Viongozi Chadema - must read | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi Chadema - must read

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, May 21, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG]

  Matamko ya mmoja mmoja hata kama anakinga ya kikatiba hayakubaliki kwa ajili ya kulinda mshikamano na umoja katika utawala wa kisheria. Ni dalili ya kuwepo ufa katika mfumo wa uongozi na nihatari kutohimili vishindo vya tetemeko la ardhi litokeapo nyumba yenye ufa.

  Narudia kauli ambayo nilishawahi kumwambia Katibu Mkuu Dr. Slaa ambaye kwa sasa amefanikiwa kurekebisha kutoka safu ya juu Chadema, lakini tatizo ni kwa Ngazi ya juu Umoja wa Vijana Chadema.

  Lazima kuondokana na mlipuko wa kujibu kwenye vyombo vya habari ghafla bila upembuzi wa kutosha, bila kutuliza kwanza nerves, bila kikao cha kushauriana nini cha kujibu na papo kuangalia upande wa pili wa sarafu athari zake kwa tamko litakalotolewa.

  Busara inavyoonekana katika uongozi wa juu kwenye Uongozi wa Chadema naheshimu na ndicho kinachotakiwa, ila ipo kazi kuwaweka sawa viongozi wa BAVICHA.
   
 2. N

  Njele JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Imekuwaje viongozi Chadema waige sera za vijana CCM kila mmoja kuitisha vyombo vya habari na kutoka tamko wakati wote wako ofisi moja? Nani anayewapa pesa hizo za kukodi kumbi za hoteli kutolea matamko kama si mafisadi wa CCM? Wasira ameshatamka akijua nini alichokifanya na matokeo ndiyo haya. Tuweni macho sana na hawa vijana.
   
 3. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2012
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wanajifunza uongozi, muda uliobakia unatosha kabisa kabla ya uchaguzi 2015. Isipokuwa huyo Heche kwa kweli alikurupuka nadhani alikuwa na kinyongo na Shibuda akasahau kufikiri kwanza kabla ya kutoa tamko. Kwa hiyo ajifunze kwamba uongozi hauendi kwa chuki na kuviziana kwenye kona
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Nakubaliana nawe, kiongozi unatakiwa kuwa na subira katika kutoa tamko, vinginevyo kauli inaweza kusababisha mkanganyiko na wabaya kupata nafasi ya kusema yao kama Wasira alivyosema jana.
   
 5. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,874
  Likes Received: 1,659
  Trophy Points: 280
  Katika hali ya kawaida Makamu Mwenyekiti alitakiwa kuwasiliana na Mwenyekiti wake kabla ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari! Hata kama Mwenyekiti alikosea lakini kitendo cha Makamu Mwenyekiti kumkosoa hadharani ni utovu wa nidhamu.

  Namshauri Makamu Mwenyekiti asifanye KUKURUPUKA kama Bibi Kiroboto alipokuwa Naibu Spika!
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwanza hakuna siyejua kwamba John Shibunda amechanganyikiwa baada ya kukosa nafasi ya uongozi kitaifa aliyoitegemea kwamba akijiunga Chadema ataipata.
  Wengi wetu tunajua Shibuda ni vuvuzela, anaropoka ovyo tu na ndicho kilichompa taabu CCM hadi kutemwa kwenye kura za awali kufanyiwa mizengwe.

  Viongozi wa juu Chadema wameshamdharau, ndo maana hawana muda kuhangaika na mtu ambaye wanamjua alivyo, kujitosa kujadiliana naye ni kukaribisha machafuko chamani, bora ni kumdharau tu.
   
 7. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Kuharisha uharishe wewe halafu alaumiwe CCM!
  Komaa kidogo mkuu.
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Pamoja na ukweli huo, hata Heche mwenyewe alifanya kosa kwani alitakiwa kuwa na kikao cha majadiliano kabla ya kutoa kauli. Kuwa mwenyekiti hakumhalalishi kutoa matamka binafsi, ila tamko litokane na kikao. Kupigiwa simu na baadhi ya wajumbe au kuomba ushauri kwa njia ya simu si sawa na kukutana katika kakao na kujadiliana kutoa tamko ambalo litakuwa limepimwa kwa pamoja.
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hujasoma kujua kuwa nukuru ndiyo njia bora ya kutoa majumuisho ya hitimisho katika uchambuzi, uamuzi? Hivi we umeshawahi kufanya utafiti? Hata hukumu mahakamani hunukuru yaliyopita hata yaliyotolewa na mahakama nyingine katika nchi nyingine.
   
