Viongozi acheni utani wa maisha ya raia wenu, chukueni hatua za haraka kabla nchi haijageuka kuwa graveyard

Feb 18, 2019
34
400
Mwaka jana tuliishinda corona kwa sababu zifuafazo:

1. Serikali ilikuwa mstari wa mbele kusimamia mapambano ya corona

2. Kulikuwa na taskforce inayoshughulika na wagonjwa wa corona. Kama mgonjwa yuko nyumbani mlikuwa hamruhusiwi kumsafirisha ila mnapiga simu anafuatwa nyumbani ili kuepusha maambukizi mapya.

3. Mazishi yote yalikuwa yanafanywa na special taskforce walopewa mafunzo ya namna ya kuhandle corona cases.

4. Kulikuwa na isolation centers na treatment centers. Hizi zilisaidia kuepusha kuwachanganya wagonjwa wa corona na wale wasio na corona.

5. Kulikuwa na upimaji kwa suspects wote.

6. Jamii yote ilikuwa inashiriki kwenye juhudi za mapambano(na ndivyo inavyotakiwa maana personal precautions hazina impact kufananisha na public precautions).

Hali ilivyo hivi sasa:

1. Serikali haijaweka wazi kama kuna corona ama laah zaidi ya maneno ya viongozi baadhi ambayo mengi ni contradicting pia. Kifupi hakuna official statement hasa kutoka wizara husika inayoeleza nini cha kufanya.

2. Hakuna taskforce yoyote inayoshughulika na wagonjwa wa corona a.k.a nyumonia kali, wanaoumwa tunachangamana nao mitaani na majumbani na hii inafanya maambukizi yaenee kwa kasi zaidi.

3. Misiba ni mingi mnoo huko mitaani. Kinachosikitisha zaidi ni kwamba misiba hii inaendelea kuendeshwa kwa taratibu zisizo na tahadhari bila kujali marehemu kafariki kwa ugonjwa gani. Hii pia inafanya maambukizi yaenee kwa kasi ya upepo. Nadhani tumeyaona yaliyompata Prof. Mamiro wa SUA na familia yake, uzembe wa kuhandle mazishi ya wazazi wao kwa taratibu zinazotakiwa yamefanya na wao waambukizwe na hawajachukua round wamewafuata wazazi wao.

4. Hakuna isolation wala treatment centers za kuwahudumia wagonjwa wa corona a.k.a nyumonia. Ni hatari sana sababu hawa wagonjwa wanachanganywa na wagonjwa wengine huko mahospitalini na hii inazidi kufanya maambukizi yazidi kusambaa.

5. HAKUNA UPIMAJI WA SUSPECTS. Hii ndio mbaya zaidi sababu hatujui yupi anaumwa corona kweli na yupi anaumwa magonjwa mengine tuu japokuwa ana dalili zinazofanana na corona.

6. Jamii haijawa sensitized ichukue mass precautions, tukumbuke kujifanya unachukua tahadhari peke yako haikusaidii chochote kulingana na research zinavyosema. Hivyo yahitaji watu wote washiriki ndipo tutaweza kuzuia maambukizi kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Hivyo kwa hali ilivyo sasa na mwanzo inaonekana kuna ombwe kubwa kwenye kuhandle mlipuko huu wa sasa. Kiukweli kwa tabia za huyu kirusi zilivyo inawezekana tukaishi naye kwa miaka nenda rudi, hakuna dalili ataondoka hivi karibuni, na sisi sio kisiwa tuseme eti kwamba kwetu hatoleta madhara, tunajidanganya.

Kabla vilio havitamalaki kila kijiji na kila mtaa ni vizuri ichukue angali mapema, the earlier the better. Kwa nini msubiri mpaka kila familia iguswe ndipo mchukue hatia madhubuti?

To a nation every life if precious and worthsome.
 
Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
3,859
2,000
Jamani, tuacheni woga, hofu, na kutishana. Tuungane pamoja, tuchape kazi kwa bidii, tuijenge nchi yetu nzuri ya Tanzania. Kama tulivyomshinda Mr Corona last year kwa nguvu ya maombi, upepo huu wa mafua na nimonia nao tutaushinda.

Don't panic!!! Kama tulimfurumua Nduli, mafua tu hayawezi kumshinda Mola wetu.
 
MISULI

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
7,389
2,000
Hivi Watu wameanza kufa mwaka huu? Nachoona now ni watu kuwa makini na misiba kila kona ya nchi.
 
Marco Polo

JF-Expert Member
Jan 16, 2014
3,762
2,000
Mkuu samahan, ukiacha mbali wazaz wao kuna mtoto yeyote wa familia ya prof Mamilo aliyefarik?
 
Ezekiel Mbaga

Verified Member
May 28, 2018
7,521
2,000
Ila watanzania tunawahi sana kusahau, si ndo nyie mliosema watu wanazikwa kinyama.

