Viongozi, Kabla ya kuongea na jamii kuweni na maamuzi ya pamoja ili kuepusha kupingana wenyewe

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Viongozi wetu mnafanya kazi kubwa sana katika kuhakikisha Jamii inafika au inapata kile ambacho inakusudia kupata kutoka kwa viongozi waliowachagua au kuwaweka madarakani. Katika kuhakikisha hili kumekuwa na mambo mbalimbali ambayo viongozi huja kwa raia na kuyatolea matamko au maagizo pamoja na maamuzi mbalimbali.

Kuna jambo la kushangaza pale ambapo viongozi wanakuja kutoa kauli ya jambo moja ila kila mmoja anatoa kauli au maamuzi yanayopingana na mwenzake, sisi kama jamii tunabaki kujiuliza ina maana hawa viongozi huwa hawana maelewano au hawakai kukubaliana na kupanga nini kinatakiwa kusemwa kwa jamii au kila mmoja anayejisikia anasema cha kwake tu bila kujali kuwa kuna kupingana kwa kauli kunakowachanganya raia.

Anaweza kuja kiongozi wa kwanza akasema nimefuta ushuru fulani watu makashangalia kuwa angalau tutapata nafuu ya maisha kwa sehemu fulani, cha kushangaza anakuja kiongozi mwingine anashangaa inakuwaje ushuru huo ufutwe kwa nini umefutwa na kuanzia sasa umerudishwa! Hii inaibua maswali mengi kwetu hawa hawana maelewano au huwa hawawasiliani,na kama hakuna mawasiliano wanawezaje kuendesha serikali au kuongoza bila kuwa na mawasiliano ya nini kifanyike, Au ndio sababu ya kuonekana kwa mashimo mengi katika uongozi wao?

Hebu fikiria fikiria unaambiwa tumefuta tozo ya mafuta halafu muda kidogo anakuja kiongozi mwingine kusema ilifutwa kimakosa huonikama manafanya tuwaone mnaongoza kwa matukio? Au mnatengenezeana uadui na jamii? Ni bora kabla ya kutoa tamko au agizo lolote mkubalieni kwanza kwa sasa hiki ndio kinatakiwa kusemwa au haya ndio maamuzi yetu kwa pamoja ili wote muwe na kauli moja. Hii itawafanya muonekana mnafanyya kazi kwa umoja na kwa mshikamano na kuondoa sintofahamu kwa jamii mnayoingoza.
 
Kiufupi nchi ipo kwenye autopilot inajiendesha yenyewe
Hata wakati wa JPM yalitokea hayo ya kuoingana.. Nakumbuka ishu ya ndoa na cheti cha kuzaliwa iliyitilewa na Mwakyembe lakini ndani ya masaa 24 JPM akatengua tena kwa kejeli kwamba inawezekana hata Mwakyembe mwenyewe hakuwa na heti cha kuzaliwa
 
Hiyo tisa, kumi ni pale hata Bunge la Jamhuri linatunga sheria fulani leo muda kidogo hata utekelezaji wake bado haujaanza wanatuletea mapendekezo ya amendment for article X, section Y. Nyingi tu hizi . Hivyo ndivyo tulivyo unapokosa watu makini ktk uongozi.
 
Back
Top Bottom