mtu au malaika aliye Duniani ,Hataki kuabudiwa Wala kusujudiwa kwa kuwa anafahamu kuwa anayesitahili hayo Ni Mwenyezi Mungu tu, Ni kiongozi anayejifunza kwa kila mtu na Nikiongozi anayefundisha na kuelekeza kila panapohitajika,

Hivyo ningependaa watanzania wenzangu na wazalendo wa nchi hii, Tumpende Sana mh Rais wetu, Tumheshimu Sana Rais wetu, kwa mlio na hoja za kumkosoa Nawaombeni mtumie lugha za staha na heshima, Tumieni maneno ya heshima na busara, kuweni Kama watu mliopata malezi Bora toka kwa wazazi wenu, utanzania wetu Ni wakuheshimiana na kupendana Sana, kuvumiliana na kukosoana kwa staha, Hawa wanaotumia lugha za matusi lazima tuwakumbushe misingi ya Taifa letu

Ni Mara ngapi tunaona watu Kama wanaharakati wanaodai Uhuru wa maoni wakiwablock watu kwenye kurasa zao kisa tu wamekosolewa? Wangapi tunaona wakiwa futa watu Hadi kwenye list zao za majina kisa wametofautiana mitizamo? Wangapi Tumeona wakiwatukana watu wanaowakosoa? Wangapi Tumeona wakiwablakilisti wenzao wanaonekana kuwa wakosoaji wao? Unazani wangekuwa na mamlaka watu Hawa wangefanya Nini? Unazani wangeua wangapi? Unazani wangetesa wakosoaji wao wangapi? Unazani wangevumilia kukosolewa? Hapana wasingevumilia hata kidogo

Sasa Kama sisi tunaumizwa tunapokosolewa tu kwa lugha Kali kwanini tusione kuwa mh Rais wetu mpendwa Naye Ni mwanadamu mwenye moyo wa nyama ambaye Naye anaumia Kama sisi? Kwanini Tusimheshimu Kama nasi tunavyopenda kuheshimiwa? Kwanini msimkosoe kwa lugha za heshima na staha? Mataifa mangapi tunaona namna wapinzani wakipigwa,wakijeruhiwa, wakifungwa vifungo vya maisha, wakimwaga Damu zisizo na Hatia, wakivunjwa viuno na mbavu, wakifirisiwa Mali zao na wakinyimwa hata nafasi ya majadiliano na watawala?

Lakini hapa Tanzania chini ya mama shupavu mama Samia suluhu Hassani huwezi kuyakuta mambo hayo, Nasema hivi mama yetu na Rais wetu Aheshimiwe, Uhuru huu alioutoa usije kuwa Kama kichaka Cha kumdhalilisha Rais wetu, vitoto vidogo vilivyokosa adabu na malezi ya wazazi wao viambiwe wazi kuwa huyu Ni Rais wa nchi anayepaswa kuheshimiwa na kulindwa kwa nguvu zote, Hii Ni Taasisi inayopaswa kuheshimiwa na kulindwa, wahuni na waliokosa adabu lazima waambiwe kuwa huyu mama yetu Ni Rais wa Tanzania na Siyo Rais wa Bendi ya mziki wa uchochoroni huko, Huyu Ni Rais mwenye mamlaka yote ya kikatiba na kisheria, Siyo Rais wa genge la walevi, Siyo Rais wa Bao huyu, Asifananishwe na yoyote kimamlaka na kimadaraka

Kazi iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Ni Mimi Lucas Mwashambwa kijana mzalendo na mpenda nchi yangu na ninayeendelea kumuunga mkono mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani katika juhudi zake za kututumikia watanzania kwa moyo wake wa upendo na uzalendo mkubwa Sana, Asante
 
I wish kujua maisha yako Lucas nje ya mitandao. Sio kwa ubaya lakini.
 