Cha msingi ni Corona ipo na serikali siishauri kutangaza ila kila mtu ajilinde, ina maana serikali ikitangaza ndo mtaanza kuchukua tahadhari?
 
UPOPO

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,910
2,000
Farao alishupaza shingo mpaka Mungu akapiga wazaliwa wakwanza wa kiume wakiwepo mtoto wa mfalme.
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
30,550
2,000
Hakuna jamii/nchi ambayo haikuwahi kulipa gharama pale wanapoweka corpses madarakani.Tunaenda kulipa gharama kubwa sana.Imagine mbunge anasimama bungeni anasema kuwa kitendo cha nchi kukataa kufanya social distance ni kitendo sahihi kitakachotupeleka sehemu sahihi!
 
EllySkyWilly

JF-Expert Member
Aug 28, 2020
2,123
2,000
Issue hapo ni kupambana kivyako, mkuu acha kufuatilia maisha yetu, kuanzia leo jifungie hapo nyumbani kwako.
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
156,270
2,000
Mwaka jana tuliishinda corona kwa sababu zifuafazo:

1. Serikali ilikuwa mstari wa mbele kusimamia mapambano ya corona

2. Kulikuwa na taskforce inayoshughulika na wagonjwa wa corona. Kama mgonjwa yuko nyumbani mlikuwa hamruhusiwi kumsafirisha ila mnapiga simu anafuatwa nyumbani ili kuepusha maambukizi mapya.

3. Mazishi yote yalikuwa yanafanywa na special taskforce walopewa mafunzo ya namna ya kuhandle corona cases.

4. Kulikuwa na isolation centers na treatment centers. Hizi zilisaidia kuepusha kuwachanganya wagonjwa wa corona na wale wasio na corona.

5. Kulikuwa na upimaji kwa suspects wote.

6. Jamii yote ilikuwa inashiriki kwenye juhudi za mapambano(na ndivyo inavyotakiwa maana personal precautions hazina impact kufananisha na public precautions).

Hali ilivyo hivi sasa:

1. Serikali haijaweka wazi kama kuna corona ama laah zaidi ya maneno ya viongozi baadhi ambayo mengi ni contradicting pia. Kifupi hakuna official statement hasa kutoka wizara husika inayoeleza nini cha kufanya.

2. Hakuna taskforce yoyote inayoshughulika na wagonjwa wa corona a.k.a nyumonia kali, wanaoumwa tunachangamana nao mitaani na majumbani na hii inafanya maambukizi yaenee kwa kasi zaidi.

3. Misiba ni mingi mnoo huko mitaani. Kinachosikitisha zaidi ni kwamba misiba hii inaendelea kuendeshwa kwa taratibu zisizo na tahadhari bila kujali marehemu kafariki kwa ugonjwa gani. Hii pia inafanya maambukizi yaenee kwa kasi ya upepo. Nadhani tumeyaona yaliyompata Prof. Mamiro wa SUA na familia yake, uzembe wa kuhandle mazishi ya wazazi wao kwa taratibu zinazotakiwa yamefanya na wao waambukizwe na hawajachukua round wamewafuata wazazi wao.

4. Hakuna isolation wala treatment centers za kuwahudumia wagonjwa wa corona a.k.a nyumonia. Ni hatari sana sababu hawa wagonjwa wanachanganywa na wagonjwa wengine huko mahospitalini na hii inazidi kufanya maambukizi yazidi kusambaa.

5. HAKUNA UPIMAJI WA SUSPECTS. Hii ndio mbaya zaidi sababu hatujui yupi anaumwa corona kweli na yupi anaumwa magonjwa mengine tuu japokuwa ana dalili zinazofanana na corona.

6. Jamii haijawa sensitized ichukue mass precautions, tukumbuke kujifanya unachukua tahadhari peke yako haikusaidii chochote kulingana na research zinavyosema. Hivyo yahitaji watu wote washiriki ndipo tutaweza kuzuia maambukizi kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Hivyo kwa hali ilivyo sasa na mwanzo inaonekana kuna ombwe kubwa kwenye kuhandle mlipuko huu wa sasa. Kiukweli kwa tabia za huyu kirusi zilivyo inawezekana tukaishi naye kwa miaka nenda rudi, hakuna dalili ataondoka hivi karibuni, na sisi sio kisiwa tuseme eti kwamba kwetu hatoleta madhara, tunajidanganya.

Kabla vilio havitamalaki kila kijiji na kila mtaa ni vizuri ichukue angali mapema, the earlier the better. Kwa nini msubiri mpaka kila familia iguswe ndipo mchukue hatia madhubuti?

To a nation every life if precious and worthsome.
Nimesoma kwa tafakuri kuu na kuogopa sana
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
156,270
2,000

Je, Mungu kalipa kisogo taifa lake pendwa?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom