Mkuu wa Wilaya Morogoro Mjini futa kauli ya kwamba ukisema umesema

Tsyamatsy

Senior Member
Sep 9, 2023
109
155
Leo asubuhi ulikuja kuonana na wazazi na majirani wa shule ya Msingi JUHUDI, kata ya Lukobe, ukiambatana na Mkurugenzi wa Manispaa. Kuja kwako ni kutokana na Jana wazazi wa wanafunzi wa JUHUDI primary school kuchoshwa na kinachoendelea na Viongozi kuchezea na KUHATARISHA MAISHA ya watoto wetu wanaosoma hapo JUHUDI.

Ni kuchezea maisha ya watoto wetu Kwa sababu pale si mahali salama kabisa Kwa watoto, pamekuwa kama dampo, nawe umejionea Wala sio kuambiwa. Kuna KIPINDUPINDU, Kuna kuharisha n.k. Au mpaka itokee na watoto wakifa ndipo mje kutoa pole! Itasaidia nini? Kinga ni Bora kuliko Tiba.

Wananchi wamekuwa wakilalamika Kwa muda mrefu sana zaidi ya miaka 3 lakini hakuna ufumbuzi Bali Viongozi wamekuwa wanakuja mara Kwa mara na kutoa Ahadi ambazo hakuna hata moja iliyotekelezwa.

Kwa iyo wazazi waliamua Jana kwamba wapange Leo kuja kuleta kilio ngazi za juu, ndipo taarifa alifikishiwa mkurugenzi, nae bila ya kuchelewa aliomba wazazi tumsubiri aje aongee nasi, na Jana hiyo hiyo Pasipo kuchelewa alifika na kuongea na wazazi na kueleza kuwa mkuu wa wilaya atakuja Leo na atatoa tamko kuhusu mustakhabali wa shule.

Leo umekuja na kutueleza kitakachoendelea kuhusu shule hiyo, sawa. Lengo la waraka huu ni kauli zako ambazo zinaonekana ni za KIBABE.

Mojawapo ya kauli hizo ni pale ulipojulishwa na wazazi kwamba walikuwa wanapanga kuleta kilio Chao kwenu, Wewe ulijibu KIBABE, kuwa 'Huwezi kuja ofisini kwangu bila ya taarifa!

Hivi, wewe ni kiongozi gani ambae unakatisha tamaa wananchi wako wakiwa na dharula wasije kukuona! Wakimbilie wapi? Ebu tueleze!

Tunavyoelewa Viongozi wa watu, milango yao Iko wazi muda wote Kuhudumia wanao waongoza. Na Kila mara Viongozi hao wamekuwa wanawarai watu wao wasisite kuwaona pindi wanapokuwa na matatizo, Sasa wewe mkuu hujui kuwa cheo ni DHAMANA?

Kauli nyingine uliyosema wewe ni Mkuu wa wilaya UKISEMA umesema, Kwa kuwa wewe ni Mkuu wa wilaya! Kwa iyo wewe ndio Alfa na Omega?? Huna waliojuu yako? Hili ndio swali watu walipokuwa wanaguna na ile minong'ono uliyoisikia pale ulipotamka Hilo. Watu walibaki wanajadiliana kuhusu hizo kauli zako.

Kwa faida yako mkuu, Jana wakati mkurugenzi alipotufahamisha kuwa mkuu wa wilaya utakuja Leo, baadhi ya wananchi wanaokuelewa walitujulisha kwamba tujiandae, kwani mkuu wa wilaya ana kauli za KIBABE, Kwa iyo pale sisi tulishajiandaa na kweli tumejionea.

Ndiyo maana hatukuwa na maneno mengi, na hatukuridhika Bali hadi alipokuja Mheshimiwa Mbunge ndiye aliyeturidhisha na kutuliwaza.

Kutokana na hayo yaliyojiri Leo wananchi wa JUHUDI wamewaambia Mbunge wao Mheshimiwa Abood na Diwani wao Mheshimiwa Mbilinyi wakufikishie ujumbe kuwa kauli zako ni mbovu! Mengine siandiki hapa ila Mbunge na Diwani wakueleze wananchi jinsi tulivyokereka na kauli zako

KUHUSU UJENZI WA SHULE:
Umetoa kauli ya kushangaza sana kuwa ni Wazazi waliolazimisha shule kujengwa hapo.

Swali kwako mkuu, Hivi, hii shule ni ya binafsi au ni ya serikali?

Jibu la dhahiri bila kupoteza muda ni ya Serikali.
Mkuu, hujui kwamba UJENZI wowote wa majengo ya Serikali unasimamiwa na waandisi wa serikali.

Haujengwi hovyo hovyo tu. Suala hata kama ni kweli wananchi walipendekeza hapo lakini ni wataalamu ndio waliokuwa na maamuzi ya mwisho kama hapo mahali ni salama au Hatarishi, na kama si salama na mtaalamu anaejua kazi yake amekubalije kuubariki huo UJENZI? Je,mwananchi anamaamuzi ya kitaalamu?

Suala la UJENZI WA majengo ya Serikali ni ya kitaalamu na Wala sio ya kiholele. Sio Siri na hata Leo ulipolitamka Hilo wananchi walikataa kabisa kuwa walitaka iyo shule ijengwe hapo, Sasa wewe unalazimisha nini! Wakati wananchi wanakataa mbele yako! Hivi mkuu hayo mazingira ulipokuwepo Leo asubui pale kweli uliona ni Halali Kwa kutoa elimu Kwa watoto pale?

Mkuu nakutaadharisha kuwa ipo siku wananchi watalalamika kuhusu hizo kauli zako za KIBABE mbele ya Viongozi ambao sisi wananchi tunaamini wanakuzidi wewe cheo tena mbele ya kadamnasi, usishangae siku iyo kiongozi mkuu anakutana na kauli zile za " Hatumtaki huyo Ondoka nae!" Wewe sio wa kwanza na nafikiri umeshajionea hayo yakitokea!

Alhamsiki!
 
Back
Top Bottom