amenikera sana!
Mkuu Candid scope, Kama huyu ni kijana mdogo basi makosa yake yangelingana na udogo wake. Umesema sawia kabisa kuwa huenda katumwa na kuna watu nyuma yake. Yeye amekubali kutumiwa akiwa kama kiongozi. Hapo hakuna udogo kuna ujinga na hilo tu linamuondolea sifa ya uongozi na kumwacha na udogo wake.Kosa ni kosa tu, ila kurudia kosa ni udhaifu usiokubalika na huhatarisha. Tukumbuke kwamba vijana bado wadogo na upeo wao katika masuala ya kijamii bado ni mdogo, ndio maana wanaandaliwa wakomae kwa siku za usoni kuwa watendaji wazuri.
Nisingependezwa sana na ibuko la hoja ya kumfukuza Makamu mwenyekiti, kwani kufukuzana si dawa ya kujenga chama, bali kudhoofisha chama. Jambo muhimu ni kumweka kitako Makamu mwenyekiti ajue kosa alilofanya ili asirudie kosa kama hilo tena. Asiposikia na kufuata ushauri hapo hakuna namna nyingine zaidi ya termination from her post. Afundwe namna bora ya utendaji katika ofisi yao kuwa ni mawasiliano, na katu asiwe tayari kutumiwa na wengine kutoa matamko. Tuelewe tamko lile si lake binafsi kuna walio nyuma ya pazia. Akifukuzwa huyu dada atakuwa ameonewa tu kwa vile ametumiwa kama chambo tu. Kuna waliojificha nyuma yake ambao hawataki wajulikane kwamba wako kinyume cha mwenyekiti. Hayo ni makovu ya uchaguzi uliopita ukiangalia kwa jicho la upembuzi.
Angefukuzwa Shibuda tangu alipoanza mizengwe yake huenda kungekuwa na athari zaidi kuliko alivyoachwa. Ndio maana dhana ya ignore imemweka Shibuda katika kapu kisiasa badala ya kuwa jukwaani kama wengine wanavyozidi kuchanja mbuga katika kutangaza magwanda yao. Aanachofanya sasa ni kujikomba upande wa CCM kwa vile ameshapoteza mwelekeo upande wa chama chake alivyotarajia.
Kwa vyo vyote vijana hawa wanahitaji kijana mwenzao kama Zitto au Mnyika kuwasaidia kukaa sawa ofisini mwao, la sivyo matamko yanayokinzana yanatoa mwanya wa kuweka nyufa za kupitisha mende kisha siafu watafuta harufu ya mende na hakutakalika huko ndani.
viongozi wanawake tanzania ni wachache sana aisee, halima mdee, is among them, huyu makamu mwenyekiti wa BAVICHA ndo nimemfahamu leo kwa upumbavu wake,huyu dada asiharibu mtazamo mzuri tulio nao kwa wanawake kuhusu kupata nafasi za uongozi na kuzitumia vema na kwa busara.
Mkuu Candid scope, Kama huyu ni kijana mdogo basi makosa yake yangelingana na udogo wake. Umesema sawia kabisa kuwa huenda katumwa na kuna watu nyuma yake. Yeye amekubali kutumiwa akiwa kama kiongozi. Hapo hakuna udogo kuna ujinga na hilo tu linamuondolea sifa ya uongozi na kumwacha na udogo wake.
Kumbuka CDM kikiwa chama tawala leo hawa ndio wanategemewa kuunda serikali, sasa tuwasamehe kwa udogo upi wakati ukubwa umeshatimia.
Kitendo cha kutumiwa ni dalili njema kuwa yeye kama kiongozi analea mbinu chafu na hilo linamuondolea sifa ya uongozi
Nimeainisha kwanini afukuzwe na nitashangaa sana kama CHADEMA hawatamfukuza uongozi. Lakini pia nimependekeza option ya yeye kuomba radhi.
Narudia tena kuwa CHADEMA huyu ni mtu hatari sana kwa ustawi wa chama chenu. Aondolewe ili waliomtuma wafahamu kuwa hakuna mkubwa zaidi ya chama na kwamba sheria ni msumeno. Akiachwa ataendelea kupika majungu na kukiangamiza chama kama CCM ilipo.
Asifukuzwe uanachama hata kidogo, AFUKUZWE UONGOZI. Hafai huyu, kuna maelefu ya vijana wenye akili nzuri, ni aibu chama pinzani kuwa na mtu mmoja anayevuruga chama kwa wiki sasa. Watu wamesahu shughuli nyingine kwasababu ya huyu Dada na chama kinazidi kupakwa matope kwa sababu ya huyu mtu mmoja.