 10. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tunawasibiri wasaliti, tuwatambue kabla hatujachukua Nchi. Shibuda ana matatizo ya Kiakili na hata huyu Binti tunamjua sana yuko kambi ya Zito kwa hiyo anakuwa na Hofu sana kwa sababu ya uropokaji... Mimi nashangaa huyu underground anaibuka leo na kumpinga mwenyekiti wake.. Huku ni kutafuta umaarufu ambao hauna Msingi wowote na ndiyo watu ambao CCM inawa finance ili wakagombee Nafaisi binafsi (Mgombea Bonafsi).

  Haya Magugu ni kuwatoa tu ili wastupunguzie Kura 2015... Mbona ANC wamemng'oa Malema na mambo yanaenda vizuri.
   
 11. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #11
  May 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Candid Scope hata mimi nilishasema humu hayo mambo ya matamko. Hapo zamani yalikuwepo sana huko nyuma kwenye uongozi wa juu. Hiyo yote mimi nilisema ni kujitafutia umaarufu wa mtu mmoja mmoja. Nadhani wataifanyia kazi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo nilikuwa na maana ya kuhimiza wapenzi wa CDM kukua na kujiangalia kwa undani makosa wanayofanya kioganaizesheni.
  Haisaidii sana kulaumu wengine kwa makosa yako ya kiutendaji.
  In short CDM should grow up and not cry wolf for their own failures.
   
 13. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #13
  May 21, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Absolutely Candid scope,

  actually kuna mahali nimesema hivi..

  I Expected BAVICHA cadres and organs to organize more activities with more appeal to young citizens, and strengthen the youth council's construction to increase the council's influence among Tanzanian's youth.Petty squables are not healthy.

  Tarehe 28/5/2012(jumatatu ijayo) Baraza la vijana Chadema Taifa linamaliza mwaka mmoja tangu lichaguliwe.

  Nategemea wiki hiii itakuwa ni wiki maalumu kwao katika kujitathmini kwamba ndani ya Mwaka mmoja BAVICHA imefanya nini.

  Nilikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kabisa kutoa tahadhari.JF haikuwa Hewani lakini waliokuwa wanachama wa JF facebook tulijadili.Nilisema Shibuda hastahili kujibiwa.Anastahili kuachwa tu bila kujibizana nae kwenye media kwani huo ndiyo mchezo anaoutaka.Anataka kupandishwa chati kisiasa(najua kamanda shibuda ni member wa hapa JF unachungulia humu).Ulichungulia humu hata nilipokuwa nakutolea mfano kuhusu mtizamo wangu na cross-carpeting za wanasiasa kutoka chhama kimoja kwenda kingine.Nilisema bila darasa la Itikadi hapa itakuwa kazi kweli kweli.Itabidi kuwe na timua timua za ovyo kwenye vyama vya siasa.

  Akiwa CCM alitangaza kugombea Urais kupambana na Jk mwaka 2010.Hakuna mwana-CCM makini aliyemjibu isipokuwa Mzee Makamba aliyeapa kwamba yupo radhi kwenda Jela kuliko kuruhusu upinzani dhidi ya JK,2010.mnalijua hilo,linajulikana

  The best way to deal with comrade Shibuda is to ignore him.

  Makosa yanafanyika pamoja na kwamba ni demokrasia lakini utani mwingine ni gharama kweli kweli.Huwezi kutangaza kugombea Urais Chadema halafu ukataka meneja kampeni wako awe mwenyekiti wa CCM halafu tukuchukulie mtu serious.Haya ni makusudi kwa kuwa Shibuda ni mzoefu wa michezo ya kisiasa na anajua analenga nini.

  Hata mimi ningekuwa mwenyekiti wa vijana nisingevumilia kuona hili.

