Mkuu MM, umenikumbusha kitu zaidi. Huyu Dada amesema maneno ya Heche si ya BAVICHA kwasababu hakuna kikao kilichofanyika kutoa kauli hizo. Sijui kama kuna kikao cha BAVICHA kilichokaa ili kutoa kauli ya kuji-dissociate na kauli za Heche kama alivyokanusha Dada yetu. Ndiyo maana nakaandika kuwa huenda ametumwa na sehemu ya uongozi au kundi ndani ya CDM. Je, kama kilikuwepo kikao, ni nani alikuwa mwenyekiti hadi Naibu wa mwenyekiti atoke na kauli ya kumdhalilisha mwenyekiti?
Ukitazama kauli ya Heche kama mwenyekiti haikuwa na maudhui au muundo wa kashfa. Alichokifanya Heche kisiasa kinakubalika'rebut' baada ya chama kudhalilishwa siyo kwa hoja ya kugombea bali hoja za udhaifu wa upinzani Shibuda akiwa mpinzani. Hata bila kauli ya Heche bado wanachama, manazi na mashabiki wa CDM walikereka.
Kauli ya Heche ilipaswa kutetewa kama ulivyonena kwa vile ni kauli ya mwenyekiti iliyolenga kulinda masilahi ya chama isiyo na matusi,kashfa bali majibu. Nimeandika (Duru za siasa) kuwa vyama lazima viwe na 'pundits' kutetea chama katika nyakati kama hizi na athari zake ndizo hizi. Mwenyekiti anaachwa nyikani mwenyewe
Ukisoma bandiko langu la mwisho katika safu ya (Duru za siasa) mara tu baada ya kauli ya Shibuda kumjibu Heche, niliweka wazi kabisa kuwa silaha anayotaka kuitumia Shibuda ni kumwandama Mwenyekiti Heche ili ugomvi uonekane ni kati yake na Heche na siyo CDM kwa minajili ya kujilinda na matokeo anayojua yatamsibu
Nilitahadharisha CDM juu ya hilo kwa bahati mbaya ushauri ukapuuziwa. Leo Shibuda ameibuka Kanda ya ziwa akiwa hana madai ya usukuma wake na kujikosha kuwa hana ugomvi na Chadema bali Heche. Hii imeshadidiwa na kauli ya Naibu BAVICHA mwanadada aliyekitenga chama na kumwacha Heche nyikani kana kwamba alikuwa anatetea familia binafsi.
Chadema wameingia katika mtego wa Shibuda hata pale tulipowapa majibu ya mtihani.
Lakini pia tujiulize kama huyu dada amedai kuwa kauli zile za Heche si za CDM, je ni kauli gani anazodhani Heche amevuka mipaka na nini msimamo wa BAVICHA kuhusu sakata la Shibuda?
Kutoa kauli tu kuwa BAVICHA haihusiki hakujajibu maswali na ni uchanga wa kisiasa usiohitaji ulezi bali kuondolewa
Naungana na MM kuwa Huyu Naibu BAVICHA(Dada) achukuliwe hatua
1. Kama alivyonena MM, aombe radhi kwa kumdhalilisha Mwenyekiti ambaye kiutaratibu ni mkuu wake wa kazi mbele ya vyombo vya habari na umma kwa ujumla
2. Aeleze wapi alipata mwongozo wa kukanusha kauli za BAVICHA na BAVICHA ipi ilimpa ridhaa ya kukanusha.
3. Alazimishwe kuachia ngazi kwasababu zifuatazo:
i] Hajui taratibu za uongozi
ii) Amekiingiza chama katika mtafaruku usio wa lazima na kuondoa mwelekeo wa kampeni zinazoendelea
iii] Anatumiwa na kundi lisilojulikana ndani ya chama kama hakupewa ridhaa na BAVICHA au uongozi
iv] Kushindwa kutetea masilahi ya chama na kuonyesha uoga kwa Shibuda bila sababu za msingi