Nitawashangaa sana CDM kama watamwacha aendelee na uongozi. Chadema watapoteza moral authority ya kunyooshea kidole CCM. CDM itakuwa inafanyia kazi template ya CCM.Ni aibu kubwa sana na hapaswi kulelewa kisiasa kwasababu dalili za awali zimeonyesha ni sumu na wala hataelewa hata kama atafundishwa. Hafai huyu CDM!
Tuliwapa 'open book exam' yeye amefeli. Tuliwatahadharisha yeye amefeli. Hafai huyu na kama BAVICHA ni tofauti na UVCCM basi imuondoe haraka sana katika uongozi. Kumuacha huyu itakuwa UVCCM-B na wakae kimya daima milele. Tusijewasikia wakisema tena maana hawatakuwa tofauti na huyu dada ambaye ni miongoni mwao. Hafai hata kwa bahati mbaya!
Mbona Heche Mnasema kakosea straight bila Kumung'unya maneno, ofcourse amekosea kweli, Lakini huyo Dada Juliana hamtaki kusema kuwa straight kuwa na yeye kakosea, Usiwe Biased Ben , watu wanaweza wakasema Pengine unachuki Binafsi na Heche coz u competed for the same post.
Nataka useme hivi, Heche alikurupuka kutoa tamko, na Pia huyo Dada alikurupuka Zaid kutoa tamko na kumkosoa Mwenyekiti bila kutumia vikao halali, tusiwe na Double standard jaman eeeh.
Nguruvi; umesema vizuri sana lakini huyu dada kadokeza kitu kimoja ambacho sidhani kama watu wamekifikiria na ambacho umekisema pia kuwa ni kufuata template ya CCM. Huyu dada alisema maneno ya Heche (mwenyekiti wa taifa) siyo ya Bavicha kwa sababu hakuna "kikao" kilichokaa na kuamua hivyo. Naita hili uongozi wa "vikao" kwamba hakuna lolote linaloweza kufanywa na viongozi au kutendwa bila vikao. Sasa hili ni zuri kwenye kupitisha sera n.k lakini linapokuja suala la kutenda wale waliopewa madaraka ya kutenda ni lazima watende.
Sijui Katiba ya BAVICHA inasema nini kuhusu madaraka ya viongoziwake lakini tunatarajia kuwa kiongozi anapokuwa kiongozi ana madaraka yote ya kiongozi. Kauli ya Heche ilipotolewa ilitakiwa kutetewa na viongozi wengine wote kwa sababu yeye ndiye kiongozi mkuu wa Bavicha na inawezekana ndiye "msemaji mkuu" wa Bavicha kwa mujibu wa katiba yao. Huyu makamu hana madaraka wala uwezo wa kusimama na kusema "ile" siyo kauli ya bavicha!
Lakini tatizo ninalolizungumzia ni hili la 'vikao'. Kwamba, watu wenye madaraka kamili wanashindwa kusema au ufanya jambo lililo ndani ya uwezo wao bila vikao. Hivi, ina maana kila wakati jambo linatokea baraza lazima liitwe liulizwe litoe kauli yake? sasa kuna maana gani ya kuwa na Mwenyekiti? Mbona ni kana kwamba dhana ya madaraka (authority) haijaeleweka? Kama kauli ya Heche ambaye ndiye kiongozi mkuu wa vijana wa CDM haina nguvu yenyewe hadi ipepewe na kufukizwa udi na kikao kuna maana gani ya kuwa na Mwenyekiti? si kamati tu iwe inaongoza na kila jambo lifanywe na kamati hiyo?
Ndio maana naamini ningekuwa na uwezo huyu binti angeomba msamaha kwanza kwa kuingilia mambo yasiyo yake na akikataa anaambiwa ajiuzulu - bila kujali watu watasema nini. Somebody in CDM needs to show leadership. Shibuda anawajaribu na sasa huyu naye mwisho 2015 itafika na tutarudi exactly at status quo ya 2010!
Mkuu Candid,
Mimi nataka nikuulize, Hivi tutafanya vikao kwa kila jambo? Hivi hata mwanachama wa Chadema akisema CDM hakiwezi na hakina uwezo wa kushika dola kumjibu tunahitaji vikao vya nini? Hicho ndicho kinachoicost CCM kutokana na viongozi hawafanyi majukumu yao wanakuja na excuses kila siku... Mimi nafikiri Shibuda alishavumiliwa sana na Mchwa wapo CDM baada ya kuona matumaini ya kupata Mpunga CDM haupo kinachotakiwa ni kazi kwa kwenda mbele, basi ameamua kuanza kuta matapishi yake tangu Baada ya Uchaguzi.
Na wote wanaomtetea Shibuda ni kuwatema Uanachama.. Ni heri kuwa wachache CDM na mkadeliver kinachoeleweka kuliko kuwa wengi halafu yaendelee yale yale ya CCM... Shibuda inaonyesha ananjaa sana na kashaahidiwa Mpuunga... Na hao wanaompa ulinzi ndani ya CDM... Wajue ulinzi huo wanaompa siyo Bure... Kama ni bure basi na wao hawastahili kuwepo kwenye Meli hii ya Ukombozi wa Taifa letu.
