Viongozi acheni utani wa maisha ya raia wenu, chukueni hatua za haraka kabla nchi haijageuka kuwa graveyard

Its not too late, serikali chukueni hatua madhubuti ikiwemo kufunga mashule na vyuo kabla hali haijawa mbaya zaidi. Its not too late.
 

Je, Mungu kalipa kisogo taifa lake pendwa?
Exactly.

Kwa kuwa Mungu anasimamia haki, hauwezi wewe Jiwe ukusimama katika Public, ukasema kuwa Taifa letu linamtegemea Mungu wetu...........

Wakati huo huo serikali yako ndiyo inayoongoza kwa ukandamizaji wa haki za binadamu!

Ni lazima huyu Mungu wetu atakuonyesha cha mtema kuni
 
Mwaka jana tuliishinda corona kwa sababu zifuafazo:

1. Serikali ilikuwa mstari wa mbele kusimamia mapambano ya corona

2. Kulikuwa na taskforce inayoshughulika na wagonjwa wa corona. Kama mgonjwa yuko nyumbani mlikuwa hamruhusiwi kumsafirisha ila mnapiga simu anafuatwa nyumbani ili kuepusha maambukizi mapya.

3. Mazishi yote yalikuwa yanafanywa na special taskforce walopewa mafunzo ya namna ya kuhandle corona cases.

4. Kulikuwa na isolation centers na treatment centers. Hizi zilisaidia kuepusha kuwachanganya wagonjwa wa corona na wale wasio na corona.

5. Kulikuwa na upimaji kwa suspects wote.

6. Jamii yote ilikuwa inashiriki kwenye juhudi za mapambano(na ndivyo inavyotakiwa maana personal precautions hazina impact kufananisha na public precautions).

Hali ilivyo hivi sasa:

1. Serikali haijaweka wazi kama kuna corona ama laah zaidi ya maneno ya viongozi baadhi ambayo mengi ni contradicting pia. Kifupi hakuna official statement hasa kutoka wizara husika inayoeleza nini cha kufanya.

2. Hakuna taskforce yoyote inayoshughulika na wagonjwa wa corona a.k.a nyumonia kali, wanaoumwa tunachangamana nao mitaani na majumbani na hii inafanya maambukizi yaenee kwa kasi zaidi.

3. Misiba ni mingi mnoo huko mitaani. Kinachosikitisha zaidi ni kwamba misiba hii inaendelea kuendeshwa kwa taratibu zisizo na tahadhari bila kujali marehemu kafariki kwa ugonjwa gani. Hii pia inafanya maambukizi yaenee kwa kasi ya upepo. Nadhani tumeyaona yaliyompata Prof. Mamiro wa SUA na familia yake, uzembe wa kuhandle mazishi ya wazazi wao kwa taratibu zinazotakiwa yamefanya na wao waambukizwe na hawajachukua round wamewafuata wazazi wao.

4. Hakuna isolation wala treatment centers za kuwahudumia wagonjwa wa corona a.k.a nyumonia. Ni hatari sana sababu hawa wagonjwa wanachanganywa na wagonjwa wengine huko mahospitalini na hii inazidi kufanya maambukizi yazidi kusambaa.

5. HAKUNA UPIMAJI WA SUSPECTS. Hii ndio mbaya zaidi sababu hatujui yupi anaumwa corona kweli na yupi anaumwa magonjwa mengine tuu japokuwa ana dalili zinazofanana na corona.

6. Jamii haijawa sensitized ichukue mass precautions, tukumbuke kujifanya unachukua tahadhari peke yako haikusaidii chochote kulingana na research zinavyosema. Hivyo yahitaji watu wote washiriki ndipo tutaweza kuzuia maambukizi kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Hivyo kwa hali ilivyo sasa na mwanzo inaonekana kuna ombwe kubwa kwenye kuhandle mlipuko huu wa sasa. Kiukweli kwa tabia za huyu kirusi zilivyo inawezekana tukaishi naye kwa miaka nenda rudi, hakuna dalili ataondoka hivi karibuni, na sisi sio kisiwa tuseme eti kwamba kwetu hatoleta madhara, tunajidanganya.

Kabla vilio havitamalaki kila kijiji na kila mtaa ni vizuri ichukue angali mapema, the earlier the better. Kwa nini msubiri mpaka kila familia iguswe ndipo mchukue hatia madhubuti?

To a nation every life if precious and worthsome.
Sijui Kama kweli hau
 

Je, Mungu kalipa kisogo taifa lake pendwa?
Labda kama tunguli lilivyofeli kwenye uchaguzi
 
Back
Top Bottom