  Sasa naamini hili suala litatauliwa kwa busara.Makamu Mwenyekiti Juliana Shonza ni kiongozi makini na shupavu kweli kweli.Ni kiongozi hodari.ni kiongozi adimu ambaye hawezi kupatikana kwingine isipokuwa ndani ya chadema tu.Anapenda kusema kile anachoamini.Nilipogombea uenyemkiti wa vijana huyu ndiye alikuwa chaguo langu.Aliniunga mkono na nilimuunga mkono.Sijawahi kutilia mashaka uwezo wake wa kuongoza.Kama kuna tatizo la flow of information nadhani tatizo hili litamalizika ndani ya vikao vya chama tu.It's not a big deal at all

  Laiti tungekuwa na muundo kama wa ANC-YL ya Afrika Kusini basi leo tungekuwa na msemaji wa kama alivyo comrade floyd shivambu wa ANCYL.Mabaraza yote na jumuiya zote za vijana ndani ya vyama vya siasa Tanzania hatuwa na muundo kama huo kitu ambacho kinaweza kutoa mwanya kwa vijana kujikanganya au kuburuzana katika uendeshaji wa shughuli za kila siku kisaiasa na pengine hata maadui wa demokrasia kutumia mwanya huo kuleta mvurugano.

  Naamini Baraza la vijana,litamaliza tatizo hili.Tusiwe na papara za kuhukumu watu.Tuwe na subira,tusikurupuke.Diplomasia na Busara inahitaji kutumika hapa.This is the right time to show leadership.

  Malumbano ya watu binafsi yasiharibu taasisi.Shutuma kwamba Baraza la vijana ni wahuni hazivumiliki
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mwenye uelewa mpana anajufa fika umuhimu wa ufafanuzi na upambanuzi na angalisho ya kauli yako. Nashukuru kwa mwono wako mpana wenye kulenga kuleta mshikamano zaidi.
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  May 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tatizo naona huyo binti anataka mambo yaendeshwe kama ccm. Tumeona mlolongo mrefu wakati wa kufanya reshuffle baraza la mawaziri. Walianza ccm bungeni, ikaja CC ya ccm DAR then wakakaa wakubwa tena ndio week mbili baadae rais anafanya mabadiliko! Huu ni udhaifu mkubwa maana baraza la mawaziri liko chini ya Rais, mambo ya vikao ni kupotezeana muda.

  Sasa huyu binti anataka issue ya kumaliza kwa dakika chache waitane kila kona na kujadili! Wajadili nini? Yeye mwenyewe anakubaliana na tamko la Shibuda?
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kosa kuhamaki kuitisha vyombo vya habari jambo ambalo Mwenyekiti na Makamu wake wamefanya. Tamko lao si lazima litolewe mapema hivyo, na pengine wangeweza kuwauliza viongozi wao wa Juu akina Mbowe, Slaa na wengineo kupata ushauri wao namna bora inayofaa badala ya kujenga ufa unaoonekana waziwazi nje kupitisha mende waingie ndani ya mjengo.
   
 17. M

  MR.PRESIDENT Member

  #17
  May 21, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani makamu mwenyekiti ana uvumilivu wa kisiasa .Sasa yeye anadhani tamko kama alilolitoa ni kwa faida ya nani?Amenufaika nini kuwa front page.Tufike hatua tujue jinsi ya kuvumiliana kusolve matatizo ndani kwa ndani hata kama mkuu wako kakosea .Hongera Heche kwa kutomjibu huyu makamu wako maana ajui alitendalo.
   
 18. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #18
  May 21, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Hapa naona point zote zimeongelewa,kutenda kosa si kosa kosa ni kurudia kosa,cha msingi ni kujipanga na kukiimarisha chama,penye mapungufu pafanyiwe kazi ili upande wa pili wasipate cha kuongea,
  CHADEMA FOR LIFE.
   
 19. n

  nyandaojiloleli JF-Expert Member

  #19
  May 21, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  muda wa kumjadili shibuda haupo bali shibuda ni wa kupuuzwa hana lolote yule na watu wote wanamjua.
   
 20. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #20
  May 21, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,461
  Likes Received: 2,506
  Trophy Points: 280
  Mbona Heche Mnasema kakosea straight bila Kumung'unya maneno, ofcourse amekosea kweli, Lakini huyo Dada Juliana hamtaki kusema kuwa straight kuwa na yeye kakosea, Usiwe Biased Ben , watu wanaweza wakasema Pengine unachuki Binafsi na Heche coz u competed for the same post.

  Nataka useme hivi, Heche alikurupuka kutoa tamko, na Pia huyo Dada alikurupuka Zaid kutoa tamko na kumkosoa Mwenyekiti bila kutumia vikao halali, tusiwe na Double standard jaman eeeh.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...