Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,898
Matamko ya mmoja mmoja hata kama anakinga ya kikatiba hayakubaliki kwa ajili ya kulinda mshikamano na umoja katika utawala wa kisheria. Ni dalili ya kuwepo ufa katika mfumo wa uongozi na nihatari kutohimili vishindo vya tetemeko la ardhi litokeapo nyumba yenye ufa.
Narudia kauli ambayo nilishawahi kumwambia Katibu Mkuu Dr. Slaa ambaye kwa sasa amefanikiwa kurekebisha kutoka safu ya juu Chadema, lakini tatizo ni kwa Ngazi ya juu Umoja wa Vijana Chadema.
Lazima kuondokana na mlipuko wa kujibu kwenye vyombo vya habari ghafla bila upembuzi wa kutosha, bila kutuliza kwanza nerves, bila kikao cha kushauriana nini cha kujibu na papo kuangalia upande wa pili wa sarafu athari zake kwa tamko litakalotolewa.
Busara inavyoonekana katika uongozi wa juu kwenye Uongozi wa Chadema naheshimu na ndicho kinachotakiwa, ila ipo kazi kuwaweka sawa viongozi wa BAVICHA.