Sifa kama hizi walipewa pia viongozi wengine wakati wa maisha ya uraisi wao. Hata wataokuja hapo baadaye watamiminiwa pengine sifa zaidi ya hizi ijapokuwa yote wanayoyafanya ni majukumu yao ya kikatiba.

Sidhani nchi zilizotuzidi kimaendeleo wana tabia kama hii ya kusifu na kuabudu viongozi wa nchi waliokuwepo madarakani. Kwa nchi yetu hii tabia sasa imezidi kipimo.

Kila afanyacho Rais ni sifa na pongezi tu, hata kwa "trivial things"!. Akiboronga kashauriwa vibaya.
 
Tuendelee kujenga nchi yetu tu
Sasa wewe mbona hujengi nchi? Unadhani wewe unajenga nchi kwa articles zako hizi au unajenga uchawa?

Inawezekana mama anafanya vyema somehow ila usizidishe sana uchawa bloo, unaharibu mwishowe.
 
Sasa wewe mbona hujengi nchi? Unadhani wewe unajenga nchi kwa articles zako hizi au unajenga uchawa?

Inawezekana mama anafanya vyema somehow ila usizidishe sana uchawa bloo, unaharibu mwishowe.
Nashukuru kwa uungwana wako wa kukubari kuwa mh Rais wetu mpendwa anafanya vizuri, huo ndio uungwana
 
Sifa kama hizi walipewa pia viongozi wengine wakati wa maisha ya uraisi wao. Hata wataokuja hapo baadaye watamiminiwa pengine sifa zaidi ya hizi ijapokuwa yote wanayoyafanya ni majukumu yao ya kikatiba.

Sidhani nchi zilizotuzidi kimaendeleo wana tabia kama hii ya kusifu na kuabudu viongozi wa nchi waliokuwepo madarakani. Kwa nchi yetu hii tabia sasa imezidi kipimo.

Kila afanyacho Rais ni sifa na pongezi tu, hata kwa "trivial things"!. Akiboronga kashauriwa vibaya.
Lazima apongezwe anapofanya vizurii hata Kama Ni wajibu wake, Kwani wangapi unaowafahamu wewe walioshindwa kutimiza majukumu yao? anapotokea kiongozi Kama mh Rais wetu mpendwa mama Samia anatekeleza wajibu wake vyema Ni wajibu wetu na tunapaswa kumpongeza na kumpa faraja ya kusonga mbele kwa kuwa tupo Naye bega kwa bega
 
Ndugu zangu lakini ukimfuatilia na kumtizama mh Rais Samia Ni mtu na kiongozi mwenye moyo wa uvumilivu Sanaa,
Mkuu Lucas mwashambwa, naunga mkono hoja na Hata akina sisi hili tumeisha lisema humu. Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye? na Psychoanalysis Trends za Viongozi Wetu, Humbleness ya Rais Samia ni Bonafide Genuine, ni asili yake, ni nature yake, ndivyo alivyo, Ila...
Ni kiongozi anayemheshimu kila mtu, Ni kiongozi ambaye Hataki amuumize mtu kwa kutumia madaraka yake ya Urais, Ni kiongozi ambaye anataka hata wateule wake watambue ya kuwa kiongozi unapaswa kuwa na ngozi ngumu na moyo unaopaswa kuwa na uvumilivu na Subira,
Haya yote ni kweli na sisi wengine tulimbaini kitambo kabla hajawa rais Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” na "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Ni kiongozi ambaye hata asemwe na kutukanwa vipi huoni akihemuka au kuamrisha vyombo vyake vya ulinzi alivyokabidhiwa kisheria kuchukua hatua
Ila pia aliishatoa onyo kwa waparaji "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

Tuendelee kumsifu rais Samia kwa mazuri yake, ili tuepuke kuanza kumuimbia mapambio na kujikuta tumevuka mipaka na kumponza bure bila sisi kujijua Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda

P
 
Back
Top Bottom