Matamko ya mmoja mmoja hata kama anakinga ya kikatiba hayakubaliki kwa ajili ya kulinda mshikamano na umoja katika utawala wa kisheria. Ni dalili ya kuwepo ufa katika mfumo wa uongozi na nihatari kutohimili vishindo vya tetemeko la ardhi litokeapo nyumba yenye ufa.
Narudia kauli ambayo nilishawahi kumwambia Katibu Mkuu Dr. Slaa ambaye kwa sasa amefanikiwa kurekebisha kutoka safu ya juu Chadema, lakini tatizo ni kwa Ngazi ya juu Umoja wa Vijana Chadema.
Lazima kuondokana na mlipuko wa kujibu kwenye vyombo vya habari ghafla bila upembuzi wa kutosha, bila kutuliza kwanza nerves, bila kikao cha kushauriana nini cha kujibu na papo kuangalia upande wa pili wa sarafu athari zake kwa tamko litakalotolewa.
Busara inavyoonekana katika uongozi wa juu kwenye Uongozi wa Chadema naheshimu na ndicho kinachotakiwa, ila ipo kazi kuwaweka sawa viongozi wa BAVICHA.
Candid Scope naheshimu michango yako na hata Avatar yako. La msingi hapa ni hawa viongozi kujifunza kwamba kwa sasa wanapoongea, wanakisemea chama hata kama wapo nyumbani au baa. Kwenye vyombo vya habari ndo kabisa. Kwa hiyo wanatakiwa kujifunza kusemea chama na siyo wao tu. Hii itawafanya kufikiria chama na kuomba ushauri kabla ya kuongea na vyombo vya habari. Kuhusu huyu makamu wa mwenyekiti, labda ndivyo alivyo shauri . Sasa tujiulize, lipi ni tamko la BAVICHA, la mwenyekiti au makamu mwenyekiti? Je tutajuaje kuwa sasa mwenyekiti anaongea mawazo yake? Mambo yanapokuwa mambaya watu huyakimbia na kuyaacha kwa mhusika, lakini yakiwa mazuri, ya chama. Wapewe semina elekezi, lakini mambo ya kuja kutoa maelezo eti ni mawazo ya kiongozi kama yeye, mimi haiji akilini. Kwa sababu inaonyesha uwezo wa kiongozi huendani na chama.
Thread tamu hii!!
Wanajifunza uongozi, muda uliobakia unatosha kabisa kabla ya uchaguzi 2015. Isipokuwa huyo Heche kwa kweli alikurupuka nadhani alikuwa na kinyongo na Shibuda akasahau kufikiri kwanza kabla ya kutoa tamko. Kwa hiyo ajifunze kwamba uongozi hauendi kwa chuki na kuviziana kwenye kona
Nyie ndio mmeiangushia Tz jehanamu halafu eti mnajidai ''tuwape muda wajifunze''. Mnajua uongozi?Leadership is a process... CDM will have to go through it... and this is the time.... Kuongoza Chama ni tofauti na Serikali... in government you can command etc... but not in political party... tuwape muda vijana wajifunze....
Mbona Heche Mnasema kakosea straight bila Kumung'unya maneno, ofcourse amekosea kweli, Lakini huyo Dada Juliana hamtaki kusema kuwa straight kuwa na yeye kakosea, Usiwe Biased Ben , watu wanaweza wakasema Pengine unachuki Binafsi na Heche coz u competed for the same post.
Nataka useme hivi, Heche alikurupuka kutoa tamko, na Pia huyo Dada alikurupuka Zaid kutoa tamko na kumkosoa Mwenyekiti bila kutumia vikao halali, tusiwe na Double standard jaman eeeh.
Lakini huyu mwana mama nae mwambieni atulize mapepo yake. Kama aliona mwenyekiti amepotoka kwanini yeye azidi kuleta matatizo? Nae ni kicheche tu. Ni kundi moja na wewe na Zitto.
Mr.Clean,
kwahiyo hata hapa bado mwaungana mikono......! nadhani bado kuungana mwili...! umeshajipambanua wazi kuwa HECHE alikubwaga mlipogombea uenyekiti. sasa utamsifia kwa lipi tena....weye siulisema waenda jimboni rombo kucompete na selasini ubunge? huyo bibie ndo meneja campaign wako ee...kaza buti kijana..!
