Viongozi wapimwe VVU kabla ya uteuzi. VVU huathiri ubongo, hivyo inawezekana ndiyo sababu ya maamuzi mabovu tunayoyaona

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,792
3,360
Nimewahi kukaa na Mzee mmoja mstaafu, akanipa kaukweli fulani kuhusu aina ya viongozi tulionao.

Kuwa ,
1. Hawashauriki kwa mambo yaliyo wazi.

2. Hawako makini kwenye maamuzi.

3. Hawana upeo wala mkakati wa kuifanya Tanzania ipate maendeleo endelevu, wanajali la leo tu.
Alitolea mfano wa uendeshaji wa bandari zetu, sera za kilimo na mifugo, na madini ikiwemo gesi na mafuta.
Kuhusu Bandari, alisema, sehemu pekee kubwa ambayo ingeweza kudhibiti utoroshaji wa maliasili zetu mfano wanyama,madini nk ni bandarini. Hivyo, bandari ilitakiwa kusimamiwa kwa 100% na serikali. Akasema, kumbukumbu zinaonyesha Waasia wakiwemo Waarabu ndo wamepatikana na visa na kesi nyingi za utoroshaji pembe za ndovu, uwindaji batili , dhahabu nk. Leo ndo tumeamua kuwapa bandari,tunatarajia nini?

Kuhusu Kilimo na Mifugo, Mawaziri waliopewa hizo nafasi, hawana sera wala malengo ya kukuza kilimo wala mifugo. Wameona kama Wakulima na Wafugaji nchini hawajui cha kufanya.

Maamuzi yao yataligharimu Taifa hapo baadaye. Alisema, Kijana anaemaliza Chuo Kikuu siyo wa kwenda kujifunza namna ya kupanda mahindi kwa mistari. Unamrudisha nyuma kwa kumpa kazi ya Mkulima au Mfugaji.

Ingekuwa hivyo, kulikuwa na maana gani msomi huyo kupoteza rasilimali za nchi kumsomesha chuo miaka yote hiyo? Eti, wanalinganisha msomi wa nchi changa na zilizoendelea¡ Anasema, huko ni kukosa ubunifu wa namna ya kutumia vyema rasilimali watu hapa nchini.

Mzee anasema, nyanya zinazolimwa hapa nchini hukosa soko, hivyo vijana hawa, walitakiwa kuanzia hapo kuondoa hali hiyo, na siyo kuongezea tatizo.

Unamchukua kijana msomi unaenda kumfukia ardhini kule Mahenge. Huko ni kuizika elimu yake. Alitarajia vijana hao wapambanie soko la ushindani na Kenya, Uganda nk kuhusu uongezaji thamani ya nyanya inayotoka kwa mkulima. Leo tomato sausage inayotumika hapa nchini 80% inatoka Kenya na nchi jirani.

Kuhusu madini, nchi haina maono ya kuendeleza vyema sera ya madini. Viongozi wengi wanaona muwekezaji wa nje ndiyo suluhisho. Anasema, bila kuwa na wataalamu wetu wenyewe na wazalendo. ni kazi bure. Wanaokuja kuchimba siyo wajomba zetu.

Kuhusu viongozi waliokasimiwa kusimamia wananchi kwa karibu mfano ma DC, RC, DED nk, hawana maadili mema. Anasema yawezekana wengi wameingizwa kindugu au wana upungufu mkubwa katika kufikiri na kuamua jambo sahihi. Wengi siyo wabunifu. Wanatupiana mipira kufanya hata maamuzi madogo tuuu. Kuna wanaopaka wanja na lipstick mida ya kazi.

Anasema, yawezekana wengi hawapimwi afya hasa za akili kabla ya teuzi. Na hii ni kwa vile siku hizi imeonekana, lengo la uteuzi ni ili Ndugu yangu fulani apate kazi. Alitolea mfano wa Mkuu wa sasa wa Mkoa wa Dar'es-salaam. Kuwa, Kufunga madanguro ndo kipaumbele kupita vyote vya kumpa umaarufu, huku Mji ukinuka kila sehemu kwa uchafu hasa kipindi hiki cha mvua.

Sasa, je kuna haja ya viongozi wetu,hasa wa kuteuliwa kupimwa afya zao kabla ya teuzi? Na ni nani wa kuthibitisha hilo?

Taarifa na ripoti mbalimbali za WHO, zinaonyesha watu chini ya miaka 45, ndiyo waatirika wakubwa wz HIV hasa nchi zinazoendelea kama Tanzania. Na bahati mbaya au nzuri,rika hilo ndo viongozi wengi wa kuteuliwa tulio nao hivi sasa hapa nchini.

Sina uhakika sana ni tafiti ya aina gani tutafanya ili kuhusianisha ninalosema lilandane na vipimo vya afya za waliotumbuliwa na Mh Rais mwaka huu kwa kushindwa kufanya kazi zao.

Ninao baadhi ambao baada ya kutumbuliwa, na kwa utafiti wangu binafsi, nimethibitisha pasi shaka kuwa, wana tatizo la msingi la muda mrefu la kiafya.
 
Hivi hili Taifa lina wazee kweli wastaafu kweli?

Je wanafurahia na yenye kuendelea kwenye taifa?

Kwa kiasi gani wanaweza kuwasaidia viongozi walio madarakani?

Deep state ya Tanzania iko na uzalendo halisi kwa taifa hili kweli?
 
Hao viongozi wamechaguliwa na/au kuteuliwa na nani kwenye nafasi zao? Madaraka yao yanadhibitiwaje? Na nani? “Deep state” ndio nini?

Hayo ndiyo maswali ya msingi ya kujiuliza na kujijibu kabla ya kuwalalamikia watu ambao huenda hata hawalazimiki kuwajibika kwa nchi wala kwa mwananchi yeyote yule.
 
Kwani Ukimwi bado upo?????
Ripoti iliyotolewa kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani Disemba 1 2023 , ni kuwa upo na unaenea kwa kasi. Mikoa ya Njombe na Iringa inaongoza kwa maambukizi ya VVU hapa nchini.
 
Back
Top Bottom