Nguruvi; umesema vizuri sana lakini huyu dada kadokeza kitu kimoja ambacho sidhani kama watu wamekifikiria na ambacho umekisema pia kuwa ni kufuata template ya CCM. Huyu dada alisema maneno ya Heche (mwenyekiti wa taifa) siyo ya Bavicha kwa sababu hakuna "kikao" kilichokaa na kuamua hivyo. Naita hili uongozi wa "vikao" kwamba hakuna lolote linaloweza kufanywa na viongozi au kutendwa bila vikao. Sasa hili ni zuri kwenye kupitisha sera n.k lakini linapokuja suala la kutenda wale waliopewa madaraka ya kutenda ni lazima watende.
Sijui Katiba ya BAVICHA inasema nini kuhusu madaraka ya viongoziwake lakini tunatarajia kuwa kiongozi anapokuwa kiongozi ana madaraka yote ya kiongozi. Kauli ya Heche ilipotolewa ilitakiwa kutetewa na viongozi wengine wote kwa sababu yeye ndiye kiongozi mkuu wa Bavicha na inawezekana ndiye "msemaji mkuu" wa Bavicha kwa mujibu wa katiba yao. Huyu makamu hana madaraka wala uwezo wa kusimama na kusema "ile" siyo kauli ya bavicha!
Lakini tatizo ninalolizungumzia ni hili la 'vikao'. Kwamba, watu wenye madaraka kamili wanashindwa kusema au ufanya jambo lililo ndani ya uwezo wao bila vikao. Hivi, ina maana kila wakati jambo linatokea baraza lazima liitwe liulizwe litoe kauli yake? sasa kuna maana gani ya kuwa na Mwenyekiti? Mbona ni kana kwamba dhana ya madaraka (authority) haijaeleweka? Kama kauli ya Heche ambaye ndiye kiongozi mkuu wa vijana wa CDM haina nguvu yenyewe hadi ipepewe na kufukizwa udi na kikao kuna maana gani ya kuwa na Mwenyekiti? si kamati tu iwe inaongoza na kila jambo lifanywe na kamati hiyo?
Ndio maana naamini ningekuwa na uwezo huyu binti angeomba msamaha kwanza kwa kuingilia mambo yasiyo yake na akikataa anaambiwa ajiuzulu - bila kujali watu watasema nini. Somebody in CDM needs to show leadership. Shibuda anawajaribu na sasa huyu naye mwisho 2015 itafika na tutarudi exactly at status quo ya 2010!
HABARI YA UHAKIKA: Kikwete ametengeneza mtandao Chadema kwa kutumia TISS. Nina info za ndani, jikoni liliko jungu likitokota. Zinatumika fedha nyingi na ahadi za vyeo kemkem. Ndio maana mambo kama haya yapo na YATAKUWEPO. Chunga sana hii listi.... Zitto, Ben, ''Mzee Shibuda'' kama anavyoitwa na huyo makamu wa mwenyekiti njaa, yeye mwenyewe (makamu bavicha). Wana jeuri mbaya sana na wameahidiwa mengi. Tunawamulika kwa karibu kila nyendo tena kwa kituo. Tumeweza kupenyeza watu wetu. Tunasubiri siku ya siku....Ninadhani hapa kutakuwa kuna mkono wa TISS dhidi ya CDM, Haiwezekani, tena nasema haingii akilini kuwa leo Makamo mwenyekiti anaweza kuwa na power ya kumuignore mwenyekiti wake! kuna kitu tusubiri... nadhani ile dhana ya juridiction na separation of power bado ni tatizo kwa walio wengi, sasa tazama jinsi huyu binti alivyo jiua kisiasa
Kukosea ni hulka ya kibinadamu na inapotokea mhusika huomba radhi. Semina elekezi haitamsaidia huyu Dada kwani ni dhahiri kuna watu wapo nyuma yake, hawa ndio watakaovuruga chama.Candid Scope naheshimu michango yako na hata Avatar yako. La msingi hapa ni hawa viongozi kujifunza kwamba kwa sasa wanapoongea, wanakisemea chama hata kama wapo nyumbani au baa. Kwenye vyombo vya habari ndo kabisa. Kwa hiyo wanatakiwa kujifunza kusemea chama na siyo wao tu. Hii itawafanya kufikiria chama na kuomba ushauri kabla ya kuongea na vyombo vya habari. Kuhusu huyu makamu wa mwenyekiti, labda ndivyo alivyo shauri . Sasa tujiulize, lipi ni tamko la BAVICHA, la mwenyekiti au makamu mwenyekiti? Je tutajuaje kuwa sasa mwenyekiti anaongea mawazo yake? Mambo yanapokuwa mambaya watu huyakimbia na kuyaacha kwa mhusika, lakini yakiwa mazuri, ya chama. Wapewe semina elekezi, lakini mambo ya kuja kutoa maelezo eti ni mawazo ya kiongozi kama yeye, mimi haiji akilini. Kwa sababu inaonyesha uwezo wa kiongozi huendani na chama.